Tanzania ni miongoni mwa nchi kumi za mwisho kwa viwango vya furaha duniani

KakaKiiza

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
11,578
8,600
Tanzania ni miongoni mwa nchi kumi za mwisho kwa viwango vya furaha kwa mujibu wa Ripoti ya Viwango vya Furaha Duniani ya 2016 ambayo imetolewa leo.

Orodha hiyo iliandaliwa kwa kuangazia pato la mtu kwa kila mwaka, miaka ambayo mtu anatarajiwa kuishi, kuwa na mtu wa kutegemea kwa usaidizi, dhana ya kuwepo uhuru wa kufanya maamuzi maishaji, uhuru kutoka kwa ufisadi, na ukarimu miongoni mwa mengine.

Mataifa yaliyo kwenye kundi la mataifa kumi ya mwisho ni Madagascar, Tanzania, Liberia, Guinea, Rwanda, Benin, Afghanistan, Togo, Syria huku Burundi ikishika mkia.

Tanzania imo nambari 149 kati ya nchi 157 ikiwa na alama 3.695 kati ya alama 10 na Rwanda nambari 152 na alama 3.315.

Uganda imo nambari 146 na alama 3.739, Malawi nambari 132 na alama 4.156, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imo nambari 125 na alama 4.272 na Kenya nambari 122 na alama 4.356.

Somalia imo nambari 76 na alama 5.44.

Ripoti hiyo imetolewa mjini Roma, Italia huku ulimwengu ukijiandaa kuadhimisha Siku ya Furaha Duniani ya Umoja wa Mataifa tarehe 20 Machi.

Orodha hiyo imetayarishwa na shirika la maendeleo endelevu ya Sustainable Development Solutions Network (SDSN) ambalo lilianzishwa na Umoja wa Mataifa.

Denmark inaongoza kwa viwango vya furaha duniani ikiwa na alama 7.526 ikifuatwa kwa karibu na Uswizi, Iceland na Norway.

Finland, Canada, Uholanz, New Zealand, Australia na Sweden zinafunga kumi bora.

Marekani imo nambari 13 na Uingereza nambari 23.

Chanzo: Ripoti: Tanzania nyuma kwa furaha duniani - BBC Swahili
 
Wadau ripoti ya shirika moja la kimataifa limetoa ripoti yake ya nchi ambazo wananchi wake wana furaha.katika nchi kumi za mwisho Tanzania ni mojawapo.Nchi ya mwisho kabisa ni Burundi.Hoja yangu ni kwamba;je ni kweli kwamba wananchi wa Tanzania hawana furaha mpaka tunapitwa na nchi kama Somalia.karibuni tujadili.
 
Subri baadae ya miaka 5 ndio tutapata kuamini ilo..subri wajuzi wajee..!
 
Moja kati ya vitu vinavyoleta furaha maishani ni kufanya kazi ya ndoto yako kufanya kazi unayoipenda......kwa uchunguzi wangu nimegundua kuwa WATANZANIA wengi wanafanya kazi wasizo zipenda isipokuwa wanavutwa na maslahi tu lakini mioyo yao haina furaha na kazi zao....ndio maana haishangazi kukuta mtu aliyefaulu kwa kiwango kizuri masomo ya biolojia na kemia baada kusome udaktari anakwenda kusomea uhasibu.....hii ni kwa sababu ya maslahi ya uhasibu na si kwa mapenzi yake kwenye fani....

Kwa kuwa kazi zetu zinachukua sehemu kubwa ya maisha yetu yaani tunatumia muda mwingi makazini basi hatuna budi kuzifurahia kazi zetu.....
 
Wametumia kigezo kipi? Kipindi hiki watanzania walio wengi wana furaha sana! Sababu ni kuwa wamepata matumaini mapya kutokana na rais Magufuli kuamua kuwatumikia kwa dhati kwa kupambana na ufisadi uliokuwa umekithiri!
 
Wametumia kigezo kipi? Kipindi hiki watanzania walio wengi wana furaha sana! Sababu ni kuwa wamepata matumaini mapya kutokana na rais Magufuli kuamua kuwatumikia kwa dhati kwa kupambana na ufisadi uliokuwa umekithiri!

