Aliyejipatia mkopo milioni 350 ahukumiwa kifungo cha nje

101 East

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
1,040
2,121
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemhukumu Mkurugenzi wa Mikocheni Shopping Mall Ltd, John Kyenkungu (67) kifungo cha nje cha miezi 18, baada ya kupatikana na hatia ya kughushi nyaraka na kujipatia mkopo wa TZS milioni 350 kutoka benki ya Equity.

Upande wa mashtaka umesema utakata rufaa kwani haujaridhishwa na adhabu hiyo.

HT: Mwanachi

=========

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemhukumu Mkurugenzi wa Mikocheni Shopping Mall Ltd, John Kyenkungu (67) kifungo cha nje cha miezi 18, baada ya kupatikana na hatia ya kughushi nyaraka na kujipatia mkopo kutoka Benki ya Equit wenye thamani ya Sh350 milioni.

Pia, mahakama imeelekeza hati iliyotumika kuchukulia mkopo, irudishwe Mikocheni Shopping Mall Ltd, ambao ndio wamiliki wa hati hiyo kwa sasa.

Kyenkungu ambaye ni mfanyabiashara pia, anadaiwa kughushi nyaraka mbalimbali ikiwemo muhtasari wa kikao cha bodi, fomu ya kusajili hati ya kiwanja na kughushi dhamana ambayo inatolewa na taasisi ya fedha.
Mshtakiwa anadaiwa kughushi nyaraka akionyesha kuwa mmoja wa wamiliki wa Mikocheni Shopping Mall Ltd, na kwamba Said Nassoro ameridhia achukue mkopo benki wenye thamani hiyo kwa kuweka dhamana ya kiwanja chao, jambo ambalo akijua ni uongo na wala Nassoro hajawahi kiridhia.

Hukumu hiyo imetolewa leo Juni 30, 2023 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Evodia Kyaruzi wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya hukumu.

Hata hivyo, upande wa mashtaka ukiongozwa na wakili Tumaini Maingu, umedai kuwa haujaridhishwa na adhabu iliyotolewa dhidi ya mshtakiwa huyo, hivyo wanakata rufaa kupinga adhabu hiyo.

Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Kyaruzi amesema kulingana na ushahidi uliotolewa mshitakiwa amekutwa na hatia katika mashitaka yote manne yaliyokuwa yanamkabili.

Amesema kutokana na umri wa mshitakiwa kuwa mkubwa na hali yake ya afya Mahakama imeamua kumpatia adhabu hiyo ambapo atakuwa akiitumikia jamii kwa kufanya kazi za kijamii ndani ya muda huo chini ya maofisa jamii, ambao wataandika ripoti na kuiletea mahakamani, baada ya kumaliza kutumikia kifungo hicho.

"Mahakama imezingatia kifungu namba 339A cha Sheria ya Makosa ya Jinai (CPA) ambacho kinazungunzia mahakama kumpa mshtakiwa adhabu yenye unafuu, kama alivyoomba wakati wa utetezi wake," amesema Hakimu Kyaruzi.

"Hivyo mahakama hii inakuhukumu kifungo cha nje cha miezi 18 ambapo atapangiwa kuhudumia jamii na anatakiwa kufuata masharti kwa kazi alizopangiwa na akikaidi ataletwa mahakamani hapa," amesema Hakimu.

Awali, kabla ya kutolewa adhabu hiyo, Wakili Maingu aliiomba Mahakama itoe adhabu kali dhidi ya mshtakiwa huyo kwa kuwa ameleta madhara kwa mlalamikaji ambaye alipaka mshtuko wa moyo baada ya kuona kiwanja chake kinauzwa na benki kwa njia ya mnada.

