Tanzania: Soda plant will not harm Flamingos

halafu,ukiangalia sana hawa watu wanaopenda sana mazingira kuliko wananchi, utakuta ni wakenya. hebu tajeni uraia wenu hapa tuone. mnatupiga mchanga wa macho tu hapa. mbona wazungu hawana hata madini?wanakuja kuchuma madini huku na wameendelea kishenzi. wangekuwa wanalinda mazingira miaka hiyo ya industrial rev.si wangekuwa kama sisi. ona china, mazingira gani yanalindwa. MI NAONA TUENDELEE KUJENGA KILE KIWANDA. KAMA FLAMINGO WAKIFA BASI.KWANI TUNAWALA FLAMINGO BWANA?, kwanini tufe njaa wakati madini yapo?
 
Sidhani kwamba hiki ndicho kinachotokea.

Where did you get that impression?
We want to prevent the extinction of those flamingos for our benefit mainly, not just bird's.

Only if you knew how much and how many of the locals do benefit from tourism.
Nazungumzia faida wanayopata wazawa moja kwa moja, achilia mbali pato linaloingia serikalini
.

ASHAKUM SI MATUSI lakini niko kwenye process ya kumkoma nyani GILADI jf style...

Benefit wanayopata wazawa yenyewe ndio hii?

huyu mtalii yuko ZANZIBAR anasukwa nywele na dada zetu

ukisikia umasikini wa akili ya kutegemea utalii ndio huu

sexy-zanzibar-261.jpg
 
Last edited by a moderator:
Mradi huu endelee...na tukimaliza huu tuendelee na ule wa reli toka Moshi kwenda Mwanza tukimaliza tujenge airport ya kisasa kule Bagamoyo, tukimaliza tujenge highways za maana nyanda za juu tukimaliza tujenge Pemba ...yaani sisi tusiwasikilize hawa wendawazimu wanaopenda sana wanyama kuliko Binadamu

Bt the way nadhani kungekuwa na umuhimu wa kupanua ule mradi wa Kamba kule MAFIA

GM give me a brake, plz don't argue for the sake of argument. You know kiwanda has cycle. Ni muda gani kiwanda kitachukua kabla hakijafa? Jee ni analysis gani hawa jamaa wamefanya ambazo zinasababisha wewe ufikie decision la kujenga hicho kiwanda?

Umuhimu wa kufanya feasiability study kabla ya kufikia maamuzi ni very important hasa kwenye swala kama hili. Huwezi kujenga freeway ikakata katikati ya Ngorongoro eti sababu you want to compete with Kenya. Don't we have any other way to compete? Au we use this kind of cheap arguments to keep mabishano going and going?

Environment has effect on alot of things, kuanzia sisi wanadamu mpaka wanyama. Najua unaweza kusema who cares kuhusu wanyama. Lakini kumbuka ecosystem ina implication kubwa sana kwetu. You don't how small action can change everything.

We have other way around. Kama tukispend muda kuresearch.
 
ASHAKUM SI MATUSI lakini niko kwenye process ya kumkoma nyani GILADI jf style...

Benefit wanayopata wazawa yenyewe ndio hii?

huyu mtalii yuko ZANZIBAR anasukwa nywele na dada zetu

ukisikia umasikini wa akili ya kutegemea utalii ndio huu

sexy-zanzibar-261.jpg

Hawa watalii wanalala kwenye Hotel, zile hotel zimeajiri watu. Hao watarii wanapanda magari yale magari yanaendwesha na watu. Kuna vijana zaidi ya laki kazi yao kutembeza watalii tuu. Kuna travel agency na tours zaidi ya half million na zimeajiri watu.

Utalii unachangia uchumi wa zanzibar kwa asilimia kubwa sana, just spend muda itazeme ungaja anzia mashamba ya spiece mpaka zile hotel za dolla 500 a night. Utaona jinsi utalii unavyoifanya znz kuwa znz

Zanzibar uchumi wake unategee utalii kwa asilimia kubwa sana. Sasa wewe unaangalia in partial way.
 
maalim mmoja kati ya wazazi wangu ni muunguja so i know what i am talking about

hivyo naua sana kuhusu utalii Unguja na bila kusahau kuwa mmoja kati ya wazazi wangu ni mtu wa Mafia

hivyo ninapozungumzia fitna zinazofanywa na hawa watu wa mazingira i know what i am talking about

lakini that said looks like we can have a good discussion on the subject baadae
 
halafu,ukiangalia sana hawa watu wanaopenda sana mazingira kuliko wananchi, utakuta ni wakenya. hebu tajeni uraia wenu hapa tuone. mnatupiga mchanga wa macho tu hapa. mbona wazungu hawana hata madini?wanakuja kuchuma madini huku na wameendelea kishenzi. wangekuwa wanalinda mazingira miaka hiyo ya industrial rev.si wangekuwa kama sisi. ona china, mazingira gani yanalindwa. MI NAONA TUENDELEE KUJENGA KILE KIWANDA. KAMA FLAMINGO WAKIFA BASI.KWANI TUNAWALA FLAMINGO BWANA?, kwanini tufe njaa wakati madini yapo?

kidzogolae Bonfanche!

Kidogo hapa naona kizungu-zungu, sijui hata nini umezungumzia!!|/*&

Hebu isome kwa makini hiyo sentensi yako niliyoipigia mstari kisha uidadavue!

Ni kweli unafahamu vizuri huu mradi?????....ama unazungumzia ushabiki bila ya kufahamu!

Sababu unachokizungumzia hapa ni minus point: Nakunukuu tena " mbona wazungu hawana hata madini?wanakuja kuchuma madini huku na wameendelea kishenzi"

Umewapigia kelele wazungu na madini wanjenga kwao Kwa hiyo hawa wahindi wa Tata Chemical watakachokivuna hapo Natron wataendeleza Tanzania? Kwa taarifa yako mhindi yeyote huwa na urafiki na mtu kwa ajili ya maslahi tu! kufa uone kama atakuja hata kwenye huo msiba wako!

kama hufahamu huu siyo mradi wa Tanzania pekee, ni wa Tata Chemical Ltd - ya Mumbai India na Tanzani inashare kupitia Shirika la NDC-Lake Natron Resources Ltd. Mwenye mradi ni Tata Chemical na Lake Natron Resources Ltd ni kibaraka tu! anasubiri hawa magarbachori wajenge ndiyo Tanzania ijikombe kupata hako ka'mgao.

Zinduka Unauza Nchi yako, bila ya faida...bora hata kama mradi wote ungekuwa wa Tanzania, tungejua faida yote yetu lakini kumbe % kubwa inakwenda kwa mwenye mtaji, na huenda kama kawaida yetu atakuwa na miaka 10 ya kurudisha gharama za ujenzi wa mradi ndiyo aanze kulipa kodi.

Kama alivyosema Mkuu Fundi Mchundo, baada ya huo muda wakadai Kiwanda kimesimama baada ya mwekezaji kudai hakilipi kutokana na madai ya mishara mikubwa ya wafanyakazi.

Mnaanza tena Ufisadi ulitumika hapo! Ukielimishwa elimika!
Barabarache?
 
Umewapigia kelele wazungu na madini wanjenga kwao Kwa hiyo hawa wahindi wa Tata Chemical watakachokivuna hapo Natron wataendeleza Tanzania? Kwa taarifa yako mhindi yeyote huwa na urafiki na mtu kwa ajili ya maslahi tu! kufa uone kama atakuja hata kwenye huo msiba wako!

kama hufahamu huu siyo mradi wa Tanzania pekee, ni wa Tata Chemical Ltd - ya Mumbai India na Tanzani inashare kupitia Shirika la NDC-Lake Natron Resources Ltd. Mwenye mradi ni Tata Chemical na Lake Natron Resources Ltd ni kibaraka tu! anasubiri hawa magarbachori wajenge ndiyo Tanzania ijikombe kupata hako ka'mgao.

Zinduka Unauza Nchi yako, bila ya faida...bora hata kama mradi wote ungekuwa wa Tanzania, tungejua faida yote yetu lakini kumbe % kubwa inakwenda kwa mwenye mtaji,

Big applause man!
 
maalim mmoja kati ya wazazi wangu ni muunguja so i know what i am talking about

hivyo naua sana kuhusu utalii Unguja na bila kusahau kuwa mmoja kati ya wazazi wangu ni mtu wa Mafia

hivyo ninapozungumzia fitna zinazofanywa na hawa watu wa mazingira i know what i am talking about

lakini that said looks like we can have a good discussion on the subject baadae

Mheshimiwa GT

Siamini na wala sina uhakika kama kunafitina yoyote inayofanywa na watu wa Mazingira; kama unaushahidi ni vyema ukauweka ukumbini ilinasi tujionee, lakini vinginevyo utakuwa unaasili ya kibaguzi!

Kwa Mfano kwenye hili la Lake Natron, "Mr.Lota Melamari, the CEO of the Wildlife Conservation Society of Tanzania (WCST, BirdLife in Tanzania) presented a strong case for the complete abandonment of the project in a presentation entitled "Flamingos of Lake Natron, a Tanzanian Treasure". In his talk, Lota described Natron’s vast flocks of shimmering pink flamingos as one of the world’s greatest wildlife attractions. “This resource must not be destroyed”, said Lota

Huyu Mzee Lota ni Mmasai tena huenda katokea Wilaya hiyohiyo ambako mradi unakusudiwa kuanzishwa, mbona anaupinga huo mradi? kama ungekuwa unamanufaa si'ndiye angekuwa wa kwanza kutaka Uanzishwe? huyu utamuweka upande gani kwa fikira zako? ..mzalendo, kibaraka wa wakenya au....

Msipende sana kuiga-iga kila inachokifanya kenya na sisi tufanye...KBC...TBC1 instead of TVT, Magadi Plant...Lake Natron Resources Ltd, jifunzeni kubuni vitu vyenu!
 
halafu,ukiangalia sana hawa watu wanaopenda sana mazingira kuliko wananchi, utakuta ni wakenya. hebu tajeni uraia wenu hapa tuone. mnatupiga mchanga wa macho tu hapa. mbona wazungu hawana hata madini?wanakuja kuchuma madini huku na wameendelea kishenzi. wangekuwa wanalinda mazingira miaka hiyo ya industrial rev.si wangekuwa kama sisi. ona china, mazingira gani yanalindwa. MI NAONA TUENDELEE KUJENGA KILE KIWANDA. KAMA FLAMINGO WAKIFA BASI.KWANI TUNAWALA FLAMINGO BWANA?, kwanini tufe njaa wakati madini yapo?

Kwa hiyo,Mkuu, mtu yeyote anayepingana na wewe ni mKenya? Basi iko kazi! Unapozungumzia wazungu una maana wakina nani? Wamarekani si wazungu?Unapozungumzia madini una maana gani? Makaa ya mawe na chuma si madini? Au unadhani madini ni dhahabu na almasi tu? Kwa maelezo yako, maendeleo ya ulaya yalichangiwa kwa kiasi kikubwa na matumizi ya makaa ya mawe na chuma. Hiyo industrial revolution inayukuchanga ilikuwa na gharama kubwa kwa maisha ya wananchi wao! Pollution na misongamano ya watu katika miji ilileta madhara makubwa. Sasa hivi utajiri wao hautokani na viwanda. Ni services, ikijumuisha na utalii ambao limbukeni kama wewe mnaubeza!

