Habari Njema: IMF yatabiri Tanzania kuongoza kiuchumi Afrika Mashariki ifikapo 2028

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,720
218,269
Hii ndio Taarifa mpya iliyotufikia hivi punde.

Toa Maoni yako

======

Mhariri wa Takwimu wa kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Halili Letea amesema ripoti ya Shirika la fedha duniani (IMF) limetabiri kwamba mpaka 2028, Tanzania itaongoza kiuchumi miongoni mwa nchi za Afrika Mashariki.

Halili amesema kuwa ripoti imekadiria kuwa na Pato la Taifa thamani yake itakuwa Dola 136 bilioni (sh340 trilioni).

(Imeandaliwa na Elizabeth Joachim)

Mwananchi
 
Na watakaokuwa wameshikilia uchumi ni wanasiasa na watoto wao.
Screenshot_2023-12-21-09-48-17.png
Screenshot_2023-12-21-09-46-59.png
Screenshot_2023-12-21-09-46-59.png
Screenshot_2023-12-21-09-43-50.png
 
Tanzania haikupaswa kuwa inaongoza East Africa, level ya hii nchi kwa jinsi ilivyobarikiwa ni kuongoza Africa nzima kiuchumi, sema tunaongozwa na viazi.
Kawaida sana, sasa kweli sisi ni wa kushindanishwa kiuchumi na nchi kama Kenya ambayo suala la chakula tu kwa wananchi ni shida.
 
Naona habari imejikita kwenye GDP bila kuangalia GDP per capita.

Kuangalia GDP bila kuangalia GDP hiyo inagawanywa kwa watu wangapi (GDP Per Capita) ni kukosa kuelewa jambo la muhimu sana.

Tuangalie nchi mbili jirani. Nchi A na nchi B.

Ukiwa na nchi A yenye watu milioni 100, na uchumi wa dola bilioni 100, hapo mkigawana mnapata GDP per capita ya $ 1,000. GDP per capita = GDP/ population. $ Bilioni 100/ watu milioni 100 = $ 1000 kwa kila mtu.

Ukiwa na nchi B yenye watu milioni 25 na uchumi wa dola bilioni 75, hapo ukigawanya uchumi (GDP)kwa idadi ya watu unapata GDP per capita ya $3,000.

Sasa, ukitaka kujivunia ukubwa wa uchumi tu, unaweza kusema ule uchumi wa nchi A ni mkubwa zaidi. Kwa sababu una GDP kubwa ya dola bilioni 100.

Lakini, ukubwa wa GDP unapandishwa na wingi wa watu tu. Maana halisi ya uchumi ni ufanisi katika uzalishaji. Uzalishaji wa nchi A ni $1,000 tu kwa mtu. GDP per capita.

Kwa hivyo, tukiangalia kwa muktadha wa GDP per capita, ingawa uchumi wa nchi B ni mdogo zaidi at $75 billion, kwa sababu nchi B ina watu wachache zaidi waliozalisha hizo $75 billion, watu milioni 25, ambao wakigawana hiyo GDP wanapata GDP per capita ya $ 3,000, uchumi wa nchi B ni mzuri zaidi.

In fact uchumi wa nchi B ni mzuri zaidi mara tatu ($ 3,000/ $1,000) ukilinganisha na uchumi wa nchi A.

Kwa hiyo, somo muhimu hapa, tunapojipongeza uchumi kuongezeka, tuangalie pia, tunaongeza uzalishaji pia? Au uchumi unakua kwa sababu ya ongezeko la watu tu bila kuongeza ufanisi na uzalishaji wa kila mtu?

Tusiangalie GDP tu, tuangalie GDP per capita pia.
 
Naona habari imejikita kwenye GDP bila kuangalia GDP per capita.

Kuangalia GDP bila kuangalia GDP hiyo inagawanywa kwa watu wangapi (GDP Per Capita) ni kukosa kuelewa jambo la muhimu sana.

Tuangalie nchi mbili jirani. Nchi A na nchi B.

Ukiwa na nchi A yenye watu milioni 100, na uchumi wa dola bilioni 100, hapo mkigawana mnapata GDP per capita ya $ 1,000. GDP per capita = GDP/ population. $ Bilioni 100/ watu milioni 100 = $ 1000 kwa kila mtu.

Ukiwa na nchi B yenye watu milioni 25 na uchumi wa dola bilioni 75, hapo ukigawanya uchumi (GDP)kwa idadi ya watu unapata GDP per capita ya $3,000.

Sasa, ukitaka kujivunia ukubwa wa uchumi tu, unaweza kusema ule uchumi wa nchi A ni mkubwa zaidi. Kwa sababu una GDP kubwa ya doka bilioni 100.

Lakini, ukubwa wa GDP unapandishwa na wingi wa watu tu. Maana halisi ya uchumi ni ufanisi katika uzalishaji. Uzalishaji wa nchi A ni $1,000 tu kwa ntu. GDP per capita.

Kwa hivyo, tukiangalia kw amuktadha wa GDP per capita, ingawa uchumi wa nchi B ni mdogo zaidi at $75 billion, kwa sababu nchi B ina watu wachache zaidi waliizalisha hizo $75 billion, watu milioni 25, ambao wakigawana hiyo GDP wanapata GDP per capita ya $ 3,000, uchumi wa nchi B ni mzuri zaidi.

In fact uchumi wa nchi B ni mzuri zaidi mara tatu ($ 3,000/ $1,000) ukilinganisha na uchumi wa nchi A.

Kwa hiyo, somo muhimu hapa, tunapojipongeza uchumi kuongezeka, tuangalie pia, tunaongeza uzalishaji pia? Au uchumi unakua kwa sababu ya ongezeko la watu tu bika kuongeza ufanisi na uzalishaji wa kika mtu?

Tusiangakue GDP tu, tuangalie GDP per capita pia.
Ahsante sana kwa elimu hii.
Lakini vipi uchumi wa nchi yenye GDP per capita ya $1000 ikawa na purchasing power kubwa zaidi kuliko hio nchi yenye GDP per capita $3000?

Gharama zangu za matumizi ya chakula nikiwa nchi yenye GDP per capta 1000 natumia dola 5 kwa siku nzima, nikienda kwenye GDP per capita ya 3000 natumia dola 30 kwa siku, almost mara 6 zaidi.

Hili unalitizamaje?
 
Hiyo tofauti inaweza kuwa na maana sana kwenye maisha ya watu ya kila siku kununua bidhaa na huduma zinazozalishwa ndani ya nchi bila kutegemea soko la kimataifa.

Unapoingia kwenye huduma na bidhaa zinazoingia kwenye soko la kimataifa advantage hiyo inapotea. Mfano chukulia kitu kama mafuta ambayo yananunuliwa kwenye soko la kimataifa, hapo purchasing power parity haiwezi kukusaidia sana kwa sababu bei katika soko la dunia ni moja tu.

Na kadiri chumi zinavyozidi kutegemea soko la kimataifa kwenye vitu kama mafuta kusafirisha mazao, kununua mbolea nje etc, ndivyo advantage ya purchasing power parity inaondoka.

Ndiyo maana ni muhimu sana kujitahidi kuzalisha vitu ndani (mfano kilimo) bila kutegemea soko la kimataifa as much as possible, where there is a competitive advantage in doing so.

Hizi habari zingeweza kuwekwa vizuri zaidi kuwa.

Mwaka 2021 GDP per capita ya Mtanzania ilikuwa ni $ 1,100.

Mwaka 2028 idadi ya watu Tanzania inategemewa kuwa milioni 73.3. Kwa hii GDP iliyotabiriwa 2028 ya dola bilioni 136, GDP per capita itapanda kutoka $ 1,100 ya mwaka 2021, mpaka $ 1,853 mwaka 2029.

