Tanzania not happy with UK visa being processed in Nairobi

Tanzania not happy with UK visa being processed in Nairobi

Mwaka ambao Julius alifunga Ubalozi wa UK hapa Tanganyika nilikuwa sijazaliwa, inakuwa vigumu kujua Waingereza walifanya nini. Kwani Kikwete hawezi kuiga ili heshima irudi?

Teh teh teh atawezaje wakati kila siku anawaibukia na kapu lake la omba omba?
 
Hapa i beg to differ, In Europe, Chinese Visas are also offered in this regard, you send your application online, they asses it, you send them a passport,they mail it back to you with a Visa, i have done this many times in UK, German and France, so i believe it is nbot a big issue for countries without security threats kama Marekani.

Tushapigwa mabomu na terrorists, bado unasema hatuna security threat?

Kwa "swaga" za wachina, hawana papara, ukishaingia MainLand wewe ni package yao, wanakupekenyua watakavyo NSA kama mchiriku tu kwa hawa watu.So i can understand their confidence.

Wengine watasema kutoa visa by mail tu ni papara tayari, kwa hiyo haijalishi huko kwao wanafanya nini.

Actually i suggest something simila kwa Tanzania, we should setup Visa Applications clusters, like one in West Europe, one in Asia Pacific,One on far East Asia, one in South America,One in North America, One in Central Asia, One in East Europe, One in China, And another one in Middle east save for Africa where costs are relatively lower.

I was not against visa by mail, the libertarian streak in me would lean towards gradually abolishing visas altogether.

I was merely pointing out the lack of reciprocity which reflects the respective economic might and relevance to each other between two countries.

I bet you the Chinese (mainland) do not allow visa by mail from Tanzania now, do they?
 
Sasa mkuu
Mtu atasaidia je wakati sio raia?
Mie ninachongelea hapa kimantiki ni hiki, tuseme wewe una uraia wa UK na TZ basi unaweka stores zako Tanzania, mfanyabiashara, anaadika contracts kwa store ya Tanzania na anaweka order bidhaa, kisha wewe unanunua na unaleta bidha kwa store yako ya Tanzania jamaa anapata bidhaa kwa wakati, na anaiuza kwa mlaji kwa bei nafuu maana hakukua na usumbufu na gharama ya maisha kwa mlaji mtanzania yanapungua.

Huyu Mtanzania aliyopo yopo kwa sasa UK, akiwa na uraia wa Tanzania na UK, basi anaweza mua aproach mzungu mwenye hela kidogo lakini ulaya hawezi fanya lolote, ama akakopa bank za uzunguni anakuja kununua viazi na mihogo ama korosho, kahawa kwa mkulima kwa bei nzuri anakuja kuuza ulaya.

Bei ya bidhaa za Tanzania ulaya ni kama ifuatavyo.
1. Viazi (viazi kama viwili)vitamu kilo ni euro 10= = 20,000 Tsh
2. Ka papai kama nusu kilo euro 10== 20,000Tsh
3. Mhogo mtamu kilo euro 10 == 20,000
4. embe dongo, ile mbaya kabisa eur 3, == 6 Tsh
5. Mchicha na mti wake wenye mbegu ambao bongo unaliwa na beberu la mbuzi, ni euro 5
6. limao kilo euro 5 == 10,000 tsh
7. Unga wa udaga(mhogo) mbaya kweli kutoka ghana == euro 5 kwa kilo
nk, nk ,nk

Mwana naenda "Whole Foods" naangalia vi korosho vinne vitano vimepangwa kwenye mfuko uliojaa hewa zaidi ya korosho, halafu unaambiwa dola saba hizo.

Vikorosho hata gram 150 havifiki.

Basi nikasema hapa kama unapata deal la ku export vitu kutoka bongo unapata na line ya ku dump huku kiwanja hata huhitaji kukaa ughaibuni sana.

Unasema tu kwa aibu "I divide my time between New York and Dar" kumbe huko NY unaenda kutembea tu.

