Uhusiano wa Mafanikio yako na umiliki wa Ardhi

Mwl Mwakujonga

JF-Expert Member
Jun 29, 2023
286
582
Utangulizi

Mungu alipomuumba mwanadamu katika vitu ambavyo alimwekea mwanadamu kumiliki na kutawala ni pamoja na Ardhi

Mwanzo 1:28 Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.

Neno Nchi Kibiblia ni Ardhi yenye mipaka Halali , ndio maana baada ya dhambi kuingia ulimwenguni adhabu ambayo alipokea mwanadamu ni pamoja na kwenye Ardhi, kwamba Ardhi itakuwa shaba kwako maana Ardhi haitatoa mazao Kwa ajili ya mwandamu

Mwanzo 3:17 Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako;

Kutokana na dhambi Ardhi iliingia katika laana, na neno laana kwa Biblia ni kinyume cha kubarikiwa kwa hiyo kile ambacho Mungu alikusudia kikuzalia matunda kutoka kwenye Ardhi hakitakuzalia matunda

Kuna uhusiano gani Kati ya Ardhi na Maisha yangu

A. kutunza kumbukumbu (tape recorder )
Ardhi imepewa nafasi katika ulimwengu wa Roho kutunza taarifa za mwanadamu

Kumbukumbu la Torati 31:28 Nikutanishieni wazee wote wa kabila zenu, na maakida yenu, ili niseme maneno haya masikioni mwao, na kuwashuhudizia mbingu na nchi juu yao.

Tafsri ya kiingeleza ya Mstari huu inasema kwamba Ardhi itunze kumbukumbu ,kwa hiyo Maisha yote ya Mwanadamu yameandikwa katika Ardhi.

B. Kuwa Shahidi
Ukiwa na kesi mahakamani ili uweze Kushinda kesi yako ni lazima kuwa na ushahidi kwa hiyo Ardhi Mungu anaitumia Kwa ajili ya kumbaliki mwanadamu na shetani anaitumia Kwa ajili ya kumlaani mwanadamu.

Kumbukumbu la Torati 4:26 nawashuhudizia mbingu na nchi hivi leo, kwamba karibu mtaangamia kabisa juu ya nchi mwivukiayo Yordani kuimiliki, hamtafanya siku zenu ziwe nyingi juu yake, ila mtaangamizwa kabisa.

I call heaven and earth to witness against you this day, that ye shall soon utterly perish from off the land whereunto ye go over Jordan to possess it; ye shall not prolong your days upon it, but shall utterly be destroyed.

Mungu anatumia Ardhi kama Shahidi, kazi ya Shahidi ni kukutetea au kukufunga kwa hiyo unaweza kuwa na Maisha mazuri Sana lakini Ardhi unayokaa iko chini ya laana kuna vitu ambavyo Mungu anataka kukubaliki hautaviona

C. Ardhi ni Mahakama ya Mungu

Mungu anapotaka kuleta hukumu Kazi ya hukumu ni kutenga Mwenye haki kupewa haki yake na ambaye Hana haki kupewa hukumu , Kwa hiyo Mungu anapotaka kukupa Haki yako kama MTU wa Mungu anakuja kama hakimu na Ardhi inakuwa ni mahakama

Zaburi 50:4 Ataziita mbingu zilizo juu, Na nchi pia awahukumu watu wake.

D.Majibu ya Maombi

Umeshajiuliza kwanini ukiwa nyumbani ukitaka kusoma Biblia au kuomba unapata usingizi , au unapiga miayo Tu , ujue kwamba Ardhi unayokaa iko chini ya utawala wa madhabahu ya Miungu migeni

Ufunuo wa Yohana 8:4-5
[4]Na moshi wa ule uvumba ukapanda mbele za Mungu pamoja na maombi ya watakatifu, kutoka mkononi mwa malaika.
.
[5]Na huyo malaika akakitwaa kile chetezo, akakijaza moto wa madhabahu, akautupa juu ya nchi, kukawa radi na sauti na umeme na tetemeko la nchi.

