Tanzania yaishitaki Malawi UN

Duh! uchumi wenyewe wa kupigana vita ukowapi? vita ya Uganda tu zaidi ya miaka 30 na bado tunadaiwa na akina Ghadafi ingawaje wameshakufa...

Kwani Ghadafi alikuwa double agent wakati wa vita vya kagera...? Ninavyokumbuka ni kuwa alikuwa mshirika wa Amini...hadi wanajeshi wake walitekwa na akina mzee mti mkavu...wakafungwa vitambaa...busara ya Mwl Nyerere ilitoa msamaha...wale mamluki wakarudishwa kwao... Sasa iweze tuwe na Deni kwa Ghadafi??
 
hawa watu wa ajabu sana- walikutana Malawi kwa nini yasiishe, mpaka UN kama tunadai uhuru!!!!!!!!! hili lilikuwa la kuishia malawi, huko ni dalili ya kupwaya na uwezo mdogo wa kuondoa katoto ka nyoka chumbani kwa hofu ya Chatu. Mungu ibariki Tanzania. Tupatie hekima ya kukabili masuala kabla ya kupeleka kwa jirani.
 
Kwani Ghadafi alikuwa double agent wakati wa vita vya kagera...? Ninavyokumbuka ni kuwa alikuwa mshirika wa Amini...hadi wanajeshi wake walitekwa na akina mzee mti mkavu...wakafungwa vitambaa...busara ya Mwl Nyerere ilitoa msamaha...wale mamluki wakarudishwa kwao... Sasa iweze tuwe na Deni kwa Ghadafi??

Inawezekana labda alikuwa pande zote mbili lakini ukweli ni kwamba Libya wanatudai pesa nyingi sana, hapo juzi tu Hoteli yetu ya Bahari Beach iliuzwa na kwa bahati mbaya mnunuzi akotokea kuwa Mlibya akatender vizuri tu na akashinda tenda ilipokuja wakati wa malipo akakataa kulipa kwa madai kwamba Serikali yao inatudai nafikiri hiyo Kampuni ilikuwa na mahusiano na Serikali ya Libya, lakini Habari ndio hiyo Hoteli imeondoka bure kabisa ndio maana nikisikia watu wanashabikia vita leo nashindwa kuelewa lakini labda hawajui hali halisi ya nchi yetu na jeshi letu ni kwamba TUMECHOKA SANA hatuwezi kupigana vita!
 
Ujinga mtupu hakuna sababu ya kuwashitaki wamalawi, Tanzania inatakiwa ku-develop kwa nguvu ukanda wa ziwa upande wetu na kuweka vitega uchumi vya kukata na shoka kama vile usafiri wa majini katika vijiji husika, uvuaji wa kisasa kwenye eneo letu na kuweka kituo cha manoari za kivita kwenye eneo letu then tuone huyo kimburu anayetaka kuleta chokochoko. Actions speaks louder.

Wakati umefika kuondoa mizoga ya CCM.

Tanzania tukaweke manowari ya kivita? Bajeti ya Tanzania ni Bilioni 8 $ kama sikosei 40% inatoka kwa wageni halafu unaongelea kuweka Manowari za kivita Ziwa Nyasa, unamaanisha kweli au unatania?

 
Mkuu hatuwezi kushindwa. Kesi hii iko wazi mno ndo maana membe anakimbilia huko, wewe unafikiri yeye mjinga. Wote wanaozungumzia kesi hii wanasema Tanzania imesimamia kwenye sheria ya kimataifa, kwa maana kuwa ikiwa sheria ya kimataifa itatumika ushindi wa Tanzania uko wazi.

Malawi ndo maana wanakataa sheria ya kimataifa na kung'ang'ania wakoloni. Maana yake ni kuwa Malawi wameshapima nguvu ya kesi yao kwenye sheria za kimataifa wakaona haiwezi kushinda. Ndo maana hawataki kwenda huko na hawataki majadiriano. Wanasema ziwa ni lao, full stop. Wanasema hivyo sababu baba yao wa Taifa, Kamuzu Banda alishawaambia hivyo. Na walipooneshwa mkataba wanaodhani umewapa ziwa lote wakagundua kuwa kumbe mkataba ule hauwapi ziwa ndo kabisa wamezidi kuchanganyikiwa.