Suala la kukosa furaha ni suala la kihistoria. Hata kama Magufuli ni mchapakazi lakini mfumo na watu anaofanyanao kazi hawatoweza kuleta matumaini mapya kwani wanafanya kazi kwa mihemuko kama maroboti.

Ili watanzania wawe ni watu wenyefuraha lazima kuwe na misingi dhabiti ya uzalendo na kiwadhamini watanzania kwanza kwa kuwa wezesha.

Katika nyanja ya viwanda,kilimo na viwanda. Tanzania tunawasomi wa kutosha kuendeleza uchumi lakini hawajatumika ipasavyo.

Kwa mfumo huu wa kuendekeza wawekezaji kwenye kila kitu hatutofika kamwe.. Tumeshindwa kuji thamini sisi wenyewe unadhani furaha itatoka wapi.
 
tusijidanganye hebu itokewe ofa hapa ya kuhamia ulaya ama marekani uone kama kuna mtu atabaki ndo ujue tunavumilia tu kuishi hapa ila sio kwamba tunafuraha na hapa
 
tusijidanganye hebu itokewe ofa hapa ya kuhamia ulaya ama marekani uone kama kuna mtu atabaki ndo ujue tunavumilia tu kuishi hapa ila sio kwamba tunafuraha na hapa
Ofa ya kuhamia ulaya au marekani wataipapatikia wasiokuwa na ufahamu kuhusu maisha ya huko! Kama ni kwenda kutalii sawa lakini si kuhamia!
 
....ni kweli nchi hizi kama TZ na Burundi(iliyoshika nafasi ya mwisho)watu wake hawana furaha kwa kweli....na kwa mtu unaefatilia utawaonea huruma sana watanzania kwa jinsi wanavyoishi kwenye lindi la umaskini....pamoja na kujaliwa raslimali tele.....ukitaka kujua machungu ya watanzania tembea huko mikoani uone....jinsi raia wa TZ wanavyopigika kuimaliza siku....watu wanakaa kwenye nyumba za madongo....wanakula wadudu/majani....mlo mmoja mbovu....maji machafu...afya duni....elimu duni...watoto wanasomea chini...shule ziko mbali...vituo vya afya viko mbali....wahudumu wa afya hamna wa kutosha....yaani shida bin shida...utashangaa wanawezaje kuishi vile.....sasa watu hawa ndio wengi TZ...kwa maana ya raia wanaoishi vijijini....Na tena ukimwona anacheka ujue kapata labda mlo wa pili siku hiyo...haya ndio maisha ya watanzania wengi huko vijijini...

...Denmark ndio nchi yenye watu wenye furaha zaidi duniani...na ukienda kule huoni maskini....kila mtu anaishi vema...nyumba za maana kwa kila raia...huoni tofauti ya matajiri na maskini....watu wote wana uwezo wa kusoma hadi chuo kikuu kwa mapenzi yao...huduma bora kabisa za afya na elimu...miundo mbinu bora kabisa...chakula bora(hata maji unakunywa moja kwa moja toka bombani)....vifo vya mama na mtoto ni zero....raia wote wana uwezo wa kumiliki vyombo vya moto.....huduma bora kabisa za usafiri na mioundo mbinu yote.....sasa kwa maisha haya kwanini raia hawa wasiwe na furaha kabisa!!
 
Somalia eti watu wana furaha kuliko Tanzania.HIYO RIPOTI NI YA MATAPELI wa kimataifa.
 
Somalia eti watu wana furaha kuliko Tanzania.HIYO RIPOTI NI YA MATAPELI wa kimataifa.
..ni kweli....watanzania kitu kinachowafanya uwaone wana furaha ni unafiki wao (haswa wanaoishi mijini)....lakini huko vijijini ni majanga kabisa...tembea TZ uone.....
 
..ni kweli....watanzania kitu kinachowafanya uwaone wana furaha ni unafiki wao (haswa wanaoishi mijini)....lakini huko vijijini ni majanga kabisa...tembea TZ uone.....
lakini huwezi linganisha na SOMALIA HIYO NAKATAA
 
..ni kweli....watanzania kitu kinachowafanya uwaone wana furaha ni unafiki wao (haswa wanaoishi mijini)....lakini huko vijijini ni majanga kabisa...tembea TZ uone.....
Hizo nchi ambazo ziko juu ya Tanzania hazina vijiji?
na kama vipo vina tofauti gani na vya Tanzania?
 
Hizi ndio nchi zisizo na furaha dunia.
Katika ripoti hii http://5c28efcb768db11c7204-4ffd2ff276d22135df4d1a53ae141422.r82.cf5.rackcdn.com/HR-V1_web.pdf inayoonyesha nchi zenye furaha duniani iliyototewa iliyotolewa hivi karibuni mataifa yafuatayo yamebainika hayana furaha baada ya utafiti uliofanywa katika mataifa 157 duniani.
148.Madagascar (3.695)
149.Tanzania (3.666)
150.Liberia (3.622)
151.Guinea (3.607)
152.Rwanda (3.515)
153.Benin (3.484)
154.Afghanistan (3.360)
155.Togo (3.303)
156.Syria (3.069)
157.Burundi (2.905)

source:World's happiest countries named - CNN.com

Katika orodha hii Syria,Afghanistan,Burundi mara kwa mara kuna machafuko na vurugu, mpaka hivi sasa kuna machafuko ya kisiasa na vita hivyo ni bayana kuwa raia wa mataifa haya hawana furaha kutokana na machafuko yanayoendelea na wengi wao wamekimbia nchi zao na kuwa wakimbizi.
1. Je Tanzania ilistahili kuwa kwenye kumi dhaifu ama nchi ya tisa kutoka mwisho?
2. Je ni kwanini Tanzania ina amani lakini watu wake hawana furaha?
3. Unafikiri nini chanzo cha ukosefu wa furaha kwa watanzania?
 
Wametumia kigezo kipi? Kipindi hiki watanzania walio wengi wana furaha sana! Sababu ni kuwa wamepata matumaini mapya kutokana na rais Magufuli kuamua kuwatumikia kwa dhati kwa kupambana na ufisadi uliokuwa umekithiri!
160316121310_happinesscountries.jpg


The World Happiness Report 2016 Update looks at trends in the data recording how highly people evaluate their lives on a scale running from 0 to 10. The rankings, which are based on surveys in 156 countries covering the three years 2013-2015, reveal an average score of 5.1 (out of 10). Seven key variables explain three-quarters of the variation in annual national average scores over time and among countries: real GDP per capita, healthy life expectancy, having someone to count on, perceived freedom to make life choices, freedom from corruption, and generosity
 
..ni kweli....watanzania kitu kinachowafanya uwaone wana furaha ni unafiki wao (haswa wanaoishi mijini)....lakini huko vijijini ni majanga kabisa...tembea TZ uone.....
mkuu majanga sio vijijini tuu, bali ni kote tena ripoti haiyasema kuwa ni watu waishio vijijini tuu ndio hawana furaha bali ni wakazi wote wa mjini na vijijini pia. Vijana hawana kazi,huduma za afya zipo duni, gharama za maisha zimepanda yani kila kitu bei juu, rushwa katika kupata huduma kwenye taasisi za umma na ufisadi, yani mtu unavuja jasho kwa kazi ngumu alafu ujira mdogo sana ila wengine wanakula kirahisi tuu kupitia kula rushwa,wizi na ufisadi. Alafu unafikiri walio wengi watakuwa na furaha wakati kuna ukali wa maisha? gepu la walionacho na wasio nacho linazidi kuongezeka kwa kasi sana, huku waliowengi wakibaki pasipo na kitu na wachache wakijilimbikizia mali na kuwa na maisha mazuri yenye furaha. Sasa waliwengi hawamudu ugumu huu wa maisha, hivi watakuwa na furaha kweli? wakati hata anachokipenda hakipati? hata mahitaji ya msingi hayapati?
 
Back
Top Bottom