Tanzania yaishitaki Malawi UN

Ujinga mtupu hakuna sababu ya kuwashitaki wamalawi, Tanzania inatakiwa ku-develop kwa nguvu ukanda wa ziwa upande wetu na kuweka vitega uchumi vya kukata na shoka kama vile usafiri wa majini katika vijiji husika, uvuaji wa kisasa kwenye eneo letu na kuweka kituo cha manoari za kivita kwenye eneo letu then tuone huyo kimburu anayetaka kuleta chokochoko. Actions speaks louder.

Wakati umefika kuondoa mizoga ya CCM.

Green colour........umechapia hicho kiinglish chako.
 
Sioni ni jinsi gani tunaweza kushinda hii kesi tukienda kwenye mahakama ya usuluhishi ile Heligoland treaty imetubana sana dawa ilikuwa ni vitisho na ubabe tu
Hii kesi imeisha isha na Wamalawi baada ya kutolewa vielelezo na mchanganuo wa kisheria ndipo walipokacha kikao cha Dar. Soma article ya Hamza Johari akimjibu advocate Fatma Karume ambae alikuwa na mawazo kama yako 'Is Anglo-German Treaty of 1890 on the Border delimination between Malawi and Tanzania Lawful under the eye of International Law?'
 
wamalawi washaoa hii ngoma nzito ndio maana wanakwepa kwepa kufanya hata mazungumzo..
cha maana ni kuwachimba mkwara wa maana hakuna kuvuka nusu ya ziwa bila kibali..........
 
Kuna Hatua Imerukwa Hapa Membe alituambia wata tafuta mtu wa waTu (third. Party Country)ambaye ana aminika kwa nchi zote akatisikiza na Akaamua...

Pili alituambia Gharama za kulipia UN ni dola 12,000 (kama sikosei) kwa Kikao kimoja...vitu vinginE watuweke. Wazi



Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Ukiwa dhaifu hata sisimzi atakupandia na kisha atakung'ata. Banda alipom-beep Mwalimu juu ya umiliki wa ziwa aliambiwa u-mwendawazimu na nidhamu ilifuata mkondo wake
 
Tanzania tukaweke manowari ya kivita? Bajeti ya Tanzania ni Bilioni 8 $ kama sikosei 40% inatoka kwa wageni halafu unaongelea kuweka Manowari za kivita Ziwa Nyasa, unamaanisha kweli au unatania?



Kwani hiyo 40% inakwenda wapi kama sio kwa wageni? Hatuhitaji misaada yao wameshindwa kujisaidia wenyewe na kuondoa matatizo yao wataweza ya kwetu?

 
Kwani hiyo 40% inakwenda wapi kama sio kwa wageni? Hatuhitaji misaada yao wameshindwa kujisaidia wenyewe na kuondoa matatizo yao wataweza ya kwetu?


Blah blah... unasema hatutaki misaada yao huku umekaa Dar kwenye kiyoyozi na iphone ukiperuzi JF, ukienda lushoto huko na vijijini vingine Tanzania huduma pekee ndugu zetu wanazopata kuanzia tiba mpaka chakula ni kwa wasamalia wema toka Ulaya na kwingineko, hata kulea wazee wetu pia ni Wazungu wanakuja kutusaidia, ukitoa hospitali za kanisa na shule hapa Tanzania watu wengi sana watakuwa hawana huduma kwa hiyo ni rahisi wewe uliyeko Dar mwenye Bima ya Afya na fungu la kwenda kutibiwa India kusema "hatutaki misaada"
lakini nakuhakikishia kuna Watanzania wengi sana vijijini hiyo hiyo misaada ya Wazungu imebadilisha maisha yao!

[/QUOTE]
 
Unajua ni mambo ya ajabu sana watu mnashabikia vita kwa kisingizio cha uzalendo hivi unajua ni Meli ngapi za kigeni zimejaa kwenye Bahari yetu zinavua samaki na kuondoka? kama hujui uliza wavuvi sasa hivi samaki wetu karibu wanaisha kwa sababu Meli kubwa zinakuja zinavua na kuondoka, tunashindwa hata kununua Patrol boat tu ya kuangalia mipaka yetu tena ambao haina mgogoro wowote, hivi unajua ni mizigo mingapi haramu inaingia kwenye Pwani yetu kuanzia Tanga mpaka Mtwara bila kukaguliwa kwa sababu tu tunashindwa kulinda mipaka yetu?
Unajua ni ndege ngapi na Meli zinaondoka na Rasilimali zetu bila kukaguliwa kila siku?
Tafuta Documentary ya " the Darwins Nightmare" kama bado hujaoiona uone jinsi rasilimali zetu zinavyoondoka, halafu unaongelea Uzalendo, mimi naita Unafiki, huo Uzalendo upo kwenye Ziwa nyasa tu? siku zote mtu akishindwa kitu anatafuta visingizio kwa upande wetu sisi tumeshindwa kujiongoza sasa tunatafuta visingizio!

Kuhusu vita ya Uganda wala usitake kuanza kuongelea huko ile ilikuwa ni "proxy war" kama vile Kenya wanavyofanya sasa Somalia au sijui Uganda na Sudan, na sisi wananchi tukajazwa propaganda tu!

Kuhusu Japan na China wao wana uwezo wa kupigana vita sisi HATUNA!

