SoC04 Tanzania tuitakayo yenye wataalam wenye majibu ya changamoto zetu katika dunia ya kishindani

Tanzania Tuitakayo competition threads

jackmichael

New Member
Sep 6, 2013
3
2
"Ugumu wa maisha kaka umenifanya nifanye kazi hii na kuachana na taaluma yangu. Huu ni mwaka wa tatu nauza simu, maisha yanapaswa kuendelea"

Ni kauli ya kijana mmoja pale Makumbushoinayoonekana yakishujaa ila ndani yake yamejaa maumivu kwanza kwa kijana kama alipoteza muda kusomea alichokisomea, pili maumivu kwa taifa kupoteza mtu ambaye angefikiria katika eneo fulani na kutoa majibu kwa ajili ya wengi.

"Asubuhi unaanka unaenda kazini mwaka wa kwanza,wa pili bora nikaendeshe bodaboda. Ni kauli ya kijana aliyekuja kwangu kuhitaji msaada apate mdhamini achukue pikipiki ya mkopo kwenye kampuni fulani. Muhitimu wa chuo kikuu mwenye shahada ya Ualimu. Nilipokuwa nikitembea maeneo ya vyuo vikubwa hapa Tanzania nikagundua wa fanya biashara wadogo wadogo wengi mfano,boda boda,wakala wadogo wa fedha,vibanda vya chips,nguo,simu n k wengi ni wahitimu wa vyuo jirani.

TATIZO LA UKOSEFU WA AJIRA LINACHANGIA VIJANA KUACHA KUFANYA WALICHOKUWA WAKIISOMEA NA KUFANYA SHUGHULI ZINGINE KUJIINGIZIA KIPATO.

Tanzania ya miaka ya 60 ilikuwa na idadi iliyokadiriwa milioni kumi na ilikuwa na kiwango cha chini cha watu waliopata elimu (literacy rate) na serikali ilifikia hatua ya kuazima wataalam kutoka nchi marafiki.

Tanzania mwaka 1988 ilikuwa na literacy rate ya 59% mpaka kufika 2022 ilikuwa 82%
( World Bank Open Data)

Ni juhudi zinazopaswa kupongezwa kutokana na kuongezeka kwa vyuo binafsi na serikali, shule za kata,mipango ya MEMKWA n.k.

Ongezeko la watu walio na elimu imeongezeka je,inaenda sambamba na ongezeko la wataam na mabingwa katika kada zao.?

Juhudi zimefanyika ongezeko la kasi la idadi ya watu imepanda sambamba na ongezeko la kiwango cha watu kupata elimu (literacy rate)lakini ongezeko la watu kuacha taaluma zao kutafuta njia mbadala kujikimu wao na familia zao ni kubwa na hii ni tishio kwa Taifa.

Tanzania tuitakayo inahitaji wataalam waliowekeza muda wao kwenye tafiti mbalimbali, waliowekeza muda katika nadharia na vitendo ili kutoa majibu ya changamoto za watanzania walio wengi na kuinufaisha taifa katika dunia ya ushindani na mabadiliko ya kasi.

Je, vijana wametengenezewa uwezo wakutoa majawabu katika changamoto za watanzania kwa mlengo wa kitanzania katika dunia yenye kasi kishindani na kimabadiliko.

Tanzania tuitakayo miaka 25 ijayo ni kuwa na watanzania wenye weledi na ubobevu katika kada zao na wenye uwezo wa kushauri na kutoa masuluhisho katika kada zao na hivyo kulinufaisha taifa katika dunia ya kishindani.

TATIZO LA WALIO AJIRIWA LAKINI WANAISHI CHINI YA KIWANGO (UNDEREMPLOYMENT ) INACHANGIA VIJANA KUACHANA NA WALICHOSOMEA NA KUFANYA SHUGHULI NYINGINE.

Hawa kiwango cha ujuzi,elimu, muda wao wa kazi hauendani na wanachoingiza.

"Nimefanya intern kwa miaka miwili nmekuwa nikilipwa kiasi kidogo sana na mwanzoni sikuwa ninapewa chochote nimevumilia na umri unaenda nahitaji kufanya maisha. Ngoja tupambane Mungu akijalia tutaendelea huko mbele"

Wengi wameacha taaluma zao kwa sababu hawana ajira kutoka katika kada zao na hakuna mazingira wezeshi kuendeleza taaluma zao.

wachache waliopata fursa wanaacha maeneo yao ya kazi kutokana na maslahi mabovu na kukosa mazingira yakuwajenga katika kada zao.

sekta binafsi ambaye ni mshirika mkubwa katika kujenga wataalam katika kada zao ameonekana kutoa fursa pasipo maslahi na sio vijana wote wanaweza kuvumilia na hivyo wengi huamua kuachana na eneo la kitaaluma walilochagua.

NINI KIFANYIKE KUITENGENEZA TANZANIA TUITAKAYO MIAKA ISHIRINI NA TANO (25)IJAYO

Sheria kanuni na sera za ajira ,elimu na vijana hasa kwenye sekta binafsi zipitiwe upya hasa katika suala Zima la maslahi ya vijana na mazingira wezeshi ya kuwajenga kama hazina katika maeneo waliyotumia miaka kadhaa kujijenga.

Kuunda program za mafunzo na uwezeshaji kwa vijana mmoja mmoja na makundi kwa taaluma walizo nazo ili kuwajenga katika maeneo yao ya kitaaluma.

Zitengenezwe program zinazowawezesha vijana kutumia taaluma zao kujiingizia kipato kuliko kutengeneza program iliyojikita katika eneo moja mfano kilimo na kushawishi watu waache career walizozijenga kwa miaka na kuingia kwenye taaluma isiyo ya ndoto zao na wala hawana misingi ya kutosha. Hii iende sambamba na utoaji mitaji kwa vijana ambao wengi hawana amana na sifa za kukopesheka.

Sheria,kanuni na Sera za ajira na vijana kutengeneza mazingira ya kuwajenga vijana katika taaluma zao ili wawe msaada kwa jamii na taifa.

Tanzania tuitakayo kwa miaka 25 inayokuja yenye uwezo wa kusimama na kushindana katika dunia yenye kasi ya ushindani na mabadiliko inahitaji wataalam waliowekeza muda wao kwenye kutafuta maarifa na ujuzi katika kada zao.AMBAO NI VIJANA WA SASA.
 
Tanzania tuitakayo miaka 25 ijayo ni kuwa na watanzania wenye weledi na ubobevu katika kada zao na wenye uwezo wa kushauri na kutoa masuluhisho katika kada zao na hivyo kulinufaisha taifa katika dunia ya kishindani.
KAbisa hiki ndicho tunachotaka. Kila kada iwe inalipa kiasi ambacho wataalamu watavutika kufanyia kazi taaluma zao.

Sheria kanuni na sera za ajira ,elimu na vijana hasa kwenye sekta binafsi zipitiwe upya hasa katika suala Zima la maslahi ya vijana na mazingira wezeshi ya kuwajenga kama hazina katika maeneo waliyotumia miaka kadhaa kujijenga.
Kweli kabisa.
 
Back
Top Bottom