Tanzania yaendelea kufanya vema kiuchumi - UNDP | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania yaendelea kufanya vema kiuchumi - UNDP

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwanajamii, Nov 4, 2011.

 1. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #1
  Nov 4, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  SHIRIKA la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), limesema Tanzania imeendelea kufanya vyema kiuchumi, licha ya changamoto kadhaa inazolikabili. Kwa mujibu wa ripoti ya Maendeleo Duniani ya mwaka 2011, iliyotolewa na UNDP jana mjini Dar es Salaam, Tanzania imeshika nafasi ya 152 kati ya 187, zilizofanyiwa utafiti, huku hali ya ukuaji wa uchumi wake ikielezwa kuendelea kukua kwa kasi.
  Ripoti hiyo iliyozinduliwa jana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Servacius Likwelile, imeionyesha Tanzania ni miongoni mwa nchi 10 ambazo uchumi wake unakua kwa kasi katika kipindi cha miaka mitano mfululizo. Nchi zingine pamoja na viwango vya ukuaji wake katika mabano, Cuba (kati ya asilimia 10 hadi 51) Venezuela na Tanzania (kati ya asilimia 7 na 73).
  Aidha, nchi 10 ambazo zinashikilia mkia katika ripoti hiyo ni Guinea, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Sierra Lione, Burkinafaso, Liberia, Chad, Msumbiji, Burundi, Niger na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambayo ni ya mwisho. Akizungumzia ripoti hiyo, Likwelile, alisema inatoa changamoto kwa Tanzania na kuhakikisha inaimarisha njia za kiuchumi ili kufika mbali zaidi na kustawisha maendeleo ya Watanzania.
  Likwelile alisema licha ya mafanikio yanayoonekana, Tanzania bado inakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo ya miundombinu ambayo ni eneo muhimu katika kuimarisha sekta ya uchumi.
  Hata hivyo, UNDP katika kaulimbiu yake ya mwaka huu ambayo ni "Uendelevu wa Usawa na Mustakabali Bora kwa Wote," inataka mafanikio ya kiuchumi yanayopatikana yaonyeshe athari kwa wananchi wote.
  Katika ripoti nchi za Norway, Australia na Netherland, ziliongoza kwa kuwa na uchumi imara huku mataifa makubwa ikiwemo Marekani, Ujerumani, Canada, Ireland na Sweeden, yakitupwa nje kutoka katika orodha ya nchi 10 bora.

  Mungu Ibariki Tanzania
   
 2. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #2
  Nov 4, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  These figures do not, in any way, help to mollify the unabating pangs of life which faces an average countryman. True development should be palpable and must trickle down to the grassroots by translating itself into such common needs like availability of food, hospital medicines etc. It is somewhat preposterous to have all these promising data on papers while millions of people are stuck in a mire of deep penury with wealth only being concentrated in the hands of few fat cats.
   
 3. F

  FJM JF-Expert Member

  #3
  Nov 4, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kama kweli uchumi wa Tanzania unakuwa kwa kasi, iweje tushike nafasi ya 152 kati ya 187? Kwa nini tusiwe wa 1, 3 au 4 hata kenye 10 bora kama kweli tuna uchumi unaokuwa kwa kasi? Halafu hii 7% wanayosema UNDP wametoa wapi wakati TRA wali-downgrade GDP growth rate kutokana na mambo mengi one being tatizo la umeme? Wakati wa Mkapa uchumi ulikuwa unakuwa kwa rate ya 5-6% na watu tuliona nafuu maana mishahara ilikuwa inatoka kwa wakati, wbajeti za wizara hakikuwa finyu kama sasa. Sasa iweje leo uchumi ukuwe kwa 7% lakini hata mishahara hakuna?

  Naona UN (body) kupitia mtoto wao UNDP wanaanza kujiingiza kwenye siasa za maji taka. Ni hawa hawa UN waliotoa tuzo kwa Tanzania kwa kile wanachoita kuwa tunaongoza kwa kutoa huduma za jamii? Then baadae tukasikia kelele za kufanya vema kwenye afya ya mama na mtoto? Asha Migiro na Ban Ki Moon wake ni bomu tu.
   
