Tanzania sio nchi masikini: Kila Idara ya serikali fedha zinachotwa

Msharika

JF-Expert Member
May 15, 2009
947
69
MHASIBU Msaidizi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam, Amos Kabisa, maarufu kwa jina la Angaya amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kusomewa mashitaka matatu likiwemo la wizi wa sh milioni 330.

Kabisa amesomewa mashitaka leo, alipelekwa Kisutu juzi na jana lakini hakusomewa madai hayo yanayomkabili.

Wakili wa Serikali, Epafras Njau, amedai mahakamani kuwa, mshitakiwa huyo alikula njama ya kutenda kosa, kughushi na akaiba fedha hizo mali ya benki ya NMB.

Njau amedai kuwa, Januari 21 mwaka huu katika benki hiyo iliyopo katika jengo la Bank House, mshitakiwa aliiba fedha hizo.

Imedaiwa kuwa, mshitakiwa huyo pia alighushi nyaraka za benki katika akaunti namba 2011000015 ya Jeshi la Polisi akionesha kuwa ni sahihi, na zilikuwa ni halali.

Wakili Njau aliiomba mahakama isimpe dhamana mshitakiwa na akatoa zuio la dhamana lililotolewa na Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP) chini ya kifungu cha sheria namba 1148 (4) cha mwenendo wa makosa ya jinai.

Mahakama ilikubaliana na ombi hilo, mshitakiwa amerudidishwa rumande hadi kesi hiyo itakapotajwa machi 10 mwaka huu.
 
Msharika - hiyo ni kweli kabisa. Kila nikisikia nchi za magharibi zinatoa msaada kwa Tz hucheka sana mie.

¬K
 
Back
Top Bottom