Tanzania: Tatizo la ajira kwa vijana ni kubwa sana, lisifanyiwe masihara! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania: Tatizo la ajira kwa vijana ni kubwa sana, lisifanyiwe masihara!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by JamiiForums, Nov 16, 2010.

 1. JamiiForums

  JamiiForums Official Robot Staff Member

  #1
  Nov 16, 2010
  Joined: Nov 9, 2006
  Messages: 5,095
  Likes Received: 2,241
  Trophy Points: 280
  Ukosefu wa ajira ni jinamizi jipya linaloikabili Tanzania na huenda ni kati ya vitu vyenye madhara kuliko kitu chochote unachoweza kufikiria.

  Takwimu za hivi karibuni zinasema karibu wanafunzi 70,000 wa vyuo vikuu huhitimu masomo yao na ni asilimia kumi tu ndiyo hufanikiwa kupata ajira.

  Je, wanafunzi walio bado vyuoni wanalijua hili? Serikali imejiandaaje na kuwa na lundo la wasomi wasio na ajira? Tunajua athari zake kwa siku za usoni? Wahitimu wameandaliwa kujiajiri?

  Tujadiliane!

  ==============
  ==================

  ==================

  ==================

  ==================

  ==================

  =================

   
 2. E

  Edes New Member

  #2
  Nov 17, 2010
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wapendwa WANAJAMII kwanza nawasalimu naomba mnipokee ni mpya ktk jukwaa hili nafahamika kama EDES. Napenda kusema ukosefu wa ajira unasababishwa na baadhi ya wenyenchi wasiyo specific analysis kuhusu uchaguzi wa viongozi.
   
 3. X

  XOXOQY JF-Expert Member

  #3
  Dec 8, 2011
  Joined: Feb 7, 2011
  Messages: 220
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Ukosefu wa ajira ni kirusi kipya kabisa na nadhani ni kati ya kirusi chenye madhara kuliko kirusi chochote unacho kifahamu wewe.Takwimu za hivi karibuni zinasema karibu wanafunzi 70000 wa vyuo vikuu huhitimu masomo yao na ni asilimia kumi tu ndiyo hufanikiwa kupata ajira.

  Je, wanafunzi wa vyuo ambao bado wako vyuoni wanalijua hili?

  Isije wakawa wanavimbisha vifuavyao huko wakijua mikazi ipo bwerere. Kama wewe umesha maliza chuo Unawashauri nini wasagalami wenzako,na nyie ambao bado mko vyuoni mnasemaje?
   
 4. M

  Mr Mayunga JF-Expert Member

  #4
  Dec 11, 2011
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 314
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Wanaoona mbali, wanasema ni bomu na litalipuka mda wowote.Haiwezekani mtu anaelimu anakaa miezi zaidi ya 6 bila kazi,kila kazi inataka experience hauoni hilo ni tatizo.

  Haya kwa wale ambao hawana elimu viwanda hamna mfano k'njaro,Moshi kulikua na kiwanda cha magogo na mgunia vimekufa.

  Vingeweza kuokoa jahazi kama vingefufuliwa,haya Bomang'ombe(HAI) ni moja kati ya miji inayokua kwa kasi lakini hamna kiwanda hata kimoja,pia sehemu nyingine nyingi
   
 5. m

  mziranda Member

  #5
  Dec 11, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ni kweli eti kila kazi inataka experience ina maana hapo hakuna maana ya kumaliza chuo sasa, yaani hawa jamaa sijui wanafikiriaga nn...mm nadhani ifike kipindi sasa mfumo wa watu kuajiriwa ubadilishwe kama mtu tayari ana ajira basi hakuna haja ya yy kuchukuliwa kwa ajili ya kufanya kazi sehemu nyingine
   
 6. s

  sosopi kapurwa New Member

  #6
  Dec 11, 2011
  Joined: Dec 11, 2011
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  we a finished cc youth, coz life litaendelea kuwa tight na hakuna miundombinu ya kutatua hili janga la ajili na weza kusema hili pia ni AJILA NI ADUI WA TAIFA.
   
 7. Sanja

  Sanja JF-Expert Member

  #7
  Dec 11, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 482
  Likes Received: 147
  Trophy Points: 60
  Eti wanadai tujiajiri, je kuna hayo mazingira ya kujiajiri kweli?
   
