Tanzania "Tumevurugwa, tukavurugika"

Tanzania "Tumevurugwa, tukavurugika"

kimatire

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2008
Posts
371
Reaction score
94
:bowl:Mara nyingi tumekuwa tukishabikia kila kinachojitokeza kwa nguvu nyingi pasipo kutafakari kwa kina.Maisha yetu yamejawa na mvurugano wa kimawazo/kifikra zaidi achalia mbali ule wa kimasilahi.

Ni kweli kwa uduni wetu wa maisha umetufikisha mahali hata ufikiri wetu Watanzania umekuwa duni na wa kutilia mashaka jinsi tunavyoenenda.

Tumepoteza umakini wa kutafakari mambo ya msingi ya kutubadili badala yake tumejitwika siasa zisizokuwa na tija katika ustawi wa maisha yetu ya kila siku.

Tunapozungumzia kumpata kiongozi wa kubeba dhamana ya kutupeleka kule nchi inakotakiwa kufika , Ni lazima tuwe na malengo ya kuwa na mwelekeo wenye kutupatia tija katika nyanja zote,ziwe za kiuchumi, za kijamii hata za kimazingira.

Tuwe na mwelekeo wa pamoja pasipo kuyumbishwa na siasa wala ilani za vyama hata na imani zetu za asili.Tukisema dira hatuna maana ya chama cha kisiasa wala imani ya mwanasiasa fulani.

Dira ni uelekeo wetu sote pasipo kuangalia itikadi zetu za kisiasa wala za kiimani , ambazo hizo zikitekelezwa shurti tufikie tulikolenga kufika.

Tufanikiwe kutimiza kile tunachoamini kinatupatia tija kimaisha.Kimsingi hayo ndiyo tunayaita maendeleo,Tutoke tulikokuwa jana tufike tulikodhamiria kuwa leo.

Sasa Taifa letu limefika pahala pa kulalamika na kulaumu kila kukicha pasipo kuwa na ufumbuzi.Kwa ujumla wake mimi nasema waTanzania ‘”tumevurugwa tukavurukika “.

Ushabiki wa vyama , ushabiki wa kisiasa ,huku tukitajana majina majukwaani na kudhalilishana ni kweli tunatafuta njia ya kupata dira au tunatekeleza dhima isiyo na dira , au ndiyo tunatimiza dira zisizo na uelekeo thabiti.

Tufanye nini basi, tujiwekee malengo kwanza! Tuwe na dira ya pamoja, ndipo tuangalie nani atatufikisha kwenye hayo malengo tunayokusudia.

Na kama uelekeo ni duni basi tuangalie njia mbadala baada ya kipindi kifupi kwa kujitathimini tena kwenye sanduku la kura kwa kurudi kwa wananchi waliotoa dhamana hiyo waone kama kweli kuna nia ya kuendelea kukuhitaji kuwaongoza.

Miaka mitano ni mingi sana, yamkini kila bada ya miaka miwili tuwe na kura ya maoni, Itatusaidia kuwa na viongozi wasiokuwa mizigo kwa walipa kodi.

 
YAani ni mvurugano tu...kama kuna nchi inataka kutuibia huu ndo wakati wake...
 
Watanzania hatuelewi tunatiririka tu
Kila jipya linalotokea mtaan sisi mashabiki
Lowasa alivokatwa - eehh Lowasa kakatwa kila mtu kakatwaa hatumtakiii eeh kakatwaa ukawa wimbo
Magufuli kachaguliwa - eeh jembee Tanzania poaaa
Lowasa kwenda chadema - eeehh team lowasaaaaa ulipo tupoooo
Panya road walivotokea - eeh panya road jaman tutakufaa
Na mengine mengi

Sasa assume slaa kajiuzulu🚶🏾

Wabongo leta Mpya moja tu tukushabikie
 
Back
Top Bottom