Inawezekana tukaendelea kwa kutegemea misaada na makusanyo ya nchi pia. Kikubwa ni uadilifu na uwajibikaji. Kuhakikisha kuwa mapato ya nchi kwa vyanzo vya ndani yanakusanywa kama ipasavyo kwa uadilifu, pia kuongeza nguvu katika uzalishaji wa viwanda, kilimo na elimu ili huduma za kijamii ziwe bora kwa maisha bora pia.
Budget isiwe inategemea zaidi misaasa (pledges), walau asilimia kama 60 - 70% iwe ni mapata ya nchi ambapo zaidi ya nusu ya budget ya maendeleo itokane na mapato ya nchi na asilimia fulani ndogo itegemee wafadhili. Tatizo ni kwamba kuna vyanzo vingi na vya kutegemeka vya mapato ya nchi vinakuwa na maslahi ya kifisadi kwa kunufaisha wachache hivyo mapato yakusanywayo hapa nchini kuwa madogo sana.
Mfano ushuru wa biashara kubwa kubwa, migodi, uingizaji wa bidhaa, utalii utaona mambo mengi yanakwepa kodi au kukusanywa kidogo ukilinganisha na uhalisia wa biashara. Hivyo hunufaisha mafisadi (wahuni) wachache. Pia siasa iwe nzuri bila kukumbatia mafisadi wachache wanaotaka vyote viwe vyao.
Pia wananchi wajikite zaidi kwenye kilimo, biashara na shughuli nyingine za kiuchumi. Tuache kuendekeza malumbano ya kijingakijinga ya haya madini tulioletewa na wageni wahuni (hasa Wazungu na Waarabu). Tuache uvivu na kujishughulisha kiakili na kimwili.
Uwekezaji uwepo ila kuhakikisha nchi inafaidi sio kupunjika, Mfano wawekezaji wa madini wanaweza kukaa miaka kadhaa eti wanachukua udongo ukapimwe nje (tonnages) na hata wakianza exploitation nchi haifaidiki sana.
Serikali kuongoza/kushauri vyanzo vya kiuchumi ili wananchi wake wapate ajira na kuwa na masha bora. Ugawanaji wa pato la nchi pia, mfano nchi yetu karibu maendeo yote yana vyanzo vizuri vya kiuchumi. Lakini sababu ya kuwa na akili ya kushikiwa hatujui au tukigundua inakuwa ni kuchelea.
Mfano Mikoa ya kusini kuna madini, pia kilimo, biashara, Uvuvi lakini no exploitation of hizo resouces. Tatizo lingine distribution of economy, ni aibu kusikia eti 70% ya pato la nchi lipo Dar Es Salaam! What is Dar es Salaam? Hivi tsunami ikija kutokea bahari na kufunika Dar ina maana TZ imekwisha!
Tuhamasishe maendeleo ya nchi nzima, ingawa ni lazima maeneo fulani yawe mbele kwa mengine, lakini sio 70% ya pato la nchi eneo moja kama inavyoonekana Dar. Badala yake kuna foleni zisizokuwa na sababu na kupoteza muda mwingi wa kufanya kazi, tatizo la high population density isiyokuwa na sababu kwa ajili ya serikali kushindwa kushughulikia na kuratibu huduma muhimu za kimaendeo sehemu nyingine za nchi.
Mkakati wa kupeleka makao makuu ya nchi Dodoma ulikuwa ni mpango mzuri sana, lakini viongozi wa serikali wameshindwa kutekeleza hilo. Ina maana kama Raisi akihama rasmi na kuacha pale ikulu karibu na soko la samaki kuwa meseum, vitu vingi vitahamia Dom na maeneo mengine na kusaidia kupunguza misongamano isiyo ya lazima Dar na pia maendeleo kusambaa maeneo mengine.
Hivyo tukijipanga na kubadili tabia tunaweza kusonga mbele kwa kwa kutegemea mapato yetu kwa kiasi kikubwa na wafadhili kwa kiasi fulani pia.