 8. b

  bkubwa Member

  #8
  Dec 12, 2011
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  ishu ya ajira tanzania kwa sasa ni kubwa kwa kifupi ni kiongozi mmoja ndiye analisemea hilo naye ni lowassa
   
 9. b

  bkubwa Member

  #9
  Dec 12, 2011
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  nawashauli wasomi wenzangu msichague kaz mim ni muhitimu wa sheria lakin ni afisa mtendaji nimeajiriwa na tamisemi
   
 10. Saint Elmo

  Saint Elmo Member

  #10
  Dec 13, 2011
  Joined: Dec 13, 2011
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani wana JF, watu wengi sana humu wanashauri na kusisitiza wahitimu wajiajiri. Hivi mtu unaweza kujiajiri kama ndio umemaliza chuo huna pesa za mtaji, benki ukienda unadaiwa dhamana kama vile hati ya nyumba.

  Huwezi kupewa mkopo kama huna kitu ambacho tayari umekianzisha na mkopo unakuwa kwa ajili ya kuiendeleza. Hivi mtu unawezaje kujiajiri katika mazingira haya wakati pesa ya nauli ya daladala na chakula kinakupiga chenga?

  And if you're lucky to get a loan, the interest is so high with a lot of strings attached. Do you guys really see the real picture?

  In my opinion, it is easy said than done. Those who sings this song, are you guys employed or entrepreneurs?

  Ushauri jamani!
   
 11. Mkare_wenu

  Mkare_wenu JF-Expert Member

  #11
  Dec 13, 2011
  Joined: Mar 11, 2011
  Messages: 1,709
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 145
  Hata mimi sikasapot hako ka wimbo,mtu kasoma Political Science/Sociology then anashauriwa ajiajiri teh teh.
   
 12. m

  mr.kifather Member

  #12
  Feb 11, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 83
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  "maisha magumu vijana hatuna ajira" kauli hii imedumu kwa miaka hamsini ya uhuru.......vijana tufumbue macho na kuchagua viongoz miamba wenye uwezo...... tusikubali propagada na kupoteza vote zetu kwa mafisadi
   
 13. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #13
  Feb 11, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Yes, vijana tunaweza kufanya changes.
  Vijana tunaweza kuwatoa hawa ******* waliotuletea maisha magumu.
  Vijana tuamke, vijana tubadilike!
   
 14. Fasta fasta

  Fasta fasta JF-Expert Member

  #14
  Feb 11, 2012
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 620
  Likes Received: 114
  Trophy Points: 60
  Kwa kweli hili suala linaniuma sana kiasi nikimwona kiongozi yeyote wa serikali ninatamani kumrukia, jinsi wanavyowadanganya hawa vijana bila kuwajali. Vijana ambao hawana ajira wanateseka mpaka wanatia huruma. Kuna kijana mmoja akikosa kupanda Dala dala ambayo anakopa analipa anapo pata hatoki nyumbani. Leo hii ukimkuta kijana ukimuuliza unakwenda wapi anaweza kukutukana kwa sababu hajui ataipata wapi rizki siku hiyo.

  Mimi ninashindwa kuelewa hawa watu wanashindwa vipi kutengeneza ajira kwa ajili ya hawa vijana wakati walijitahidi sana kugombania kuuza viwanda vyetu. Mimi sikuona sababu ya kuuza au kubinafsisha viwanda vyetu, ila walikuwa wakamatwe waliokuwa wanaviendesha. Sasa walikaa na kugawana mali za watanzani leo hii wanatuona sisi ni wajinga.
   
 15. Desteo

  Desteo JF-Expert Member

  #15
  Feb 11, 2012
  Joined: Jul 27, 2011
  Messages: 448
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  to hell with ajira. Kila siku mnawaza tu kuajiriwa? It has been said if one door is closed, many more are open. Fungueni macho vijana na tujiajiri. Inashangaza kwa mfano mtu anasoma cpa kwa miaka 5! Unatafuta nini? As far as opportunity cost is concerned, huo muda wa kusubiri kuajiriwa ungeu convert kwenye kuwaza kujiajiri ungekuwa mbali
   
 16. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #16
  Feb 13, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  [FONT=&amp]Wahenga walisema palipo na miti hapana wajenzi, ni vigumu kujua mtunzi wa methali hiyo alikuwa na maana gani lakini walimu wengi wa Kiswahili huitafsiri kuwa "palipo na mali hakuna watu wa kuweza kuitumia (utilize)".

  Na ukiangalia katika dunia ya sasa ni kitu ambacho kikowazi kwa sababu kwani mataifa mengi yaliyoendelea sio kwamba yote yana mali asili za kutosha ukilinganisha na Tanzania. Rejea thread hii https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/223192-secrets-of-nations.html

  [/FONT][FONT=&amp]Tanzania ni kati ya nchi chache duniani zilizojaliwa na mali asili za kutosha na kila aina. Mfano ardhi yenye rutuba, madini, hali nzuri ya hewa, mito na maziwa yenye samaki, wanyama pori na milima ya aina mbali mbali ambavyo hivyo vyote ni vivutio vya watalii.

