Tanzania ya Kidemokrasia itapendeza, lakini haya tunayafanyaje? Wengine tunaogopa kweli

Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,789
2,000
Declaration of interest
*********
Interest 1. Mimi ni moja ya watu wanaoamini kuwa, pamoja na changamoto zake, bado mfumo wa demokrasia ndio mfumo bora zaidi wa kiutawala unaopaswa kufuatwa na mataifa yote duniani kwa sababu ya ubora wake ukilinganisha na mfumo mingine. Kwa mantiki hiyo, natamani tuwe na nchi yenye demokrasia makini na imara.
*******"
2. Naamini chini ya uongozi wa Rais huyu wa awamu ya sita, demokrasia itaimarika 'relatively' na hapo kabla licha ya presha ya makundi maslahi. Hii ni kwa sababu mama ni mtu muungwana na mwenye hekma.
*********
Hoja yangu sasa, pamoja na uzuri wa demokrasia, kuna hatari mbaya sana kutokana na jamii yetu ilivyo ambayo kwa bahati mbaya huwa haijadiliwi sijui ni kwa nini.

Ikumbukwe kanuni mama ya demokrasia ni 'kuendeana na upepo wa wengi huku wachache wakivumiliwa na kulindwa'.

Kwa mantiki hiyo, katika demokrasia iliyokomaa;maamuzi ya wengi ndio hutakiwa kutekelezwa bila kujali ni mazuri au mabaya. Aidha, ili uchaguliwe kuongoza umma kwa mfano, unatakiwa kuendeana na mapigo ya wengi hata kama hao wengi wanataka ufanye jambo la kijinga.

Sasa basi, kwa bahati mbaya kwenye jamii yetu iko hivi:-

Tuna watu wengi wanaopenda kushangilia ujinga kuliko mambo ya maana. Kwa mantiki hiyo, kama kuna demokrasia kamili kuna hatari kubwa mbili.

Kwanza, wanaotaka kuchaguliwa watajikuta wakiwajibika kufanya mambo ambayo hayaingii akilini na pengine ya kijinga kabisa ili kuliridhisha kundi hili kubwa tu ili wachaguliwe na

pili, tunaweza kufika hatua tukakuta nchi inasimamia mawazo ya ajabu sana simply kwa sababu ndio mawazo ya wengi.

Aidha, tuna watu wengi sana ambao hupenda kusikia story mbaya kutoka kwa wenzao kuliko story za mafanikio. Watu hawa hupata raha sana kuona waliko juu wanashushwa chini kuliko wanavyofurahi wao wenyewe wakinyanyuliwa juu.

Kwa mantiki hiyo, katika mazingira ya fully democracy kwenye jamii ya namna hii, kiongozi anaweza kujikuta akilazimika kuwashusha waliofanikiwa ambao ni wachache ili kuwaridhisha wengi waliokwama badala ya kinyume chake. Wakati flani kiongozi mwenyewe anaweza kuwa hapendi, lakini ndio demokrasia inataka.

Nitaomba nitoe mifano kadhaa zaidi ili kuweka vizuri mada hii.

Tanzania tuna watu ambao hawakubali kabisa hoja za ukweli bali wanakubali sana propaganda, na ndio maana tumekuwa watu wa cheap propaganda ili kuridhisha kundi hili ambalo ni kubwa kweli.

Tuna watu wanapenda 'ubuyu' kuliko hoja za maana. Ndio maana hata kwenye social media mijadala ya maana haina wafuatiliaji wala wachagiaji.

Kwa hiyo katika democrasia kamili ambayo ni upepo wa wengi, ukitaka kushika wengi unatakiwa uwe unaongea umbea ujingaujinga na uzandiki. Just think about it!

Tanzania tuna watu ambao wako tayari kumsapoti darasa la saba kwa kuwa anachekesha na kumkataa profesa ambaye amefanya reserch kwenye jambo 'profesional' pengine kwenye mjadala juu ya namna ya kudhibiti mtungi wa neuclear usivuje.

