Tanzania tunarudi kwenye mfumo wa chama kimoja?

Seif al Islam

JF-Expert Member
Nov 14, 2011
2,156
638
Waswahili husema dalili ya mvua ni mawingu. Japo sio kila mara mawingu huleta mvua lakini kila yaonekanapo walau kunakuwepoa matumaini au labda hisia kuwa mvua itanyesha. Hali ya kisiasa ya nchi yetu chini ya awamu hii ina dalili nyingi ambazo zikitazamwa kwa pamoja na haiba na kaliba za viongozi mbalimbali, zinaleta ouicha moja mbaya na isiyopendeza. Ni dalili kuwa kwa kujua au kutokujua, tunarudi au kurudishwa kwenye Mfumo wa Chama kimoja. Ili kueleweka nitaweka baadhi ya mifano ya matukio na mambo yanyotia mashka juu ya mwenendo wa demokrasia yetu:

1. Kukatazwa kwa mikutano ya kisiasa.

Hili ni kinyume cha Katiba ya nchi na Sheria ya Vyama vya Siasa. Lakini tukumbuke chini ya Mfumo wa Chama kimoja, Katiba na Sheria huwa haziheshimiwi na zaidi kinachotawala ni hisia, matakwa na amtamanio ya mtu binafsi.

2. Kuminywa kwa uhuru wa Habari.

Tumeshuhudia jinsi ambavyo sharia kandamizi zinavyotumika kuminya uhuru wa Vyombo vya Habari, Media House na hata Bloggers pamoja na Mitandao ya Kijamii (Sizunumzii Jamii Forums) inaandamwa na kuoigwa vita. Vyombo vya habari vimegeuka maadui na hata wapo walioomba Malaika wahuke kuja kuzima Social Media. Viongozi wanataka kuwapangia wahariri ni icha ipi iwekwe gazetini na ipi isiwekwe. Vitisho vya wazi wazi kwa uhuru wa vyobo vya habari vimekithiri. Hapa sitazungumzia uvamizi wa Clouds NMedia. Mtindo huu ni moja ya mitindo ya utawala wa chama kimoja.

3. Kutoheshimika kwa Mifumo na Taasisi.

Tunashuhudia jinsi viongozi wanavyoshindwa kutambua na kuheshimu mammlaka na taasisi zilizopo kwa mujibu wa sharia na kujitwalia mamlaka ya taasisi hizo. Sakata la Dawa za Kulevya ni mfano mzuri wa hali hii. Kiongozi ambaye ni Kada wa Chama Tawala anaweza hata kumuamrisha mtu aliyemzidi nafasi kisa tuu anajuana na kiongozi fukani wa chama. Mkuu wa Mkoa anaweza kumuamrisha Kamanda wa Polisi wa Mkoa. Ni katika nchi za mfumo wa chama kimoja na hata hapa Tanzania kipindi cha mfumo wa Chama kimoja ambapo makada wa Chama walikuwa na nguvu kuliko watendai wa Serikali.

4. Kutoweka kwa watu katika mzingira yasiyojulikana

Alianza Ben Saanane na sasa tupo kwa Roma Mkatoliki. Hawa ni baadhi tuu ya watu waliopotea katika mazingira yanayotia shaka na yanayoonyesha weleddi mkubwa katika utekelezwaji wake. Kinachouma zaidi ni kuwa hawa wote ni wakosoaji wa serikali. Ben alihoji sana kuusu uhalali wa elimu ya kigogo mmoja wa serikali. Haya ni matukio ya kila siku huko Korea ya Kaskazini nan chi nyingine za Chama Kimoja.

5. Kuingiliwa kwa uhuru wa Mihimili mingine ya Dola

Ni katika kipindi hiki ambapo tuliambiwa kuwa japo kuna mihimili mitatu ya dola, upo mhimili mmoja uliojikita chini zaidi na ambao huipa mihimii mingine fedha za kujiendesha. Tulishuhudia jinsi watendaji wa muhiili mmoja walivyojaribu kushawishi mhimili mwingine kwa fedh za umma ili mihimili huo ufanye kazi kwa amsalhi yake. Haya yote yanafanyika hadharani na bila aibu. Ni katia nchi ya mfumo wa Chama kimoja ambapo mhimili mmoja huiegemea mingine na hata kuiminya uhuru wake.

Wataalamu wa afya hutukumbusha kila siku kuwa sio kila homa ni malaria. Homa yaweza kuwa na uginjwa mwingine na sio malaria. Kma falsafa hiyo itahusika pia katika kuzitazama na kuzipima dalili tajwa hapo juu, basi demakrasia yetu itasalimika, vinginevyo ni bahati mbaya.

Nawasilisha
 
Hivi Akina Askof Valentino Mokiwa walipokuwa wanamsakama Jk walisema anahitajika Rais Kama Kagame jee walimaanisha

1) Mkristo

2) Mrefu Chembamba Cheusi

3) Mbabe, Dikteta na Muuaji?
 
Kutokana na shinikizo linatolewa na CCM dhidi ya vyama vingine vya siasa kwa kutumia dola na vyombo vyake. Jee ni sawa kama Tanzania tukirudi kwenye mfumo wa chama kimoja cha siasa!?
 
Kuna mtu ana azima kutufanya wote kondoo ama mgambo, mbele tembea!!! Nyuma geuka!!!!! Atufanye atakavyo kokote bila hiari yetu!!!!
 
Kutokana na shinikizo linatolewa na CCM dhidi ya vyama vingine vya siasa kwa kutumia dola na vyombo vyake. Jee ni sawa kama Tanzania tukirudi kwenye mfumo wa chama kimoja cha siasa!?
Tusema ukweli wapinzani wenyewe ndio wanaoua upinzani Tanzania.

Mfano Chadema ,Mbowe alikabidhiwa chama kikiwa na demokrasia kuliko vyama vyote mpaka mwalimu Nyerere alikisifia kuwa chama mbadala wa CCM lakini Mbowe akabadili katiba bila aibu kwa manufaa yake binafsi bila kuangalia heshima ya chama na uhalali wa kusimamia demokrasia nje ya chama na akalaghai watu ili awe mwenyekiti wa Kudumu. Mbali na uenyekiti wake wa kudumu lakini akawa ni dikteta hatari sana ndani ya Chadema na mfano mbaya ambaye anaigwa na wababe wa vyama vingine kwa kuwa eti udikteta ni msimamo mzuri dhidi ya wapinzani wa MTU kisiasa.
Alijitangaza kuwa yeye pekee ndani ya chadema ndiye kiboko ya CCM na vyama vingine. Amewaaminisha watu kuwa udikteta unapeleka mbele maendeleo ya chama na sasa wengine wamemuiga. Sasa analalamika kuwa Vyama vingi bora vifutwe.
Vifutwe vipi !! Kwa nini asiondoko yeye kama ni kufa vife vyenyewe chini ya uongozi wa MTU mwingine? Kwa nini anasema Mara kwa Mara vifutwe wakati vipo Kikatiba? Kwa hiyo ikibaki CCM pekee ndio atapata nafasi ya kuandamana na nafasi ya kuipinga na kuikejeli serikali?

Mbowe ajiulize tu Uganda Bob Wine amepigwa tena kwa sababu ambazo huenda ingekua Kwetu pangekua na parapanda za kutosha mana kushambulia msafara wa Rais na kunyanganya walinzi silaha ni kosa kubwa sana, hata hivyo dunia nzima imelaani kitendo cha kupigwa kwake. Mpaka Bunge la uingereza limezungumzia habari hiyo na Trump pia. Why hata watanzania wa kawaida wengi hawamuungi mkono ? Jibu ni moja ,amepoteza ujasiri ,haki na uhalali wa kusimamia demokrasia iliyopo Kikatiba kwa sababu ameua demokrasia ndani ya Chama chake.(Charity begins at home.)
 
Hivi Akina Askof Valentino Mokiwa walipokuwa wanamsakama Jk walisema anahitajika Rais Kama Kagame jee walimaanisha

1) Mkristo

2) Mrefu Chembamba Cheusi

3) Mbabe, Dikteta na Muuaji?
Uongo na propoganda nyepesi,lini na wapi walisema anahitajika kama Kagame,hata hivyo hawajachaguliwa na Watanzania kuwa wasemaji wa watu takribani mil50
 
Back
Top Bottom