Tanzania: Tatizo la ajira kwa vijana ni kubwa sana, lisifanyiwe masihara!

Yani mngejua ninavyo mchukia mtu huyu na yule tuliyempangisha Luthuli street kwenye ile nyumba ya umma sipenda hata kuyasoma wala kuyasikia majina yao
 
Si ndio huyo aliyetaka kwenda kununua mvua??????????????:disapointed:

EL amedandia hoja juu juu. Wapambe wake wangemweleza badala ya kuloloma kuhusu ajira za vijana, angezungumza atafanya nini kuondoka tatizo hili. hebu muulize kama na mkakati endelevu wa tatizo hilo.
 
Wakuu,nahisi EL anaogopa vijana watajiandikisha kupiga kura na wote ni cdm.anaona ni bomu linalo msubiri.nawasirisha

Mytake.hata yeye mwenyewe Lowasa ana solution ya tatizo analolisema anataka kulitumia kama issue ya kumbeba 2015
 
Kama inavyoeleweka hakuna mwenye afadhali katika janga la ajira hapa nchini. Si wahandisi, wataalamu wa I.T, wanauchumi, wanasheria na fani nyingine. Sidhani kama Tanzania yetu tatizo la ajira litaisha leo au kesho. Tukiwa walengwa wa suala hili kwa namna moja au nyingine, nini kifanyike kwa anayeanza aliyepo na aliyehitimu chuo kuhakikisha anakabiliana na tatizo la ajira?
 
Mdau,,,me nachakata akili nijiajiri,honestly sitaki tena kuajiriwa naona nachelewa,wakat utakapofika ntaondoka kwenye kuajiriwa,HAKUNA TIJA,nadhan na wewe sugua kichwa jinsi ya kujiajiri,na ukiajiriwa basi iwe ni starting point
 
ushamaliza chuo? Tatizo wengi wanakosa pa kuanzia, hata iyo ajira ambayo utaifanya kama starting point inakuwa utata kuipata bro!
 
Ikiwa kama wanafunzi tunaoanza chuo na hata wale wanaoendelea na waliomaliza kwa mawazo yangu naona bora tuwe na mawazo endelevu ya kufaham ni vipi tutaweza kujiajiri kulingana na fani tulizosomea vyuon kusubir serikali ni kupoteza muda kwa sababu idadi ya wanaohitimu vyuon kwa kila mwaka ni kubwa kuliko idadi ya wanaoajiriwa. Tuwe na mawazo chana katika kujiajiri wenyewe.
 
Mkuu swala la kujiajiri sio la mchezo ati..assume umemaliza chuo hauna hata mbele wala nyuma ndo unaingia street huo mtaji utatoa wapi...?
 
Nimekuwa ni mdau wa kushughulikia tatizo hili kwa vijana kwa muda wa zaidi ya miaka 10 sasa. Kwa uzoefu wangu tatizo kubwa lipo kwenye utasihi wa kisiasa wa kulimaliza suala hili.

Tatizo la pili ni mfumo wetu wa elimu ambao umeshindwa kuendana na hali halisi. Unaandaa watu kukabiliana na mazingira ambayo sio yetu.

Tatizo la tatu ambalo naliona ni mtazamo wetu sisi wenyewe wahitaji wa ajira. Wengi wetu hatuji tunataka nini na tunakimbilia kwenye suala la mtaji kama kisizingizio cha kukaa bila kazi. Utakuta kijana anasema tatizo ni mtaji lakini ukimstukiza na kusema haya sema nikupe shilingi ngapi anakutolea macho na hata akijafanya mjanja akataja kiwango ukimuuliza kwanini umesema kwa mfano milioni 5, kwanini sio 3m au 10m anakutolea macho.

Nigusie la utashi wa kisiasa, sasa hivi tupo kwenye zama za TEKINOHAMA lakini ukienda kwenye ofisi za serikali bado wapo kwenye mfumo wa manual. Hivi kwa mfano serikali ikiamua kuwa huduma zote za serikali ziwepo kwenye mtandao, unajua ni ajira ngapi zitatokea hapo? Mfano mmoja mafile ya wafanyakazi tu yaingie online. Kazi ya kuyachapa, kuedit, kuscan na kupost online inaweza kuajili watu si chini ya milioni. Ikaamua tena kuwa kuanzia next year hakuna mfanyakazi wa serikali atakayeendelea na ajira kama hajui kutumia computer, unajua kuwatraini wafanyakazi wote itatengeneza ajira ngapi? Hicho ni kipengele kimoja tu cha IT. Sector zingine je zikisimamiwa vizuri?

Simple logic, hatuwezi kuwa maskini halafu tunalalamika hakuna kazi, sasa tutatokaje kwenye umaskini bila kufanya kazi? Serikali ikiamua kwa dhati, ndani ya miaka miwili tatizo litapungua zaidi ya nusu.
 
habari wakuu??? sasa mimi nlikua na waoz moja..kiukwel ajira imekua mbovu...
ivi inakuaje wanafunzi mfano wa engineering wakajiunga kama group flan hiv then wakaomba hata loan na kuanzisha hata kampuni yao...naiman hii itasaidia sio kwa wao tu kwani wataweza kuajiri wenzao(engineers)..
hii njia naiman itasaidia kwan wengi tumekua tukimaliza tu tunawaza kuajiriwa afu mbaya zaidi unakuta hali mbaya,ajira hakunaga!!! mhh!! ieleweke kwamba hii njia inaweza tumika hata na kada nyingine mfano lawyers,scientists...na wengineo!!
TO BE HONEST HALI NI MBAYA,NAENDA CHUO KARIBUN ILA CJUI HALI ITAKUAJE BAADAE,HAYO NI MAWAZO TU MWENYE NYONGEZA ANAKARIBISHWA...NAWASILISHA....
 
Kama inavyoeleweka hakuna mwenye afadhali katika janga la ajira hapa nchini. Si wahandisi, wataalamu wa I.T, wanauchumi, wanasheria na fani nyingine. Sidhani kama Tanzania yetu tatizo la ajira litaisha leo au kesho. Tukiwa walengwa wa suala hili kwa namna moja au nyingine, nini kifanyike kwa anayeanza aliyepo na aliyehitimu chuo kuhakikisha anakabiliana na tatizo la ajira?

Serikali iwaandae wahitimu wake kwenda kufanya kazi nje ya nchi.......lugha iboreshwe, pasiwepo una urasimu wa kutoa viza
 
Kama inavyoeleweka hakuna mwenye afadhali katika janga la ajira hapa nchini. Si wahandisi, wataalamu wa I.T, wanauchumi, wanasheria na fani nyingine. Sidhani kama Tanzania yetu tatizo la ajira litaisha leo au kesho. Tukiwa walengwa wa suala hili kwa namna moja au nyingine, nini kifanyike kwa anayeanza aliyepo na aliyehitimu chuo kuhakikisha anakabiliana na tatizo la ajira?

Kwani wahandisi wa Dar Tech nao wana shida ya ajira?, teh teh teh?!!
Anyway, ushauri wangu mdogo ni kuwa kama ingewezekana kuunganisha nguvu na kuweka mikakati ya kujiajiri kadri fani zinavyoruhusu. Maana inakuwa rahisi kupata kazi kama third parties in some of these companies when opportunity arises kuliko kuwa na permanent employment.
Kuna vitu vingi vya kitaalamu bado havijaguswa au kufanywa hata kwetu. Ila inataka watu wajue mwanzo sio lelemama...itabidi kujituma sana.
 
habari wakuu??? sasa mimi nlikua na waoz moja..kiukwel ajira imekua mbovu...
ivi inakuaje wanafunzi mfano wa engineering wakajiunga kama group flan hiv then wakaomba hata loan na kuanzisha hata kampuni yao...naiman hii itasaidia sio kwa wao tu kwani wataweza kuajiri wenzao(engineers)..
hii njia naiman itasaidia kwan wengi tumekua tukimaliza tu tunawaza kuajiriwa afu mbaya zaidi unakuta hali mbaya,ajira hakunaga!!! mhh!! ieleweke kwamba hii njia inaweza tumika hata na kada nyingine mfano lawyers,scientists...na wengineo!!
TO BE HONEST HALI NI MBAYA,NAENDA CHUO KARIBUN ILA CJUI HALI ITAKUAJE BAADAE,HAYO NI MAWAZO TU MWENYE NYONGEZA ANAKARIBISHWA...NAWASILISHA....

