Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,595
- 215,282
Mwezi June mwaka huu nilikuwa na interview saa nne asubuhi. Nilinunua ticket ya train ya saa saba mchana kurudi kwenye mji wa mwenyeji wangu ambako ni masaa matatu kwa train.
Mategemeo yangu ilikuwa mpaka saa tano interview itakuwa imekwisha. Nitapata muda wa kula na kupumzika kabla sijaingia kwenye train. Lakini mahojiano yalichukua masaa mawili nilipewa dakika 15 za kahawa ngoma ikaanza tena. Tulimaliza interview saa sita.
Kutoka na na ugeni kwenye mji ule, niliamua kwenda kituo cha train moja kwa moja nisichelewe train yangu. Nikiwa njiani niliamua kununua vyakula ambavyo nitakula kwenye train.
Nilipofika train station nilikuwa na nusu saa kabla train haijaondoka. Nilikaa kwenye bench kusubiri. Alikuja kuja kijana mtanashati na nguo zake ziko kwenye mpangilio wa kuvutia.
Alinisalimia na kuniuliza kama ninasubiri train anayosubiri yeye. Nilimjibu ndiyo, kutoka pale tulianza maongezi.
Aliniambia yeye anatoka South Africa, ndiyo kwanza amemaliza Masters ya Engineering na ameapply PhD programme kuanzia September 2018, application yake na interview vilitegemea first degree results lakini professor aliridhika na amemwambia majibu yake yakitoka July aya scan ila alikuwa na offer.
Katika maongezi akaniambia na yeye hakutegemea kuwa interview yake ingekuwa ndefu. Hajupata nafasi ya kula alikuwa na chupa ya coke.
Nilimwambia pole tuko katika hali sawa na tunaweza kugawana chakula changu . Katika maongezi aliniambia mategemeo waliyonayo kwa rais wao mpya. Pia alisema nyinyi uhuru wa ardhi mlionao mnabahati sana. Kwetu ardhi wanamiliki wazungu na vijana hawana ajira wala hawawezi kujiajiri kwa kilimo.
Tuliongekea pia kwanini Mandela hakugusia swala la ardhi baada ya kutoka gerezani. Maoni yangu yalikuwa alishapitia mateso mengi akiwa ndani kutoka nje alitaka kwanza waafrika wazoee uhuru na demokrasia kwanza kabla ya kuanza malumbano ya ardhi.
Tuliongelea Zimbabwe enzi ikiitwa Rhodesia ilizalisha mahindi ya kulisha Afrika pamoja na mifugo. Sasa viongozi wa ZANU PF wanamiliki ardhi isiyozalisha.
Aliniambia hata Makaboru wa South Africa sikuhizi hawazalishi kama awali wakiwa na hofu ya kunyang’anywa ardhi. Hali ni tete mno huko kwao na swala ka ardhi ndiyo kete ya viongozi kupatia kura za Waafrika.
Ninakumbuka kusoma kwenye kitabu kuwa Kwame Nkrumah alisema wakati ule wa kupigania uhuru diaspora yeyote atakae kwenda Ghana apewe ardhi akiomba. Kuna Wamarekani weusi wanamiliki ardhi na nyumba Ghana na wanakwenda likizo.