Msambichaka Mkinga
JF-Expert Member
- Oct 22, 2015
- 1,649
- 2,911
Wengi wanaamini kuwa tumepiga hatua kubwa katika kila sekta ikiwemo katika sekta za uchumi na huduma. Lakini kwa uhakika ni kwamba Tanzania imerudi sana nyuma ukilinganisha na uchumi wa miaka ya kabla ya 1978. Wengi wanailinganisha Tanzania ya leo na ya miaka ya 1980 na siyo Tanzania kwa ujumla.
Leo naongelea maendeleo ya viwanda maana lengo la serikali ya sasa ni kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda japo hilo lilikwishakuwepo kwa vitendo nyakati za uongozi wa Mwalimu Nyerere. Tofauti kubwa ni kwamba wakati huo, vitendo vilitumika zaidi kuongea kuliko maneno.
Nchi hii mpaka leo, hakuna Rais/Kiongozi mkuu aliyekuwa na maono ya mbali katika maendeleo kama Mwalimu Nyerere. Tatizo kubwa alilokutana nalo Mwalimu lilikuwa namna sahihi ya kutekeleza maono yake.
Mwalimu Nyerere, wakati wa utawala wake, aliweza kujenga viwanda vingi, na vingine mtaviongeza, kama nimesahau:
1) Kiwanda cha nguo Urafiki
2) Kiwanda cha Nguo cha Mwatex
3) Kiwanda cha nguo Mutex
4) Kiwanda cha nguo Mbeyatex
5) Kiwanda cha zana za kilimo Mbeya ZZK
6) Kiwanda cha kuunganisha malori aina ya Scania Kibaha
7) Kiwanda cha kuunganisha matrekta aina ya Valmet
8) Kiwanda cha maturubai Morogoro Canvas
9) Kiwanda cha Viatu Moro Shoes
10) Kiwanda cha Sigara Dar
11) Kiwanda cha Bia TBL
12) Kiwanda cha matairi general Tyre
13) Kiwanda cha mabati Alaf
14) Kiwanda cha kusindika nyama Tanganyika packers
15) Kiwanda cha sabuni Mbuni na nyinginezo
16) Kiwanda cha mafuta ya kula VOIL
17) Viwanda vya soda
18) Kiwanda cha juice
19) Kiwanda cha dawa za meno
20) Viwanda vya kusindika unga NMC
21) Viwanda vya kutengeneza betri za redio - panasonic
22) Viwanda vya nyavu za kuvulia samaki
23) Kiwanda Kikubwa cha pili cha karatasi Southern Paper Mills Mgololo
Endeleeni kujaza
Mwalimu alielewa kuwa sehemu rahisi ya mapinduzi ya viwanda, historia inaonesha huanzia kwenye viwanda vya nguo. Kwa sababu viwanda vya nguo hutumia teknolojia rahisi, huajiri watu wengi, hutoa soko la pamba ya wakulima lakini nguo hupata soko lake la kwanza ndani ya nchi. Ukiangalia hivyo viwanda vyote, kwanza viliangalia soko la ndani, na pili vililenga kutoa soko la ndani kwa mazao ya wakulima.
Mambo ya kujiuliza:
1) Baada ya miaka zaidi ya 30 tangu Mwalimu aondoke kwenye madaraka tumeongeza viwanda vingapi?
2) Kwa nini tunajidanganya kuwa sahizi kuna mambo makubwa kwenye sekta ya viwanda yanayofanyika wakati ukweli ni kwamba tumerudi nyuma sana kwenye sekta hii?
3) Nini kilisababisha maendeleo haya makubwa ya viwanda tuliyoyafikia, yakapotea kwa namna ya ajabu?
Wale ambao hawakuwepo wakati huo, napenda kuwaambia kuwa ukiacha maendeleo ya mawasiliano ambayo hayakuwepo wakati huo, Tanzania ya wakati huo ilikuwa na uchumi uliokuwa imara kuliko wa sasa. Ni wakati huo U$1 = TZS 5. Ndiyo wakati ambao mabasi ya safari fupi Dar yaliyokuwa yakitoza sh. 5 kwa kila safari yaliitwa dala dala (dollar dollar) ikimaanisha sh. 5; na noti ya sh. 20 iliitwa paundi kwa sababu paundi 1 ya Uingereza = sh. 20. Wakati huo kila aliyepanda basi aliweza kulipa sh.5 bila tatizo lakini leo wananchi wa Dar hawawezi kulipa sh.2,200 kwa safari ambayo ndiyo sawa na dollar 1, tena hata dollar yenyewe ikiwa imeshuka thamani yake ukilinganisha na ya wakati huo.
Ni uwezo wa uchumi wa wakati huo ndiyo uliiwezesha Tanzania kutoa misaada ya aina mbalimbali kwa wapigania uhuru wa nchi kusini mwa Afrika. Ni uchumi huo ndiyo uliiwezesha Tanzania kugharamia vita vya Uganda vilivyokuwa vikitumia karibia U$40 millioni kwa siku. Ni baada ya vita vya Uganda maisha yalibadilika ghafla, bidhaa zilikosekana, ugumu wa maisha ulitawala kila mahali, na ubinafsi wa ajabu ulipoanza kumea. Dhiki ya maisha ilisababisha Watanzania kurudi kwenye asili ya binadamu, ambayo ni ubinafsi. Ubinafsi na siasa za kijamaa zilizo kinyume na asili ya mwanadamu, viliua viwanda.
TUTATOKAJE?
Kwa kawaida mtu mwerevu hujifunza kutokana na makosa ya aliyetangulia.
Niliishangaa sana serikali ya Magufuli iliposema inaanza kufufua baadhi ya viwanda kwa yenyewe kutoa hela na kusimamia uendeshaji, ikianzia na kiwanda cha Matairi Arusha. Serikali ya Magufuli kwa kufanya hivyo inamaanisha haikujifunza lolote toka kwenye utawala wa Mwalimu juu ya ugumu kwa serikali kuanzisha na kuendesha biashara ya viwanda.
Mwanadamu ana asili ya ubinafsi, na ndiyo maana hata mtoto mchanga huanza na hatua ya kupokea, ukimnyang'anya alichopewa analia. Kutoa ni hatua ya baadaye. Kinachoifanya sekta binafsi ifanikiwe katika biashara ni asili ya ubinafsi wa mwanadamu, hamu ya kutaka kuzalisha zaidi kwaajili yake na walio karibu naye. Miradi ya umma inakosa personal commitment bali husimamiwa na sheria tu. Wakati ukweli ni kwamba biashara hufanikiwa kutokana na personal commitment na siyo sheria.
Serikali ikitaka kuifanya Tanzania iwe nchi ya viwanda ni lazima ifanye yafuatayo:
1) Iache kabisa fikra kuwa serikali ina uwezo wa kufanya biashara ya viwanda
2) Iache fikra, vitendo na dhana zinazoleta hisia za kuwachukia matajiri wa ndani na nje ambao kimsingi ndiyo pekee wenye uwezo wa kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa viwanda
3) Serikali iweke sheria za biashara, kodi, ajira na mazingira zilizo imara na zinazovutia ujenzi wa viwanda. Na sheria hizo zisiwe zinazobadilika kila mwaka wa fedha au kila baada ya mabadiliko ya uongozi. Hakuna mwekezaji mjinga atakayejenga kiwanda katika nchi ambayo kila siku sheria zinabadilika
4) Serikali iwatambue waagizaji wakubwa wote wa kila bidhaa, ikae nao na kujadiliana nao juu ya nini kifanyike ili wabadilike kutoka kuwa waingizaji wa bidhaa toka nje na kuwa wazalishaji wa ndani
NB: Umasikini mkubwa wa Watanzania walio wengi utaondoka kutokana na nguvu ya pamoja ya ushirikiano kati ya serikali na matajiri wawekezaji katika sekta mbalimbali kuliko kuwatazama matajiri kama maadui. Matajiri kama walivyo maskini, wapo wahalifu pia, wale wanaokwepa kulipa kodi, lakini hiyo isiwe sababu ya kuwaona matajiri wote ni watu wabaya kama serikali inavyotaka kuwaaminisha watu. Wapo maskini ambao ni majambazi lakini hatuwaiti maskini wote ni majambazi. Kauli ya Rais kuwa yeye ni Rais wa maskini ilikosa umakini, na Rais ajiepushe na kauli kama hizo maana japo ni fupi lakini madhara yake ni makubwa sana.