Huitaji kuomba loan kuanzisha kampuni; mkiwa chuoni "savings" zenye mfano kazi za vitendo zinatosha kusajili kampuni; Serikali inatakiwa itoe kipaumbele kwa wahitimu wapya kupewa kazi mfano kupitia JKT ili kuwajengea uwezo kabla ya kusimama wenyewe. Mngeanza kwa kuomba "sub-contracts" toka kampuni zinazoaminika ili mjijengee uwezo. Kuhusu mtaji, malipo ya awali na kukopa hapa na pale (creditors) ndio chanzo kikuu cha mtaji
 
Nimekuwa ni mdau wa kushughulikia tatizo hili kwa vijana kwa muda wa zaidi ya miaka 10 sasa. Kwa uzoefu wangu tatizo kubwa lipo kwenye utasihi wa kisiasa wa kulimaliza suala hili. Tatizo la pili ni mfumo wetu wa elimu ambao umeshindwa kuendana na hali halisi. Unaandaa watu kukabiliana na mazingira ambayo sio yetu. Tatizo la tatu ambalo naliona ni mtazamo wetu sisi wenyewe wahitaji wa ajira. Wengi wetu hatuji tunataka nini na tunakimbilia kwenye suala la mtaji kama kisizingizio cha kukaa bila kazi. Utakuta kijana anasema tatizo ni mtaji lakini ukimstukiza na kusema haya sema nikupe shilingi ngapi anakutolea macho na hata akijafanya mjanja akataja kiwango ukimuuliza kwanini umesema kwa mfano milioni 5, kwanini sio 3m au 10m anakutolea macho. Nigusie la utashi wa kisiasa, sasa hivi tupo kwenye zama za TEKINOHAMA lakini ukienda kwenye ofisi za serikali bado wapo kwenye mfumo wa manual. Hivi kwa mfano serikali ikiamua kuwa huduma zote za serikali ziwepo kwenye mtandao, unajua ni ajira ngapi zitatokea hapo? Mfano mmoja mafile ya wafanyakazi tu yaingie online. Kazi ya kuyachapa, kuedit, kuscan na kupost online inaweza kuajili watu si chini ya milioni. Ikaamua tena kuwa kuanzia next year hakuna mfanyakazi wa serikali atakayeendelea na ajira kama hajui kutumia computer, unajua kuwatraini wafanyakazi wote itatengeneza ajira ngapi? Hicho ni kipengele kimoja tu cha IT. Sector zingine je zikisimamiwa vizuri?
Simple logic, hatuwezi kuwa maskini halafu tunalalamika hakuna kazi, sasa tutatokaje kwenye umaskini bila kufanya kazi? Serikali ikiamua kwa dhati, ndani ya miaka miwili tatizo litapungua zaidi ya nusu.

umetufungua macho!! Hata suala la mfumo wa elimu kutoendana na mazingira halisi linasababishwa au llinaweza kutatuliwa KISIASA, unalizungumziaje? Hatujaanza kuzungumzia leo kuwe elimu yetu especially sayansi haimwandai mwanafunzi kukabiliana na maisha ya kila siku.
 
habari wakuu??? sasa mimi nlikua na waoz moja..kiukwel ajira imekua mbovu...
ivi inakuaje wanafunzi mfano wa engineering wakajiunga kama group flan hiv then wakaomba hata loan na kuanzisha hata kampuni yao...naiman hii itasaidia sio kwa wao tu kwani wataweza kuajiri wenzao(engineers)..
hii njia naiman itasaidia kwan wengi tumekua tukimaliza tu tunawaza kuajiriwa afu mbaya zaidi unakuta hali mbaya,ajira hakunaga!!! mhh!! ieleweke kwamba hii njia inaweza tumika hata na kada nyingine mfano lawyers,scientists...na wengineo!!
TO BE HONEST HALI NI MBAYA,NAENDA CHUO KARIBUN ILA CJUI HALI ITAKUAJE BAADAE,HAYO NI MAWAZO TU MWENYE NYONGEZA ANAKARIBISHWA...NAWASILISHA....