Ongezeko la wastani wa dola 753.

Hapo mtu anaona vizuri ongezeko la GDP oer capita.

Ingawa hata hiyo GDP per capita nayo ina matatizo yake, kwa sababu ni average.
 
Hiyo tofauti inaweza kuwa na maana sana kwenye maisha ya watu ya kila siku kununua bidhaa na huduma zinazozalishwa ndani ya nchi bila kutegemea soko la kimataifa.

Unapoingia kwenye huduma na bidhaa zinazoingia kwenye soko la kimataifa advantage hiyo inapotea. Mfano chukulia kitu kama mafuta ambayo yananunuliwa kwenye soko la kimataifa, hapo purchasing power parity haiwezi kukusaidia sana kwa sababu bei katika soko la dunia ni moja tu.

Na kadiri chumi zinavyozidi kutegemea soko la kimataifa kwenye vitu kama mafuta kusafirisha mazao, kununua mbolea nje etc, ndivyo advantage ya purchasing power parity inaondoka.

Ndiyo maana ni muhimu sana kujitahidi kuzalisha vitu ndani (mfano kilimo) bila kutegemea soko la kimataifa as much as possibke, where there is a competitive advantage in doing so.

Hizi habari zingeweza kuwekwa vizuri zaidi kuwa.

Mwaka 2021 GDP per capita ya Mtanzania ilikuwa ni $ 1,100.

Mwaka 2028 idadi ya watu Tanzania inategemewa kuwa milioni 73.3. Kwa hii GDP iliyotabiriwa 2028 ya dola bilioni 136, GDP per capita itapanda kutoka $ 1,100 ya mwaka 2021, mpaka $ 1,853 mwaka 2029.

Ongezeko la wastani wa dola 753.

Hapo mtu anaona vizuri ongezeko la GDP oer capita.

Ingawa hata hiyo GDP per capita nayo ina matatizo yake, kwa sababu ni average.
Ahsante sana mkuu.
Lakini huoni PPP inaweza pelekea uwekezaji mkubwa nchini tokana na cheap labor ?, pia huoni kama nchi inaweza zalisha bidhaa za ndani kwa gharama nafuu tokana na PPP kuwa kubwa hivyo kupelekea kupandisha GDP ya nchi?
 
Yote hayo ni kweli.

Lakini, kitu muhimu ni uongozi kutambua hayo na kujipanga kutumia hayo ili kujiongeza kiuchumi.

Kwa sasa, uongozi haujajipanga kutumia advantages hizo.

Mfano, cheap labor na PPP ya kununua bidhaa za ngozi ingetuwezesha kuwa na viwanda vingi vya bidhaa za ngozi, kama viatu, mikanda, mikoba.

Tungetengeneza kwa gharama nafuu. Hatuhitaji dola kununua ngozi. Hatuhitaji dola kulipa watu wetu.

Tungeweza kutengeneza mkoba wa ngozi kwa $10 na kuuza kwa $100 - 150.

NIlivyokuwa Wall St. kuna sehemu walikuwa wanauza mikoba $150- 200. Wa Colombia nilikuwa naona wana export bidhaa zao.

Sisi nani ana export finished products za ngozi? Huo mfano mmoja tu.
 
Hii ndio Taarifa mpya iliyotufikia hivi punde.

Toa Maoni yako

======

Mhariri wa Takwimu wa kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Halili Letea amesema ripoti ya Shirika la fedha duniani (IMF) limetabiri kwamba mpaka 2028, Tanzania itaongoza kiuchumi miongoni mwa nchi za Afrika Mashariki.

Halili amesema kuwa ripoti imekadiria kuwa na Pato la Taifa thamani yake itakuwa Dola 136 bilioni (sh340 trilioni).

(Imeandaliwa na Elizabeth Joachim)

Mwananchi
Kwani ule uchumi wa kati uko wapi?

Hata hivyo tumekuwa dona kantre kitambo sana ni wakati wetu wa kuongoza EAC
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom