TANZANIA: Turekebishe la Ustaafu wa Siasa!

Apr 27, 2006
26,588
10,375
- Heshima mbele wakuu wote JF, baada ya muda mrefu sana tupo wote tena unajua mishe mishe ya maisha.

Leo ya ustaafu kutoka kwenye siasa zetu Tanzania, I mean tufike pahali tujikite as a nation kulitengeneza hili la Ustaafu kutoka kwenye politics, hatuna mazingara yanayofaa as the results Wazee wetu wengi hawataki kustaafu ni kwa sababu wanaogopa wataenda wapi? Leo kule US kina Condoleeeza Rice, Cohen, Kissinger, wamestaafu siasa na wamerudi kwenye professional zao za Ualimu pamoja na kulipwa posho nzito wanapotoa hotuba kwenye midhahara. Hivi karibuni Rais Kaunda, alikuwa anafundisha Boston College, wamemlipa vizuri tu as of their standards na sasa naamini yupo sawa sana kuliko alivyokuwa kabla ya kwenda kufundisha tena kazi yake ya zamani.

- My point ni kwamba panahitajika a serious National agenda au Kipengele kipya kwenye katiba cha kusimamia Ustaafu wa Wazee wetu kutoka kwenye siasa na kuwahakikishia comfortability na kuwezeshwa pamoja na heshima, ili wakitoka kwenye politics zetu warudi walikokuwa kabla, kama Udakitari, kama ni ualimu, Sheria hili linahitaji nguvu ya Taifa kulisimamia, ama sivyo hii vita kali iliyopo sasa ya kuingia kwenye uongozi wetu wa Siasa za taifa haitapungua karibuni na ndio chanzo cha siasa za majitaka na makundi, ambazo zinalitafuna sana hili taifa tunaishia kukosa viongozi bora wengi kwa sababu ya Vita kali ya kuingia na wasiotaka kutoka, uchaguzi ukiisha kunabaki makovu na majeraha makubwa sana mpaka hatuwezi kusameheana kisa simply hatuna pengine pa kwenda na tulishaamini kwamba nafasi tulizonazo ni zetu milele kumbe ni za wananchi na infact ni za Taifa na ni haki kwa kila mwananchi kugombea!

MUNGU AIBARIKI TANZANIA!

Field Marshall Es: WAZEE WA SAUTI YA UMEME!
 
Hili mkuu kwa Kiafrika afrika viongozi wetu watapata mwanya wa kujilimbikizia mali mara dufu kuliko ilivyo sasa itakuwa kila mtu anakula kwa urefu wa kamba yake.

Karibu sana SAUTI YA ZEGE
 
Duh,

Hivi hizi hawa wanasiasa wetu wanazojilipa wanapostaafu haziwatoshi? Hivi tunawatunuku kwa lipi, kugawa rasilimali zetu kama sadaka kwa maswahiba wao wa nje? If anything, katiba mpya iangalie uwezekano wa kutoa malipo ya haki na stahiki kwa hawa wastaafu na si huu wizi wanaotufanyia.
 
FMes, Karibu tena jamvini!

Tatizo la wazee kuogopa kutoka kwenye siasa ni la kujitakia zaidi. Tungeweza kuweka utaratibu mzuri ambao unaeleweka rasmi wa namna ya kuwatumia wazee hawa katika nyanja nyingine mbali ya uongozi wa kisiasa.

Siasa zetu zimekuwa za kinafiki zaidi na ndio maana kuna woga mkubwa kama wakitoka mambo yao yataishia vipi. Njaa ina msukumo mkubwa zaidi kuliko ukweli wanaotaka kuusimamia kama viongozi. Na hii inakwenda mbali zaidi wanapojaribu kurithisha hata generations zao.
 
- Tatizo ni la Vijana sio Wazee, sasa ni wakati wa Vijana kushauri solutions ninaamini kwamba Wazee wanapokuwa kwenye power wanahitaji kukatwa hela nyingi kwenye malipo yao na ziwe heavily invested specifically kwa ajili yao ili ziweze kuwawezesha time ikifika, badala ya kuendelea kupigania uongozi wa siasa tuu!

