sikutaka nichangie lakini imebidi kwasababu wazo lako hilo ni baya sijawahi kuona. kwamba hatuwezi kujiendesha bila mikopo eti kwasababu Marekani na china wanakopa!!! kwa taarifa yako china hawadaiwi na nchi yoyote, UJERUMANI PIA hawadiwi na nchi yoyote duniani. SISI TUNASHINDWA KUJIENDESHA KWANZA KWASABABU TUMEPANUA NA KUONGEZA TAASISI ZA SERIKALI KULIKO TUNAVYO WEZA KUHIMLI. Mfano taasisi kama TAKUKURU NA POLISI wanafanyakazi zinazofanana hatukuwa na sababu ya kuanzisha takukuru!
Pili, uwezo wa kukusanya kodi na kubuni vyanzo vingine vya kodi ni mdogo.population ya TANZANIA imefikia watu mil 45 lakini vyanzo vya kodi vimebaki vilevile kwa zaidi ya miaka 40.hakuna ubunifu!!! ni lazima watanzania tubanane tusioneane huruma kodi kila mtu lazima alipe kwa kadri anavyozalisha na kutumia huduma mbalimbali.
Tatu, matumizi mabaya ya fedha za serikali. ni lazima tuwe na dhamira ya kweli ya kutumia fedha za umma kwa malengo yaliyokusudiwa na manunuzi yoyote yawe na thamani halisi ya fedha iliyotumika.Yeyote anayethibitika kutumia vibaya fedha za umma lazima akumbane na adhabu kali ikiwamo kufilisiwa.
Nne, usimamizi mbaya wa rasilimali za Nchi kupitia mikataba mibovu na isiyo na tija kwa nchi. Kama unakubali kuruhusu madini yachimbwe na Nchi ipate asilimia 3 tu kutoka kwenye madini hayo maana yake ni kwamba wewe ni mjinga ambaye huna lengo la kujinasua kutoka kwenye umasikini !!! Ni kama unasema hivi, UNAMKODISHA MTU SHAMBA LAKO ZURI SANA NA LENYE RUTUBA MKATABA UNAKUWA ATAKAYE LIMA AKIVUNA AKUPE ASLIMIA 3TU YA MAVUNO YAKE.AKIPATA MAGUNI 100 WEWE AKUPE MAGUNIA 3 TU!!!! HAKUNA NCHI YOYOTE YA ULAYA INAYOWEZA KUKUPA MKATABA WA AINA HIYO kifupi ni kwamba hatuangalii masilahi mapana ya NCHI badala yake kila mtu anaangalia mambo yake tu.
mwisho, kwa maoni yangu tunaweza tukajitegemea bila msaada au mkopo wowote kama tukijpanga na kutumia vizuri BANDARI ZETU,MISITU YETU,MBUGA ZA WANYAMA, MADINI,TUKAKAMUA KODI MAKAMPUNI KAMA VODACOM,TIGO,AIRTEL,HOTEL KUBWA ZOOOTE,NA KUWEKEZA KATIKA UZALISHAJI WA MAZAO BORA YA KILIMO NA BIDHAA ZA VIWANDANI.