Ikumbukwe hata kwenye tume ya kuwauliza watanzania kama wanataka vyama vingi au la? Wengi walisema hawataki. Kwa hiyo Nyerere asingetumia logic binafsi kuforce viwepo, ungekuta hakuna vyama vingi hadi leo na ni maamuzi ya kidemokrasia.

Mifano ni mingi, haiwezi kuisha.

Sasa Swali ni je! Wakati tunaitetea Tanzania ya kidemokrasia kwa upande mmoja, Tunashugulikia je Janga hili la kijamii kwa upande wa pili?

Kwa upande wangu, nadhani tunatakiwa kupigania kutoa elimu kwa jamii na kuishawishi ibadilike kuliko hata nguvu tunayotumia kuipigania demokrasia yenyewe. Hata hiyo hii haimaanishi kwamba hatuhitaji Tanzania ya kidemokrasia, tunaihitaji sana.
 
Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
57,300
2,000
Declaration of interest

Interest 1. Mimi ni moja ya watu wanaoamini kuwa, pamoja na changamoto zake, bado mfumo wa dwmokrasia ndio mfumo bora zaidi wa kiutawala duniani ukilinganisha na mfumo mingine. Kwa mantiki hiyo, natamani tuwe na nchi yenye dwmokrasia makini na imara.

2. Naamini chini ya uongozi wa Rais huyu wa awamu ya sita, demokrasia itaimarika relatively na hapo kabla licha ya presha ya makundi maslahi. Hii ni kwa sababu mama ni mtu muungwana na mwenye hekma.

Ila sasa, pamoja na uzuri wa demokrasia, kuna hatari mbaya sana kutokana na jamii yetu ilivyo ambayo kwa bahati mbaya huwa haijadiliwi sijui ni kwa nini.

Ikumbukwe kanuni mama ya demokrasia ni 'kuendeana na upepo wa wengi huku wachache wakivumiliwa na kulindwa'

Kwa mantiki hiyo, katika demokrasia iliyokomaa, maamuzi ya wengi ndio hutakiwa kutekelezwa bila kujali ni mazuri au mabaya. Aidha, ili uchaguliwe kuongoza umma, unatakiwa kuendeana na mapigo ya wengi hata kama hao wengi wanataka ufanye jambo la kijinga.

Sasa basi, kwa bahati mbaya kwenye jamii yetu iko hivi:-

Tuna watu wengi wanaopenda kushangilia ujinga kuliko mambo ya maana. Kwa mantiki hiyo, kama kuna demokrasia kamili kuna hatari mbili. Kwanza wanaotaka kuchaguliwa watajikuta wakiwajibika kufanya mambo ambayo hayaingii akilini ili kuridhisha wengi ili wachaguliwe na pili, tunaweza kufika hatua tukakuta nchi inasimamia mawazo ya ajabu sana simply kwa sababu ndio mawazo ya wengi.

Tuna watu wengi sana ambao hupenda kusikia story mbaya kutoka kwa wenzao kuliko story za mafanikio. Watu hawa hupata raha sana kuona waliko juu wanashushwa chini kuliko wanavyofurahi wao wenyewe wakinyanyuliwa juu. Kwa mantiki hiyo, katika mazingira ya fully democracy, kiongozi anaweza kujikuta akilazimika kuwashusha waliofanikiwa ambao ni wachache ili kuwaridhisha wengi waliokwama badala ya kinyume chake.

Nitaomba nitoe mifano michache kuweka vizuri mada hii.

Tanzania tuna watu ambao hawakubali kabisa hoja za ukweli wanakubali sana propaganda, na ndio maana tumekuwa watu wa cheap propaganda ili kuridhisha kundi hili ambao ni kwa

Tuna watu wanapenda ubuyu kuliko hoja za maana. Ndio maana hata kwenye social media mijadala ya maana haina wafuatiliaji wala wachagiaji. Kwa hiyo katika democrasia kamili ambayo ni upepo wa wengi, ukitaka kushika wengi unatakiwa uwe unaongea umbea na uzandiki.

