Haya ngoja tuanze kukupa masuala makubwa machache
1.Kuungana nchi lazima kwanza nchi ziwe na usalama na amani ya kutosha ndani ya nchi husika.Rwanda wana vita na waasi ambazo hazijaisha,Uganda usiseme kuna LRA,Kenya ukabila haujaisha na wana Ukabila na wakimbizi wa ndani wanao hadi leo na mavita na AL SHABAB,Burundi vita na waasi bado ipo utulivu na amani bado.Uganda,Rwanda ni mabwana wa vita wanatuhumiwa kongo.Huwezi kuwa na muungano na nchi zisizokuwa na amani na utulivu.Hili ni eneo nyeti huwezi ungana na nchi ziko vitani masaa 24.Kwenye hili tunaona hakuna faida kuungana nao.Cost ni kubwa kuliko benefit.
2.Suala la ardhi wao ardhi ni bidhaa tu na inamilikiwa na wachache sisi hatutaki.Tulipigania uhuru ili tupate ardhi.Wao walipigania uhuru watawale tu ndio maana hawajali wananchi wao kukosa ardhi.Na hili ndilo wanalitaka sana.Watanzania tunasema hatutaki suala la ardhi liwemo kwenye jumuiya.Wananchi wao wanahaha kuhusu ardhi hatutaki litukute ndio maana hatutaki na watuelewe tu.hatuoni benefit kwenye hilo na wasisogee suala la ardhi tumesema hatutaki.
3.Watanzania wengi hawapendi kwenda kuishi na kufanya kazi nchi hizo za jumuiya.Wakati wananchi wa nchi hizo wanapenda mno kuja nchini Tanzania.Udenda unawatoka mdomoni na machozi yanawalengalenga kuja Tanzania.Sasa muungano ni kuangalia wananchi wako watafaidika sana? Huangalii kuwa wananchi wa wa nchi nyingine watafaidika sana? Kwa hiyo hiyo hatuwezi sainia raia wa nchi nyingine.Watanzania wengi wanapenda nchi yao na kuishi nchini kwao.
4.Muungano ni uhusiano kwanza Uhusiano wa raia wa nchi hizi si mzuri sana.Wananchi wa kawaida hawawaoni wanyarwanda,warundi,waganda na wakenya kama raia wema sana wa kuishi nao kijiji kimoja,au mtaa mmoja.Kila wanapoishi au kufanya kazi na watanzania sehemu moja watanzania hawaongelei vizuri.Wanawajua kama watu wa majidai,wenye dharau na wababe.Watu wa nchi hizo bado hawajawaridhisha watanzania wa kawaida kabisa kama wanaweza kuwa majirani zao wazuri.Wananchi huko mipakani,na ambao wamekutana na watu toka mataifa hayo katika shughuli mbali mbali ziwe za kikazi,kidini,kibiashara, KIKUOANA, kikuishi nao kijirani n.k hawafurahii uhusiano nao wana vitabia si vizuri.Wana ushuhuda mbaya kwa watanzania.Hivyo serikali haiwezi kukurupuka kuruhusu haraka kuwa tuwe na mahusiano ya chap chap kama ya mwanaume na changudoa waliyekutana naye usiku bar.
Hayo ni baadhi tu yako mengi.Niachie hapo.