Mungu anapojibu maombi yanatumwa katika nchi/ Ardhi
na kwakuwa Ardhi na mbingu zinafanya kazi Kwa pamoja unapokea majibu yako

E. Ardhi na Mbingu kufanya kazi pamoja

Ardhi na mbingu zinafanya kazi Kwa pamoja , Ardhi ikiwa upande wako na mbingu pia kadharika pia Ardhi ikiwa kinyume chako na mbingu pia.

Mwanzo 1:1Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.

In the beginning God created the heaven and the earth.
 
Sasa hujatuambia tumiliki Ardhi au hapana
Kumiliki Ardhi ni agizo kutoka Kwa Mungu kila MTU ambaye amezaliwa na Mungu anatakiwa kumiliki Ardhi , sio kimwili pekee ni pamoja na kiroho, Ardhi ina Hatimiliki ya kimwili na kiroho, watu wengi Wana Hatimiliki ya Ardhi ya kimwili pekee ndio maana wanakosa mafanikio katika Ardhi wanayo miliki
 
namna ya kufanikiwa kupitia Ardhi

A. Ardhi inabeba Roho

Ardhi ni kibebeo inaweza kubeba uzima au kubeba mauti, ulishawai kujiuliza kwanini ulikuwa eneo A uliolpoaminia eneo B Maisha yako yamebadilika? Au mko mtaa mmoja lakini wewe unafunga biashara na mwenzako anaendelea na biashara ? Ardhi inaweka mipaka ya biashara ya Nani Ife au biashara ya Nani estawi kwenye Ardhi kunaweza kutangaza Nani afanikiwe na Nani asifanikiwe

Soma shuhuda hizi mbili kutoka kwa watu wawili tofauti hapa hapa jukwaani

Ushuhuda WA Kwanza

Twende kwenye mada direct!

Kuna Ustadhi ana duka la samaki wabichi mtaa mmoja huku Dar. Kaweka vijana 2 wanauza. Sijui ni ndugu zake au ni wafanyakazi tu.

Hili duka la samaki bei ni ya kawaida tu kama maduka mengine. Samaki wake na maduka mengine wapo pia. Cha ajabu anapanga foleni ya wateja kuanzia saa moja asubuhi mpaka jioni na giza. Siku moja nilimwambia wife twende kwenye lile duka ukajionee maajabu.

Tulifika dukani alasiri tukakuta duka limefungwa, majirani wakasema kuwa vijana wako msikitini basi tukavuta benchi kusubiri. Dk. kama 4 hivi wakarudi, ile kumaliza kufungua milango tu wateja wamejaa mpaka sisi wa kwanza kufika tukawa wa 4 kuhudumiwa.

Tulipoondoka nyuma watu wamepanga foleni wengi. Nimeona foleni kwenye biashara ila hii ni too much. Jirani yake ameshafungasha na kukimbia mtaa. Huyo jirani yake nilijua hana samaki aina nyingi au bei zake ni kubwa kumbe bei ni sawa tu na jamaa very humble kwa wateja ila anaishia kuharibikiwa na samaki huku mwenzake akitajirika. Bongo nyoso!

Anayetaka kuthibitisha aje Chanika sokoni nimpeleke ajionee maajabu.
 
Mfano mwingine

1. Taasisi na wananchi juu ya mashamba. Taasisi iligoma kuwakodishia wanakijiji mashamba(walikodisha eneo dogo tu) sasa balaa likaanza wadudu wanakula mazao yaliyolimwa kwenye mashamba ya taasisi ila kwenye mashamba ya nje ya eneo la taasisi hamna wadudu yan ata kama mashamba yapo karibu aje ilimradi sio la taasisi wadudu hawaingii. Kwenye mvua ndio ulikuwa maajabu mvua nyingi inanyesha kwenye mashamba ya wanakijiji kuna mda unaweza ona mvua inanyesha kuzunguka mpaka wa mashamba ya taasisi. Mvua ilikuwa ikitukuta nje ya eneo la taasisi tulikuwa tunambizana tujitaidi kutembea had eneo la taasisi maana hapo kutakuwa hakuna mvua ama kuna manyunyu tu.