Tanzania tuna watu ambao watu tayari kumsapoti darasa la saba na kumkataa profesa kwenye jambo 'profesional' unaweza kukuta ni mjadala juu ya kudhibiti mtungi wa neuclear usivuje.

Ikumbukwe hata kwenye tume ya kuwauliza watanzania kama wanataka vyama vingi au la? Wengi walisema hawataki. Kwa hiyo Nyerere asingetumia logic binafsi kuforce viwepo, ungekuta hakuna vyama vingi hadi leo na ni maamuzi ya kidemokrasia.

Mifano ni mingi, haiwezi kuisha.

Swali ni je! Wakati tunaitetea Tanzania ya kidemokrasia kwa upande mmoja? Tunashugulikiaje? Janga hili la kijamii kwa upande wa pili?

Kwa upande wengi nadhani tunatakiwa kupigania kutoa elimu kwa jamii na kuishawishi ibadilike kuliko hata nguvu tunayotumia kuipigania demokrasia yenyewe.
Huwezi kuwa na demokrasia bila ya kuwa na elimu.

Kwa sababu mtu mjinga ni mtu asiyejua kuchagua nini kitamfaa, na anaweza kudanganywa kirahisi.

Kwa hivyo, tunavyoongelea kuongeza demokrasia, tusisahau kuongeza elimu.
 
Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,789
2,000
Huwezi kuwa na demokrasia bila ya kuwa na elimu.

Kwa sababu mtu mjinga ni mtu asiyejua kuchagua nini kitamfaa, na anaweza kudanganywa kirahisi.

Kwa hivyo, tunavyoongelea kuongeza demokrasia, tusisahau kuongeza elimu.
Umeongea jambo la maana sana mkuu. Sasa changomoto nyingine ni kwamba kinyume cha demokrasia ni udicteta wa mtu mmoja au kikundi cha watu.

Kwa bahati mbaya ni kwamba nje ya demokrasia, hakuna mfumo mzuri unaoeleweka unaoeleza viongozi wapatikaneje na wanapata wapi mamlaka ya kutawala wengine na haki hiyo wanaipataje.

Kwa bahati mbaya zaidi, viongozi wa nchi ni zao la jamii husika. Kwa hiyo kama jamii imejaa watu waliotajwa kwenye hoja ya msingi, it is likely kuwa na viongozi wenye fikra hizo hizo halafu kwa kuwa hakuna demokrasia , wanakuwa uncontrolable na kufanya uharibifu mkumbwa katika ardhi na jamii ya mwanadamu kwa ujumla huku kukiwa hakuna hata anayekohoa! Anaanzia watu labda?

Ndio maana nafikiri jambo hili tunatakiwa kuliangalia kwa umakini mkubwa huku kwenye grassroot 'jamii yenyewe'.
 
Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,789
2,000
Nitoe mfano mmoja wa kijinga sana kwa ajili ya kujenga uelewa kwa njia nyepesi.

Mfano siku moja kwenye mkutano wa hadhara wenye watu 10,000. Rais asimame ameshika fimbo, pembeni yake yuko kiongozi yoyote wa cheo chochote.

Kisha aulize hadhira ' huyu nimpige bakora au nisimpige' ( bila kufafanua wala shida ni nini) unadhani wengi watajibu nini?

Sasa fikiria katika mazingira kama hayo, demokrasia kamili bila kuibadili jamii kifikira kwenye shina chini huku nini kinaweza kutokea?
 
Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
57,300
2,000
Umeongea jambo la maana sana mkuu. Sasa changomoto nyingine ni kwamba kinyume cha demokrasia ni udicteta wa mtu mmoja au kikundi cha watu.

