Tanzania vs Malawi

Kama mimi sijali wachezaji wengi wanatoka pande ipi ninachojali mimi ni wenye uwezo wawe utilized effectively for the betterment of Tanzania's footbal....kipindi kile Simba ilivyokuwa na Kanoni na Mgosi tu tulikuwa tunapata matokeo ndo maana hata tuliingia CHAN Kombe la Mataifa ya Africa wa wachezaji wa ndani,lkn hii team yenu ya sasa hivi ya kushinda kwa sare nani anaitaka?
Huyu Mzungu ananiacha hoi sana,nimeanza kuwa na wasiwasi na taaluma yake ya ufundishaji,mechi ya kujipima nguvu anapiga Sub 1 hapohapo anadai hajapata kikosi cha kwanza,sasa atapataje kikosi cha kwanza kama hajaribu wachezaji wake kwenye mechi za kirafiki,au anasubiri mechi za mashindano ndo aje kujaribu wachezaji?....haya anachagua makinda halafu ndo anategemea wasimame kwenye mechi kubwa,mfano yule midfielder wa kutoka Ruvu(Frank Dumayo)...sawa ni kinda na ana kipaji lkn mechi zenyewe za Ligi kuu hana uzoefu nazo(amecheza ligi kuu akitokea mchangani msimu mmoja tu) ndo itakuwa mechi za kimataifa,halafu cha ajabu zaidi kocha anataka amtegemee pale kwenye dimba la kati kwa dakika 90 zote za mechi,huu si ukichaa...yaani atoke pale uwanja wa Twiga Tabata Kisiwani tulipokuwa tunakabana naye hadi kwenda kukabana na kina Toure? halafu tunategemea kushinda....tukijitahidi tutakuwa tunashinda hivihivi kwa sare.
Mkuu Anselm kama ungekuwa unatoa mawazo constructively hivi ambayo hayako biased kila siku kama kwenye hii post yako hata mimi nisingekuona mnazi lakini kila mnapoombea timu ya Taifa kufungwa kwa sababu ina wachezaji wachache wa Yanga sio sawa, maana kwa staili hii itafikia hata mimi ninayetoka kanda ya ziwa nitasema timu gani hii acha ifungwe kwanza haina mchezaji hata mmoja wa kwetu, kwa sababu swala la ubaguzi huwa linaanza na makundi makubwa kuelekea madogo, itafikia sehemu wachaga nao watasema hii timu ya Taifa haijawahi kuwa na mchaga hivyo siishabikii, tuacheni kocha afanye mambo yake.

Ni kweli Yanga kuna wachezaji wazuri ambao hata mimi nawakubali mfano Nsajigwa, Cannavaro na Juma Seif ni wachezaji wazuri, hawa nimewashuhudia kwenye mechi nyingi ni wazuri wanaweza kutoa msaada lakini maadam kocha hajawaita tumpe support kwa hao aliowaita na sio kila siku kuombea afungwe, mimi nilikuwepo uwanjani kwenye ile mechi ya kirafiki, ni kweli yule dogo namba tatu na namba nane hawakucheza vizuri lakini walijitahidi kulingana na uchanga wao.

Sub moja nayo hatuwezi jua kocha alikuwa anafikiria nini ila binafsi sikuona kama ilikuwa ni vizuri, yote kwa yote hii ndo timu yetu na hao ndo wachezaji tulionao bado nasisitiza mambo ya Simba na Yanga tuyaache kwenye ligi, timu ya Taifa ibaki kuwa ya Taifa hata ikitokea siku wamechagua bila mchezaji hata mmoja wa Simba timu ambayo mimi naishabikia bado sitakaa niombe ifungwe kama sijaridhika na uteuzi huu bora niache kwenda uwanjani kuliko kwenda uwanjani na kushabikia wageni halafu nasimama kwa heshima wakati wimbo wao wa Taifa unaimbwa nasema huo ni ujuha na inabidi tuachane nao.

Uzalendo sio kumiliki passport tu ya nchi yako ni pamoja na kupenda vitu ambavyo ni nembo ya Taifa kama unadhani si vizuri kiasi cha kuvipenda toa mawazo mbadala ila virekebike na kuwa vizuri.
 
Eti mechi ya SIMBA na wale waarabu wa SUDAN imeahirishwa nini naona wanazunguka tu mtaani
 
Sasa ile si alichezesha Israel Nkongo,au na hii(against Ivory Coast) atachezesha yuleyule Israel Nkongo?