"Mheshimiwa hakimu, naiomba Mahakama yako kupitia kifungu namba 236 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), mahakama ifikirie kumpa adhabu kali mshtakiwa kwa sababu tuna taarifa kuwa mshtakiwa hastahili kupewa adhabu ndogo na ni mtu hatari katika jamii" amedai Maingu na
"Tangu mshtakiwa aghushi nyaraka hizi, mlalamikaji amepata hasara kwa sababu eneo hilo la kiwanja walikuwa wamekodisha na walikuwa wanalipwa Sh 3milioni kwa mwezi" amedai Maingu huku akiiomba Mahakama hati iliyotumika kuchukulia mkopo benki apewe mlalamikaji katika kesi hiyo ambaye ni Said Nassoro.

Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, mahakama hiyo ilitoa nafasi kwa mshtakiwa kujitetea kwanini apunguziwe adhabu.

Mshtakiwa huyo kupitia wakili wake, Derick Kahigi, alimuomba Mahakama izingatie umri alionao mteja wake na wakati anashtakiwa alikuwa miaka 65, hivyo apunguziwe adhabu.

Hata hivyo, hakimu alizingatia maombi ya mshtakiwa na kumhukumi kifungo cha nje cha miezi 18.
Katika kesi ya msingi, mshtakiwa anakabiliwa na kesi ya jinai namba 51/2021.

Katika shtaka la kwanza, mshtakiwa anadaiwa tarehe isiyofahamika mwaka 2014 katika mkoa wa Dar es Salaam mshitakiwa alighushi nyaraka inayoonyesha haki ya umiliki wa kiwanja kwa kutumia jina na sahihi ya Said Nassoro ambaye alikuwa mkurugenzi mwenza katika kampuni ya Mikocheni Shopping Mall Ltd kuonyesha kuwa kwa pamoja wameridhia kuchukua mkopo jambo ambalo halikuwa na ukweli.

Katika shitaka la pili mshitakiwa alighushi muhtasari wa kikao cha bodi ya wakurugenzi wa kampuni hiyo kilichofanyika cha Julai 18, 2014 kwa kuweka jina na sahihi ya Nassoro.

Katika shitaka la tatu, anadaiwa kughushi fomu ya hati ya kiwanja namba 40 iliyoonyesha kusainiwa na Said Nassoro jambo ambalo Said alilikataa katika ushahidi aliotoa.

Mwaka 2018 tarehe isiyojulikana mshitakiwa alighushi nyaraka inayoonyesha dhamana ya kampuni na kutumia jina la Said Nassoro kuonyesha kuwa amekubaliana kuweka rehani kampuni ya kama sehemu ya ulinzi wa mkopo huo wa Sh 350milioni.

Mwananchi
 
Kwenye maelezo wamesema eneo ilikuwa lipigwe mnada, hivyo sidhani kama analipa ipasavyo.
Yani una foji documents kupata mkopo kimagumashi, unapata mkopo, halafu mkopo wenyewe hulipi.

This is what I call tempting fate.

Kuna watu wanajua kujimwambafy.

Yani angalau kama unalipa mkopo vizuri, unaweza kumshawishi jaji.

Unamwambia jaji nimefanya makosa kupata mkopo, lakini mbona naulipa vizuri tu, na ukinifunga utawapa hasara walionipa mkopo, kwa sababu nitakuwa silipi mkopo (chances are collateral yenyewe magumashi hapo).

Lakini huyu mkopo kaupata kwa mafafa, halafu kulipa halipi!
 
Nyie akina kyenkungu na kyaruzi mnatuonaje wahaya nyie ?

Embu wekeni mambo sawa mlipe hela za watu
 
Yani una foji documents kupata mkopo kimagumashi, unapata mkopo, halafu mkopo wenyewe hulipi.

This is what I call tempting fate.

Kuna watu wanajua kujimwambafy.

Yani angalau kama unalipa mkopo vizuri, unaweza kumshawishi jaji.

Unamwambia jaji nimefanya makosa kupata mkopo, lakini mbona naulipa vizuri tu, na ukinifunga utawapa hasara walionipa mkopo, kwa sababu nitakuwa silipi mkopo (chances are collateral yenyewe magumashi hapo).

Lakini huyu mkopo kaupata kwa mafafa, halafu kulipa halipi!
kafoji dokoma akapate mkopo!
Kulipa napo alikausha

Ova
 
Back
Top Bottom