Kwa bahati mbaya ni kwamba nje ya demokrasia, hakuna mfumo mzuri unaoeleweka unaoeleza viongozi wapatikaneje na wanapata wapi mamlaka ya kutawala wengine na haki hiyo wanaipataje.

Kwa bahati mbaya zaidi, viongozi wa nchi ni zao la jamii husika. Kwa hiyo kama jamii imejaa watu waliotajwa kwenye hoja ya msingi, it is likely kuwa na viongozi wenye fikra hizo hizo halafu kwa kuwa hakuna demokrasia , wanakuwa uncontrolable na kufanya uharibifu mkumbwa katika ardhi na jamii ya mwanadamu kwa ujumla huku kukiwa hakuna hata anayekohoa! Anaanzia watu labda?

Ndio maana nafikiri jambo hili tunatakiwa kuliangalia kwa umakini mkubwa huku kwenye grassroot 'jamii yenyewe'.
Ukiangalia sehemu zote ambazo demokrasia imeota mizizi, imeota mizizi hivyo kama matokeo ya mambo mawili makubwa.

1. Matatizo ya kijamii (some of this is what Marx called "clas struggle"). Ulaya watu wameuana sana, Wafaransa wamechinjana kwenye French Revolution. Waingereza wamepigana mpaka wakaanzisha Bunge kama sehemu ya ku limit nguvu za kifalme, Wamarekani wamepigana Civil War North and South. Hawa wote wamemwaga damu na kupigana, wamejifunza kutokana na matatizo.

2. Kutokana na ugumu wa maisha unaotokana na uchumi wa kisasa, ongezeko la watu, mapinduzi wa viwanda na watu kuhamia mijini, watu imewabidi waelimike sana ili kumudu maisha.Maisha yamekuwa yanaendeshwa kwa teknolojia na habari badala ya kilimo cha kijima na uchuuzi mdogo tu. Elimu imeoanda, muamko wa kisiasa umepanda, watu wamejua haki zao.

Muunganiko wa mambo mawili haya umetengeneza demokrasia iliyokua kutokana na historia halisi za hawa watu, si demokrasia ya kuletewa na kuhutubiwa kisiasa.

Sisi bado hatujapata mnyukano na elimu ya kujenga demokrasia yetu, ndiyo maana tuna demokrasia ya vitabuni inayosema mbunge ni lazima awe mwanachama wa chama cha kisiasa, lakini kuna wabunge hawana chama cha siasa. Ndiyo maana katiba inasema maandamano ya kisiasa ni haki ya watu, lakini rais Magufuli aliyapiga marufuku.

Mpaka sasa tunaigiza demokrasia kwa sababu ni kitu tylichopewa kitabuni, hatujaipata kwa kuipigania wenyewe.
 
Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,789
2,000
Mkuu Kiranga umeongea mambo ya msingi sana. Swali sasa ni je? Tuende vipi kwenye mazingira yetu haya, maana tayari mazingira yetu ni tofauti yet, tunatakiwa tupate matokeo yaliyo bora kwa kadiri iwezekanavyo?
 
Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,789
2,000
Demokrasia ni mfano wa bunduki. Yenyewe kama yenyewe sio mbaya wala sio nzuri,uzuri au ubaya unategemea inatumikaje, na kinachoamua itumikeje ni fikra za wanaoimiliki.

Demokrasia kamili kwa watu wenye fikra na mitizamo tata ni sawa na umiliki wa bunduki kuangukia mikononi mwa wendawazimu kamili.
 
Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,789
2,000
Sio kwamba Nyerere alipenda mfumo wa vyama Vingi,bali mashart ya WB&IMF yaliwabana kufanya hivyo.huyo Nyerere mwenyewe alipenda mfumo wa Chama kimoja.
Nyerere ni chanzo cha matatizo yote ya Kielimu,kijamii,kiuchumi na kisiasa hapa Tanzania.
Kwa maana kwamba ili awe sahihi, hakupashwa kuruhusu? Ama unakusudia nini mkuu?
 
4 7mbatizaji

JF-Expert Member
Dec 8, 2019
1,982
2,000
Declaration of interest
*********
Interest 1. Mimi ni moja ya watu wanaoamini kuwa, pamoja na changamoto zake, bado mfumo wa demokrasia ndio mfumo bora zaidi wa kiutawala unaopaswa kufuatwa na mataifa yote duniani kwa sababu ya ubora wake ukilinganisha na mfumo mingine. Kwa mantiki hiyo, natamani tuwe na nchi yenye demokrasia makini na imara.
*******"
2. Naamini chini ya uongozi wa Rais huyu wa awamu ya sita, demokrasia itaimarika 'relatively' na hapo kabla licha ya presha ya makundi maslahi. Hii ni kwa sababu mama ni mtu muungwana na mwenye hekma.
*********
Hoja yangu sasa, pamoja na uzuri wa demokrasia, kuna hatari mbaya sana kutokana na jamii yetu ilivyo ambayo kwa bahati mbaya huwa haijadiliwi sijui ni kwa nini.

Ikumbukwe kanuni mama ya demokrasia ni 'kuendeana na upepo wa wengi huku wachache wakivumiliwa na kulindwa'.

Kwa mantiki hiyo, katika demokrasia iliyokomaa;maamuzi ya wengi ndio hutakiwa kutekelezwa bila kujali ni mazuri au mabaya. Aidha, ili uchaguliwe kuongoza umma kwa mfano, unatakiwa kuendeana na mapigo ya wengi hata kama hao wengi wanataka ufanye jambo la kijinga.

Sasa basi, kwa bahati mbaya kwenye jamii yetu iko hivi:-

Tuna watu wengi wanaopenda kushangilia ujinga kuliko mambo ya maana. Kwa mantiki hiyo, kama kuna demokrasia kamili kuna hatari kubwa mbili.

Kwanza, wanaotaka kuchaguliwa watajikuta wakiwajibika kufanya mambo ambayo hayaingii akilini na pengine ya kijinga kabisa ili kuliridhisha kundi hili kubwa tu ili wachaguliwe na

pili, tunaweza kufika hatua tukakuta nchi inasimamia mawazo ya ajabu sana simply kwa sababu ndio mawazo ya wengi.

Aidha, tuna watu wengi sana ambao hupenda kusikia story mbaya kutoka kwa wenzao kuliko story za mafanikio. Watu hawa hupata raha sana kuona waliko juu wanashushwa chini kuliko wanavyofurahi wao wenyewe wakinyanyuliwa juu.

Kwa mantiki hiyo, katika mazingira ya fully democracy kwenye jamii ya namna hii, kiongozi anaweza kujikuta akilazimika kuwashusha waliofanikiwa ambao ni wachache ili kuwaridhisha wengi waliokwama badala ya kinyume chake. Wakati flani kiongozi mwenyewe anaweza kuwa hapendi, lakini ndio demokrasia inataka.

Nitaomba nitoe mifano kadhaa zaidi ili kuweka vizuri mada hii.

Tanzania tuna watu ambao hawakubali kabisa hoja za ukweli bali wanakubali sana propaganda, na ndio maana tumekuwa watu wa cheap propaganda ili kuridhisha kundi hili ambalo ni kubwa kweli.

Tuna watu wanapenda 'ubuyu' kuliko hoja za maana. Ndio maana hata kwenye social media mijadala ya maana haina wafuatiliaji wala wachagiaji.

Kwa hiyo katika democrasia kamili ambayo ni upepo wa wengi, ukitaka kushika wengi unatakiwa uwe unaongea umbea ujingaujinga na uzandiki. Just think about it!

Tanzania tuna watu ambao wako tayari kumsapoti darasa la saba kwa kuwa anachekesha na kumkataa profesa ambaye amefanya reserch kwenye jambo 'profesional' pengine kwenye mjadala juu ya namna ya kudhibiti mtungi wa neuclear usivuje.

Ikumbukwe hata kwenye tume ya kuwauliza watanzania kama wanataka vyama vingi au la? Wengi walisema hawataki. Kwa hiyo Nyerere asingetumia logic binafsi kuforce viwepo, ungekuta hakuna vyama vingi hadi leo na ni maamuzi ya kidemokrasia.

Mifano ni mingi, haiwezi kuisha.

Sasa Swali ni je! Wakati tunaitetea Tanzania ya kidemokrasia kwa upande mmoja, Tunashugulikia je Janga hili la kijamii kwa upande wa pili?

Kwa upande wangu, nadhani tunatakiwa kupigania kutoa elimu kwa jamii na kuishawishi ibadilike kuliko hata nguvu tunayotumia kuipigania demokrasia yenyewe. Hata hiyo hii haimaanishi kwamba hatuhitaji Tanzania ya kidemokrasia, tunaihitaji sana.
Mkuu ,umeanza vizuri ila sehem flan umenipoteza,so Kati ya mfumo wa democracy na wa mabavu upi bora,maana wa mabavu umejalibiwa chini ya mwendazake na kuleta matokeo hasi, mfumo wa mabavu haujawahi leta tija kwenye taifa lolote nje ya vikwazo na maisha magum KWA wananchi ikiwa na kuzalisha vikundi vya uhasi nchi,
Leo unasema wananchi kuandaliwa why hujiulizi katika kipindi kidogo,Cha Rais SSH Nchi inafuraha, na ipo tuli??
Mkuu kuongoza taifa lilo paranganyika ni KAZI kubwa watu walisha jizira , na tulisha fika sehem mbaya Kama taifa yangetukuta makubwa nasema Kama BWANA haishivyo, but taifa tehule la mungu hataliacha, mh KINYATA Rais wa Kenya kafanikiwa kuliunganisha taifa why sie tushindwe ,wamebarikiwa wote wnye nia ya kuliunganisha taifa, Asema bwana
 
jabulani

JF-Expert Member
Aug 1, 2015
4,684
2,000
Kwa kuwa Samia hatateuliwa kugombea urais 2025 basi itapendeza akituachia tume huru.
 
Eng. Zezudu

JF-Expert Member
Aug 23, 2012
4,276
2,000
Hakuna mtanzania anaeshangilia ujinga ,except the dead one and his gang, ndo mana watu walitekwa , walipotea , walipigwa risasi na hakuna aliyekamatwa, kusema watanzania wanashingilia ujinga hapo inabidi ubadili fikra zako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,789
2,000
Mkuu ,umeanza vizuri ila sehem flan umenipoteza,so Kati ya mfumo wa democracy na wa mabavu upi bora,maana wa mabavu umejalibiwa chini ya mwendazake na kuleta matokeo hasi, mfumo wa mabavu haujawahi leta tija kwenye taifa lolote nje ya vikwazo na maisha magum KWA wananchi ikiwa na kuzalisha vikundi vya uhasi nchi,
Leo unasema wananchi kuandaliwa why hujiulizi katika kipindi kidogo,Cha Rais SSH Nchi inafuraha, na ipo tuli??
Mkuu kuongoza taifa lilo paranganyika ni KAZI kubwa watu walisha jizira , na tulisha fika sehem mbaya Kama taifa yangetukuta makubwa nasema Kama BWANA haishivyo, but taifa tehule la mungu hataliacha, mh KINYATA Rais wa Kenya kafanikiwa kuliunganisha taifa why sie tushindwe ,wamebarikiwa wote wnye nia ya kuliunganisha taifa, Asema bwana
Mkuu, mimi natetea demokrasia. Siungi mkono udikteta maana ni hatari.

Umemzungumzia SSH, huyo ana busara na hekima katikati ya jamii yenyewe watu kibao walioelezwa kwenye mada ya msingi. Kwa hiyo tushukuru Mungu huyo katokea na kwa bahati ni muungwana. Yaani ni sawa na kushida betting, kwa maana upo uwezekano siku moja akatokea mtu ambaye hakuwahi kutarajiwa na akafanya miujiza.
 
Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,789
2,000
Hakuna mtanzania anaeshangilia ujinga ,except the dead one and his gang, ndo mana watu walitekwa , walipotea , walipigwa risasi na hakuna aliyekamatwa, kusema watanzania wanashingilia ujinga hapo inabidi ubadili fikra zako.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sio wote, ila lipo kundi kubwa la namna hiyo. Hao ndio ambao mama huwaita 'Wazandiki wa mitandaoni' lakini in reality ni sehemu ya jamii, mitandaoni ni mwangwi tu.
 
imhotep

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
28,682
2,000
Sio kwamba Nyerere alipenda mfumo wa vyama Vingi,bali mashart ya WB&IMF yaliwabana kufanya hivyo.huyo
Na pia Nyerere aliogopa sana matukio yaliyokuwa yakitokea Ulaya ya Mashariki na haswa kwa Rafiki yake mkubwa Nicolai Chausescu wa Romania aliyeuwawa kinyama
 
imhotep

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
28,682
2,000
Tujaribuni mfumo wa Kisultani kwa maana ukiangalia leo Nchi za kisultani zinafanya vizuri sana

Mnaonaje Wakuu!
 
denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
5,650
2,000
Nakusoma mpaka nacheka kimya kimya, yaani wewe asie wa upande wako kwako ni mjinga, unaamini hapo ulipo ndio sehemu sahihi na wengine wote lazima wawe hapo, kinyume na hapo kwako taifa litatumbukizwa gizani kwasababu hao "wajinga" wakiachwa wakue kwa idadi wanaweza shika hatamu.

Kwangu demokrasia ni maendeleo, vyama vinatakiwa vibadilike ili kuleta mawazo mapya ya maendeleo, mfano Democrats na Republican wanaijenga USA, hili taifa linapigana na maadui watatu ( ujinga, umasikini, na maradhi) toka lipate uhuru, more than 60 years ago, huoni kwa hali hiyo hao unaowaamini wameshindwa kuwasogeza mbele watanzania?

Kwa mawazo yako haya unataka tubaki tulipo tusijaribu kitu tofauti kwasababu hawa "wajinga" wataleta mawazo ya "ajabu" sasa nikwambie, hayo mawazo ya ajabu unayoyaogopa ndio yatakayolikomboa hili taifa, kwasababu hao "werevu" unaowaamini walishafeli zamani.

All in all as a matured person unatakiwa ujue siasa za vyama vingi sio ujinga, vyama vya upinzani kupewa haki sawa ni haki yao kwasababu nao ni watanzania wanaijenga Tanzania, hakuna haja kuwaona vichaa kwasababu tu unatofautiana nao itikadi au vinginevyo, na Rais kutoa mazingira bora ya siasa kwao sio hisani ni takwa la kisheria.
 
JF Member

JF-Expert Member
Dec 14, 2014
3,945
2,000
Ni ngumu Sana kuifikia democracy.

Nchi zinazijaribu kufanya democracy Mara nyingi zimejikuta zikinyonya upande mwingine ili kuufurahisha upande mwingine.
 
Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,789
2,000
Tujaribuni mfumo wa Kisultani kwa maana ukiangalia leo Nchi za kisultani zinafanya vizuri sana

Mnaonaje Wakuu!
Mkuu, kuna nchi moja inaitwa Brunei. Inaongozwa na sultan said ibn khabus. Ni nchi moja maridhawa kabisa.mji wake mkuu unaitwa daru es salaam
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom