Tanzania ya Viwanda - Nchi Imerudi Nyuma

Tanzania ya Viwanda - Nchi Imerudi Nyuma

Serikali haina tafiti za kutosha kuhusu ongezeko la kuzalina watu madhara yake kwenye ukuaji wa uchumi,pi haija tenga maeneo maalumi ya viwanda vijijini na mijini (LOCALIZATION).PAMPOJA NA madhara ya watu kuhama vijijini kuja kurundikana mijini(RURAL-URBAN EMIGRATION) NA MADHARA YA UKUAJI VIWANDA"Maendeleo ya viwanda yenye usawa ni ngumu kufikiwa TANZANIA

Financial economist
 
Naungana na raisi mtaasfu Allhasani mwinyi ktk kushauri serikali kama inania yadhati basi iwaandae wananchi kifikra kuhusu uchumi wa viwanda. fursa zilizopo(Mitaji na uwekezaji) na michanganua ya viwanda vidogo na vyakati kwa kuandaa semina kutumia medias,kuingiza kwenye mtaala wa elimu masomo ya viwanda na kilimo,wahitimu wawezejiajiri pia.TUFANYE SIASA NA TUTFUNDISHE ELIMU ZA VIWANDA NADARASANI NA MITAANI KTK FIKRA ZA HADHIRA(WANANCHI)
Financial Economist
 
Naungana na raisi mtaasfu Allhasani mwinyi ktk kushauri serikali kama inania yadhati basi iwaandae wananchi kifikra kuhusu uchumi wa viwanda. fursa zilizopo(Mitaji na uwekezaji) na michanganua ya viwanda vidogo na vyakati kwa kuandaa semina kutumia medias,kuingiza kwenye mtaala wa elimu masomo ya viwanda na kilimo,wahitimu wawezejiajiri pia.TUFANYE SIASA NA TUTFUNDISHE ELIMU ZA VIWANDA NADARASANI NA MITAANI KTK FIKRA ZA HADHIRA(WANANCHI) ili kupata maendeleo ya viwanda yenye usawa kwa haraka.
Financial Economist
 
Kwenye ofisi za umma hali tete hata karatasi ni shida
 
Lengo la raisi wetu naamini litafanikiwa kutokana na kuwa watanzania wa leo wengi ni waelewa sana na kama atasikiliza maoni ya wataalam kuhusu maswala viwanda na uchumi pia wananchi wanatakiwa waandaliwe kiakili ili iwe rahisi wao kuelewa lengo la raisi, maana kwa sasa watu wengi tunalaumu sana bila kufikiria na kuona wapi tunatakiwa kuwa na tufanye nn.
Mfano leo hii rais anazungumzia kufufua viwanda vya ngozi Tanzania lakini kijana anaenda kusoma chuo kikuu anaenda kusomea masomo ambayo kwa utawala hayatakuwa na nafasi na wengi watalalamika sana mtaani kwa kukosa ajira kwa sababu tunasoma kwa kuangalia baba alisoma nn ila hatusomi kulingana na nahitaji ya soko LA ajira.
 
Wengi wanaamini kuwa tumepiga hatua kubwa katika kila sekta ikiwemo katika sekta za uchumi na huduma. Lakini kwa uhakika ni kwamba Tanzania imerudi sana nyuma ukilinganisha na uchumi wa miaka ya kabla ya 1978. Wengi wanailinganisha Tanzania ya leo na ya miaka ya 1980 na siyo Tanzania kwa ujumla.

Leo naongelea maendeleo ya viwanda maana lengo la serikali ya sasa ni kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda japo hilo lilikwishakuwepo kwa vitendo nyakati za uongozi wa Mwalimu Nyerere. Tofauti kubwa ni kwamba wakati huo, vitendo vilitumika zaidi kuongea kuliko maneno.

Nchi hii mpaka leo, hakuna Rais/Kiongozi mkuu aliyekuwa na maono ya mbali katika maendeleo kama Mwalimu Nyerere. Tatizo kubwa alilokutana nalo Mwalimu lilikuwa namna sahihi ya kutekeleza maono yake.

Mwalimu Nyerere, wakati wa utawala wake, aliweza kujenga viwanda vingi, na vingine mtaviongeza, kama nimesahau:
1) Kiwanda cha nguo Urafiki
2) Kiwanda cha Nguo cha Mwatex
3) Kiwanda cha nguo Mutex
4) Kiwanda cha nguo Mbeyatex
5) Kiwanda cha zana za kilimo Mbeya ZZK
6) Kiwanda cha kuunganisha malori aina ya Scania Kibaha
7) Kiwanda cha kuunganisha matrekta aina ya Valmet
8) Kiwanda cha maturubai Morogoro Canvas
9) Kiwanda cha Viatu Moro Shoes
10) Kiwanda cha Sigara Dar
11) Kiwanda cha Bia TBL
12) Kiwanda cha matairi general Tyre
13) Kiwanda cha mabati Alaf
14) Kiwanda cha kusindika nyama Tanganyika packers
15) Kiwanda cha sabuni Mbuni na nyinginezo
16) Kiwanda cha mafuta ya kula VOIL
17) Viwanda vya soda
18) Kiwanda cha juice
19) Kiwanda cha dawa za meno
20) Viwanda vya kusindika unga NMC
21) Viwanda vya kutengeneza betri za redio - panasonic
22) Viwanda vya nyavu za kuvulia samaki
23) Kiwanda Kikubwa cha pili cha karatasi Southern Paper Mills Mgololo
Endeleeni kujaza

Mwalimu alielewa kuwa sehemu rahisi ya mapinduzi ya viwanda, historia inaonesha huanzia kwenye viwanda vya nguo. Kwa sababu viwanda vya nguo hutumia teknolojia rahisi, huajiri watu wengi, hutoa soko la pamba ya wakulima lakini nguo hupata soko lake la kwanza ndani ya nchi. Ukiangalia hivyo viwanda vyote, kwanza viliangalia soko la ndani, na pili vililenga kutoa soko la ndani kwa mazao ya wakulima.

Mambo ya kujiuliza:
1) Baada ya miaka zaidi ya 30 tangu Mwalimu aondoke kwenye madaraka tumeongeza viwanda vingapi?
2) Kwa nini tunajidanganya kuwa sahizi kuna mambo makubwa kwenye sekta ya viwanda yanayofanyika wakati ukweli ni kwamba tumerudi nyuma sana kwenye sekta hii?
3) Nini kilisababisha maendeleo haya makubwa ya viwanda tuliyoyafikia, yakapotea kwa namna ya ajabu?

Wale ambao hawakuwepo wakati huo, napenda kuwaambia kuwa ukiacha maendeleo ya mawasiliano ambayo hayakuwepo wakati huo, Tanzania ya wakati huo ilikuwa na uchumi uliokuwa imara kuliko wa sasa. Ni wakati huo U$1 = TZS 5. Ndiyo wakati ambao mabasi ya safari fupi Dar yaliyokuwa yakitoza sh. 5 kwa kila safari yaliitwa dala dala (dollar dollar) ikimaanisha sh. 5; na noti ya sh. 20 iliitwa paundi kwa sababu paundi 1 ya Uingereza = sh. 20. Wakati huo kila aliyepanda basi aliweza kulipa sh.5 bila tatizo lakini leo wananchi wa Dar hawawezi kulipa sh.2,200 kwa safari ambayo ndiyo sawa na dollar 1, tena hata dollar yenyewe ikiwa imeshuka thamani yake ukilinganisha na ya wakati huo.

Ni uwezo wa uchumi wa wakati huo ndiyo uliiwezesha Tanzania kutoa misaada ya aina mbalimbali kwa wapigania uhuru wa nchi kusini mwa Afrika. Ni uchumi huo ndiyo uliiwezesha Tanzania kugharamia vita vya Uganda vilivyokuwa vikitumia karibia U$40 millioni kwa siku. Ni baada ya vita vya Uganda maisha yalibadilika ghafla, bidhaa zilikosekana, ugumu wa maisha ulitawala kila mahali, na ubinafsi wa ajabu ulipoanza kumea. Dhiki ya maisha ilisababisha Watanzania kurudi kwenye asili ya binadamu, ambayo ni ubinafsi. Ubinafsi na siasa za kijamaa zilizo kinyume na asili ya mwanadamu, viliua viwanda.

TUTATOKAJE?
Kwa kawaida mtu mwerevu hujifunza kutokana na makosa ya aliyetangulia.

Niliishangaa sana serikali ya Magufuli iliposema inaanza kufufua baadhi ya viwanda kwa yenyewe kutoa hela na kusimamia uendeshaji, ikianzia na kiwanda cha Matairi Arusha. Serikali ya Magufuli kwa kufanya hivyo inamaanisha haikujifunza lolote toka kwenye utawala wa Mwalimu juu ya ugumu kwa serikali kuanzisha na kuendesha biashara ya viwanda.

Mwanadamu ana asili ya ubinafsi, na ndiyo maana hata mtoto mchanga huanza na hatua ya kupokea, ukimnyang'anya alichopewa analia. Kutoa ni hatua ya baadaye. Kinachoifanya sekta binafsi ifanikiwe katika biashara ni asili ya ubinafsi wa mwanadamu, hamu ya kutaka kuzalisha zaidi kwaajili yake na walio karibu naye. Miradi ya umma inakosa personal commitment bali husimamiwa na sheria tu. Wakati ukweli ni kwamba biashara hufanikiwa kutokana na personal commitment na siyo sheria.

