Kiranja wa jamii
JF-Expert Member
- Jan 2, 2023
- 1,126
- 2,658
Siasa zimekuwa sumu inayoua utaifa wetu kimya kimya kuja kushituka tutajikuta mateka kati yetu wenyewe
Leo vyuo vikuu vimekuwa wazalishaji wakubwa wa machawa badala ya wataalamu
Vijana wengi wameamua kuingia kwenye siasa za vyama kwa ajili ya kulinda kesho yao. Hawana uhakika wa kuishi bila kuwa machawa wa kijani na njano
Kutwa kucha wanahangaika kutafuta kumbukumbu za picha wakiwa wamevaa magwanda ya kijani na njano au fulana za "Mama asemewe" ilimradi tu akimaliza chuo atumie kama sehemu ya kujitetea kusaka tonge lake
Ajira za serikali haziangalii uwezo bali itikadi. Wengi wameajiriwa kwa "kudhani" ni kwasababu wa kujiweka kimbelembele katika siasa
Wale wanaoachwa wakihangaika mtaani wanaamini kadi za chama ni sehemu ya kigezo cha ajira
Walioko kwenye utumishi wa umma wamefunga midomo kukemea makosa, kukosoa hata kushauri wakihofia ulimi ukiteleza watakosa ugali wao
Wale wanaotaka vyeo hawawezi kuongea bila kumtaja asiyewafahamu wale asiyehiyehitaji kutajwa kila muda. wanadhani kufanya hivyo ndio kulinda vyeo vyao
Maskini ya Mungu kila program utawakuta hata kwa kujilazimisha
Marathoni wapo, mchakamchaka wapo, makongamano wamo, mwenge wapo...haijalishi wanaumwa wala wanamajukumu mengine ya kifamilia, wanaamini wasipoonekana watasemwa
Mungu tuepushe na hii dhambi ya siasa kula utu wetu