Tanzania ya wafanyakazi, wafanyabiashara na wakulima

mkwapuaji

Member
Jan 6, 2012
49
20
Kila uchwao ni kilio cha maisha magumu ambacho hutoka kwa mnyonge kwenda kwa mtawala. Dhamana ya kilio hiki anayo mtawala ambaye ana matakwa ya kutatua ama kutokuitatua changamoto husika kutokana na uwepo wa rasilimali za kutosha au maamuzi binafsi.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo kwa sasa inaongozwa na Mh. Samia Suluhu Hassan chini ya mwavuli wa Chama Cha Mapinduzi inapaswa kulitazama hili kwa mapana zaidi.

Mosi serikali inapaswa kupunguza matumizi yasiyo ya lazima hasa kwa viongozi wa juu ambayo ni kichefu chefu kwa watawaliwa. Mshahara na marupurupu ya mbunge au mwanasiasa mwingine wala sio siri kwa Watanzania na ni mara 21 zaidi ya mshahara wa mwalimu mmoja wa degree kwa mwezi. Hii inakatisha tamaa kwa watumishi na pia inajenga matabaka hasa kwakuwa kuna upande mmoja ni wa utaalamu na mwingine ni hobi tu.

Pili ipo haja ya kuinua thamani ya fedha yetu kumpa nguvu ya manunuzi mmiliki wa TSH. Toka awamu ya tatu kumekuwa na ugunduzi mkubwa wa rasilimali madini na hata ugunduzi wa gesi katika awamu ya nne. Leo tunaishia tu kusomewa tarakimu za mapato na matumizi na kukua kwa uchumi lakini hatuoni athari chanya katika thamani ya TSH dhidi ya fedha nyingine. Zambia miaka kumi nyuma Kwacha yao ilikuwa Haina thamani kama ya leo kwani wote ni mashuhuda kuwa fedha ya Zambia ni moja ya fedha imara Afrika kwa sasa.

Tatu serikali ilipokee na kutekeleza jukumu la kuwatua mzigo watawaliwa hasa kwenye changamoto kam wanavyokuwa wakijinadi wakati wa uchaguzi. Mtumishi wa Umma wa Tanzania ni moja ya watu masikini na wanaaminishwa mengi sana hasa yenye tija na yasiyo na tija ilimradi tu aamini. Ubora wa kimaisha wa mtumishi ndio chanzo cha ufanisi makazini kwani mtumishi mwenye changamoto kamwe hawezi kukupa ufanisi wa 76% katika majukumu.
 
Back
Top Bottom