Serikali ikitaka kuifanya Tanzania iwe nchi ya viwanda ni lazima ifanye yafuatayo:
1) Iache kabisa fikra kuwa serikali ina uwezo wa kufanya biashara ya viwanda
2) Iache fikra, vitendo na dhana zinazoleta hisia za kuwachukia matajiri wa ndani na nje ambao kimsingi ndiyo pekee wenye uwezo wa kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa viwanda
3) Serikali iweke sheria za biashara, kodi, ajira na mazingira zilizo imara na zinazovutia ujenzi wa viwanda. Na sheria hizo zisiwe zinazobadilika kila mwaka wa fedha au kila baada ya mabadiliko ya uongozi. Hakuna mwekezaji mjinga atakayejenga kiwanda katika nchi ambayo kila siku sheria zinabadilika
4) Serikali iwatambue waagizaji wakubwa wote wa kila bidhaa, ikae nao na kujadiliana nao juu ya nini kifanyike ili wabadilike kutoka kuwa waingizaji wa bidhaa toka nje na kuwa wazalishaji wa ndani

NB: Umasikini mkubwa wa Watanzania walio wengi utaondoka kutokana na nguvu ya pamoja ya ushirikiano kati ya serikali na matajiri wawekezaji katika sekta mbalimbali kuliko kuwatazama matajiri kama maadui. Matajiri kama walivyo maskini, wapo wahalifu pia, wale wanaokwepa kulipa kodi, lakini hiyo isiwe sababu ya kuwaona matajiri wote ni watu wabaya kama serikali inavyotaka kuwaaminisha watu. Wapo maskini ambao ni majambazi lakini hatuwaiti maskini wote ni majambazi. Kauli ya Rais kuwa yeye ni Rais wa maskini ilikosa umakini, na Rais ajiepushe na kauli kama hizo maana japo ni fupi lakini madhara yake ni makubwa sana.
Eti anajiita rais wa masikini ivi anajua bei ya sukari ikoje mpaka sasa

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Wonderful post ongeza na
24. Ubungo Farm Implements (UFI)
 
Nashauri serikali ituambie ni mrengo wa teknolojia ya aina gani tunapo kwenda katika uchumi wa viwanda tutatumia.Hata wawekezaji hawaambiwi tunasikia chapuo ya raisi kuwa viwanda vitaleta jaira lakini je vile vilivyopo au vipya vikitumia mfumo au mrengo wa CAPITAL INTENSIVE METHOD OF PRODUCTION yani njia ya uzalishaji kwa kutumia mashine zaidi katika uzalishaji njia hii inahitaji sehemu kubwa ya uzalishaji ni mashine itumike kitu ambacho haitoi nafasi kwa nguvu kazi ya vibarua wengi kutumika na wataalamu wengi kutumika sasa hapo utatengenezaje ajira?
Ipo njia ya Labour Intensive method yani uzalishaji kwa kutumia kwa wingi nguvu kazi ya vibarua na wataalamu wengi maana hapa mashine siyo kwa nafasi kubwa.SASA AJABU NI PALE SERIKALI HAITUMBII NA WAZIRI MWIJAGE HASEMI NINI MAONO YA SERIKALI NI KUTUMIA NJIA ZOTE AU MOJA AU KWA BAADHI YA UZALISHAJI KUTUMIA NJIA FULANI NA BAADHI YA UZALISHAJI KUTUMIA NJIA FULANI KULINGANA NA IDADI LABDA YA MALIGHAFI NA UKOSEFU WA AJIRA KATIKA ENEO HUSIKA.
hahahaha Nimerudi Facebook Samsoni waagano jipya....twitter Zoka Paul
FINANCIAL ECONOMIST----and business consultant
SINA UHAKIKA KAMA TUNA UWEZO AU NAFASI YA KUAMUA HILO. HII NI KWA VILE,TUNAALIKA AU KUKARIBISHA WAWEKEZAJI WANAOKUJA NA TEKNOLOJIA ZAO. NA HATUJAWEKA SHERIA IMARA ZA KUWABANA WAFANYE TUNAVYOTAKA .
 
Viwanda vya nini sasa ili tuishi kama malaika?

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Amekimbilia Chato kupumzika kwa lipi?? Sijaona alichokifanya zaidi kutoa povu kila kukicha!! Kujenga barabara si kazi ya waziri?? Yeye Amefanya kazi gani? Zaidi amekuwa mpokea wageni ikulu.....na kupiga deal zake pale! Uchumi unaporomoka amekaa tu pale pale hajui afanye nini!!! Ameua uchumi......!!!
 
Nyerere alijenga viwanda vingi bila mbwembwe na akafanikiwa.
Huyu wa sasa, mbwembwe nyingi na hakuna la maana linalofanyika.
 
Back
Top Bottom