Kuna mtoto wa Jackie Robinson yuko Mbozi analima kahawa na Coop yake, last I heard alikuwa ana line ya kuwauzia Starbucks kitu cha ukwee kutoka Mbozi, na mnayamwezi si unajua anavyohusudu exotic coffee tena, hukawii kuambiwa kikombe kidogo tu dala tatu nne (I don't drink Starbucks - coffee really- so I would hardly know the current going rate)

Inawezekana kabisa haya mambo ya dual ndiyo yakalet the needed paradign shift alakini watu wanasuasua kwa habari za mtego wa panya unasao waliokusudiwa na wasiokusudiwa, wanakosa maendeleo kwa kuogopa ufanisi.

Mie nishaamua kuacha kufuatilia, kama vipi ndo tuwe hyphenated kabisa.
 
Wabongo hatuwezi kufanya hivyo kwa sababu tunataka kuvutia watalii na wawekezaji.

Usishangae hata ukisikia kuna mwingereza kapewa ubalozi wa heshima UK may be Scotland ili kuwavutia wascotish kutalii Tanzania na anapewa power of consular.
 
Usishangae hata ukisikia kuna mwingereza kapewa ubalozi wa heshima UK may be Scotland ili kuwavutia wascotish kutalii Tanzania na anapewa power of consular.

Yeah, hii ishatokea mara kadhaa, wengine mpaka wakapiga madeal ya hatari ya kufa mtu.

Alikuwepo mmoja kipande hichohicho hapo, Uholanzi au Ubelgiji Igorgot the exact xountry off the top of my head, ikikuwa a big story mpaka wabongo huko wakalalamika sana tu.

Noma.
 
Teh teh teh atawezaje wakati kila siku anawaibukia na kapu lake la omba omba?

Umeikamaka ile core point mkuu.

Huwezi ku negotiate mambo ya national dignity kwa kutumia reciprocity na sovereignty wakati you are sovereign in name only.

Bajeti yako inakamilishwa na misaada kibao. Unategemea utalii wa hao hao wazungu kuja kwako, huwezi kuwawekea masharti magumu kupata visa, utaua utalii watoto wafe na njaa.
 
Hawa Waingereza wanatudharau sana Watanzania, unafanya taratibu zote za viza unalipia pesa wanakupa tarehe unakwenda ubalozini wanakupa bahasha yako unafungua unakuta viza wamekunyima na pesa wamechua, wanakuambia kama una malalamiko wasiliana online.

Ongea na mshua
 
Mgombea ubunge Chalinze na Mwigulu wametuponza... Kwa wenye akili mmenisoma.
 
Mwana naenda "Whole Foods" naangalia vi korosho vinne vitano vimepangwa kwenye mfuko uliojaa hewa zaidi ya korosho, halafu unaambiwa dola saba hizo.

Vikorosho hata gram 150 havifiki.

Basi nikasema hapa kama unapata deal la ku export vitu kutoka bongo unapata na line ya ku dump huku kiwanja hata huhitaji kukaa ughaibuni sana.

Unasema tu kwa aibu "I divide my time between New York and Dar" kumbe huko NY unaenda kutembea tu.

Kuna mtoto wa Kackie Robinson yuko Mbozi analima kahawa na Coop yake, last I heard alikuwa ana line ya kuwauzia Starbucks kitu cha ukwee kutoka Mbozi, na mnayamwezi si unajua anavyohusudu exotic coffee tena, hukawii kuambiwa kikombe kidogo tu dala tatu nne (I don't drink Starbucks - coffee really- so I would hardly know the current going rate)

Inawezekana kabisa haya mambo ya dual ndiyo yakalet the needed paradign shift alakini watu wanasuasua kwa habari za mtego wa panya unasao waliokusudiwa na wasiokusudiwa, wanakosa maendeleo kwa kuogopa ufanisi.

Mie nishaamua kuacha kufuatilia, kama vipi ndo tuwe hyphenated kabisa.

