TANZANIA PEKEE: Basi linachukua abiria 95!

Du me najua basi nyingi max kama abiria 65 sasa hao 30 waliozidi walikaa vp humo ndani? Mkuu wa usalama barabara ni wa tbr ajiuzulu tu kwa manufaa ya umma!
Kuna mengine hata sehemu ya kukanyaga inakuwa hakuna.
 
na sisis abiria wewe unaona gari limejaa bado unapanda ili iweje..watanzania tunajidai tunajua kuwahi sana mfano niko kwenye hiace hapa badala ibebe 16 inabeba 25..

Mkuu kwa ujumla hili suala linahitaji uelewa. kuna baadhi ya NJIA ZINA MAHITAJI MAALUMU kwani kuna abiria wengi, lakini mabasi ni machache hasa hizi barabara za vifusi. halafu ukumbuke hali ya maisha nayo inawafanya watu wasafiri huku na kule kujitafutia riziki, katika hali kama hii inafika sehemu unalazimika kusimama kwenye gari, ili uwahi mishe zako.

Ni ngumu kuwalaumu sana abiria, sanasana labda tuwalaumu hawa wenye mabasi kwa nini huwa wanakubali kupandisha abiria zaidi kwenye gari wakati anajua siti zimeenea?? ok, tuseme labda anataka kipato zaidi, SAWA, lakini bado unakuta mabasi yenyewe hayana SERVICES za uhakika, magurudumu yamechakaa hapohapo tena anakwenda mwendokasi mkali, yaani we acha tu.

Kwa kweli, mi nadhani kwenye hili BUSARA zaidi ndo inahitajika. kuzuia tu watu kusimama, haitoshi maana kwa njia zenye miundombinu duni, mabasi ni machache abiria ni wengi, hivyo kuzuia tu utatesa watu.

USHAURI WANGU KWA SERIKALI: Hizi NJIA ZENYE MAHITAJI MAALUMU, zitambuliwe, halafu waweke kiwango maalumu cha mwendokasi, na mabasi yanayotoa huduma yakaguliwe mara kwa mara. Ila kusema eti level seat tu, haitasaidia.

Ila kwa suala ma-traffic, duh!! hili naona kama lilishashindikana, labda kwa Tanzania ijayo ya mwaka 2040..na kuendelea.

Level seat inawezekana kwa njia zenye lami tu, maana kuna mabasi mengi ya kutosha.
 
na sisis abiria wewe unaona gari limejaa bado unapanda ili iweje..watanzania tunajidai tunajua kuwahi sana mfano niko kwenye hiace hapa badala ibebe 16 inabeba 25..

katika hali hiz me huwa naona ni lazima kutoa taarifa kwa vyombo husika lakini pia kushuka kwenye hilo basi hasa unapohis hakuna dalili za kuchukua hatua, ikiwa ni pamoja na kuwashusha abiria waliozid,its so sad that among the deceased is police constable kheri of tabora police station.
 
kwa kumbukumbu zangu hii na ajali ya pili mbaya kwa basi linalotumia jina la sabena. kati ya mwaka 1978-1980 basi lenye jina hilo lilipata ajali ambayo iliuwa watu wengi pia maeneo ya mbezi na kibaha na ile kukukumbu inashidwa kutoka kwenye akili yangu mpaka leo
bora trani zikamilike huwenda maisha yetu kwenye ajali yanaweza kupata suluhisho
poleni mlio umia na kufiwa na ndugu na jaa zenu Mungu awape nguvu katika hali hii ngumu iliyowakuta.
 
Mkuu kwa ujumla hili suala linahitaji uelewa. kuna baadhi ya NJIA ZINA MAHITAJI MAALUMU kwani kuna abiria wengi, lakini mabasi ni machache hasa hizi barabara za vifusi. halafu ukumbuke hali ya maisha nayo inawafanya watu wasafiri huku na kule kujitafutia riziki, katika hali kama hii inafika sehemu unalazimika kusimama kwenye gari, ili uwahi mishe zako.

Ni ngumu kuwalaumu sana abiria, sanasana labda tuwalaumu hawa wenye mabasi kwa nini huwa wanakubali kupandisha abiria zaidi kwenye gari wakati anajua siti zimeenea?? ok, tuseme labda anataka kipato zaidi, SAWA, lakini bado unakuta mabasi yenyewe hayana SERVICES za uhakika, magurudumu yamechakaa hapohapo tena anakwenda mwendokasi mkali, yaani we acha tu.

Kwa kweli, mi nadhani kwenye hili BUSARA zaidi ndo inahitajika. kuzuia tu watu kusimama, haitoshi maana kwa njia zenye miundombinu duni, mabasi ni machache abiria ni wengi, hivyo kuzuia tu utatesa watu.

USHAURI WANGU KWA SERIKALI: Hizi NJIA ZENYE MAHITAJI MAALUMU, zitambuliwe, halafu waweke kiwango maalumu cha mwendokasi, na mabasi yanayotoa huduma yakaguliwe mara kwa mara. Ila kusema eti level seat tu, haitasaidia.

Ila kwa suala ma-traffic, duh!! hili naona kama lilishashindikana, labda kwa Tanzania ijayo ya mwaka 2040..na kuendelea.

Level seat inawezekana kwa njia zenye lami tu, maana kuna mabasi mengi ya kutosha.
Mkuu issue iko hivi wanao siama pesa huwa haimfikii mwenye basi ni pesa ya dereva na koda na hukimbiza ili ampite alioko mbele ili aweze kupata wale abiri wa njiani mfano basi lina toka dar basi vichwa vinavyopandia same, moshi kwenda Arusha ni pesa ya dereva na konda wake sasa kama ataendesha taratibu wenzake siatawabeba hao abiria....kama unaenda mbeya kutoka Arusha abiria wanao pandia kuazia moro,iringa mpaka moro ni pesa ya dereva...nikupe kisa kimoja kuna siku nilikuwa natoka mafikanga ni kapanda hood ya Moro tukiwa njiani nikawa naomba ticket yangu konda anazuga nitakupa hakuna shida. tulipo fika Moro barabara ya kwenda mzumbe chuoni, Basi likasimamishwa na marakatokea meneja wa mabasi wa HOOD. moja kwamoja akaomba kitabu na kuanza kupitia abiria mmoja baada ya mwingine alipo maliza alikuta abiri 14 hawana ticket na bado kuna wengine walishukia Iringa, konda kuulizwa akaanza kujikanyaka..hivyo kuna tatizo lingine la wengi kutokudai ticket na wakati mwingine makonda wana ticket fake ndiyo maana hawa hawa watu ukiwatishia kuwapeleka mbele ya vyombo vya sheria watataka muya malize ama ukupe seat au pesa yako.
kuhusu kiwango cha mwendo pona upo wazi, tatizo ni abiria kutokuchukua hatua, basi lilisimama kutafuta abria kwa muda wa nusu saa likija kuanza safari litataka kufidia huo muda na ukifika kwenye check point polisi wakiuliza kuna tatizo kimya au wengine wana sema hakuna..
umesema level seat inawezekana kwenye lami tu hii siyo kweli ni udhaifu wa abiria kama usafi ni shida si ukati ticket siku 3 kabla.
 
katika hali hiz me huwa naona ni lazima kutoa taarifa kwa vyombo husika lakini pia kushuka kwenye hilo basi hasa unapohis hakuna dalili za kuchukua hatua, ikiwa ni pamoja na kuwashusha abiria waliozid,its so sad that among the deceased is police constable kheri of tabora police station.
Usikute alipakiwa bure hivyo hana ubavu wa kukemea...
 
Sisi nao wananchi tuamke, tusilalame tu inakuaje watu wenye akili wanapanda bus wakiwa idadi yote hiyo?!! kwanini wasikatae na kuona mwendo mkali wakomae derev apunguze mwendo?!! raia nao ni shida sawa na mapolisi wezi tu...
 
Huyu Dogo Chapa nafikiri kwa hili atakuwa na matatizo zaidi. Kwa Tabora, magari yanajazwa na kushindiliwa kwa sana tu.

Unakuta Konda anarudi nyuma na kuanza kupanga abiria huku akiwakatia ticket.

Mtu anashonana kama ng'ombe kwenye kunywa maji bwawani.

Cha ajabu ni kimoja, unakuta Bus moja lenye uwezo wa kwenda Tabora mjini mara mbili na kurudi Nzega, Igunga, Urambo, Sikonge nk huenda mara moja na mwisho wa safari. Huwa wanataka faida kubwa kwa kazi ndogo bila kujali maisha ya watu. Kibaya kingine ni kuwa mtu akileta Bus huko watampiga vita hadi akimbie.

269710_348677631882269_442393005_n.jpg

308983_348679111882121_242228468_n.jpg

Picture by Hamisi Kimwaga, SIKONGE.
 
Labda ni basi la deki mbili hilo au?
...Bora ingekuwa hivyo...abiria walijaa kwenye viti na waliobaki walisimamishwa line mbili mnapeana migongo then mnashika bomba. Na kuna soldier alikuwemo humo alimwambia dereva mwendo ni mkali jamaa akampotezea na mwisho wa yote ndio hivyo na dereva kala chocholo!!!..
 
Wenye mabasi ni wafadhili wa hao wasimamia sheria
unategemea nini!!!

the only solution ni ku overhaul the system,tutatoa mapovu sana
bila mabadiliko yoyote KUNA askari wa morogoro ayijiuwa juzi alisema ukweli mwishowe yuko wapi////????
 
La deki 2 lingebeba abiria 200.

kama INDIA wengine hukaa juu ya Carye mungine huka bus linaenda amebeba mzigo mukichwa maana akiweka mzigo chini hakuna pakusimama watu bora BONGO ...SUDAN kutoa WAU mwisho wa SOUTH SUDANI mpaka KARTUM siku 7 unakaa ju ya kipaa inje watu kama 300 kwa TREN tembea uone TANZANIA bado mzuri sana hata ma Bus yake mazuri sana 2 hayo ni makosa madogo madogo ya kiutendaji yanatokea
 
hii ni hatari kama tusipobadilika sisi wenyewe basi hali itakua mbaya sana kwani ukiona gari imejaa huwezi kusubiri nyingine? tukubali kua wakati mwingine huwa tunajitafutia matatizo sisi wenyewe. mbona wenzetu jirani kenya na uganda wameamua kufanya utaratibu wa kutokupanda gari isiyokua na siti na wamefanikiwa? watz hatumkomoi mtu kama tukiamua kufuata utaratibu huu bali itachangia kujiweka huru na salama kwa maisha yetu wenyewe kwani ni kweli kua sio waTanzania wote wenye uwezo wa kutumia magari binafsi.
 
Ajali basi la SABENA huko Tabora laua 17, yajeruhi 78. Hivi Tz kuna basi linaweza chukua watu 95? askari kwa nini wasiwajibike? Source ITV

.
Unakumbuka ajali ya hiace mbeya? Ilikuwa imebeba abiria 30 na wote walikufa ukijumlisha na mchawi aliyeuawa katika tukio kwa kukutwa akiokota spear parts za viongo kutoka kwa miili ya marehemu ni wa 31.
Sasa jiulize serikali hii sikivu ilijifunza chochote? Jibu unalo mwenyewe.
.
 
Back
Top Bottom