Tanzania na Misaada: Tujadili hili...

Mkuu umenisoma hasa.. Wewe ndiye mlengwa wa kuchangia hii mada,kwani una AKILI timamu...
Mtoa mada amezingatia 'Utegemezi'...mfano bajeti yetu more or less 40% inatoka kwa wahisani. Hao wamerekani na nchi nyingine zilizoendelea wanajitosheleza na bajeti zao.
 
Inawezekana tena mia kwa mia.Kama tukipata viongovi wazalendo na wachapa kazi itawezekana,Tukitumia rasilimali tulizo nazo na wasomi wetu vizuri na vile vile kuajiri wazungu ambao wametuzidi kwa teknolojia tutafika mbali sana na uwezo kwa tunao.Tz imekamilika kwa kila sekta, madini ya kila aina, Ardi nzuri, Bandari, Korosho na mengineyo.

Uholanzi inategemea usafiri wa anga kwa asilimia mia,je kama sisi tunavyote hivyo kwanini tutegemee msaada toka kwa mtu ambaye anategemea tuu njia moja ya kuingiza hela?

Kwanza tujiulize swali moja kabla ya maendeleo kufika nchi za ulaya miaka ya 1600 walikuwa wanapata wapi misaada? baada ya hapa tutaweza pata majibu mazuri zaidi
 
Asante mtoa mada kwa wazo zuri.naamini hili linawezekana kujiendesha bila misaada lakini pia kwa mikopo ambayo ni kwa lazima sana mfano wameshafanya analysisi ya any project then ndio wanakopa tatizo linakuja wanakopa hawajui hela wafanyie nini wakubwa wankwapua yote, tatizo lililopo tanzania ni uongozi mbovu wa serikali yetu na viongozi kuwa wabinafsi, na kutokuwa na mfumo mzuri wa ukusanyaji wa kodi.

Tanganyika ni nchi iliyobarikiwa sana kati ya nchi nyingi duniani ina rasilimali nyingi-madini ,vyanzo vizuri vya maji. Mbuga za wanyama.

Kwa kuzingatia mambo haya nafikiri ingeepukana na misaada na mikopo isiyokuwa ya lazima

1.Sera madhubuti kwa wawekezaji wa aina yyte ile hasa kwenye secta ya madini,na viwanda hamna msamaha wa kodi ,maana mpaka mwekezaji kaamua kuja kuwekeza ameshafanya research kwamba inalipa.

2 .ukusanyaji wa kodi na ufuatiliaji mzuri

3. Kuboresha miundombinu karibu sehemu nyingi ziwe zinafikika sio mijini tu hii itanyanyua secta ya kilimo na ufugaji.
Yapo mengi ngoja ntarudi nimetumwa na boss
 
Tanzania
tunaweza kujiendesha iwapo tutaiondoa CCM madarakani.

We need sensible conflicts and possible civil war to have Tanzanian in
full consciousness. Mahubiri, mikutano and the like is useless
kumtengeneza Mtanzania mwenye akili timamu yenye uwezo wa Kujitegemea. Kutanua UFAHAMU NA AKILI YAHITAJI MAUMIVU SI PhD!
 
Yote yanawezzekana bila ya kuwa na CCM Madarakani...............Kama CCM itaendelea kuwa madarakani hali itazidi kuwa mbaya na mwishowe tutakuja kula mizizi nchi hii.

Nahisi ukweli hapo.. Kwani umasikini ktk familia ni aibu na wakuwajibishwa ni BABA....
 
Asante mtoa mada kwa wazo zuri.naamini hili linawezekana kujiendesha bila misaada lakini pia kwa mikopo ambayo ni kwa lazima sana mfano wameshafanya analysisi ya any project then ndio wanakopa tatizo linakuja wanakopa hawajui hela wafanyie nini wakubwa wankwapua yote ,tatizo lililopo tanzania ni uongozi mbovu wa serikali yetu na viongozi kuwa wabinafsi,na kutokuwa na mfumo mzuri wa ukusanyaji wa kodi.tanganyika ni nchi iliyobarikiwa sana kati ya nchi nyingi duniani ina rasilimali nyingi-madini ,vyanzo vizuri vya maji . Mbuga za wanyama .
Kwa kuzingatia mambo haya nafikiri ingeepukana na misaada na mikopo isiyokuwa ya lazima
1.sera madhubuti kwa wawekezaji wa aina yyte ile hasa kwenye secta ya madini,na viwanda hamna msamaha wa kodi ,maana mpaka mwekezaji kaamua kuja kuwekeza ameshafanya research kwamba inalipa.
2 .ukusanyaji wa kodi na ufuatiliaji mzuri
3.kuboresha miundombinu karibu sehemu nyingi ziwe zinafikika sio mijini tu hii itanyanyua secta ya kilimo na ufugaji.
Yapo mengi ngoja ntarudi nimetumwa na boss
4.