Unajua watu wanajinyima fursa bila kufahamu, harafu baadae wanalialia ohh serikali hawalipi bei nzuri ya mazao yao. Kitu Expresso ya kiitaliano ama espaniola yaweza toka mbozi, hata ule mpunga wa kyela ama kinyamwezi.
 
Mwaka ambao Julius alifunga Ubalozi wa UK hapa Tanganyika nilikuwa sijazaliwa, inakuwa vigumu kujua Waingereza walifanya nini. Kwani Kikwete hawezi kuiga ili heshima irudi?
Ilitokana na uingereza kupiga danadana uhuru wa zimbambwe. Nchi za afrika katika mkutano wa O.A.U. zilikubaliana kuvunja uhusiano na uingereza kutokana na kuwazulumu uhuru wa nchi yao waafrika wa zimbabwe. Nchi nyingi ziligwaya kutekeleza ila nne tu tz ikiwa mojawapo.
 
Mbona hatulalamikii visa ya Canada kutoka Nairobi miaka yote hii.
 
Tushapigwa mabomu na terrorists, bado unasema hatuna security threat?

Wengine watasema kutoa visa by mail tu ni papara tayari, kwa hiyo haijalishi huko kwao wanafanya nini.

I was not against visa by mail, the libertarian streak in me would lean towards gradually abolishing visas altogether.

I was merely pointing out the lack of reciprocity which reflects the respective economic might and relevance to each other between two countries.

I bet you the Chinese (mainland) do not allow visa by mail from Tanzania now, do they?

My Angle as not Tanzania, but China, The tiny eyed dudes are one of the most secure from external threats,so they worry less about people who are coming in. You can't survive a for a long period in China as u can in US with forgery docs.Ingawa kuna wabishi pale Guangzhou.

Tanzania, kudaiwa kuapply Visa ni Halali yetu kutokana na Geopolitcs za Eastern Horn of Africa, Ugaidi umetuchafua, na Umaskini hausaidii pia. we are suspects from multiple points. Hizi visa zinawaondolea Jamaa Noise ili wa-deal na signal.

Reciprocity wanaiweza Russia na China, sisi wenye uchumi fake as useful as a "Zero before a number" when it comes to global issues, we are just there to decorate.

Sikumbuki kama hawa jamaa wa China wamewahi kuruhusu Mail-in or Mail-out Visa, Posta yenyewe ile, itakuwa lawama unaaply visa unapata unasikia Jirani ghafla anasafiri. Kumbe Visa yako ishakuwa intercepted Mkwepu.

Haya mambo ni kwa wenzetu wenye Zipcodes za kueleweka, sio za kwetu zinazoishi TCRA
 
Unajua watu wanajinyima fursa bila kufahamu, harafu baadae wanalialia ohh serikali hawalipi bei nzuri ya mazao yao. Kitu Expresso ya kiitaliano ama espaniola yaweza toka mbozi, hata ule mpunga wa kyela ama kinyamwezi.

Watanzania wengi Tu-wavivu kaisi flani, pia kufanyiwa kila kitu na serikali kulitulemaza. Kuingia kwenye hizi Database za hawa Global Food Chains kunahitaji commitment, kwani Jamaa wana-adhere to strict standards. sasa ------ wa chalinze strictness wapi na wapi? Ndio maana tuliwaachia wahindi wawe Madalali wetu kwani at least hawa kina Dewji na wenzie wana ka-heshima kwenye kutimiza obligations zao.

Vyama vyetu vya ushirika vingewezeshwa kisasa vingeweza kabisa kuwawezesha hawa wakulima wadogowadogo waweze kudeal na hizi MNCs moja kwa moja kupitia umoja wao. Wanafanya Hivi sana South America, kwenye Ndizi, Viazi n.k kwa nini sisi tushindwe?

Hawa waganga njaa zetu wakenda kwenye kampeni vijijini kutwa kucha kudanganya shangazi zetu na babu zetu kuwa watawaletea Barabara.Watu ambao hata Viatu hawana.Wanasiasa vichwa maji, wananchi wamejichokea. perfect recipe for mediocrity.
 
Ilitokana na uingereza kupiga danadana uhuru wa zimbambwe. Nchi za afrika katika mkutano wa O.A.U. zilikubaliana kuvunja uhusiano na uingereza kutokana na kuwazulumu uhuru wa nchi yao waafrika wa zimbabwe. Nchi nyingi ziligwaya kutekeleza ila nne tu tz ikiwa mojawapo.

Kuwa Mwanaume si kuning'iniza kende tu kama wengi wanavyofikiri- Hiki kibabu kilikuwa kinajua kinachokifanya. with all his faults a, A Statesman sure he was. Huyu wa sasa hivi ni galasha tu.Guts za kufanya ya Nyerere hana.
 
Inasikitisha sana ujinga wa kutojitambua...huu ni uhuni hawa wazungu tunawaogopa sana sana pesa mbili za misaada basi kimyaa hatusemi kitu.
Canada hawa wamejaa kwenye madini ...tukawa kiwanja kikubwa cha kujenga ubalozi pale Ohio leo lile jengo halina masna yoyote..wao visa hata maombi hupeleki pale "ubalozini" bali unakusanya fomu zako na kuwapelekea Fedex ambao huzipeleka nairobi...sisi hawa wa canada tunawapa visa wakifika airport.
Uingereza nao tumewapa eneo zuri wakajenga ubalozi lakini leo ubalozi huu ni useless tu. Visa mpaka nairobi..huu ni ujinga wa kutojiamini...
Tuki amua na sisi kufanya the same lazima watabadili msimamo...wao ndio wanataka dhahamu na gas yetu....hii slavery mentality lazima tuiache tudiwe mabwege tu.tukidinda kwenye hili na wao wachukue visa nchi ya jirani basi watabadilisha msimamo..wanajua wazi wakichelewa china atajitanua ..yaani vile viwanja tulivo wapa hawa bora zingejengwa hotel tukapata kodi.
 
Afu bakuli za omba omba muache kuwapelekea pia. Hapo mtaheshimika tu. Sisi tuliwatetemesha hawa baada ya kutengeneza budget bila kuhusisha hela za misaada wala mikopo yao. Nadhani hili liliwababaisha ndo maana kwetu hapa Kenya wanakuja tu na kwa wingi hata kama mabomu yanalipuka ovyo kila sehemu.
 
With current insecurity watakuja wenyewe Tz. Si kwamba nafurahishwa na al shabab ila ndio fursa yenyewe hiyo...

Kuna jamaa alienda kuwabana ubalozi wa Marekani kuhusu hizi habari za Wamarekani ku recruit watu kutoka Tanzania, sorta like kuhakikisha kama kampuni ni legit au siyo.

Counselor ubalozini kashazoea kila siku watu wanakuja sana kuomba student visa na visa za kutembea, hakutegemea kama mbongo anaweza kuuliza maswali kama haya ubalozini.

Wakamzungusha zungusha pale, wakaitana itana, wakakosa majibu.

Ikabidi wamwambie kwamba swali lake linatakiwa kupelekwa Nairobi kwani ubalozi wa Dar hauna Labor attache.

Naona nchi nyingi za magharibi zinafanya Nairobi kuwa a notch higher than Tanzania. Australia nakumbuka walikuwa hawana ubalozi kabisa bongo, ukitaka kwenda Aussie inabidi kwenda Nairobi. Nafikiri bado ni hivyo.
 
Nadhani Kenya imekuwa chaguo la nchi Bepari toka enzi na si sababu ya Budget...kutokana na sera za nchi yenu na ukweli kwamba kwa muda mrefu mmekuwa mbele ki miundo mbinu ni wazi hakuna taifa lingechagua Tanzania...

Ila mambo yameanza kubadilika...labda in future tutakuwa hatuna tofauti...

Back
Top Bottom