“ Nasikia harufu” kumbe miswada ya uchaguzi ni moto!

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,609
8,753
Serikali kwa bahati mbaya sana walifikiria kiurahisi tu watapetesha mishada ili Tanzania tuonekane na sisi tuna chaguzi za kidemokrasia. Matokeo yake ni kwamba Serikali ielewe nchi inabadilika. Hakuna kitu kitakuwa kirahisi. Pamoja na kwamba Watanzania wengi wameonyesha upole lakini ukweli ni kwamba mitandao imeongeza sana uelewa kwa Watanzania kwa ujumla. Sheria za kijinga hazifichiki tena. Hivyo serikali bado inaweza kulazimisha mambo lakini kwenye idara ya kuaminika kwa Watanzania kwa kusema uongongo haitawezekana kirahisi.

Mimi ushauri wangu na kwa mapenzi yangu kwa nchi naendelea kushauri. Tusaidie kuweka demokrasia ya kweli ili kudumisha uchumi wa nchi zetu kwa vizazi vijavyo badala ya kufikiria chaguzi pekee. Demokrasia ni kubadilisha utamaduni kuongeza ushandani na matokeo yake ni mapana kuliko vyama vya siasa. Viongozi wengi wanajuta baada ya kuchezea na kulewa madaraka wakiondoka.
 
Back
Top Bottom