Tanzania: Viwanda na ajira kwa vijana 2020

Masalu Jacob

JF-Expert Member
Jul 26, 2017
948
1,092
Habari Tanzania !

Napenda kutoa na kupendekeza mawazo yangu juu ya kuondoa na kupunguza tatizo la ajira hapa nchini.

Inahitajika Tsh.10 bilioni tu kwa kila mkoa.

Mfano case study ni Mkoa wa Mwanza.

1. Kiwanda cha kushona nguo ( viwanda 2 @ Tsh.1.5 bilioni = Tsh.3 bilioni)

Viwanda vitatengeneza ajira zisizo rasmi 100 na ajira rasmi 500. Jumla vijana watapata ajira 1,200 katika hivyo viwanda.

2. Kiwanda cha kuku ( 1 @ Tsh.3.5 bilioni)

Hiki kiwanda kitatengeneza ajira zisizo rasmi na rasmi 3,000.

3. Kiwanda cha urembo ( 3 @ Tsh.1 bilioni = Tsh.3 bilioni )

Viwanda hivi vitaweza kuajiri vijana zaidi ya 1000 kwa kila kiwanda maana yake ni jumla ya wafanyakazi 3,000.

4. Kiwanda cha Samani ( 1 @Tsh. 500 milioni)

Hiki kiwanda kitaweza kuajiri vijana 350.

Jumla ya mtaji ni Tsh.10 bilioni kwa mkoa.

Ajira ( Vijana ) ni 7,550 hii ni kwa mkoa wa Mwanza tu.

Jumla viwanda 7 vipya kabisa.

NB

a) Nyaraka muhimu kuhusu biashara zipo kabisa.

b) Serikali mtakusanya mapato mpaka mkimbie.

c) Nchi itapata maendeleo ya kasi sana.

d) Soko la bidhaa lipo kubwa sana.

CHUKUA MAAMUZI.
 
Ngoja waje,wao wanajua tu kupambana na Mbowe,Kuficha Takwimu za yule mdudu,na Kulisifu jina la Mwalimu Mkuu as if kama n nafsi ya 4 ya Utatu mtakatifu.

Kweli Maendeleo hayana Vyama.Subiri nikalale wifi yenu ananisubir Bed room.
 
Viongozi wenyewe top wabunge wakitaka kufungua viwanda wanakutana na sarakasi mpaka wanasalimu amri.
Ukiritimba mwingi sana.
Ukitaka na ukiwa mwenye uhitaji utafanikiwa kiongozi.
 
Viongozi wenyewe top wabunge wakitaka kufungua viwanda wanakutana na sarakasi mpaka wanasalimu amri.
Ukiritimba mwingi sana.
Kwa niliyokutana nayo kipindi Cha kuanzia January mpaka March 2020 wakati nipo kwenye harakati za kusajili microfinance company, nasema hii nchi kuingia kwenye viwanda na uchumi wa Kati bado Sana unless kila kiwanda kimilikiwe na serikali.
Nchi imejaa ukiritimba Sana, maofisini wapo watu wasiojua majukumu yao hasa Ni yapi, kila mtu anaongea lake.
 
Kabisa kabisa.
Ilitakiwa wakushike mkonp ufanikishe hilo lakini wao hawana hata wazo hilo.
 
Back
Top Bottom