hp4510
JF-Expert Member
- Jan 16, 2012
- 6,451
- 6,325
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imesema kuwa uchumi wa Tanzania unaendelea kuimarika baada ya kukua kwa wastani wa asilimia 7.2 katika robo pili ya mwaka 2019 kutoka asilimia 6.1 kipindi kama hicho mwaka 2018 ukichangiwa zaidi na shughuli za ujenzi, madini, habari na mawasiliano.
Kwa mujibu wa ripoti ya pato la Taifa ya robo ya pili ya mwaka 2019 (Aprili-Juni) inaeleza kuwa shughuli za ujenzi ndiyo zilikua kwa kiwango cha juu zaidi katika kipindi hicho kwa asilimia 19.6 huku zikiongoza kwa kuchangia kwa sehemu kikubwa ukuaji wa pato halisi la Taifa (Real GDP).
Jaribu kwenda kijijini kwenu then copy ulichokiandika uwaeleze wanakijiji uone kama watakuelewa