ArD67
JF-Expert Member
- Nov 14, 2016
- 2,817
- 2,045
Tena sio jamii za kiafrika tu, ni kwa jamii zote zenye kujitambua. Hakuna sababu ya kumiliki range la kutembelea wakati maisha yako ni mwajiriwa na kwenda kazini kuna usafiri wa umma wa uwakika, ni ulimbukeni tu.Umaskini au utajiri ni perception yao na mtizamo wao. Hawajui jamii nyingi, hasa za kiafrika utajiri si kuwa na majumba marefu ya maghorofa na kuwa na pesa nyingi, bali ni umiliki wa mifugo na ardhi hata kama ni pori
Mahekalu ambayo hata baadhi ya vyumba vyake huvitumii miaka, kuvaa dhahabu nk yote ni kutoijua kweli ya maisha. Utanunuaje bia ya safari ml. 500 kwa sh. 5000 wakati hiyohiyo pengine huuzwa 2500?
Budha alisema, "maisha ni masumbuko au ni shida tupu, na hizi shida zote huletwa na 'tamaa' za wanadamu, ni lazima mwanadamu aziondoe hizi tamaa ndo aishi vizuri" Angalia wanadamu wanavyohangaika kufanya utafiti za silaha na modeli za vifaa ambavyo vingi wala si mahitaji ya msingi ya wanadamu, huku wengi wakikosa mahitaji ya msingi... Ni ujinga tu.