Wachina nao wameanza kuvuna walichokipanda. Haya matetemeko yanayowakumba sio bure. Gharama ya 3 Gorges dam bado haijajulikana. Na wao pia wameanza kuangalia gharama za athari katika mazingira.

Wanaopiga kelele kuhusu mazingira ni wale walioona madhara yake kwao na wanajaribu kutuasi kuwa si lazima turudie makosa yao. Lakini kama wahenga walivyosema, mtoo akililia wembe.......mpe. Tukumbuke hata hivyo kuwa hiyo, global warming wanayoizungumzia vichaa hao itakuwa na madhara makubwa zaidi kwetu kuliko kwao!
 
maalim mmoja kati ya wazazi wangu ni muunguja so i know what i am talking about

hivyo naua sana kuhusu utalii Unguja na bila kusahau kuwa mmoja kati ya wazazi wangu ni mtu wa Mafia

hivyo ninapozungumzia fitna zinazofanywa na hawa watu wa mazingira i know what i am talking about

lakini that said looks like we can have a good discussion on the subject baadae

Yale yale ya kuishiwa hoja!

Kwa hiyo kwa sababu mmoja wa wazazi wako ni muunguja kwa hiyo ushakuwa mtaalam wa masuala ya unguja! Kwa mtazamo huo Barack Obama ameshakuwa mtaalam wa masuala ya Kenya.

Conveniently, vile vile mzazi wako mwingine ni mtu wa Mafia! Kwa hiyo athatri ya miradi kama ya Marine Park iliyowazuia wamafia na wenzao kutumia uvuvi wa baruti unaijua! Unaamini vilevile kuwa sasa hivi kisiwa hicho kitaukata kutokana na mradi wa ukulima wa kamba ambao warufiji kwa upuuzi wao waliukataa! Iko kazi. Wakina Abunuwasi kumbe mko wengi!

Lakini kwa nini tuandikie mate wakati ushasema kuwa utamwaga ushahidi humu kwa mtindo maarufu wa kumkoma nyani whatever! Tunasubiri, Mkuu. Fanya kweli.
 
Lakini kwa nini tuandikie mate wakati ushasema kuwa utamwaga ushahidi humu kwa mtindo maarufu wa kumkoma nyani whatever! Tunasubiri, Mkuu. Fanya kweli.

Usikute ndo ile picha alotuletea, I hope not.
Nategemea mtu atuambie,

"eebwana information mlizotuletea kuna makosa hapa."​
Au,
"Mapungufu kwenye Environmental and Social Impact Assessment (ESIA) Report mbona sio kweli"
Au labda,
"Tundu Lissu kwenye hiyo document hapo juu kasema hivi, napendekeza marekebisho haya".​
Au pengine,
"Huko Kenya tunakoelezwa kutizama, mbona mambo ni kinyume na wanavyotaka tuamini, na ushahidi uko kwenye website fulani"​
...or something of that sort.

If we try to avoid doing the easy part of TALKING, but READ what is before our very eyes for our own sake, ni namna moja ya kuwaunga mkono akina Tundu Lissu!

.
 
ASHAKUM SI MATUSI lakini niko kwenye process ya kumkoma nyani GILADI jf style...

Benefit wanayopata wazawa yenyewe ndio hii?

huyu mtalii yuko ZANZIBAR anasukwa nywele na dada zetu

ukisikia umasikini wa akili ya kutegemea utalii ndio huu

sexy-zanzibar-261.jpg

Sidhani kwamba hiki ndicho kinachotokea.

Where did you get that impression?
We want to prevent the extinction of those flamingos for our benefit mainly, not just bird's.

Only if you knew how much and how many of the locals do benefit from tourism.
Nazungumzia faida wanayopata wazawa moja kwa moja, achilia mbali pato linaloingia serikalini.

Lazydog said:
If we try to avoid doing the easy part of TALKING, but READ what is before our very eyes for our own sake, ni namna moja ya kuwaunga mkono akina Tundu Lissu!

Wanasema "Practice What You Preach" au sio!?
I bumped into this today :)
See below

Nasikitika kuona logic ya Mzee ES imekuwa tena ya wasiwasi. Tunataka kuvutia watalii wengi kwa faida yetu, sio kwa faida ya hao watalii. Mwaka jana, tulipata watalii laki sita, na waliingiza fedha za kigeni $700 million. Mazao ya kilimo yaliingiza chini ya $500 million.

Mzee ES, iweje ukemee watu kuishi na mbuzi na kuku na huku unataka tuendelee kukazania majiko ya mafuta ya taa? Inabidi kukumbatia mabadiliko ya kuleta maendeleo moja kwa moja, sio nusu nusu. You cannot be a little bit pregnant.

Mzee wa kijiji anasema haiwezekani kuleta maendeleo kwa kutegemea utalii na madini. Mbona Misri imeleta maendeleo (relatively) kwa kutegemea utalii? Nguvu ya uchumi wa Kenya ni utalii. Mwaka huu, Kenya wanatarajia watalii 1.8 mil. That should bring in about $2.5 billion. Yaani Kenya itaweza kuingiza zaidi ya nusu ya fedha za bajeti yote ya tanzania kwa njia ya utalii peke yake.

Inabidi tulime, kwani kama alivyosema Mwalimu, tusipolima tutakufa. Lakini, ili kupata fedha nyingi za kigeni, inabidi kukazania zaidi utalii. Utalii ndiyo sekta yenye uwezo mkubwa kuliko zote Tanzania, wa kuingiza fedha nyingi za kigeni.

Nashauri msome vile vile hii paper kuhusu bajeti ya kilimo (2006) ambayo imeandikwa na mtaalamu wa SUA. Iko hapa:

Augustine Moshi

SOURCE: Tanzania Tunayoitaka
 
Asante Wakuu Lazydog na Augustine Moshi!

Moja ya biashara kubwa huko ulaya tunakokuonea gele ni utalii! Nchi za ufaransa, italia, Spain (na visiwa vyake vya Canary), Portugal, uingereza, marekani,n.k. zinaupa utalii kipaumbele maana si tu unaongeza pato la nchi bali linatoa ajira kwa sehemu kubwa ya wananchi!

Logic za GT na kidzogolae, zinanikumbusha wale wakina dada wa mtaa wa Ohio, Jolly, Kinondoni, Uwanja wa Fisi, kwa macheni na sehemu nyingine kama hizo, ambao wakiaswa kuangalia upya biashara yao kwa sababu ya huu ugonjwa wa kisasa, huwa wanajitetea kwa kusema ni lazima waishi leo na kama kufa si kila mtu anakufa! Yanapowapata ndipo wanapojutia lakini wakati wako bomba na wateja kibao, athari za baadaye zinaonekana kama mirage tu! Au ndugu zetu wa kusini wanaochoma mpingo kutengenezea mkaa maana mkaa wake safi sana! Au wa Lushoto na Tukuyu waliokata misitu na leo wanasumbuliwa na malaria(ambayo haikuweko zamani), hali ya joto na ukame! Au wa Bagamoyo anayeachia maghofu ya kale yaanguke ili auze kifusi kwa wanaojenga Mji mpya!

Na bado waheshimiwa wanakazania kuganga njaa? Ati tunaowapinga ni waKenya kwa hiyo hatuna mapenzi na nchi yao! Na tusijidanganye, tukishaharibu ni vigumu kama sio impossible ku'reverse' na kurudia hali ya baadae.

Kweli sikio la kufa................

Amandla!
 
maalim mmoja kati ya wazazi wangu ni muunguja so i know what i am talking about

hivyo naua sana kuhusu utalii Unguja na bila kusahau kuwa mmoja kati ya wazazi wangu ni mtu wa Mafia

hivyo ninapozungumzia fitna zinazofanywa na hawa watu wa mazingira i know what i am talking about

lakini that said looks like we can have a good discussion on the subject baadae

I want you to explain how utalii cripple Unguja Economy. Labda you need facts concern the cornerstone of Unguja Economy.

I am more than happy kufanya discussion kuhusu ili swala, sababu i know more than one family zinaishi kwa biashara ya utalii. I have a friend own Maya tours, naongelea biashara ninayoijua. So, bring facts.
 
It says the lesser flamingo could become extinct in five years if its habitat is destroyed. Paul Matiku of Nature Kenya said the death of the rare birds would put regional tourism earnings at risk.

Sometimes nashindwa kuelewa jinsi tunavyofanya mambo na kufikiri. The big picture ambayo viongozi wetu hawaioni ni ile long term cost ya project nzima.

TUnasema tunataka tujichimbie magadi yetu wenyewe ili tupunguze bei kwa asilimia 30%.

Lakini tuko tayari kuua kianzi kikubwa cha utalii na mazingira ambayo yanauwezo wa kuingia Taifa pato asilimia 500% zaidi ya manufaa ya kuchimba haya magadi!

Hata nikisema kuwa labda kuna manufaa flani, haya magadi yatasaidia vipi viwanda vyetu ikiwa asilimia kubwa ya bidhaa zitakazozalisha kwa kutumia magadi haya bado vinaagizwa kutoka nje?

Ni lini mara ya mwisho ulitumia sabuni ya mbuni na si kukimbilia "omo"?
 
Political considerations
• The Government of Tanzania signed the Convention on Wetlands of International Importance especially as Waterfowl Habitat (the Ramsar Convention), and listed Lake Natron as a Ramsar Site. Contracting Parties are required to take all necessary measures to safeguard the integrity of such sites.

• Lake Natron has been designated as an Important Bird Area – a site of global significance for bird conservation – by BirdLife International.

• Tanzania is a signatory to the Convention on Biological Diversity (CBD), the Bonn Convention on Migratory Species (CMS), and the CMS Agreement on the Conservation of African-Eurasian Migratory Waterbirds (AEWA). These agreements require signatories to seek consensus from neighbouring states in the management and development of shared ecosystems. Other Eastern African states have not been consulted and involved in the proposal process.

Savimbi,

Umesahau kuwa Serikali yetu ni "kihiyo" mkubwa sana na hiii ilikuwa ni safari ya kwenda kununua suti na TV mpya na si kuingia kwenye mkatabawa kulinda mazingira?

I curious to know who represented usas country kwenye kusaini hii mikataba na makubaliano ya kimataifa. Je alikuwa waziri wa mamb o ya nje, waziri wa utalii, waziri wa mazingira au...?
 
Ni lini mara ya mwisho ulitumia sabuni ya mbuni na si kukimbilia "omo"?

..babu,mbuni inatumika sana tu,tena inatafutwa hasa.

..halafu,mbuni na omo matumizi yanapishana kidogo;huwezi ogea omo!

..anyways,tukirudi kwenye hoja. kenya wao wameharibu mazingira kwa kiasi gani? what's the best practice kwenye kitu kama hii?
 
Mambo mengine yanachekesha kama sio kuchefua
Hapo juu waziri amesema,

Ili kwamba wasiwa-disturb flamingos

Bottom line ni kuwa viongozi wetu na Watanzania hatujui kusema nitakujibu baadaye ngoja niende tafakari. Hawa jamaa walipomfuata Maghembe alikubali mara moja kwa kuwa anaona kuwa tutapata kipato.

Lakini hakuna nayezungumzia gharama halisi. Long term hata kama kiwanda kitajengwa Kilometa 32, bado kuna polution ya hewa na hata underground water kwa zile industrial waste.

Ajira yenyewe itakuwa kwa watu 100! Watanzania tu wavivu wa kufikiri sana. Sasa kama tungeendelezahapo ziwani na kulifanya liwe kivutio cha utalii, basi tungeweza pata hata ajira 1000.

Sisi tunaona kila kitu ni lazima kifanyike, tukifuatwa tukaambiwa tunataka kujenga gorofa la gorofa 100 pale Serengeti, tutakubali haraka harama maana litakuwa jengo refu Afrika nzima! Tunasahau kuwa wale wanyama wote watakimbia na kutafuta mahala papya na hivyo utalii wetu kufa!
 
Mambo mengine yanachekesha kama sio kuchefua
Hapo juu waziri amesema,

Ili kwamba wasiwa-disturb flamingos

GM give me a brake, plz don't argue for the sake of argument. You know kiwanda has cycle. Ni muda gani kiwanda kitachukua kabla hakijafa? Jee ni analysis gani hawa jamaa wamefanya ambazo zinasababisha wewe ufikie decision la kujenga hicho kiwanda?

Umuhimu wa kufanya feasiability study kabla ya kufikia maamuzi ni very important hasa kwenye swala kama hili. Huwezi kujenga freeway ikakata katikati ya Ngorongoro eti sababu you want to compete with Kenya. Don't we have any other way to compete? Au we use this kind of cheap arguments to keep mabishano going and going?

Environment has effect on alot of things, kuanzia sisi wanadamu mpaka wanyama. Najua unaweza kusema who cares kuhusu wanyama. Lakini kumbuka ecosystem ina implication kubwa sana kwetu. You don't how small action can change everything.

We have other way around. Kama tukispend muda kuresearch.

Mtanganyika,

Watanzania tumesahau sana jinsi Jute ilivyohatarisha mapato ya Taifa kutokana na mauzo ya katani.

Wenzetu kila siku wako kwenye medani za kutafuta environmental friendly substitute product. Ndio maana wajenga magari wanajenga injini kutumia aluminium na si steel. Kuna nano technology na uvumbuzi mwingine mwingi hata GMO ambayo sikubaliani nayo.

Sisi tunakimbilia kujenga mradi ambao utakufa in 10 years.

Tuwauliwe wao NDC what happened to Kiwira? mbona makaa ya mawe bado yapo na hatuyatumii?

What happened to SPM Mgololo? Viberiti Moshi na upupu wa mashirika na viwanda ambavyo vilikuwa chini ya NDC?

Sasa kama watashindwa kutupa tathmini ya faida zilizopotea, kuna faida gani kuvuna magadi kwa miaka 10, kisha tukabakia na magofu na kurudi kule kule kuagiza kutoka nje au kutumia substitue products?
 
Bottom line ni kuwa viongozi wetu na Watanzania hatujui kusema nitakujibu baadaye ngoja niende tafakari. Hawa jamaa walipomfuata Maghembe alikubali mara moja kwa kuwa anaona kuwa tutapata kipato.

Lakini hakuna nayezungumzia gharama halisi. Long term hata kama kiwanda kitajengwa Kilometa 32, bado kuna polution ya hewa na hata underground water kwa zile industrial waste.

Ajira yenyewe itakuwa kwa watu 100! Watanzania tu wavivu wa kufikiri sana. Sasa kama tungeendelezahapo ziwani na kulifanya liwe kivutio cha utalii, basi tungeweza pata hata ajira 1000.

Sisi tunaona kila kitu ni lazima kifanyike, tukifuatwa tukaambiwa tunataka kujenga gorofa la gorofa 100 pale Serengeti, tutakubali haraka harama maana litakuwa jengo refu Afrika nzima! Tunasahau kuwa wale wanyama wote watakimbia na kutafuta mahala papya na hivyo utalii wetu kufa!

..watanzania tungekuwa imara kwenye masuala ya uchafu mijini na mipango miji tungefaidika zaidi na huo utalii.

..hili hatulishikii bango. tuna-nag kile ambacho hata hakijaanza na kimewekewa masharti kibao kuhakikisha watu hawafanyi mzaha.
 
Back
Top Bottom