ERTUGRUL BEY
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 11,529
- 21,530
My people,
Kumekuwa bado na mijadala ya hapa na pale kuhusiana na je Tanzania kuna amani? Na wengine wakisema hakuna haki au wanasema haki kwanza,au amani ni tunda la haki
Haki huja baada ya amani kuwepo sehemu yoyote ile duniani,kwani uwepo wa amani ndio hufungua kurasa nyingine za mazungumzo na maelewano,mfano kinachoendelea leo pale Ukraine na Urusi ni vita na hakuna amani,kwa mazingira yale hakutakuwa na haki kwasababu haki ni zao la amani,vita visimame ndio wazungumze,kuona je Ukraine ana haki kama nchi huru kujiunga na Umoja wa Nato au kujiunga kwake anahatarisha usalama wa Urusi
Wote ni mashahidi baada ya vita ya siku 12 kati ya Iran na Israel,ili amani ipatikane,ilibidi wasimamishe vita na kufanya mazungumzo ya kusitisha vita na kuleta amani ndio kisha mambo mengine yaendelee
Hapana haki inayoweza kupiganiwa au kudaiwa kwenye mazingira ya vita,hakuna haki inayoweza kudaiwa kwenye mazingira ya fujo na vurugu,lazima kwanza pawepo na Amani kisha mambo mengine ndio yafuatiye
Na amani ni moja ikiwepo utaona athari zake mara moja na amani isipokuwepo pia utaona athari mara moja,lakini haki ikiwepo au isipokuwepo huwezi ona athari yake mara moja kwasababu haki ni mjumuisho wa vipengele vingi au mambo mengi ambayo hayana athari ya moja kwa moja kama ambavyo amani ikiondoka utaona athari ya moja kwa moja
Mfano leo hii amani ya Tanzania ikiondoka mara moja,wote tutaathirika tupende tusipende,kwakuwa penye mazingira ya fujo na vurugu hakuna shughuli ambazo zitafanyika
Lakini inapokosekana haki ya kutoa maoni na mawazo ambayo hatuna sasa sio wote tunao athirika bali ni wale ambao wanadai haki hiyo tu ndio wanao athirika,mfano wanaotekwa wote ni wale ambao wanatoa mawazo yao na maoni yao dhidi ya Serikali, kwahiyo ukiwa mtulivu na kujua kujichunga na kujiweka mbali na matatizo utakuwa salama
Kwahiyo mpaka hapo tumeona kwamba Tanzania tuna amani na ndio maana shughuli zinaendelea kama kawaida,wanao lima wanalima,wanafabiashara wanafanya biashara zao na wanao beti wanabeti ingawa ni haramu,pamoja na kwamba kuna haki tunazikosa .
Tanzania hakuna uhuru wa kutoa maoni na mawazo,hakuna uhuru wa kuchagua viongozi tunao wataka,maana uhuru ni kujifanyia mambo yetu bila kubagazwa au kubanangwa
Na si kila haki yenye kugaiwa,mfano huwezi kudai haki ya kutambuliwa kwa mashoga hapa Tanzania,lakini bado utainjoy amani ya nchi hii,hakuna haki ya kutoa mawazo yako na maoni yako pasina kuchunga mipaka,kwasababu uhuru wako wa kutoa maoni na mawazo unaishia pale uhuru na haki ya wengine inapoanzia
Kwahiyo ndugu zangu watanzania, hapa Tanzania tuna amani na tuendelee kuilinda amani yetu kwani ni tunu kubwa sana basi tuilinde kwa wivu mkubwa sana
Mungu ibariki Afrika na Mungu ibariki Tanzania
Ni hayo tu!