TANZANIA PEKEE: Basi linachukua abiria 95! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TANZANIA PEKEE: Basi linachukua abiria 95!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by steering, Aug 9, 2012.

 1. s

  steering Member

  #1
  Aug 9, 2012
  Joined: Nov 28, 2011
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ajali basi la SABENA huko Tabora laua 17, yajeruhi 78. Hivi Tz kuna basi linaweza chukua watu 95? askari kwa nini wasiwajibike? Source ITV
   
 2. UPOPO

  UPOPO JF-Expert Member

  #2
  Aug 9, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 1,371
  Likes Received: 718
  Trophy Points: 280
  shangaa hii ipo Tanzania tu dunia nzima
   
 3. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #3
  Aug 9, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Matrafiki wanawakamata sana na kuwatoa upepo. Hivyo usishangae hiyo idadi inayozidi ndiyo chakula ya matrafiki. Mkiambiwa nchi imeuzwa mnadhani ni uzushi na uchochezi. Nenda kwenye machimbo na walipo wawekezaji mtalia sana. Maana wakati trafiki wakiuza roho zenu kwa wenye mabasi wachoyo, watawala wenu wanaunza kila kitu kwa wawekezaji. Hiyo ndiyo Tanzania iliyogeuzwa shamba la bibi.
   
 4. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #4
  Aug 9, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  ndio hivyo sasa maana tulishajizoelea kuwa hivyo so hakuna cha kushangaa..

  RIP wote Mliokufa ajalini
   
 5. mzurimie

  mzurimie JF-Expert Member

  #5
  Aug 9, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 6,151
  Likes Received: 1,604
  Trophy Points: 280
  Labda ni basi la deki mbili hilo au?
   
 6. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #6
  Aug 9, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Tatizo letu ni kukosa wakumnyooshea kidole mwenzie. Wala hakuna kujifunza kutokana na makosa. Ndio maana ajali za meli zinarudia, milipuko ya mabomu ilirudia na hakuna walionyooshewa kidole.
   
 7. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #7
  Aug 9, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Hii ndio Tanzania.. Kuna ajali ilitokea mto Nduruma ambapo DCM ilikuwa inatoka Arusha kwenda Mererani ilisombwa na maji, watu 19 walikufa hapohapo, 53 walijeruhuwa na kukimbizwa hospitali ya mkoa. DCM yenye uwezo wa kubeba watu 33 tu, ilikuwa na abiria 72! Na hadi leo hakuna aliyeulizwa!
   
 8. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #8
  Aug 9, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,816
  Likes Received: 10,106
  Trophy Points: 280
  nilipanda basi la kampuni ya Ally's mwaka jana wkati naenda Kigoma, basi lilikua limejaza kupita maelezo na barabara ilikua ni rough road tulipofika junction ya Burundi na Kigoma kuna kituo cha Polisi hapo Kondakta alishuka akaenda kumpa trafic pesa na safari ikaendelea, yaani tungepata ajali naaamini wangekufa wale wote waliosimama kwanza tukafuatiwa na sisi, naamini ilikua na watu zaidi ya mia moja achilia mbali mizigo na spidi ni zaidi ya mia pia!!!!
   
 9. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #9
  Aug 9, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,400
  Trophy Points: 280
  Du me najua basi nyingi max kama abiria 65 sasa hao 30 waliozidi walikaa vp humo ndani? Mkuu wa usalama barabara ni wa tbr ajiuzulu tu kwa manufaa ya umma!
   
 10. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #10
  Aug 9, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  na sisis abiria wewe unaona gari limejaa bado unapanda ili iweje..watanzania tunajidai tunajua kuwahi sana mfano niko kwenye hiace hapa badala ibebe 16 inabeba 25..
   
 11. Joel

  Joel JF-Expert Member

  #11
  Aug 9, 2012
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 908
  Likes Received: 259
  Trophy Points: 80
  mimi kwa kweli hawa trafik wananitia kichefuchefu kwani wanaacha magari ya abiria kufanya watakavyo humo barabarani halafu ajali ikitokea wanasema gari lilikuwa linakimbia kupita kiac,sasa kwa nini lizidishe speed wakat wao wamejazana kila umbal fulani na matochi yao!!
   
 12. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #12
  Aug 9, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  halafu wa tanzania huwa hatutaki kujifunga mikanda mpaka ukimuona polisi sasa mimi huwa najiuliza hivi mikanda inamsaidia traffic au wewe abiria kama tunataka kupunguza vifo vinavyotokana na ajari, zitungwe sheria ukikutwa umesimama ni viboko na kifungo hata ya siku moja na ukikutwa hujafunga mkanda viboko..
   