 4. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #4
  Nov 4, 2011
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,600
  Likes Received: 1,678
  Trophy Points: 280
  duh!
  haya!
   
 5. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #5
  Nov 4, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,163
  Trophy Points: 280
  We have enough food to last us our life time.
  Our economy is so good we can afford to be treated outside Tanzania, ask Zitto.
   
 6. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #6
  Nov 4, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,030
  Likes Received: 2,678
  Trophy Points: 280
  Mambo ya kuvishana vilemba vya ukoka haya siyapendi kabisa.
   
 7. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #7
  Nov 4, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Huwa nasema kila siku km mtu hujui kitu ni bora usichangie, sasa ona unavyo jiaibisha mbele ya umati wa watu !
   
 8. Zinedine

  Zinedine JF-Expert Member

  #8
  Nov 4, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,189
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Watangazaji wa Uhuru FM utawajua tu!
   
 9. Zinedine

  Zinedine JF-Expert Member

  #9
  Nov 4, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,189
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hahaha, hao wanawadhihaki ili muwe mashoga tu hawana lolote, uchumi unakuwa wakati serikali imebadilisha nyakati kinyemela na sasa mwezi una mpaka tarehe 38!
   
 10. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #10
  Nov 4, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  mkuu kipindi cha mkapa mlifaidika tu nyinyi, sisi wengine tulikuwa kwenye shida za ajabu, mlifikia hata kutuambia tule mpaka majani. Na ninachokiona hapa ni kuwa unajifikiria wewe tu ambaye ni mwaajiriwa. Nyinyi watu msiozidi 400000 hamwezi kutudrive the rest 40000000. Kwenye hii report ya Un ninachokiona wamefikira vitu vingi kama juu ya kuimaria kwa miundombinu na hasa barabara, kuongezeka kwa mashule na wanafunzi japokuwa bado out put yake si nzuri na mengineyo kama haya. Nadhani hawajaconsider ni wangapi leo hii wanapata milo 3 per day au wanapata huduma nzuri hosipitali.
   
 11. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #11
  Nov 4, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,136
  Likes Received: 6,631
  Trophy Points: 280
  nafasi ya 152 kati ya 187
  aibu tena aibu.
   
 12. F

  FJM JF-Expert Member

  #12
  Nov 4, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  What makes you think sijui kitu? Hivi GeniusBrain mtoto wako akishika nafasi ya 152 kati ya wanafunzi 187 utasema 'huyu mtoto kafaya vizuri sana'?Na hapo atakuwa anapata tuition ya nguvu?

  Tanzania ina kila aina ya rasilimali (kuanzia watu, madini, ardhi hadi hali ya hewa). Isitoshe, Tanzania iko kwenye 1st tier ya nchi zinazopata misaada kwa wingi katika ukanda wa Sub-Sahara. But look what they are telling us, 152 out of 187! Na ukiangalia povety index utagundua tunarudi nyuma. Then angalia gini coeffecient (income inequality), wachache ndio wanafaidi- EPA maybe?

  Kwa maoni yangu, fiscal descpline imepotea kabisa tofauti na pre-2005. Mkapa kaingia Ikulu Inflation ilikuwa double-digit (20%plus), GDP growth rate almost stagnant. Kaondoka GDP growth rate ikiwa kwenye 6.4% infaltion less than 5%. Na tulishaanza kulipia miradi mingi ya maendeleo ya pesa zetu wenyewe i.e daraja la Mkapa. Sasa hivi ni kukopa kama wendawizimu na tunakopa kulipa mishahara na sio miradi ya maendeleo. Msingi mbove.
   
 13. Somji Juma

  Somji Juma Verified User

  #13
  Nov 4, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,514
  Likes Received: 2,066
  Trophy Points: 280
  umetumwa.?mi sina elimu ya uchumi wala uelewa wowote kwenye uchumi ila ninajua UCHUMI WA TANZANIA UNASHUKA KWA KASI YA AJABU..
   
 14. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #14
  Nov 4, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,030
  Likes Received: 2,678
  Trophy Points: 280
  Haushuki bali UNAMWAGIKA.
   
Loading...