Tanzania uhusiano wa ardhi tulionao Waafrika wengi wanautamani

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,595
215,272
Mwezi June mwaka huu nilikuwa na interview saa nne asubuhi. Nilinunua ticket ya train ya saa saba mchana kurudi kwenye mji wa mwenyeji wangu ambako ni masaa matatu kwa train.

Mategemeo yangu ilikuwa mpaka saa tano interview itakuwa imekwisha. Nitapata muda wa kula na kupumzika kabla sijaingia kwenye train. Lakini mahojiano yalichukua masaa mawili nilipewa dakika 15 za kahawa ngoma ikaanza tena. Tulimaliza interview saa sita.
Kutoka na na ugeni kwenye mji ule, niliamua kwenda kituo cha train moja kwa moja nisichelewe train yangu. Nikiwa njiani niliamua kununua vyakula ambavyo nitakula kwenye train.

Nilipofika train station nilikuwa na nusu saa kabla train haijaondoka. Nilikaa kwenye bench kusubiri. Alikuja kuja kijana mtanashati na nguo zake ziko kwenye mpangilio wa kuvutia.

Alinisalimia na kuniuliza kama ninasubiri train anayosubiri yeye. Nilimjibu ndiyo, kutoka pale tulianza maongezi.

Aliniambia yeye anatoka South Africa, ndiyo kwanza amemaliza Masters ya Engineering na ameapply PhD programme kuanzia September 2018, application yake na interview vilitegemea first degree results lakini professor aliridhika na amemwambia majibu yake yakitoka July aya scan ila alikuwa na offer.

Katika maongezi akaniambia na yeye hakutegemea kuwa interview yake ingekuwa ndefu. Hajupata nafasi ya kula alikuwa na chupa ya coke.

Nilimwambia pole tuko katika hali sawa na tunaweza kugawana chakula changu . Katika maongezi aliniambia mategemeo waliyonayo kwa rais wao mpya. Pia alisema nyinyi uhuru wa ardhi mlionao mnabahati sana. Kwetu ardhi wanamiliki wazungu na vijana hawana ajira wala hawawezi kujiajiri kwa kilimo.

Tuliongekea pia kwanini Mandela hakugusia swala la ardhi baada ya kutoka gerezani. Maoni yangu yalikuwa alishapitia mateso mengi akiwa ndani kutoka nje alitaka kwanza waafrika wazoee uhuru na demokrasia kwanza kabla ya kuanza malumbano ya ardhi.

Tuliongelea Zimbabwe enzi ikiitwa Rhodesia ilizalisha mahindi ya kulisha Afrika pamoja na mifugo. Sasa viongozi wa ZANU PF wanamiliki ardhi isiyozalisha.

Aliniambia hata Makaboru wa South Africa sikuhizi hawazalishi kama awali wakiwa na hofu ya kunyang’anywa ardhi. Hali ni tete mno huko kwao na swala ka ardhi ndiyo kete ya viongozi kupatia kura za Waafrika.

Ninakumbuka kusoma kwenye kitabu kuwa Kwame Nkrumah alisema wakati ule wa kupigania uhuru diaspora yeyote atakae kwenda Ghana apewe ardhi akiomba. Kuna Wamarekani weusi wanamiliki ardhi na nyumba Ghana na wanakwenda likizo.
 
Huu uzi naona umechambua zaidi kuhusu safari yako tofauti na kichwa cha uzi, nilitegemea ungechambua zaidi kuhusu ardhi yetu na kwanini hao wengi wanautamani kama ulivyo ainisha kwenye kichwa cha uzi.
Anajifunza namna ya kuwasilisha maoni kwa fanani.!
Hii kitu huwa ni ngumu sana inahitaji mda ili uweze kuleta Uzi unaoeleweka kama za barafu na wengine.
Ndo maana wengi humu huwa tunakomenti na kulike tu kuliko kuleta uzi maana ni ngumu sana.!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sisi pamoja na ukubwa wa ardhi lakini bado tunataka kuajiriwa kwa sababu ya liccm, South Africa wazungu ni asilimia 8 ya watu wote lakini wanamiliki asilimia 70 ya ardhi yote ya Africa kusini tetetetete
 
Thanks mleta uzimzuri ila umekosa nyama hasa kwenye ajenda kuu (ardhi),ardhi ni swala nyeti na aliyekuwa presidents wetu wa awamu ya kwanza President Nyerere(RIP)aliliona hili na kulipa kipau mbele kuwa ni moja ya zana katika kufikia maendeleo,historia ya swala la ardhi kati ya Tanzania na Africa Kusini lina utofauti mkubwa sana,ardhi kwetu ni mali ya taifa wakati SA imemilikishwa kwa watu binafsi na hii ni kutokana na historia yao kuwa tofauti na ya kwetu,walowezi wa kwanza kuingia SA waliingilia jimbo la magharibi ambalo wakazi wake wengi ni khohsani sio wazulu au Xhosa n.k.,hawa wenyeji walipigania ardhi yao ila walizidiwa na wageni na wakaishia kupoteza hii ardhi,baada ya miaka mingi ya siasa za kibaguzi wa rangi sehemu kubwa ya ardhi ambayo ni productive ilichukuliwa na wazungu,baada ya serikali ya kidemokrasia kuchukua uongozi wa nchi wamajitahidi to remedy the situations pamoja na changamoto nyingi wanazokabiliwa nazo(elewa katiba yao inaruhusu kumiliki ardhi kisheria) na ili ruling party wapate nguvu za kuchukua ardhi kwa nguvu bila kulipa fidia ni lazima wabadilishe katiba (huu ni mtihani mkubwa mno);EFF wao wanazungumza siasa maana hata wao hawawezi kutekeleza hili kisheria ila kama watatumia nguvu na hili athari yake itakuwa kama ya majirani zao,mtoa mada wako huyo mgeni wako alikuwa mchoyo wa ukweli,serikali ya sasa(ANC)ina ardhi kubwa kupitia SOEs zake amabazo zikigawiwa vema kwa wananchi wake kutapunguza mno tatizo hili.na tuelewe tatizo kubwa wanalokabiliwa nao SA ni uhamiaji mkubwa wa raia kutoka rural areas kwenda urbani areas na wahamiaji wengine wengi wanaotoka nje ya mipaka yake,kwa hiyo watu wengi wanahitaji ardhi ya kujenga makazi sio kuendesha kilimo au ufugaji,their presidents anafanya kazi nzuri sana pamoja na changamoto alizonazo,elewa kutawala SA SIO KAMA TANZANIA..
 
Mwezi June mwaka huu nilikuwa na interview saa nne asubuhi. Nilinunua ticket ya train ya saa saba mchana kurudi kwenye mji wa mwenyeji wangu ambako ni masaa matatu kwa train.

Mategemeo yangu ilikuwa mpaka saa tano interview itakuwa imekwisha. Nitapata muda wa kula na kupumzika kabla sijaingia kwenye train. Lakini mahojiano yalichukua masaa mawili nilipewa Dakota 15 za kahawa ngoma ikaanza tena. Tulimaliza interview saa sita.
Kutoka na na ugeni kwenye maji ule, niliamua kwenda kituo cha train moja kwa moja nusichelewe train yangu. Nikiwa njiani niliamua kununua vyakula ambavyo nitakula kwenye train.

Nilipofika train station nilikuwa na nusu saa kabla train haijaondoka. Nilikaa kwenye bench kusubiri. Alikuja kuja kijana mtanashati na nguo zake ziko kwenye mpangilio wa kuvutia.

Alinisalimia na kuniuliza kama ninasubiri train anayosubiri yeye. Nilimjibu ndiyo, kutoka pale tulianza maongezi.

Aliniambia yeye anatoka South Africa, ndiyo kwanza amemaliza Masters ya Engineering na ameapply PhD programme kuanzia September 2018, application yake na interview vilitegemea first degree results lakini professor aliridhika na amemwambia majibu yake yakitoka July aya scan ila alikuwa na offer.

Katia maongezi akaniambia na yeye hakutegemea kuwa interview yake ingekuwa ndefu. Hajupata nafasi ya kula alikuwa na chupa ya coke.

Nilimwambia pole tuko katika hali sawa na tunaweza kugawana chakula changu . Katika maongezi aliniambia mategemeo waliyonayo kwa rais wao mpya. Pia alisema nyinyi uhuru wa ardhi mlionao mnabahati sana. Kwetu radhi wanamiliki wazungu na vijana hawana ajira wala hawawezi kujiajiri kwa kilimo.
Kwa hiyo mama yetu hebu tuambie mlipotelemka na huyo kijana mtanashati nini kiliendelea mpaka mwisho maana naamini mwisho ulikuwa mzuri sana
 
Hao wa South si ndio wanaobagua waafrica wenzao,,? Muosha huoshwa,, zile nguvu walizotumia kuwafurusha wageni wa kiafrika ilitakiwa wazitumie kuwafurusha wazungu mashambani ili walime wao
 
Punguza haraka utafikiri umewaona wasiojulikana my love umekurupuka mno,narudi kwenye mada yes Watanzania kwa hilo nyerere aliona mbali,kama Zimbabwe na south zilitakiwa kufanya hivyo baada ya kupata uhuru.
 
Nilimuuliza mkenya mmoja baada ya kulalamika na maisha
Nilamwambia huna shamba? Akaniambia ninalo nyuma ya nyumba
Hapo nikamwambia garden au shamba?

Kwa kweli tunamshukuru Mungu kwa hili ingawa Prince amejimilikisha sehemu na kuweka minara yake ya itisalat
Tukiendelea kuuza ardhi tutakuwa kama jirani kina zim na sa na kq

Sent from my SM using Tapatalk
 
Ndiyo maana mandela anapendwa na wazungu alitimiza matakwa yao kama hayo ya ardhi kuwaacha waendelee kumiliki ardhi wageni.RIP mwalimu mkombozi wa kweli africa huyu mwingine mtoto aliye wakataa wazazi wake akawakubali wageni ndiyo maana bado wanamwangalia yy

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndiyo maana mandela anapendwa na wazungu alitimiza matakwa yao kama hayo ya ardhi kuwaacha waendelee kumiliki ardhi wageni.RIP mwalimu mkombozi wa kweli africa huyu mwingine mtoto aliye wakataa wazazi wake akawakubali wageni ndiyo maana bado wanamwangalia yy

Sent using Jamii Forums mobile app
Mandela alitaka watu wazoee uhuru wa kujitawala kwanza. Bahati mbaya muda haukuwa mikononi mwake
 
Back
Top Bottom