- Wachezaji wa Football na Basketball kule US, wanafanyiwa hivyo ndio maana OJ Simpson alikuwa vizuri tu kabla ya matatizo yake ya kishera kwa sababu alipokuwa anacheza mpira walikuwa wanamkata hela nyingi sana ambazo zikawa invested na NFL, hivyo muda wa ku-retire ulipofika hakukuwa na matatizo ya yeye kulilia kubaki kwenye mpira tu na kugombanan na vijana wanaotaka kuingia, najua US ni big kwa mfano, lakini walianzaia somewhere kufikia walipo sasa!

- Viongozi wetu kwani hawawezi kutangaza vipindi vya siasa na wakalipwa vyema kama huko nchi za wenzetu? Sasa kama hatutengenzi wenyewe tutasubiri nani wafadhili?

Es!
 
Ya umeme karibu mkuu!,umenena la maana sana,nalo tulijadili kiundani,kwa sasa napita tu nataka kudili na hawa mgambo walochoshwa na serikali ya ss em.Wanataka kumdhulumu mdogo wangu kwangu wamefika!
 
Well said Sauti ya "Tanesco", karibu jamvini tena baada ya ukimya mkubwa.

Mimi kwa mtazamo wangu naona hili linawezekana, na kwa kuanzia nafikiri ni muhimu sana kuangalia package wanayoondoka nayo baada ya kustaafu. Najua wako baadhi yao (Wachache sana) wanaoondoka na vitita vikubwa lakini kundi kubwa linaondoka na fungu dogo sana.

Na kwa kuanzia nadhani tuangalie mafao ya uzeeni yanayotolewa na mifuko yetu ya pensheni, kwa kuzingatia uwekezaji unaofanywa na mifuko hii na kiwango kikubwa cha faida wanachokipata kwa kutumia fedha zetu kuwekeza, basi tuangalie ni kwa namna gani tunaweza kunufaika na uwekezaji huo.

Mtu lazima ang'ang'anie kubaki kwenye siasa kwakuwa anajua package yake ya kustaafu ni ndogo na malipo anayopokea toka mifuko ya pensheni ni ndogo sana na haitoki kwa wakati, nadhani tuanzie hapo huku tukiangalia na maeneo mengine.
 
Hapa nakubaliana na kabisa na sauti ya umeme.....
Nitarudi kwa mchango mnene,
Mitaanza na mzee Malechela:cool:

Wanasiasa wengi hawataki kun'gatuka kwasababu ya madhambi yao walioyatenda wakiwa madarakani hivyo huogopa kuwa hao wapya wanaweza kuwapeleka kizimbani; tungekuwa na mifumo mizuri ya kuwathibiti wasifanye madhambi hayo kwamfano kupora mali za umma wawapo madakani wengi wasingeogopa!! Kuna social aspect pia kuwa mara nyingi hawa wazee wanapopata wake wadogo wanawaendesha sana kuwa wasiondoke ili nao wapate kufaidika na hivyo vyeo ; mfano mzuri ni Grace Mugabe kule Zimbabwe na hapa bongo nawaachia mtajaza wenyewe!!
 
Mkuu,

Malipo kwa wanasiasa wetu wastaafu ni mazuru tu na yanawatosha kabisa pamoja na marupurupu wanayoyapata. Wana uhakika wa kuishi maisha mazuri hadi mungu awatwae. Nakumbuka JK aliulizwa kuhusu kujilimbikizia mali akiwa Rais, akasema hana shida ya mali kwa kuwa akishakuwa Rais ana uhakika wa kutunzwa yeye na familia yake hadi kifo.

Tatizo la wanasiasa wengi wa kiafrika ni kwamba wanapokuwa kwenye madaraka wanayatumia vibaya ikiwa ni pamoja na kujinyakulia mimali ya wanyonge bila utaratibu. Hivyo basi wanasiasa wengi huamua kujikita kwenye siasa na hawataki kuondoka kwa ajili ya kujilinda dhidi ya maovu waliyoyatenda.