Wewe usitake kujidanganya Tanzania hatuna uwezo wa kuingia vitani sasa hivi achilia Malawi hata kuichukua Zanzibar tu wakiamua kuasi hatuwezi huo ndio ukweli ulio wazi!

Kuhusu Ziwa Nyasa na ndio maana nikatumia neno IKIBIDI kama imefikia kweli kuingia vitani baada ya njia zote za kidiplomasia kushindwa basi tukubali tuwe wapole kwani hatujui hao Wamalawi wamejiandaa vipi, huwezi jua labda wameahidiwa kusaidiwa na makapitalist ambao wako tayari wanafanya Utafiti wa Mafuta!

Ninajali sana maisha ya Watanzania wenzetu wanaoishi mwambao mwa Ziwa Nyasa na ndio maana sitaki vita itokee na ikibidi kama hamna jinsi basi wacha Ziwa liende kuliko kuingia vitani! Na baada ya hapo tuchukulie hilo kama fundisho tujipange, tujenge uchumi wetu imara ili huko baadaye tuwe na nguvu ya kujitetea, kinyume na hapo ni kujidanganya tu hata Raisi Kikwete analijua hilo na ndio maana ameshasema tena na tena, hatuna uwezo kama nchi wa kuingia vitani kwa sasa na yeye ni Amiri Jeshi Mkuu anapajua kila kitu kuhusu uwezo wetu wa kiuchumi!

Umewahi kufika Malawi? ..... usingesema hayo.
 
[/SIZE]
Blah blah... unasema hatutaki misaada yao huku umekaa Dar kwenye kiyoyozi na iphone ukiperuzi JF, ukienda lushoto huko na vijijini vingine Tanzania huduma pekee ndugu zetu wanazopata kuanzia tiba mpaka chakula ni kwa wasamalia wema toka Ulaya na kwingineko, hata kulea wazee wetu pia ni Wazungu wanakuja kutusaidia, ukitoa hospitali za kanisa na shule hapa Tanzania watu wengi sana watakuwa hawana huduma kwa hiyo ni rahisi wewe uliyeko Dar mwenye Bima ya Afya na fungu la kwenda kutibiwa India kusema "hatutaki misaada"
lakini nakuhakikishia kuna Watanzania wengi sana vijijini hiyo hiyo misaada ya Wazungu imebadilisha maisha yao!

Mkuu unaongea hayo maneno upo serious au unataka kufurahisha baraza?

 
tuwekeeni hiyo article ya hamza johari alliyomjibu fatma karume ili tupate ilimu na sisi
 
Mkuu unaongea hayo maneno upo serious au unataka kufurahisha baraza?

Nafikiri hilo swali nikuulize wewe unaesema "hatutaki misaada" wakati ukweli ni kwamba inahitajika na inasaidia watu!
 
Tanzania is already savouring the prospect of energy wealth with the announcement in February that Norwegian oil group Statoil and US company ExxonMobil had together discovered there a large natural gas field with reserves estimated at 140 billion cubic metres.
Now it also wants a slice of anything discovered near its shores in Lake Malawi.
"The lake historically belongs to us. Malawi must be firm on this and not relent," political pundit and rights activist Billy Mayaya told AFP, in an unforgiving tone that reflects the national mood on this issue.
"No inch of the lake must be given away... even at gunpoint," he said

sasa wtz inabidi jeshi lijipange maana msela huyo kasema hata cha mguu wa kuku hawatatoa hata inch moko werawera :)
chanzo...cha habari..Malawi banks on history to cling to lake in Tanzania dispute - Times LIVE
 
[/SIZE]
Blah blah... unasema hatutaki misaada yao huku umekaa Dar kwenyekiyoyozina iphone ukiperuzi JF, ukienda lushoto huko na vijijini vingine Tanzania huduma pekee ndugu zetu wanazopata kuanzia tiba mpaka chakula ni kwa wasamalia wema toka Ulaya na kwingineko, hata kulea wazee wetu pia ni Wazungu wanakuja kutusaidia, ukitoa hospitali za kanisa na shule hapa Tanzania watu wengi sana watakuwa hawana huduma kwa hiyo ni rahisi wewe uliyeko Dar mwenye Bima ya Afya na fungu la kwenda kutibiwa India kusema "hatutaki misaada"
lakini nakuhakikishia kuna Watanzania wengi sana vijijini hiyo hiyo misaada ya Wazungu imebadilisha maisha yao!
[/QUOTE]


Hivi unafahamu malighafi zimetoka wapi? Hapo kwenye rangi!



Nafikiri hilo swali nikuulize wewe unaesema "hatutaki misaada" wakati ukweli ni kwamba inahitajika na inasaidia watu!


Je, unafahamu ni asilimia ngapi ya pesa za misaada zinarudi zilikotoka? Ukweli ni kwamba tusiposaidiwa tutaendelea mapema zaidi. Hii tabia ya kutenga bakuli haitalinusuru hili taifa. Nchi ina uranium, mafuta, gas na utalii ambao huwezi kuupata kokote kule duniani ati bado ipo kwenye dunia ya tatu .... .... does that make sense to you?

Au wewe unaiamini hii sarafu hapa chini .... .... ...



article-2180369-13202661000005DC-888_306x288.jpg




Au unawaamini hawa hapa chini .... ..... ..... walinde mali zako ....


rsz_-24%288%29.jpg


Diamond quits over rate fixing scandal


Tanzania ikitaka kuendelea isitishe misaada yote mara moja.
 
Back
Top Bottom