  Kama vingetumika vema Taifa lingejipatia pato la kutosha kuendeleza shughuli za kiserikali pamoja na jamii kwa ujumla, lakini kwetu hali ni tofauti, tuna matatizo mengi hata zaidi ya Nchi ambazo hawana kitu chochote, na tatizo kubwa linalolikabiri Taifa kwa sasa ni ajira kwa vijana.[/FONT] [FONT=&amp]

  Kwa mtazamo wa haraka haraka tunaweza kugawa sababu zinazosababisha hali hii katika makundii mawili. Kundi la kwanza ni zile sababu zote zinazosababishwa na serikali kutokana na sera zake butu juu ya swala hili, mfano mzuri ni mfumo wa elimu.

  Elimu ya Tanzania ina mapungufu ya kutosha, hii ni kwa sababu kijana anapomaliza elimu ya sekondari ambayo ni ya msingi kabisa, huwa hana ujuzi wowote wa kazi.

  Kwa sababu sio wote anaopata nafasi ya kuendelea na elimu ya juu, hii inasababisha kundi kubwa la vijana kurundikana mitaani,na kuleta athari zingine kama ubakaji, uporaji, madawa ya kulevya[/FONT] .

  [FONT=&amp]Na sababu nyingine, ni zile zinazosababishwa moja kwa moja na jamii ya watanzania wenyewe. Katika moja yaa hotuba zake, Mh. Mkapa aliwahi kusema, "Watanzania wasingoje serikali ifanye kila kitu, wanalo jukumu la kujiletea maendeleo wenyewe".

  Ni sahihi kusema kwamba baadhi ya vijana hawapendi kujituma ili kujikomboa na umasikini, zaidi ya kulaumu na kuishia kuomba kuomba.[/FONT] [FONT=&amp]Lakini Je, wale walioamua kujishughulisha wanasaidiwa vipi?

  Kuna tatizo la kutowapatia msaada (support) vijana hasa wanapo anziasha vikundi vidogo-vidogo kwa ajili ya kujiajiri wenyewe. Wataanza kufuatiliwa juu ya ushuru ambao sio halari bali ulio kwa ajiri ya masilahi ya wachache tu wakati kuna mashirika na viwanda vikubwa ambavyo hawalipi ushuru[/FONT][FONT=&amp]. [/FONT][FONT=&amp]

  Vijana hawa walioamua kujiajiri wengi wao hawakopesheki na wanaokopesheka hawawezi kumudu riba zinazotozwa na taasisi za kifedha. Kuna Mabenki lukuki yanatoa mikopo ila tatizo ni viwango vya riba, viko juu sana.

  Sasa jiulize ni biashara gani ambayo ni productive kiasi kwamba hao vijana wanaweza kupata hiyo riba na bado kubakia na kiasi fulani kwa ajiri ya kuendeleza miradi yao?[/FONT]

  [FONT=&amp]
  Jambo la kushangaza ni kwamba serikali imeshindwa kuanzisha vyanzo vya ajira kwa vijana,Tanzania tuna ardhi kubwa ya kutosha na yenye rutuba jambo la msingi ni kuanzisha Plantation and Agro-based Industries (huko site wanaona wanaopewa kipaumbele ni wawekezaji wa nje tu).

  Kwani viwanda vingapi vidogo vidogo tunaweza kuanzisha kwa mazao tunayozalisha na kuuza kwa Nchi jirani? Au ni ajira ngapi tunaweza kutengeneza kama tukianzisha viwanda hivyo, lakini serikali haioni hilo zaidi ya hapo ina-imports kila kitu na hii mpaka toothpick tena baada ya miaka hamsini ya uhuru. Hii ni aibu[/FONT] .

  [FONT=&amp]Wakati haya yakiendelea bado tunashuhudia wimbi kubwa la kulundikiana vyeo kwa mtu mmoja kana kwamba hakuna watu wengine wenye uwezo. Bado tunashuhudia wastaafu waliopata pesheni zao wakirudi makazini wakati vijana wapo na hawaajiriwi.

  [/FONT][FONT=&amp]Huko serikalini, w[/FONT][FONT=&amp]apo waliosema tatizo hili ni bomu "Ni bomu ambalo likiachiwa bila kushughulikiwa ipasavyo, litakuwa chanzo kikubwa cha kuyumba kwa nchi zetu zote," Rais Kikwete alipata kuwaambia viongozi wenzake.

  Sasa kama janga hili limeshajulikana ni Bomu kuna haja ya kusubiri lilete machafuko? [/FONT]
  [FONT=&amp]Je nini kifanyike?[/FONT]
   
 17. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #17
  Mar 24, 2012
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  Hili swala la ajira kwa kuwa haba kwa vijana lilitakiwa kupewa kipaumbele tangia tunapata uhuru. Kenya sasa unemployment rate ni 40% Botswana 35% Ivory Cost, Ghana na Nigeria nazo zimepiga hatua kali kutatua tatizo hili la ajira na ukosefu wa kazi kwa vija na wao hakuzidi 40%.

  Lakini hapa tanzania unemplyment rate ni zaidi ya 85%. Hii sio utani wananchi wetu wapo pabaya kimaisha na hawana uhai. katika mikoa 32 ya Tanzania , mikoa inayotoa ajira ni Dar Es Salaam, Arusha, kilimanjaro, mwanza na Mbeya tuu lakini mikoa mingine yote hakuna hata viwanda wala shughuli za kuajili watu.

  Awamu ya kwanza ya utawala ndio yenye kubeba mzigo wote huu wa lawama na sio mtu mwingine yeyote. Hiyo awamu ilikuwa inadanganya uuma kuwa tanzania ni nchi ya wakulima na wafanyakazi. hao wakulima walikuwa sio wakulima wa kujilisha bali ni kuganga njaa tuu ili hali wakitafuta kazi za ajiraya kudumu kujikimu maisha yao. wakija mjini kutafuta kazi walikuwa wanaitwa wazururaji n awakibaki vijijini walikuwa wnaitwa wakulima.

  Siasa yetu ya mabo ya nje ni imechangia sana kurundika vijana mitaani bila ya ajira. Hii siasa ya kumchukia mmarekani na myurope wakipanua mitaji yao ndio chanzo cha kutopata wawekerezaji wa maana kututatulia swala la ajira,. Israel ina viwanda mamilion na imewekeza sana Kenya, Botswana na Ghana na nchi za asia mashariki kama Taiwan, singapole na malaysia. Sasa sisi hapa Tanzania eti hatutaki kufungua full ubalozi na Israel kwa sababu tuu ya wapalestina hawana Taifa. Sasas nani nakomolewa hapa kama sio vijana wetu kuzidi kukosa viwanda vya kuwaajiri?

  Serikali inakosa mamilion ya pesa kila mwezi kutokana na kodi ya P.A.YE kwa sababu vijana wengi hawana kazi. Azimio la Arusha lilikuwa sio kiboko cha mabepari bali ni chanzo cha kuwatia umasikini mkubwa watanzania. Nchi bila bepari ni sawa na mechi ya soka bila mpira. Kenya ina watu kama mengi wenye viwanda 125! Nigeria sasa ina mabepari wawili namba 6 wenje utajili duniani. Hawa ukiwa nao wengi nchi inakuwa na nafuu ya ajira kwa vijana.

  Kuweka kipaumbele maswala ya kukomboa africa,kusaidia wakimbizi na kkunga mkono wapalestina bila hata kujali swala la ajira kwa vijana ni kichekesho ambacho hata maiti anacheka!
   
 18. Mwigamba son

  Mwigamba son Member

  #18
  Apr 1, 2012
  Joined: Jan 11, 2012
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Habari wanajamii forums, kwa kuwa imeonekana wazi kwamba watanzania wengi kwa sasa wamesoma na nafasi za ajira zimekuwa ni haba. katika hili wengi wana mitazamo tofauti kuhusiana na namna ya kulishugulikia.

  Mara kadhaa suruhisho la walio wengi ni kuwa watu wajiajiri wenyewe bila ya kufahamu kuwa mitaji ni tatizo. Kwa mtazamo wangu nafikili kuwa ingekuwepo sheria inayoruhusu mtu kuajiriwa sehemu yeyote katika kipindi fulani hata kama ni miaka 5 kisha aachie ngazi na wengine wazikusanye kwa miaka 5 nao wapigwe chini na wengine pia waingie nao wapige kazi kwa muda wawaachie wengine.

  Kwani kwa kufanya hivyo mzunguko wa ajira utakuwepo mkubwa na kuondoa manung'uniko ya walio wengi. Nafikiri hapa wengi watakuwa na matumaini ya maisha kwani mitaji itapatikana na si mtu mmoja akalie utumishi toka tumezaliwa mpaka tumemaliza vyuo yeye bado yupo tu.

  Na mbaya zaidi ni pale unapokuta anahodhi nyadhifa nyingi kana kwamba watu wengine hawapo.
   
 19. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #19
  Apr 5, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Wakuu,nahisi EL anaogopa vijana watajiandikisha kupiga kura na wote ni cdm.anaona ni bomu linalo msubiri.nawasirisha
   
 20. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #20
  Apr 5, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Na litawalipua kweli ziko wapi ajira milion walizotuahidi?
  huyu bwana huwa simuelewi ni mpinzani ndani ya chama au mwanaharakati ndani ya chama au mpambanaji
   
Loading...