Kwa mfano jirani yetu Mugabe hataki kuondoka mamlakani kwa kuwa anaogopa kwamba akitoka tu kuna watu wataitaka shingo yake hivyo bora afe akiwa Rais kuliko kudhalilishwa kama akina Banda. Hivi tunadhani Mugabe hana akiba ya kutosha kweli iwe ya halali ama haramu?
 
100% nasapot manake ukimwona mtu kama Mkapa ni rais mstaafu, lakini mambo anayoyafanya yanamshushia hadhi, ukiwa level ya rais, hupaswi(kwa mtazamo wangu) kubeba kundi fulani ndani ya nchi, watu wote ni wa kwako, ukihitajika kutoa wazo utatoa kwa ballance na siyo kufanya kama anavofanya yeye, kwa mimi hii siyo demokrasia
 
- Heshima mbele wakuu wote JF, baada ya muda mrefu sana tupo wote tena unajua mishe mishe ya maisha.

Leo ya ustaafu kutoka kwenye siasa zetu Tanzania, I mean tufike pahali tujikite as a nation kulitengeneza hili la Ustaafu kutoka kwenye politics, hatuna mazingara yanayofaa as the results Wazee wetu wengi hawataki kustaafu ni kwa sababu wanaogopa wataenda wapi? Leo kule US kina Condoleeeza Rice, Cohen, Kissinger, wamestaafu siasa na wamerudi kwenye professional zao za Ualimu pamoja na kulipwa posho nzito wanapotoa hotuba kwenye midhahara. Hivi karibuni Rais Kaunda, alikuwa anafundisha Boston College, wamemlipa vizuri tu as of their standards na sasa naamini yupo sawa sana kuliko alivyokuwa kabla ya kwenda kufundisha tena kazi yake ya zamani.

- My point ni kwamba panahitajika a serious National agenda au Kipengele kipya kwenye katiba cha kusimamia Ustaafu wa Wazee wetu kutoka kwenye siasa na kuwahakikishia comfortability na kuwezeshwa pamoja na heshima, ili wakitoka kwenye politics zetu warudi walikokuwa kabla, kama Udakitari, kama ni ualimu, Sheria hili linahitaji nguvu ya Taifa kulisimamia, ama sivyo hii vita kali iliyopo sasa ya kuingia kwenye uongozi wetu wa Siasa za taifa haitapungua karibuni na ndio chanzo cha siasa za majitaka na makundi, ambazo zinalitafuna sana hili taifa tunaishia kukosa viongozi bora wengi kwa sababu ya Vita kali ya kuingia na wasiotaka kutoka, uchaguzi ukiisha kunabaki makovu na majeraha makubwa sana mpaka hatuwezi kusameheana kisa simply hatuna pengine pa kwenda na tulishaamini kwamba nafasi tulizonazo ni zetu milele kumbe ni za wananchi na infact ni za Taifa na ni haki kwa kila mwananchi kugombea!

MUNGU AIBARIKI TANZANIA!

Field Marshall Es: WAZEE WA SAUTI YA UMEME!
Mkuu mada nzuri tatizo wachangiaji unao? humu JF uelewa wa watu unashuka siku hadi siku. Hiyo mada yako labda ungeitengenea jukwaa lake ili wenye akili zetu tukahamia huko tukajenga Tanzania yenye uzalengo , mshikamano na amani. Hii JF ya akina tikiti sijui!
 
Kwa hiyo unataka Mkapa arudi kwenye ukanjanja pale Habari-Maelezo?! Hudhani kuwa yu salama zaidi kuendelea kuvaa nguo za kijani na kupiga porojo jukwaani ili CCM iendelee kukaa madarakani? Hudhani kwamba wakiingia wapinzani madarakani equation inaweza kubadilika na maisha ya Mkapa kuwa ya taabu?
 