Ni kweli alichezesha Nkongo lakini unachotakiwa kujua asilimia kubwa ya wachezaji wa Tanzani viwango vyao vinatofautiana kwa kiasi kidogo sana labda wanazidiana tu exposure hata kama angeteua wote toka Mtibwa, Kagera au hata Toto na kuwapa mazoezi ya pamoja na mecchi za kirafiki bado wangeweza kufanya vizuri kama vile tu ambavyo angeteua toka Simba, Yanga na Azam.

Ukiangalia kwa makini hata kwa timu yetu ya Simba kufanya Vizuri mchango mkubwa umetoka kwa Okwi, Mafisango (RIP) pamoja na Sunzu ambao wote si watanzania, kwa watanzani waliofanya Vizuri ni Kaseja, Kapombe, Haruna pamoja na Kelvin, kidogo na Amir lakini wengine yeyote angeweza cheza, hata kwenye mashindano ya CAF, Simba ilipata mabao tisa, matatu kafunga Okwi, Sunzu mawili, Mafisango moja na matatu tu ndo yamefungwa na wenyeji, Ukiangalia kwenye ligi zaidi ya 60% ya magoli ya Simba yamefungwa na wageni.

Ukija kwa timu yenu ya Yanga, Niyonzima, Kiiza wamefanya kazi kubwa, Asamoah na Mwape nao wamefanya kazi kubwa ingawa mnawaita magarasa, Berko naye asingekuwa majeruhi pengine Yanga wangefanya Vizuri zaidi ya walivyofanya sasa.

Azam wale mapacha wa Ivory Coast wamefanya kazi kubwa sana.

Kwa ujumla matokeo mazuri ya timu zetu hizi tatu yamechangiwa na wachezaji wa kigeni.
 
Huu unazi unakotupeleka sio, nakumbuka kuna timu ya Taifa iliitwa ilikuwa na wachezaji wawili tu wa Simba, Salum Kanoni na Musa Mgosi lakini sikuona huu wendawazimu unaofanywa hivi sasa, sasa kuona wachezaji wengi wanatoka timu usioishabikia na kuamua kuiita Simba mseto sijui hata tunaelekea wapi, hivi ikifikia Tanzania ikawa na wachezaji wengi wanaocheza nje ya Tanzania na ndo wakatumika kuunda timu ya Taifa kwa maana hiyo kama na washabiki wa Simba wakiwa na akili kama hizi itakuwa inaitwa timu ya wawekezaji au mtakuwa mnaiita jina gani.

sio hvo mkuu tatizo ni kuacha wachezaji wazuri unenda kusanya wachezaji eti ili mladi tu katoka simba,. Huwez ukamwacha canavaro eti nyoso ndo atasimama huo ni ukichaa
 
sio hvo mkuu tatizo ni kuacha wachezaji wazuri unenda kusanya wachezaji eti ili mladi tu katoka simba,. Huwez ukamwacha canavaro eti nyoso ndo atasimama huo ni ukichaa
Ukweli mtupu ukisoma kuna post yangu moja nimeeleza uzuri wa baadhi ya wachezaji wa Yanga na nimewataja kwa majina, Nsajigwa, Cannavaro pamoja na Juma Seif, sasa kuwaacha sijui kocha kwa nini kawaacha, hata siku ile ya mechi ya Malawa tulikuwa tunadiscus na jamaa fulani wadau wenzangu wa Simba tulisema Cannavaro bado ni mzuri labda zile ngumi zake huenda ndo sababu ya kuachwa.

Nyoso naye sio mbaya na bado anastahili kuchezea timu ya Taifa tatizo lake ni upuuzi wake wa kufanya faulo ambazo hazina maana, aliicost timu ya Taifa kwenye CECAFA dhidi ya Uganda, aliicost timu yetu ya Simba dhidi ya wale wa Algeria hata kutolewa na Wasudan bado lawama tunaweza kuwaangushi yeye na Cholo kwa kupata kadi rahisi ambazo ziliicost timu, fikiria kocha unapoondokewa na mabeki wawili wa kikosi cha kwanza unategemea nini? Labda uwe na mabeki wengi kama Chelsea.
 
Ni kweli alichezesha Nkongo lakini unachotakiwa kujua asilimia kubwa ya wachezaji wa Tanzani viwango vyao vinatofautiana kwa kiasi kidogo sana labda wanazidiana tu exposure hata kama angeteua wote toka Mtibwa, Kagera au hata Toto na kuwapa mazoezi ya pamoja na mecchi za kirafiki bado wangeweza kufanya vizuri kama vile tu ambavyo angeteua toka Simba, Yanga na Azam.