Suala lako nakuunga mkono. Graduates kuungana na kuanzisha kitu kama kampuni. Cha msingi hapa tukibadilisha mawazo yetu, yaliegemea kwenye kuajiriwa hii kitu ita work out.
 
umetufungua macho!! Hata suala la mfumo wa elimu kutoendana na mazingira halisi linasababishwa au llinaweza kutatuliwa KISIASA, unalizungumziaje? Hatujaanza kuzungumzia leo kuwe elimu yetu especially sayansi haimwandai mwanafunzi kukabiliana na maisha ya kila siku.
Hili la elimu naweza kulizungumzia kwa urahisi zaidi kwa kuuliza maswali madogo tu. Hivi mtu akimaliza kidato cha 4 au hata 6 anakuwa na ujuzi gani? kwamfano kwao ni pale kwa Manzese, akienda kuomba kuomba kazi kiwanda cha urafiki ataomba kazi gani na atakuwa na mchango gani pale kwenye kiwanda? 2. Akitaka kwenda kujiunga kwenye kuuza mitumba atamzidi nini yule aliyemaliza darasa la saba akijiunga na wauza mitumba kwa kupiga debe tu la kuita wateja na sasa anauzoefu wa miaka 7 kiasi cha kwamba akimuangalia mteja anajua kabisa huyu ni mnunuaji au muangaliaji? Na kama lengo kuu la elimu ni kumpa mtu stadi na maarifa za kukabiliana na mazingira yake, je huyu form 6 yake imemsaidia nini kukabiliana na mazingira yake ya kwao Manzese? Ukienda kwenye hizi sijui mnaita St. Said au Mhogo mchungu academy huko nako mambo si mambo, wanaandaa kasuku, wanajua kuongea sana na wameharibika kitabia kuliko hata wamarekani weusi wenyewe. Binafsi naamini kuwa mfumo wa elimu aliotuachia Nyerere ulikuwa na uhalisia kwa kiwango kikubwa kuliko huu wa sasa ambao unaandaa kasuku na ni wa kila mtu na lwake. Huku suala la uzalendo likiwa limefutwa kabisaaaaaaaa. Mfumo wa nyerere ulikuwa na michepuo na mimi nimemaliza form four najua jinsi ya kulima mboga mboga na matunda ikiwa ni pamoja na matumizi sahihi ya mbolea na viwatilifu. Leo form four wa sekondari ya kata ndiyo kwanza akimaliza tu anajiona hafanani na wenzake kijijini hivyo anastahili kwenda kuishi mjini ambako wala hajawahi kufika
 
Kwani wahandisi wa Dar Tech nao wana shida ya ajira?, teh teh teh?!!
Anyway, ushauri wangu mdogo ni kuwa kama ingewezekana kuunganisha nguvu na kuweka mikakati ya kujiajiri kadri fani zinavyoruhusu. Maana inakuwa rahisi kupata kazi kama third parties in some of these companies when opportunity arises kuliko kuwa na permanent employment.
Kuna vitu vingi vya kitaalamu bado havijaguswa au kufanywa hata kwetu. Ila inataka watu wajue mwanzo sio lelemama...itabidi kujituma sana.

ha! ha! ha! Nimejalibu kuweka pembeni u-sisi na wao kwenye suala hili kaka Ndahani.
Hebu nielezee zaidi Urahisi wa kupata kazi kama third parties kwenye haya makampuni ulivyoeleza sijakupata ipasavyo.
 
ha! ha! ha! Nimejalibu kuweka pembeni u-sisi na wao kwenye suala hili kaka Ndahani.
Hebu nielezee zaidi Urahisi wa kupata kazi kama third parties kwenye haya makampuni ulivyoeleza sijakupata ipasavyo.

makampuni mengi sasa hivi yanapendelea kutoa kwa watu wa nje baadhi ya service wanazohitaji. Mfano kama kandarasi za ujenzi zilivyo ndani ya serikali, hata kwenye mashirika mengi binafsi, kandarasi hizo pia zipo. Na naona karibu maeneo yote kwa mfano IT, human resources especially kwenye kutafuta watu wanaotafutwa kwa ajiri ya kazi mbalimbali, kufanya kazi za usafi na ku handle labors wanaohitajika kwenye makampuni etc...ingawa upatikanaji wa kazi unaweza ukawa pale zinapotokea lakini zipo na huwa zinalipa sana...mwanzo mgumu na Kitu kingine kinachosumbua sana Tanzania ni imani watu wakikupa kazi utaifanya bila kuleta za kuleta. Maana wengi wanafikiri bado kuna shamba la bibi la kwenda kuchukua hela bila kuifanyia kazi.
Hata hivyo ile thread yako angalia isitumike kukubomoa,lol!
 
Back
Top Bottom