Tanzania ya Kidemokrasia itapendeza, lakini haya tunayafanyaje? Wengine tunaogopa kweli

Mkuu, kuna nchi moja inaitwa Brunei. Inaongozwa na sultan said ibn khabus. Ni nchi moja maridhawa kabisa.mji wake mkuu unaitwa daru es salaam
Kwahiyo unakubaliana na mimi kuwa hebu tujaribu kuitawaza familia moja ya Kitanzania ili wawe absolute Power halafu tuwaachie watuongoze tuone

Kuna shida moja tunaweza kujikuta kama Swaziland ambako Mfalme majukumu ya Nchi anaacha anaanza kukimbizana na kuwabikiri Wasichana wadogo

Lakini mbona nje ya Bara hili wameweza?
 
Hapana mkuu, nimechombeza tu ila sikubaliani na wazo hilo.

Wazo hilo litaleta matatizo mengi. Tatizo la kwanza ni tatizo la legitimacy. Familia hiyo itapatavwapi mamlaka dhidi ya familia nyingine? Yaani kwa nini hiyo?

Tatizo la pili, je ikiwa familia ya wendawazimu?

Tatizo la tatu wabunge na madiwani watakuwepo au hawatakuwepo?
 
Nimekuelewa MKUU, BWANA awe juu YAKO MKUU, na imekua
 
Labda wale mabinti ndio wanasababisha stability huko uswazini. Si unajua nguvu ya mwanamke hahahhh
Mkuu labda tatizo liko kwenye IQ zetu,kulikuwa na minong'ono kuwa sisi Waafrika Weusi hatuna uwezo wa kujitawala na kuanzisha ustaarabu.
 
Mkuu labda tatizo liko kwenye IQ zetu,kulikuwa na minong'ono kuwa sisi Waafrika Weusi hatuna uwezo wa kujitawala na kuanzisha ustaarabu.
Au labda tujaribu usultan, tunakuwa na sultan mmoja hivi halafu anatafutiwa mabinti kama 30 kama regulator, yaani kama mswati flani hivi, halafu tunasoma upepo tuone hahahahahh
 
Hoja yako ni nzuri,ila kiongozi aliye bora na mzuri ni yule mwenye ushawisi kwa watu wake,na mwenye mtazamo wenye kuzingatia mambo mema,kwa maana hiyo anauwezo wakuielekeza jamii kufuata yaliyo mema mbali na uamuzi wa wengi tu.Hivyo anauwezo wa kushawishi wa uandaaji na upitishwaji wa sheria zilizo bora kwa manufaa ya wote bado zikizingatia maslahi ya hata walio wachache,kwa yale mambo ya msingi.
 

Umezungumzia demokrasia kama jambo gumu sana, ukweli hiyo demokrasia kwetu inakuwa ngumu kwasababu sehemu kubwa watu wanaoongozwa na hila, na madaraka ni sehemu ya ulaji.
 
Mkuu hoja yako ni nzuri sana ma inafikirisha sana. Lakini kama uliyodokeza tatizo la msingi hapa ni elimu.

Sasa swali ni je tuendelee na udikteta ambapo hata fursa ya kuelimisha jamii kuondokana na ujinga inakuwa finyu. Au turuhusu demokrasia ambapo tupata fursa na mazingira mazuri ya kuwaelimisha watu bila bughdha.

Binafsi naona ni bora tuwe na demokrasia hata kama watu watatumia nafasi hiyo kuwalisha watu uongo na kwakuwa wengi wetu tunapenda sana ubuyu kuliko uhalisi kutokana na kiwango chetu cha elimu ya ufahamu wa masuala ya msingi kuwa ndogo. Kuliko ilivyo sasa watu hawatumii tena ushawishi zaidi ya kupora au kutimia vitisho katika kutafuta uungwaji mkono.
 
Umezungumzia demokrasia kama jambo gumu sana, ukweli hiyo demokrasia kwetu inakuwa ngumu kwasababu sehemu kubwa watu wanaoongozwa na hila, na madaraka ni sehemu ya ulaji.
Uko sahihi kabisa. Sasa kwa nini inakuwa hila na ulaji? Jibu ni kwa sababu ya vile jamii ilivyo. Jamii ikoje? Iko kama ilivyoelezwa kwenye post no.1.

Tufanye nini sasa? Kwa maoni yangu pamoja na kuipigania demokrasia yenyewe , tuwekeze nguvu kubwa zaidi kwenye kubadili mtizamo wa jamii kuwa positive.
 

Hao wananchi ni kama unawasingizia tu, kwa sasa hata hao wananchi hawana uwezo wa kuchagua tena viongozi, na viongozi wanaoingia madarakani kwa shuruti, wanafanya watakavyo kwa kuwaburuza wananchi. Mimi naamini kabisa, rasimu ya Warioba inaweza kuliweka taifa letu kwenye njia nzuri ya demokrasia, lakini mpaka ipite, machafuko tu ndio njia iliyobaki. Hizo nyingine ni porojo tu kaka.
 
H
Au labda tujaribu usultan, tunakuwa na sultan mmoja hivi halafu anatafutiwa mabinti kama 30 kama regulator, yaani kama mswati flani hivi, halafu tunasoma upepo tuone hahahahahh
Huyo sultani atapatikaneje?
 
Tusiwe waoga wa demokrasia, ni muhimu mno kwetu au bado mnamwogopa mfu?
 
Do not underestimate the power of combined fools
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…