 13. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #13
  Aug 9, 2012
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,256
  Likes Received: 2,079
  Trophy Points: 280
  ...hilo basi litakuwa jamii ya treni...
   
 14. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #14
  Aug 9, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  hakuna atakae jiuzulu hata sisimizi.
   
 15. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #15
  Aug 9, 2012
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,256
  Likes Received: 2,079
  Trophy Points: 280
  ...mkuu natamani hii kazi, mbona watakoma!
   
 16. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #16
  Aug 9, 2012
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ....Ingekuwa ikitokea ajali ya nmna hii, kabla ya kitu chochote Mkulu anamtimua mkuu wa trafiki wa mkoa na mule mwote basi lilimopita. labda watu wangeogopa na kuanza kuheshimu kazi zao. Si mnakumbuka lile basi la kutoka Tanga, sijui ni Zafanana vile, lilipita pale Muheza likiwa limejaza abiria hadi pomoni lakini baada ya 'mazungumzo' trafiki wakaliacha liendelee na safari na hatua mia tu mbele lote likasombwa na maji na ikawa kilio! Kama matrafiki waliohusika hawakutimuliwa pale, watatimuliwa wapi tena???
   
 17. Shixi889

  Shixi889 JF-Expert Member

  #17
  Aug 9, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 322
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Mkuu trust me basi kama la sabena halina mikanda na ni mabasi mengi tu hayana mikanda na kama ipo basi ni viti vichache sana sasa unategemea mtu ufanye nn na kuna mabasi yanaongoza kwa kuua kwa kuzidisha abiria na kukimbia sana lakini hayafungiwi leseni na ajali zinazidi kila siku trafik nao ndo hivo tena watakula wapi??yani sjui ni nn kifanyike maana kila siku tunaangamia kwenye hizi ajali.
   
 18. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #18
  Aug 9, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Mkuu nakubaliana kabisa na wewe lakini bado mimi nitawalaumu watanzania kwasabau vitu ninavyo viongea siyo wa kuambiwa ni vyakujionea kutokana na shughuli zangu huwa na safari mara kwa mara.. kuna wakati mna fika kwenye mizani mnaambiwa mshuke mtangulie kwa miguu au mnakodishiwa hiace iwatangulize...mimi niseme kwasasa usafiri wa mikoani mabasi ni mengi sana kama basi hilo lina matatizo kwanini ulipande? ni kweli Tabora mbeya ni basi hilo tu? bado kwenye mabasi ambayo kuna mikanda abiria huwa hawajifungi ukumbuke safari hizo ni ndefu huku mmejazwa kama mizigo na kunapotokea na tatizo kuna sehemu ukifika unaulizwa na traffic kama kuna tatizo unasema hakuna tatizo wakati basi linakimbizwa speed mpaka 120...
   
 19. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #19
  Aug 9, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  baadhi ya matrafic huwa wanapeleka % kwa wakubwa wao hivyo linapotokea tatizo kama hilo huwatetea...hivyo ni sisi abiri kuchukua hatua tunapoona tatizo mfano kuna mabasi seat moja hukatiwa watu zaidi ya mmoja mkishaingia kwenye gari mnaanza kugombana abiri kwa abiria badala udai nauli urudishiwe au kushitaki kwa wahusika maana napo kuhahirisha safari ni gharama saa zingine..
   
 20. M

  Mkwe21 JF-Expert Member

  #20
  Aug 9, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,834
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Jamani Tupo Kwenye Utandawazi na Biashara ni Huria!! Hivi ni kweli Mabasi ni Adimu Kihivyo hadi Basi lichukue watu Zaidi ya mia Tanzania Hii hii? Ndugu Mheshimiwa Pinda amka Huko Uliko Haya ni maeneo ya kwenu!!
  Pia Ikumbukwe ni Tanzania Pekee ambako Mtunza Sheria (Kamanda wa Polisi) anatokea Bila kukiri Uzembe anaeleza Hadharani Basi lilibeba abiria zaidi ya 100 bila Aibu!! Je Nyie polisi siku zote Mko wapi? Kila siku tunaugulia Maumivu ya Vifo vya ndugu zetu? Kazi yenu ni nini hasa? Kupokea Vijirushwa kwa wavunja sheria?
  Hapa ninachotaka Kusema Mtuhumiwa Numba moja ni Kamanda Mpinga aliyeruhusu Jeshi la Polisi (Usalama barabarani) kuwa kama sehemu binafsi ya kuongeza Kipato kwa polisi!!
   
Loading...