Nafarijika na Uwingi wa WENYE AKILI TIMAMU kuchangia kwa uelewa ktk mada hii.. God bless u.. Pamoja tutaliokoa Taifa hili...
 
Tanzania ni tegemezi na masikini kwasababu viongozi wa CCM wanataka Watanzania tuendelea kuwa masikini na tegemezi.

Suluhisho ni kuiondoa CCM madarakani period.

Hatuwezi kuwa nchi ya tatu barani Afrika kwa kue export dhahabu but at the same time tuwe nchi ya tatu duniani kwa omba omba. Viongozi wa CCM ndiyo wanatu let down.
 
Ili tuendelee tunahitaji vitu vinne: watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora - Nyerere (Azimio la Arusha)

  1. Watanzania hivi sasa siasa inaongoza uchumi badala ya uchumi kuongoza siasa - hilo ni kosa
  2. Viongozi wetu wengi wamekosa uzalendo na wako tayari kuuza rasilimali zetu au kuziweka rehani kwa maslahi binafsi - hilo ni kosa jingine
Hivyo ili tujikombowe tunahitaji kijisahihisha katika maeneo hayo mawili. Nchi za Mashariki ya Mbali k.m. Malaysia na Singapore ambazo katika miaka ya 1960s tulikuwa tunafanana kiumaskini zimepiga hatua katika maendeleo. Na hii inatokana na viongozi wao kuamua kujenga uchumi na siyo siasa.

Tujisahihishe!
 
Tuna huwezo kabisa wakujitegemea bila kuomba misaada kwani tuna rasilimali za kutosha kama

: ardhi: ambozo tungeweza kuzalisha chakula cha kutosha na kuuza nje ya nchi

:Migodi: tuna migodi mingi ambayo inatoa madini tofauti, hasa tanzanite ambayo ina patikana tanzania tu, hii ingekuwa ikiongoza kuliingizia pato taifa.

Sekta ya madini ni sababu tosha ya kuto tembeza bakuli kama tuki hamua kufanya usimamizi wa hii sekta, nchi nyingi zinategemea madini kama kipato.


; Utalii nao kama ukipata usimamizi wa kutosha na kuachana na ubinafsi ni sekta ambayo ingekuwa ina liingizia taifa pesa nyingi za kigeni.Tatizo watu wachache ndio wananufaika na hii sekta!

Watanzania tunadharirika sana, kwa viongozi wetu kutembeza bakuli wakati nchi ina rasilimali za kutosha.


Jana niliona kibonzo cha masoud kipanya kikimuonesha jamaa ana omba msaada huku amekalia kigoda cha dhahabu, yule mzungu akampa msaada alaf akaanza kujiuliza huyu jamaa anaombaje msaada wakati amekalia kigoda cha dhahabu? Hlli lilikuwa dongo kwa viongozi wetu wasio jua kutumia rasilimali tulizo nazo.


Ni haibu sana nchi kama tanzania kutegemea pombe na sigara kama ndio chanzo kikuu cha mapato!


"Tanzania bila kutembeza bakuli ina wezekana"
 
Utajiri wa nchi hii ni mali yangu mimi na wewe unayesoma maneno haya na yule mtanzania mwenzetu ambaye hajabahatika kuwa hapa jf.
Cha kushangaza wengi wetu ikiwepo mimi na wewe tuna mawazo na uchungu wa namna gani wachache wanafaidika na rasilimali zetu ila hakuna wa kuchukua hatua.
Tunaona wachache wanajitahidi pale bungeni
 
Na tujiulize, Iweje tukopeshwe zaidi ikiwa Madeni ya mwanzo hatujamaliza kulipa?
KUNA NINI KIMEJIFICHA HAPO?
NA NDIO MAANA TUNAFUATA MATAKWA YAO KILE WANACHOSEMA UMEMSAHAU DAVID CAMEROON,UMESAHAU WANAVYOUTAKA MJI WA KIGAMBONI NA WAMEPEWA BWEREREEEEE,KWANI WATANZANIA HAWATAKI KUISHI SEHEMU NZURIIIII.nikuu ya mbunge wa kigamboni
 
Utajiri wa nchi hii ni mali yangu mimi na wewe unayesoma maneno haya na yule mtanzania mwenzetu ambaye hajabahatika kuwa hapa jf.
Cha kushangaza wengi wetu ikiwepo mimi na wewe tuna mawazo na uchungu wa namna gani wachache wanafaidika na rasilimali zetu ila hakuna wa kuchukua hatua.
Tunaona wachache wanajitahidi pale bungeni
na kadri wanavyojitahidi ndio jinsi wanavyousogelea msitu wa mabwepande
 
Ki vipi Mkuu? Mchango wako muhimu ....
ni kweli lakin huwaga nakasirika akujadili mambo ya serikali yetu na tanzania kwa ujumla manak eyanatia hasira sana.

hivi mkuu kwa kuangalia tu pasi hata kukaa darasani mkoa wa pwani wapaswa kuwa nyuma kimaendeleo kama ulivyo ukicompare na mabonde mazuri waliyonayo tena yenye maji? angalia nazi tu na embe dodo zinazopatikana huku pwani kabla hata ya kuangalia korosho na mabonde kama ruvu na rufiji.

hebu angalia uwekezaji pekee ktk mkoa wa pwani ni vituo vya mafuta na mahotel ambayo mengi yak bagamoyo na haya hayawez kuwa na tija hasa ya ajira kwa vijana wengi, lkn kutwa nzima hakuna la maana zaid ya misafara ya rais kwennda kwake huku akichekelea vituo vya mafuta akasahau mashamba na maji yanayotirirka bure pasi kuwa na tija.stupid kabisa
 
elimu bora,tuwe na viwanda vingi,tu export zaidi ya importation!utawala bora na creativity kama kagame
 
Uko Sahihi mkuu...
Ili tuendelee tunahitaji vitu vinne: watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora - Nyerere (Azimio la Arusha)

  1. Watanzania hivi sasa siasa inaongoza uchumi badala ya uchumi kuongoza siasa - hilo ni kosa
  2. Viongozi wetu wengi wamekosa uzalendo na wako tayari kuuza rasilimali zetu au kuziweka rehani kwa maslahi binafsi - hilo ni kosa jingine
Hivyo ili tujikombowe tunahitaji kijisahihisha katika maeneo hayo mawili. Nchi za Mashariki ya Mbali k.m. Malaysia na Singapore ambazo katika miaka ya 1960s tulikuwa tunafanana kiumaskini zimepiga hatua katika maendeleo. Na hii inatokana na viongozi wao kuamua kujenga uchumi na siyo siasa.

Tujisahihishe!
 
Jamani mimi nilikwenda moshi na arusha mwez uliopita nilishangaa kukutana na mashamba makubwa sana yaliyopendeza kwa mahindi yenye rangi nzuri na yaliyo nawiri. cha ajabu sana mvua za mwaka huu zimekuwa haba lkn hatuoni jthd za makusudi za serikali katika kuwasaidia wakulima hawa hata kidogo.

nilijiuliza hivi kwanini badala ya wakaulima hawa waliohamasishwa na kilimo kwanza wasifikiriwe mbadala wa mvua? of course lazima ofisi ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali itoe tathmini ya hali ya uchumi na jinsi ya kuuinua. sasa waforeseen badala ya kusema watu walime watoe na alternatve ya mvua. kwanini wasikipe mashine tools uwezo wa kutengeneza mitambo ya kumwagilia ili wananchi waweze kukopeshwa wanyeshee mashamba yao kisasa zaid?

leo hii inatia aibu sana kukuta mkulima amekamata jembe anatifua maji katika mfereji ili amwagilie hekari 3-10 alizolima, unaposogelea unakuta zaid ya soil erosion hakuna tija yeyote na mwishowe ni mazao kuharibika kwa kukusa rutuba. ukiangalia umwagiliaji wa kisasa unawezekana na siyo gharama kwani kwa mfano wale wakulima wa moshi almost 80% wapo karibu na mito mikubwa kama kikafu , weruweru himo nk lkn sijui watu wanawaza na makalio ama
 
haiwezi kujiendesha bila mikopo/misaada kwa sababu viongozi walioko madarakani hawana vision ya kuliondoa taifa hili kutoka iliopo sasa na kuipeleka kwenye mafanikio...
wao wameweka matumbo mbele maslahi ya taifa nyuma...
uwezekano wa kujiendesha yenyewe upo, hii itatokea endapo wananchi/umma utakapojua hatua stahiki za kuwachukulia hawa watawala wanaotanguliza mbele matumbo yao badala ya maslahi ya umma...
 
Back
Top Bottom