Ukiangalia kwa makini hata kwa timu yetu ya Simba kufanya Vizuri mchango mkubwa umetoka kwa Okwi, Mafisango (RIP) pamoja na Sunzu ambao wote si watanzania, kwa watanzani waliofanya Vizuri ni Kaseja, Kapombe, Haruna pamoja na Kelvin, kidogo na Amir lakini wengine yeyote angeweza cheza, hata kwenye mashindano ya CAF, Simba ilipata mabao tisa, matatu kafunga Okwi, Sunzu mawili, Mafisango moja na matatu tu ndo yamefungwa na wenyeji, Ukiangalia kwenye ligi zaidi ya 60% ya magoli ya Simba yamefungwa na wageni.

Ukija kwa timu yenu ya Yanga, Niyonzima, Kiiza wamefanya kazi kubwa, Asamoah na Mwape nao wamefanya kazi kubwa ingawa mnawaita magarasa, Berko naye asingekuwa majeruhi pengine Yanga wangefanya Vizuri zaidi ya walivyofanya sasa.

Azam wale mapacha wa Ivory Coast wamefanya kazi kubwa sana.

Kwa ujumla matokeo mazuri ya timu zetu hizi tatu yamechangiwa na wachezaji wa kigeni.

Ninachokikubali kutoka kwako ni ufahamu wako kuhusu soka, I like arguing with somebody knowing what he's saying...kama ulivyosema Nsajigwa,Canavaro na Kijiko walipaswa wajumuishwe kwenye squad wangeweza kuwa na mchango positive kwa team na mimi namuongeza Omega Seme pale kati,Seme pamoja na kuwa kinda lakini amekomaa kidogo ukimlinganisha na Frank Dumayo kwani amecheza mechi nyingi zaidi za ushindani za ligi na hata some za kimataifa,hlf ikumbukwe Seme ndo nahodha wake kule NgoroX2 Herois mimi sielewi kwanini amemuacha.
Mimi sikatai Dogo ni mzuri na kuna uwezekano akaja kuwa middle mzuri sana mbele ya safari lkn kumkabidhi mikoba ya dimba la kati tena katika mashindano yanahusisha team gwiji za Africa ni kumwonea,yeye alipaswa awe anajumuishwa kwenye team apate udhoefu kidogokidogo kama ilivyokuwa kwa Jerry Tegete kipindi kile na alivyokuwa anazunguka na Maximo
 
Timu apewe Fred Minziro matatizo ya kutoka sare na kuzomewa yatakwisha.Tutaona mpira na masumbwi
kwa tiketi MOJA na tutamaliza tatizo la uendawazimu wa kuzomea TIMU YA TAIFA.Win win situation.
 
Ninachokikubali kutoka kwako ni ufahamu wako kuhusu soka, I like arguing with somebody knowing what he's saying...kama ulivyosema Nsajigwa,Canavaro na Kijiko walipaswa wajumuishwe kwenye squad wangeweza kuwa na mchango positive kwa team na mimi namuongeza Omega Seme pale kati,Seme pamoja na kuwa kinda lakini amekomaa kidogo ukimlinganisha na Frank Dumayo kwani amecheza mechi nyingi zaidi za ushindani za ligi na hata some za kimataifa,hlf ikumbukwe Seme ndo nahodha wake kule NgoroX2 Herois mimi sielewi kwanini amemuacha.
Mimi sikatai Dogo ni mzuri na kuna uwezekano akaja kuwa middle mzuri sana mbele ya safari lkn kumkabidhi mikoba ya dimba la kati tena katika mashindano yanahusisha team gwiji za Africa ni kumwonea,yeye alipaswa awe anajumuishwa kwenye team apate udhoefu kidogokidogo kama ilivyokuwa kwa Jerry Tegete kipindi kile na alivyokuwa anazunguka na Maximo
Omega Seme sijamtaja kwa sababu sijamwona mara nyingi sana uwanjani lakini naye kwa ajili ya kupata uzoefu inawezekana alitakiwa ajumuishwe, kingine kinachonipa faraja timu ya Taifa hasa yetu hii ya Tanzania haina wachezaji wa kudumu, kwa sasa naona ni Shaban Nditi peke yake ambaye amekuwa akiitwa mara kwa mara toka aitwe kwa mara ya kwanza, kwa hiyo kama Omega Seme ni mzuri lazima ataitwa tena kabla hata ya mwaka huu haujaisha, Kagame inakuja wengi tutawaona uzuri wao na ndo nafasi nyingine ya kocha kuamua vinginevyo kuhusiana na kikosi chake.
 
Back
Top Bottom