Mkuu mada nzuri tatizo wachangiaji unao? humu JF uelewa wa watu unashuka siku hadi siku. Hiyo mada yako labda ungeitengenea jukwaa lake ili wenye akili zetu tukahamia huko tukajenga Tanzania yenyeuzalengo , mshikamano na amani. Hii JF ya akina tikiti sijui!
UMEHARIBU HAPO ULIPOSEMA "wenye akili zetu"...!Vinginevyo nisingekuumbua!
 
Aidha kungalikuwa na taasisi ya Wastaafu,(ikijumuisha Kuanzia Marais, Mawaziri na Top Executives wengine) ambayo ingekuwa Neutral kabisa na masuala ya siasa, yenyewe ingekuwa kama Advisory Board ya Masuala ya Kitaifa!
Hii ingesaidia sana kulinda heshima za Wastaafu, na kuwaepusha na kashfa, na kudharaulika na Jamii baada ya vipindi vyao vya uongozi.
Kama alivyosema mleta mada, watu hawa wanalazimika kukilamba miguu chama baada ya kuzeeka ili kwamba aidha wasishitakiwe, au waendelee kupata baadhi ya favors zinazo'emanate kutoka kwenye chama!
 
..Mkuu Taasisi unazopendekeza ziundwe, tayari zipo, mojawapo ni Mwalimu Nyerere Foundation, wanaoiongoza hio Taasisi ni wazee wetu wastaafu, wengine wana CV nzuri tu, tatizo ni hizo siasa za Visasi, uchwara, majitaka. Kwamba ni mwiko kuikosoa Serikali iliyopo madarakani, ukifanya hivyo utakiona. Leo hii Mwalimu Nyerere Foundation ipo wapi??!!!
..Badala yake Wastaafu hao wanabaki kama ulivyooandika @Red hapo juu.
 
Vijana wanaoandaliwa na wanasiasa wetu wengi nao ni wa mashaka mashaka tu. They have nothing to offer. Ukiona wanaongea, usifikiri ni kutokana na busara au uelewa wao...ujue wametumwa na mabwana wakubwa ambao wanapenda kutupa moyo kwamba your time will come...uheshimu wazee. Kama siku watapata madaraka, kitu ambacho nina shaka nacho sana, watatuangusha big time.
 
..mkuu taasisi unazopendekeza ziundwe, tayari zipo, mojawapo ni mwalimu nyerere foundation, wanaoiongoza hio taasisi ni wazee wetu wastaafu, wengine wana cv nzuri tu, tatizo ni hizo siasa za visasi, uchwara, majitaka. Kwamba ni mwiko kuikosoa serikali iliyopo madarakani, ukifanya hivyo utakiona. Leo hii mwalimu nyerere foundation ipo wapi??!!!
..badala yake wastaafu hao wanabaki kama ulivyooandika @red hapo juu.

hapo nakuunga mkono mkuu hii taasisi ya mwalimu nyerere ingeweza kuwa mfano mzuri kwa hilo lakini tatizo ndio kama hilo ulilosema, la msingi ni kujipanga na kuweka mwongozo utakaotoa nafasi kwa wazee kuondoka kwa wakati na kuachia vijana la sivyo kuna vingunge wengi tutawatarajia huko mbeleni
 
Zambia wamejiwekea sheria kwamba ukishakuwa mstaafu katika vyeo vya kisiasa.. na ili waendelee kupata huduma na mafao toka serikalini hawatakiwa kushiriki katika siasa kwa njia yeyote ile.. Na ikitokea kiongozi mstaafu ameshiriki katika mambo ya siasa then anakuwa amepoteza huduma zote toka serikalini.. Nadhani huo unakuwa ni mwanzo mzuri kwa maana mwisho wa ciku kwa kuwa hawana la kufanya (kisiasa) itabidi warudi kwenye professions zao.. Tukianzia na sie hapa kama walivyoanza Wazambia.. then 2naweza kabisa kutengeneza cream ya viongozi wastaafu ambao wamerudi kwenye professions zao na wanawatumikia watanzania kwenye medani nyingine..
 
Back
Top Bottom