Tanzania ya kijasusi

Vitalis Konga

Senior Member
Sep 22, 2018
127
231
Na.Vitalis Konga

Kwa nchi za kiafrika, Ujasusi wa Kidola Tz ndio mwamuzi wa siasa za Afrika. Hil linatazamwa tangu vuguvugu la uhuru wa Afrika mpaka kunako Karne ya 21. Kwa lugha laini ni kuwa TISS ndio idara yenye nguvu Afrika katika medani ya Ujasusi wa Kidola.

Kwa mujibu wa Takwamu za mwaka 2014, zilizotolewa na mtandao wa onlinenewspoint.com, Orodha ya Mashirika Kumi Bora ya Ujasusi Duniani ni kama ifuatavyo:

-Inter Service Intelligence (ISI) la Pakistan;

-Central Intelligence Agency (CIA) la Marekani;

-Secret Intelligence Services (MI6) la Uingereza;

-Ministry of State Security (MSS) la China;

-Federal Security Services (FSB) la Urusi;

-The Institute For Intelligence and Special Operation (MOSAD) la Israel;

-Direction Generale De La Securite Exterieure (DGSE) la Ufaransa;

-Canadian Security Intelligence Service (CSIS) la Canada;

-Research and Analysis Wing (RAW) la India;

-Australian Secret Intelligence Service (ASIS) la Australia.

Katika Afrika, hakuna takwimu muafaka zinazoainisha lipi shirika bora la ujasusi lakini mtandao wa africaintelligence.com unaojihusisha na habari za kijasusi, mwaka 2015, ulizua mjadala wa kijasusi ambapo jasusi mstaafu(retired)Lizo Gibson wa The National Intelligence Agency (NIA) ya Afrika Kusini alisema SASS (South African Secret Service) ndiyo shirika bora akitumia kigezo cha ukubwa wa bajeti yao kwa mwaka.

Hata hivyo, hoja hiyo ilipingwa vikali na wadau wa Ujasusi kutoka nchi za Morocco, Ghana na Misri. Kwa pamoja wakakubaliana kutumia vigezo viwili vikuu: misheni ilizoshiriki idara husika; na majaribio ya mapinduzi kwa viongozi wa ndani hasa yale yaliyoshindwa kufanikiwa baada ya zuio la nguvu za shirika/idara husika. Idara ya ujasusi (TISS) ya Tanzania ilitajwa kuwa ya kwanza, ikifuatiwa na CIO (Central Intelligence Organisation) la Zimbabwe, DST (Direction de la Surveillance du Territoire) la Morocco, GID (General Intelligence Directorate) la Misri na SASS la Afrika Kusini.

Even kwa upande wa Jeshi bora na lenye nguvu Barani Africa, mwandishi wa habari za kijasusi, Micky Wren, katika andiko lake la kitafiti la mwaka 2015 aliloliita 35 Most Badass Fighting Units From Arround the world ameorodhesha kikosi hatari Afrika kiitwacho Koboko (black mamba) kilicho chini ya Jeshi la Tanzania, JWTZ, katika orodha hiyo kikosi hicho kipo nambari 27 ya vikosi kazi bora kabisa duniani, huku nambari moja ikishikwa na US Navy SEAL ya Marekani.

Takwimu hizi zinaitambua JWTZ kuwa ndio kikosi bora namba moja Afrika. Pamoja na changamoto za ndani hasa ujio wa mfumo wa vyama vingi, ambapo siasa za vyama kupewa kipaumbele cha taifa, na kuporomoka kwa Maadili ya Taifa na hasa mvurugano wa elimu ya Tanzania, bado TISS ni chombo madhubuti na ina watu makini sana. Zaidi, TISS imekuwa mkufunzi imara wa taasisi na idara nyingi za ujasusi barani Afrika.

IN MAGUFULI AND SHEIN WE TRUST

Vitalis Konga(Mwana Vasamwenda)
Njombe Mjini
 
Tiss wamefeli saana kwenye uchumi na nadhani hii inasababishwa na kubanwa na katiba
 
Ninakubaliana na wewe. Hata Burundi wanatambua kuwa Nkurunziza alisaidiwa pale ambapo alikuwa hati hati kupinduliewa.

RIP Piere
 
Back
Top Bottom