Tanzania should send a 50 strong team to Haiti


South Africa: Gift of the Givers Team Arrives in Haiti

Ernest Mabuza
18 January 2010

Johannesburg - A 10-MEMBER South African rescue team from Gift of the Givers arrived in Haiti yesterday as part of a R15m effort to help victims of the earthquake that struck last week.
The Haitian government said more than 50 000 people had been killed and 250 000 injured by the earthquake that devastated the capital Port-au-Prince.
Gift of the Givers chairman Imtiaz Sooliman said yesterday that the team left SA for Paris on Friday but could not fly directly to Haiti as the the airport was closed.
The team, which includes professionals skilled in disaster response, urban rescue and advanced life support, travelled by land from the Dominican Republic. It is carrying emergency medicines and R2,5m worth of heavy equipment to locate survivors in the rubble.
Two more teams will leave for Haiti this week. The first will leave tonight. On Wednesday, a 20-member medical team will follow.
It includes skilled trauma medical specialists including orthopaedic, facial surgeons, anaesthetists and advanced life-support paramedics.
Sooliman said the charity had been negotiating with the government to fund a cargo plane to transport hundreds of tons of emergency supplies. The plane will leave towards the end of the week, when the airport has been reopened. Supplies include medicines, tents, blankets, water, food and water tablets.
Sooliman said the Gift of the Givers mission was supported by the President' s Office, the Department of International Relations and Co-operation and the Department of Health. Support had also been received from the Southern African Catholic Bishops Conference and the Anglican Church.
 
It seems like Gift of the Givers is a private organization...do we have private orgs like this that can volunteer to go on their own resources than wait for the govt. to act...?
 
Nimesoma hii mawazo ya Mwanakijiji na yale ya wachangiaji wengine na kuona kuwa watanzania tunawajibika kubadilika, tena kwa kwa kiwango kikubwa kabisa. Mataifa yale ambayo yapomakini kabisa katika kulinda usalama wa raia wake kwa namna moja au nyingine wanachukulia majanga kama haya ya Haiti ni wakati mzuri wa kupima uwezo wao waliojijengea katika kukabiliana na majanga. Matokeo ya majanga hayachagui nchi tajiri au maskini na hakuna huruma pale yanapotokea. Kwa kawaida tumezoea kusikia kuwa nchi fulani inafanya mazoezi ya kijeshi tena kwa gharama kubwa kabisa, je ni kwanini wanafanya hivyo? Jibu ni katika kupima uwezo wao wa kukabiliana na majanga na kadhalika. Sasa inapotokea janga halisi kama hili la Haiti ni wakati mzuri kwa mataifa mbalimbali pamoja na kuokoa maisha ya watu vilevile wanafanya tathmini ya nguvu zao katika kukabiliana na majanga. Kwa mfano baada ya zoezi zima kukamilika washiriki huangalia je wametumia uharaka wa kiasi gani? je wameweza kukusanya resources kwa namna gani? je vifaa na wataalam wao wameweza kuperform kwa kiasi gani? haya pamoja na mambo mengi huwa ni hazina kubwa kwa washiriki kama taifa na jumuiya ya dunia hii.
Kwa mtazamo wangu, nchi za kiafrika (hasa zilizo kusini mwa jangwa la sahara isipokuwa South Africa) zimekuwa na mwelekeo wa mawazo tegemezi kiasi cha kwamba tumebweteka na kufikiria kila janga linalotokea hapa duniani halituhusu na wakati mwingine hata yale yanayotokea ndani ya nchi zetu tunadhani kuwa ni wajibu wa 'wafadhili' kuja kutusaidia.
Ningependa mjadala huu ulete changamoto na migongano ya fikra miongoni mwetu ili ikibidi nchi yetu iwe trailblazer katika eneo hili la kusini na kati ya Africa. I believe kama Tanzania ingeamua kwenda Haiti, na Rais wetu akaamua kwa makusudi mazima kabisa kuwaita majirani zake na kuwaomba kuchangia, nadhani tungekuwa tumesaidia kubadilisha muonekano wetu (waafrika) katika sura ya dunia. Pamoja na nchi kubwa kutumia resources zao, lakini bado michango mingi midogo-midogo ambayo ndiyo inafanya sehemu kubwa ya msaada inatoka kwa watu wa kawaida kabisa. Nchi kama Marekani uchangiaji kutoka kwa wananchi wa kawaida kwa sasa unafanyika kwa nguvu kubwa. Endapo Tanzania itaonesha njia basi ni wazi kabisa majirani zetu watapenda kuona kuwa uwezo wa kukabiliana na majanga katika sehemu hii unajengwa kwa manufaa ya wadau wote.
Kwa kuhitimisha, ni kwamba serikali kazi yake ni kuongoza, lakini sisi wananchi ndiyo tunatakiwa kujenga uwezo mkubwa wa kuelekeza yale ambayo tunataka serikali iyafanyie kazi.
 
..kwanini twende Haiti wakati hapahapa Tanzania kuna matatizo kama hayo ya Haiti?

..kama ni kujifunza tunaweza kwenda wakati mwingine, na sehemu nyingine, not this time wakati wananchi wetu wenyewe wa Kilosa na Kilombero wanataabika.

NB:

..suala la kuhakikisha kwamba majeshi yetu yanakuwa na uwezo na nyenzo za kushughulikia shughuli za maafa wengine tulilisema toka wakati tunapelekea wanajeshi Comoro.
 
Mkuu una scientific proof ya hii unayosema.

Mimi nianungana kabisa na Mzee MM kuwa kuna faida kubwa sana ya kupeleka nguvukazi Haiti. Mfano mdogo tumeshauona kwenye majanga madogomadogo tu ya moto kuwa hatupo tayari kwa catasrophic desaster. Mwaka 1996 MV Bukoba ilibinuka kulikuwa na chance naweza sema 98% ya kuokoa maisha karibu ya 80% ya waliokufa. Meli ilipinduka ikawa inaelea kilichotakiwa ni kuivutia kwenye maji mafupi na kuitoboa kwa technolojia ya wakati huo, Ila kila mtu alikuwa na mawazo yake matokeo wakatoboa meli kwenye kina kirefu kutoa mtu mmoja na meli kuzama, walisahau kuwa kilichokuwa kinaifanya ielee ni traped air inside.

Sasa tukiwa na watu wenye uzoefu katika uokoaji baada ya kwenda kujifunza kwa kujionea vifaa na mbinu zitumikazo huko kweli tunaweza kuwa na initial responders wazuri.

Nina hakina na ninachokisema kwani ndio field yangu hiyo mkuu. Sijaongea kufurahisha genge. Ikihitaji kozi binafsi naweza kukupa ya hicho ninachokiongea.
 
Hili wazo ni zuri sana, nadhani one of the best idea ever. Tanzania tuachane na tabia ya kuomba misaada tunapiokutwa na majanga halafu tunajificha kwenye mvungu wakati wenzetu wakikumbwa na majanga.

Tuna uwezo wa kusaidia mambo mengi sana huko Haiti hata bila kuingilia bajeti ya serikali kama alivyyonyesha Mwanakijiji. Nimeshaona kuwa inapotokea michango ya kisiasa kama vile kuichangia CCM ishinde jimbo fulani la uchaguzi, viongozi wanakuwa mstali wa mbele kuongoza harambee. Yakitokea majanga, viongozi hao hawaonekani kuendesha harambee za aina hiyo, hata kwa majanga yaliyoko ndani ya nchi: jambo la ajabu kweli kweli.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom