Tanzania ya 28 kwa umasikini duniani

hiram

JF-Expert Member
Aug 1, 2013
266
393
tanzapoor.jpg
Nimekutana nayo hii hivi ina maana hawa jamaa hawajaona MLIMANI CITY

https://country-facts.findthedata.c...in&utm_campaign=i3.cm.ob.dt.11256#88-Tanzania
 
Viwango na vipimo vinavyotumika na hao wa magharibi kupimia huo utajiri na umasikini wa nchi tunavijua? Kwa vipimo vyao si haba, tunaweza hata kuwa wa mwisho duniani. Ila niwakumbushe tu, Botswana ni nchi masikini wakati India ni tajiri. Tz tungepata akina Dangote watano tu, na mengine yote yabaki hivihivi, tungepanda viwango hivyo, na hivyo ndivyo vipimo vyao vikuu.

Wakikutajia elimu, afya, chakula, makazi, mavazi, furaha, nk wao watakusetia viweje viwe hata vipimike, eti mmasai ni maskini kwakuwa nyumba yake ni ya miti kaezeka nyasi, hapa hata awe na ng'ombe 2000, sawa.
 
Umaskini au utajiri ni perception yao na mtizamo wao. Hawajui jamii nyingi, hasa za kiafrika utajiri si kuwa na majumba marefu ya maghorofa na kuwa na pesa nyingi, bali ni umiliki wa mifugo na ardhi hata kama ni pori
 
Wana lana Hao! Hawajui kama hayo ni makumbusho yetu..
Halafu ukifikiri vya kutosha, kila jamii na ujenzi wake, ulitokana na mazingira yao husika na shughuli zao, mikoa ya Pwani kipindi cha joto utajisikia raha sana kulala kwenye nyumba ilioezekwa kwa makuti. Leo wamemfosi mmasai ajenge kwa zege na vigae, mengi tu yametekelezwa maporini huko, waetimka kutafuta marisho.
 
Umaskini au utajiri ni perception yao na mtizamo wao. Hawajui jamii nyingi, hasa za kiafrika utajiri si kuwa na majumba marefu ya maghorofa na kuwa na pesa nyingi, bali ni umiliki wa mifugo na ardhi hata kama ni pori
Ukishakuwa na mifugo mingi, ardhi kubwa, then unashindwa kuafford your basic needs huo ni umaskini

Umaskini unapimwa kwa kipato chako unaingiza na vp unaweza mudu mahitaji yako
 
Tanzania ina idadi ya watu wanaokadiriwa kuwa milioni 48...mpaka milioni 50. Kweli kuna improvement kubwa imefanyika kwenye maeneo machache ya baadhi ya miji mikubwa. Ila kwa kiasi kikubwa watanzania wengi wako kwenye dimbwi la umaskini. Huwezi kuamini kuna shule za nyasi ndugu zetu wanasoma. Kuna watu Wa Ashlindia mlo mmoja.

Jamani mkizunguka hii nchi ndio mtafahamu. Ila tukibaki Dar es Salaam tutajipa matumaini sana kwamba nchi yetu tajiri. Viongozi waliotangulia baadhi yao hawakuwa na msukumo wa kuinua maisha ya watanzania maskini. Mimi nimezunguka nchi hii hivo umaskini ni tatizo. Serious interventions zinahitajika maeneo mengi. Mungu ibariki Tanzania itoke hapa iende mbali zaidi na iimarike zaidi.
 
It is our duty to move it up the ladder...hakuna mjomba wa kutusaidia
 
Viwango na vipimo vinavyotumika na hao wa magharibi kupimia huo utajiri na umasikini wa nchi tunavijua? Kwa vipimo vyao si haba, tunaweza hata kuwa wa mwisho duniani. Ila niwakumbushe tu, Botswana ni nchi masikini wakati India ni tajiri. Tz tungepata akina Dangote watano tu, na mengine yote yabaki hivihivi, tungepanda viwango hivyo, na hivyo ndivyo vipimo vyao vikuu.

Wakikutajia elimu, afya, chakula, makazi, mavazi, furaha, nk wao watakusetia viweje viwe hata vipimike, eti mmasai ni maskini kwakuwa nyumba yake ni ya miti kaezeka nyasi, hapa hata awe na ng'ombe 2000, sawa.

Ulichoandika sijui hata mwenyewe umekielewa.. sasa unabisha kuwa Tanzania sio miongoni ya nchi masikini?? Weka vigezo vyako halafu tuvitumie hivyo kupima umasikini wa Tanzania..
 
Tanzania ni ya 28/kwa umasikini wa Nini..?
Umasikini wa mali au umasikini wa fikra..?
Umasikini wa kipato au umasikini wa njaa..?
 
Viwango na vipimo vinavyotumika na hao wa magharibi kupimia huo utajiri na umasikini wa nchi tunavijua? Kwa vipimo vyao si haba, tunaweza hata kuwa wa mwisho duniani. Ila niwakumbushe tu, Botswana ni nchi masikini wakati India ni tajiri. Tz tungepata akina Dangote watano tu, na mengine yote yabaki hivihivi, tungepanda viwango hivyo, na hivyo ndivyo vipimo vyao vikuu.

Wakikutajia elimu, afya, chakula, makazi, mavazi, furaha, nk wao watakusetia viweje viwe hata vipimike, eti mmasai ni maskini kwakuwa nyumba yake ni ya miti kaezeka nyasi, hapa hata awe na ng'ombe 2000, sawa.

Wana vipimo vyao kweli,mfano juzi wametangaza mtuu aloe mzee zaidi afariki akiwa na miaka 106.wakat kijijin kwetu wapo wazee wana miaka zaidi ya iyo
 
Back
Top Bottom