Ila wanasiasa wa Malawi wanajua kitu kimoja; atakayewaambia wamalawi kuwa ziwa lote si la kwao, yaani wamelichangia na Tanzania na Msumbiji, atakuwa amejinyima kura. Na siasa za malawi unazijua. Ndo maana kina Chiume baada ya kuona hoja zao ni dhaifu wameamua kugomea majadiriano. Kwa ujumla suala hili linachukua uzito mno kwenye siasa za Malawi. Hakuna mwanasiasa aliye tayari kuwaambia wamalawi kuwa msimamo wa Banda si sahihi.

Mkuu KipimaPembe,
Naskia hiyo sheria ya Kimataifa ya Kugawana ziwa equally ipo applicable only if hakukuwa na Mkataba awali. Binafsi siijui vizuri Historia lakini kuna watu wanasema sijui hiyo 'Heligoland Treaty' ilikuwepo muda mrefu na ina favour Malawi. Sasa ni kweli hiyo International Rule itatumika ku rule hii kesi?

TUMBIRI (PhD, University of HULL - UK),
tumbiri@jamiiforums.com
 
Nahisi wewe ndo umemeza moto tena kaa la moto kwani unafikiri kwa kukurupuka na unaitaka nchi nayo ikurupuke. Membe fanya kazi, kila taasisi inamfumo, fuata mfumo unaokuongoza baba, tumekutuma kazi sio kukurupuka
you are contradicting yourself,do you realy understand the gravity of the words membe spoke during his budgetary presentation in the parliament?what about now?huko sio kumeza moto?
 
Nashangaa sana watu huwa hatusomi, ila naona ushabiki ni mwingi sana kuliko kuangalia facts. Heligoland Treaty haiwapi umiliki wa Ziwa Nyasa lote watu wa Malawi.

Heligoland Treaty iliacha nafasi kwa mataifa husika kukubaliana kuhusu mpaka. Kwa hiyo hapa nguvu ya Heligoland Treaty iko questionable kwa sababu yenyewe haikusema conclusively kuwa mpaka uko kwenye ufukwe upande wa Tanzania. Heligoland iliwaachia mataifa husika kukubaliana mipaka kwa kunzingatia "local conditions".

Hayo makubaliano ndo hayajafanyika (ndo wamalawi hawataki) na kilichotakiwa ni watu wa Malawi (Wanasheria) waje wajadiliane na wale wa Tanzania maana ya Kipengere hicho cha kwenye mkataba. Watu wa Malawi kwa kuogopa siasa za kwao, hakuna aliye tayari kujadiri.

Haya maneno eti Heligoland Treaty iliwapa wamalawi ziwa ndo "ubwabwa" unaorudiwa rudiwa sana na wale ambao hawaujui huo mkataba na hawajajishughulisha hata kusikiliza waliousoma huo mkataba wanasemaje!!!
 
Duh! uchumi wenyewe wa kupigana vita ukowapi? vita ya Uganda tu zaidi ya miaka 30 na bado tunadaiwa na akina Ghadafi ingawaje wameshakufa, yaani uchumi wa kuexport kahawa, tumbaku na chai tena ghafi wala sio processed ndio unajigamba kwamba utapigana vita? Hao wanajeshi tu wenyewe, mabuti na kombati zina viraka hamna hela ya kununua zingine itakuwa vifaru!

Sahau mambo ya vita hatuwezi, tumechoka sana tena sana, kwangu mimi bora hata walichukue hilo Ziwa kama ikibidi kuliko kuingia vitani, hailipi kabisa bado tuna mengine mengi tu akina Ziwa Rukwa, Natron, Tanganyika, Nyanza na hayo yote yana utajiri wa kufa mtu, ukienda Natron hapo kuna Magadi (soda Ash) ya kufa mtu, Tanganyika Mafuta ya kufa mtu, Ziwa Nyanza nao maji na samaki wa kufa mtu mito mikubwa ambayo karibu yote ipo ndani ya mipaka yetu kabisa
mingine haikauki mwaka mzima akina Ruaha, Rufiji, Pangani n.k

Kushindwa kupigana vita hakuna maana kuwa tutoe sehemu ya nchi yetu kwa watu wanaosema kuwa hapo ni kwao! Huo ni woga usiokuwa na msingi tena ni kukosa uzalendo wa kuwajali watanzania wenzio. Hivi unafikiri hatima ya watanzania wapatao milioni moja wanaoishi mwambao wa ziwa hilo itakuwaje ikiwa watanzania kama wewe wataingia Ikulu? You can't be a coward, because you are poor!!

Vita ya Uganda ilitugharim sana, lakini unafikiria Maisha ya Watanzania waliouawa na Majeshi ya idd amin kule Kagera gharama yake ni nini?? Hiyo gharama ni kitu gani kwa uhai uliopotea? Hiyo gharama ni kitu gani kwa uhai ambao ungepotea ikiwa tusingepigana ile vita? Tunacholipia hadi leo ni gharama ya uhuru na haki, na siku zote vitu hivyo vitapiganiwa na si kupewa bure.

Kwa kifupi tu ni kuwa Banda alishawaaminisha watu wa Malawi kuwa hata Ardhi yote ya Tanzania na Msumbiji iliyoko mwambao wa ziwa lile ni sehemu ya Malawi (Wilaya zote zinazozunguka ziwa Nyasa). Huwezi uka-give in kwa madai ya kipuuzi kama hayo eti tu kwa kuwa Tanzania tuna maeneo kibao - huko ni kukosa uzalendo. Kaangalie ukubwa wa China halafu ukaangalie kile kisiwa wanachogombania na Japan!!
 
Well done minister Membe, ubabe wa kisasa unatangulia wewe polisi kuripoti.
 
Kushindwa kupigana vita hakuna maana kuwa tutoe sehemu ya nchi yetu kwa watu wanaosema kuwa hapo ni kwao! Huo ni woga usiokuwa na msingi tena ni kukosa uzalendo wa kuwajali watanzania wenzio. Hivi unafikiri hatima ya watanzania wapatao milioni moja wanaoishi mwambao wa ziwa hilo itakuwaje ikiwa watanzania kama wewe wataingia Ikulu? You can't be a coward, because you are poor!!

Vita ya Uganda ilitugharim sana, lakini unafikiria Maisha ya Watanzania waliouawa na Majeshi ya idd amin kule Kagera?? Hiyo gharama ni kitu gani kwa uhai uliopotea? Hiyo gharama ni kitu gani kwa uhai ambao ungepotea ikiwa tusingepigana ile vita? Tunacholipia hadi leo ni gharama ya uhuru na haki, na siku zote vitu hivyo vitapiganiwa na si kupewa bure.

Kwa kifupi tu ni kuwa Banda alishawaaminisha watu wa Malawi kuwa hata Ardhi yote ya Tanzania na Msumbiji iliyoko mwambao wa ziwa lile ni sehemu ya Malawi (Wilaya zote zinazozunguka ziwa Nyasa). Huwezi uka-give in kwa madai ya kipuuzi kama hayo eti tu kwa kuwa Tanzania tuna maeneo kibao - huko ni kukosa uzalendo. Kaangalie ukubwa wa China halafu ukaangalie kile kisiwa wanachogombania na Japan!!

Unajua ni mambo ya ajabu sana watu mnashabikia vita kwa kisingizio cha uzalendo hivi unajua ni Meli ngapi za kigeni zimejaa kwenye Bahari yetu zinavua samaki na kuondoka? kama hujui uliza wavuvi sasa hivi samaki wetu karibu wanaisha kwa sababu Meli kubwa zinakuja zinavua na kuondoka, tunashindwa hata kununua Patrol boat tu ya kuangalia mipaka yetu tena ambao haina mgogoro wowote, hivi unajua ni mizigo mingapi haramu inaingia kwenye Pwani yetu kuanzia Tanga mpaka Mtwara bila kukaguliwa kwa sababu tu tunashindwa kulinda mipaka yetu?
Unajua ni ndege ngapi na Meli zinaondoka na Rasilimali zetu bila kukaguliwa kila siku?
Tafuta Documentary ya " the Darwins Nightmare" kama bado hujaoiona uone jinsi rasilimali zetu zinavyoondoka, halafu unaongelea Uzalendo, mimi naita Unafiki, huo Uzalendo upo kwenye Ziwa nyasa tu? siku zote mtu akishindwa kitu anatafuta visingizio kwa upande wetu sisi tumeshindwa kujiongoza sasa tunatafuta visingizio!

Kuhusu vita ya Uganda wala usitake kuanza kuongelea huko ile ilikuwa ni "proxy war" kama vile Kenya wanavyofanya sasa Somalia au sijui Uganda na Sudan, na sisi wananchi tukajazwa propaganda tu!

Kuhusu Japan na China wao wana uwezo wa kupigana vita sisi HATUNA!

Wewe usitake kujidanganya Tanzania hatuna uwezo wa kuingia vitani sasa hivi achilia Malawi hata kuichukua Zanzibar tu wakiamua kuasi hatuwezi huo ndio ukweli ulio wazi!

Kuhusu Ziwa Nyasa na ndio maana nikatumia neno IKIBIDI kama imefikia kweli kuingia vitani baada ya njia zote za kidiplomasia kushindwa basi tukubali tuwe wapole kwani hatujui hao Wamalawi wamejiandaa vipi, huwezi jua labda wameahidiwa kusaidiwa na makapitalist ambao wako tayari wanafanya Utafiti wa Mafuta!

Ninajali sana maisha ya Watanzania wenzetu wanaoishi mwambao mwa Ziwa Nyasa na ndio maana sitaki vita itokee na ikibidi kama hamna jinsi basi wacha Ziwa liende kuliko kuingia vitani! Na baada ya hapo tuchukulie hilo kama fundisho tujipange, tujenge uchumi wetu imara ili huko baadaye tuwe na nguvu ya kujitetea, kinyume na hapo ni kujidanganya tu hata Raisi Kikwete analijua hilo na ndio maana ameshasema tena na tena, hatuna uwezo kama nchi wa kuingia vitani kwa sasa na yeye ni Amiri Jeshi Mkuu anapajua kila kitu kuhusu uwezo wetu wa kiuchumi!

 
Tatizo la mpaka ni tatizo la mpaka. Halina uhusiano na mlolongo huo wa mambo mengi tuliyoshindwa uliyoorodhesha. Vita haishabikiwi na hakuna anayeshabikia vita.

Toka mwanzo nimesema approach ya Membe ni nzuri. Kama Malawi wanaamini wana "just cause" kwa nini wanaepa usuluhishi wa kimataifa? Vita ni silaha ya mwisho "when all fail" na huwezi kulalama tu eti kwa kuwa tumeshindwa hiki na kile kwa hiyo na hilo la mpaka hatuliwezi!!! No.

Malawi wamegomea majadiriano kwa sababu wameona hawawezi kushinda kwa majadiriano. Usuluhisho wa kimataifa hawataki. Kwa hiyo tuwaachie tu kwa sababu wanataka na kwa sababu tumeshindwa mengine mengi.
 
Tatizo la mpaka ni tatizo la mpaka. Halina uhusiano na mlolongo huo wa mambo mengi tuliyoshindwa uliyoorodhesha. Vita haishabikiwi na hakuna anayeshabikia vita. Toka mwanzo nimesema approach ya Membe ni nzuri. Kama Malawi wanaamini wana "just cause" kwa nini wanaepa usuluhishi wa kimataifa? Vita ni silaha ya mwisho "when all fail" na huwezi kulalama tu eti kwa kuwa tumeshindwa hiki na kile kwa hiyo na hilo la mpaka hatuliwezi!!! No.

Malawi wamegomea majadiriano kwa sababu wameona hawawezi kushinda kwa majadiriano. Usuluhisho wa kimataifa hawataki. Kwa hiyo tuwaachie tu kwa sababu wanataka na kwa sababu tumeshindwa mengine mengi!!!

Kama wamegomea majadiliano huwezi jua ni nini kinawasukuma kwa nini hizi chokochoko zianze sasa hivi?

Raisi wa JMT ambaye ndiye Amiri Jeshi Mkuu na ambaye anajua hali ya nchi yetu vizuri kuliko mimi na wewe ameshasema hatuna uwezo wa kuingia vitani kwa sasa, na huo ndio ukweli mengine yote yanabaki kuwa hisia na hasira ambazo hazitusaidii, kwa hiyo kama unapinga hilo basi jipange umpindue Raisi upeleke majeshi vitani, vinginevyo kila kitu kinabaki kilivyo hatuna UWEZO WA KUPIGANA VITA
 
Kama wamegomea majadiliano huwezi jua ni nini kinawasukuma kwa nini hizi chokochoko zianze sasa hivi?

Raisi wa JMT ambaye ndiye Amiri Jeshi Mkuu na ambaye anajua hali ya nchi yetu vizuri kuliko mimi na wewe ameshasema hatuna uwezo wa kuingia vitani kwa sasa, na huo ndio ukweli mengine yote yanabaki kuwa hisia na hasira ambazo hazitusaidii, kwa hiyo kama unapinga hilo basi jipange umpindue Raisi upeleke majeshi vitani, vinginevyo kila kitu kinabaki kilivyo hatuna UWEZO WA KUPIGANA VITA

Rais wetu hakusema hatuna uwezo wa kupigana vita!! Ukweli ni kuwa rais alisema tunatoa nafasi kwa diplomasia lakini hakutangaza kuwa ikiwa diplomasia itashindwa hivyo tutawaachia Malawi ziwa eti kwa kuwa kuna mambo mengi tumeshindwa. Sidhani kama ulimwelewa. Hivi huko UN alikoenda Membe unadhani kaenda bila ruhusa ya rais? Na ikiwa rais ameshaona kuwa mambo ya vita hatuyawezi, huko UN basi anaenda kufanya nini? Si awatangazie tu kuwa Tanzania tumewaachia ziwa Nyasa?

Niseme tena, Membe yuko sahihi kwenda UN. Watanzania tuna-explore options zote zilizopo za kutatua mgogoro huo bila kulazimika kufanya confrontation. Kuwaachia Wamalawi eti kwa kuwa tu wamesema ziwa ni lao na hatuwezi kupigana vita kwa kuwa kuna mambo mengi yametushinda, halipo na halitakuwepo!!
 
Kaka Membe usiwache mbachao kwa msala uupitao...Ya Bongo yamekushinda hadi leo kunafukuta tu vuguvugu la siasa hapa Hom na mbona hakuna anaepatanisha watu wanauliwa kila leo...na suala la kusema kua Tanzania inasema usiseme ivo kma sisi wazanzibari tupo tayari huo mpaka wachukue malawi utasemaje na hilo suala unaloongea rais wa znz anajua chochote???
 
Isije ikawa Dowans nyingine hii. Wanasheria wa Kitanzania huwa siwaamini sana hasa linapokuja suala la sheria za kimataifa.
 
Nchi kwanza. I support Membe
Hakukuwa na njia mbadala hasa baada ya wenzetu kususia kikao kilichopangwa kufanyika Dar 10-14 mwezi wa tisa.

Maadhimio ya Mzuzu yalikuwa ni kama hatutaelewana/kufikia mwafaka, basi kwa pamoja tungetafuta msuluhishi (nchi yoyote ya jirani Afrika) kisha nae akishindwa ndipo twende UN.

Sasa wao wamesusa hasa baada ya ujumbe wetu makini ulioongozwa na Mh B. Membe na Prof A. Tibaijuka kuwamwagia vielelezo lukuki kiasi chakuwaacha midomo wazi.

Sasa naamini haki ya kila mmoja itaamuliwa na jicho la dunia.
 
membe ni dhaifu wewe kitu chako una haki nacho unaenda kushtaki kwa manufaa ya nani?
Hivi hajui Malawi wametumika tu nyuma yake kuna mataifa makubwa ambayo yako tayari yafanye chochote iukiwemo kumwaga damu ili wapate mafuta na gesi iwapo atapeleka hiyo kesi Un na Tanzania tukashindwa kutokana mfumo wa Un kulinda interest za mataifa makubwa hatatupa jibu gani sisi watanzania.Haya ndio madhara ya kuwapa watu vyeo bila kuangalia uwezo wao kama ziwa ni letu litaendelea kuwa letu Malawi wao ndio wakashtaki kokote wanakotaka.
 
Kiufupi tu vita sio jibu sahihi unless othrwise,lakini inatubidi tuweke ulinzi mkali ktk maeneo sahihi huku tukijaribu suluhu ya utulivu.Na vilevile ni muhimu kuwa makini na nchi jirani pamoja na zile zenye uhusiani wa karibu kwa pande zote wanaweza wakatugeuka na kutumiliwa.Na pengine ni ishu za kupangwa kwani sitostaajabu Kenya na wao wakaanza kudai mlima wa Kilimanjaro.
 
Back
Top Bottom