2. Kijiji hicho hicho kuna jamaa waliamua kukodi mashamba ili walime sasa wakaweka ratiba ya kuamka saa 9 au 10 alfajiri ili wawe wanalima then saa 12 wanarudi kujiandaa kwenda kwenye vipindi (kulikuwa kuna chuo hapo hapo) sasa balaa ikawa wakienda kulima wanatumia mda mwingi kulima na wanaona kweli wamelima hatua nyingi ila wakigeuka nyuma wanajikuta ndio kwanza wanaanza kulima yan bado wapo pale pale walioanzia kulima mda wanafika shambani. Ilibidi waachane na kilimo tu
 
Vitu ambavyo vinasababisha Ardhi kumilikiwa na Miungu mingine kihualali

A. Damu

Ardhi inauwezo wa kutunza kumbukumbu, na kila kitu kinachofanyika kwenye Ardhi kinaingia kwenye kumbukumbu , Damu yoyote ya Mwanadamu hisopokuwa Damu ya Yesu inapoingia kwenye Ardhi , inanena kisasi na kisasi ambacho inachotangaza ni kisasi cha mauti na hakuna kitu cha kuondoa Damu kwenye Ardhi isipokuwa Damu yingine kumwagika

Ufunuo wa Yohana 6:10 Wakalia kwa sauti kuu, wakisema, Ee Mola, Mtakatifu, Mwenye kweli, hata lini kutokuhukumu, wala kuipatia haki damu yetu kwa hao wakaao juu ya nchi?

Kisasi cha Damu, kwahiyo kunakomwagika Damu Ardhi inakuwa ni najisi kwa Mungu kunakuwa na adhabu ya laana na shetani anapata uhalali wa kumiliki na kutawala Ardhi Kwa njia ya laana ya Mungu hivyo ili kutoka hapa ni lazima kufanyika toba kwa Mungu


B. Maneno ya laana

Ardhi inatunza maneno ya laana, ulishawai kusikia mtu anakwambia utaona kama utapata mtoto Tena anaweka kihapo kwamba ukipata mtoto labda sio Mimi kijukuu cha flani? Kazi ya Ardhi ni kuandika , kwahiyo maneno kama hayo Yana anadikwa kwenye Ardhi, na Ardhi inakuwa Shahidi juu ya kile kitu kilichosemwa juu yako, ndio maana unashangaa yanakupata kama yalivyosemwa

Yeremia 22:29-30 Ee nchi, nchi, nchi, lisikie neno la BWANA. BWANA asema hivi, Andikeni habari za mtu huyu kwamba hana watoto, kwamba mtu huyu hatafanikiwa siku zake zote; maana hapana mtu katika wazao wake atakayefanikiwa, akiketi katika kiti cha enzi cha Daudi, na kutawala tena katika Yuda.


C. Madhabahu

Ardhi inabeba madhabahu, ulishawai kusikia MTU anapewa ilizi anakwenda kuchimbia kwenye eneo lake? Mahali popote ambapo mwandamu anakutana na Miungu hapo ni eneo la madhabahu

Kumbukumbu la Torati 12:1-2 Hizi ndizo amri na hukumu mtakazotunza kuzifanya katika nchi aliyokupa BWANA, Mungu wa baba zako, uimiliki, siku zote mtakazoishi juu ya nchi.
.
[2]Vunjeni kabisa mahali pote walipokuwa wakiitumikia miungu yao mataifa mtakayoyamiliki, juu ya milima mirefu, na juu ya vilima, na chini ya kila mti wenye majani mabichi;
:

Kumbukumbu la Torati 12:3
[3]nanyi zivunjeni madhabahu zao, zibomoeni nguzo zao, na maashera yao yateketezeni kwa moto, na sanamu za kuchonga za miungu yao zikateni; na jina lao lifutilieni mbali na mahali hapo.
And ye shall overthrow their .

E.Uovu
Ardhi inabeba uovu, kama eneo ambalo unakaa kuna Mambo ya uzinzi na uasherati yanafanyika katika eneo lenu, ujue kuna uovu kwenye eneo

Hosea 1:2 Hapo kwanza BWANA aliponena kwa kinywa cha Hosea, BWANA alimwambia Hosea, Enenda ukatwae mke wa uzinzi, na watoto wa uzinzi; kwa maana nchi hii inafanya uzinzi mwingi, kwa kumwacha .

Kuna maeneo umeskia yaani Mambo ya uzinzi hayajawai kuisha kwanini maeneo mengi ya vyuoni uzinzi unatawala , unaweza ukaenda binti mzuri kabsa na unashangaa Tu unajikuta umeshajiingiza kwenye uzinzi ? Kwa sababu Ardhi imebeba uovu, vitu hivi shetani anatumia kutawala Maisha ya watu.

Tutaendelea
 
Namna maneno ya laana yanavyofanya kazi

Yoshua 6:26 Naye Yoshua akawaapisha kiapo wakati ule, akasema, Na alaaniwe mbele za BWANA mtu yule atakayeinuka na kuujenga tena mji huu wa Yeriko; ataweka msingi wake kwa kufiliwa na mzaliwa wa kwanza wake, tena atayasimamisha malango yake kwa kufiliwa na mtoto wake mwanamume aliye mdogo.

Kuna maeneo nchi hii, watu hawajengi nyumba nzuri Kwa sababu wanaskia MTU akijenga pale nyumba nzuri yaani kabla nyumba kuisha yeye Mwenye atakufa au kufiwa na ndugu , na ndio maana unakuta kijiji kizima hakuna nyumba ya bati zote za nyasi mbavu za mbwa , ujue kuna zuio la kiroho Katika Ardhi na kama haujui ilo zuio kufanikiwa kwako Katika Eneo ilo ni shida


Kuna Mikoa hapa nchini kama Una ndoa yako na hauko vizuri na Kristo utashangaa tu Mume wako anatekwa na ndoa nyingi ni za mtaala kwa sababu Ardhi imeweka aina ya kiwango cha ndoa katika eneo husika
 
Namna maneno ya laana yanavyofanya kazi

Yoshua 6:26 Naye Yoshua akawaapisha kiapo wakati ule, akasema, Na alaaniwe mbele za BWANA mtu yule atakayeinuka na kuujenga tena mji huu wa Yeriko; ataweka msingi wake kwa kufiliwa na mzaliwa wa kwanza wake, tena atayasimamisha malango yake kwa kufiliwa na mtoto wake mwanamume aliye mdogo.

Kuna maeneo nchi hii, watu hawajengi nyumba nzuri Kwa sababu wanaskia MTU akijenga pale nyumba nzuri yaani kabla nyumba kuisha yeye Mwenye atakufa au kufiwa na ndugu , na ndio maana unakuta kijiji kizima hakuna nyumba ya bati zote za nyasi mbavu za mbwa , ujue kuna zuio la kiroho Katika Ardhi na kama haujui ilo zuio kufanikiwa kwako Katika Eneo ilo ni shida


Kuna Mikoa hapa nchini kama Una ndoa yako na hauko vizuri na Kristo utashangaa tu Mume wako anatekwa na ndoa nyingi ni za mtaala kwa sababu Ardhi imeweka aina ya kiwango cha ndoa katika eneo husika
Tufanye nini ili kuondoa laana ya ardhi?Je unaweza kuondoa laana ya ardhi ya nchi flani au mkoa flani?

Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app
 
Mwl Mwakujonga:
Maombi ya kuombea Ardhi ikae upande wako uweze kuyaona mafanikio yako

Jambo la Kwanza
Omba toba kwa Mungu juu ya dawa zisizonaatia zilizomwagika kwenye Ardhi, kwa kutumia Damu ya Yesu kuomba toba kwenye madhabahu ya Mungu

Waebrania 10:19 Basi, ndugu, kwa kuwa tuna ujasiri wa kupaingia patakatifu kwa damu ya Yesu.

Waebrania 12:24 na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili.
.

Jambo la pili
Omba toba juu ya Maneno ya Laana yaliyotamkwa ambayo yemeandikwa kwenye Ardhi kwa Damu ya Yesu

Waebrania 12:24 na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili.

Jambo la Tatu

Omba toba kwa ajili ya Madhabahu za Miungu zilizoko kwenye Ardhi ambazo , zinazuia mafanikio yako ya kila siku,

madhabahu za Miungu zinapokuwa na uhalali juu ya Ardhi ambayo inahusika na Maisha yako ujue hizo madhabahu ndizo zitakazo kuwa zinaongoza Maisha yako juu ya kile ambacho imemiliki na kutawala, kwa hiyo omba toba kwa Mungu juu ya hiyo madhabahu za Miungu kupata uhalali wa kumiliki eneo lako kihualali kwa Damu ya Yesu

Jambo la Nne
Ondoa uhalali wowote wa dhambi katika Ardhi kwa Damu ya Yesu , ondoa madhabahu Kwa damu ya Yesu , futa maneno ya laana kwa Damu ya Yesu


Jambo la Tano

Lipa uhalali wowote wa dhambi kumiliki na kutawala Ardhi unayomiliki kwa Damu ya Yesu na kwa Nafsi ya Yesu

Warumi 6:23 Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.


Marko 10:45 Kwa maana Mwana wa Adamu naye hakuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi.

Jambo la Sita

Isemeshe Ardhi Kwa Jina la Yesu kufungua kinywa na kutoa madhabahu zote za Miungu na kutoa mauti usiendelee kutawala Ardhi yako

Mambo ya Walawi 18:28 ili kwamba hiyo nchi isiwatapike na ninyi pia, hapo mtakapoitia unajisi, kama ilivyoitapika hiyo taifa iliyotangulia mbele yenu.

Jambo la Saba
Shemesha Ardhi kuwa upande wako , isemeshe Ardhi na mbingu kuwa upande wako , isishirikiane na adui kupigana na wewe

Ufunuo wa Yohana 12:16 Nchi ikamsaidia mwanamke; nchi ikafunua kinywa chake, ikaumeza mto ule alioutoa yule joka katika kinywa chake.


Jambo la nane

Kemea kwa Jina la Yesu kila roho ambazo zinamiliki na kutawala kwenye Ardhi zipate kuachia na kuondoka kwa Jina la Yesu

Jambo la Nane
Omba uponyaji WA Ardhi Kwa Jina la Yesu, Ardhi ikapokee uponyaji, Mungu akapate kuiponya Ardhi

2 Mambo ya Nyakati 7:14 ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.


Sio lazima kufuata taratibu zote hizi , omba Mungu amuongoze unapokuwa unaiombea Ardhi ya eneo uliloko na Mungu atakupa maelekezo kama Aya au ziaid au pungufu na Mungu akusaidie


Angalizo

Maombi ya Ardhi ni maombi ambayo muombaji anatakiwa kuwa na uelewa WA kile anachokiombea kama uwezi, tafuta Mtumishi wa Mungu Mwenye uelewa juu ya Ardhi.

Umeme ni hatari Ila kuna wataalamu wa umeme wanaingia na kutoka kwenye nyaya za umeme kwa sababu wanajua wapipakushika na pasipo kushika kadharika maombi ya Ardhi.

ukikosea Tu unaweza kuingia kwenye matatizo makubwa , hakikisha uhusiano wako na Mungu katika Kristo Yesu uko sawasawa usije ukaumia na Mungu akubariki
 
Back
Top Bottom