Tanzania na Maendeleo ya Wajinga - What did Nyerere do?

Tunang'an'gania misaada na kusifu matokeo ya misaada, na ifike siku tuone aibu kujivunia misaada na hapo ndipo kweli tutaenda mbele. Tujifunze kuona aibu kwa vya bure na tusivitukeze. Hivi kwa nini hua hatuna aibu! Sasa hivi ujuzi wa kuomba misaada imekuwa ni SIFA KUBWA TANZANIA.
Mimi nadhani hata wote tungejua kuandika ama kusoma, chini ya CCM hamna maendeleo kwani sera zao zinalenga utegemezi na ufisadi wakati Nyerere ndiye aliyeweka misingi imara ya CCM kukubalika na wadanganyika.
 
kuanzia awamu ya pili hadi ya nne wamezembea na kuachia mafanikio makubwa yaliyopatikana wakati wa Nyerere kwa kujua kusoma na kuandika kupitia elimu ya watu wazima yapotee bure sasa hivi tumerudi nyuma zaidi kuliko hata tulipokuwa 1970.

Son:

Unaboronga hapa. Jibu ni lilelile sahihi. Elimu ilikuwa kwa kutumia misaada. Na wahisani walipobadilisha sera zao, tumejamba.

Ilikuwa ni mipango ambayo haiko-sustained na rasimali zetu wenyewe (period, koniec, end of story).

Z10

sasa ilikuwaje Nyerere aliweza kuwashawishi wafadhili au wafadhili kushawishika na sera za nyerere kuhusu "kufuta ujinga" kiasi kwamba walioko madarakani leo hii wameshindwa kufanya hivyo?

Kwanini wakati wa Mwalimu tuliweeza kufikia 90% ya watu wetu kujua kusoma na kuandika lakini leo tuko kwenye 69%? .

So, ni kitu gani kina Mwinyi, Mkapa na Kikwete wanakikosea ambacho Nyerere alikifanya sahii kwenye kufuta ujinga?

Mwanakijiji:

Mafanikio kwenye afya, elimu yalionekana lakini uchumi haukukua. Hivyo hatukuweza ku-sustain huduma za jamii.

1985 wakati anang'atuka tayari stats za elimu zishaanza kuporomoka. Literacy rate ya 90% ilifikiwa mwishoni mwa 70. Na 1985 ilikuwa kwenye 75%.

Wakuu,
haya pia ni matokeo ya SAPs za miaka ya 80 ambapo masharti yaliyowekwa na Brettonwood Institutions ( IMF na World Bank)kama njia ya kufufua uchumi yakawa ni kuondoa ruzuku katika huduma za jamii - wananchi wakalazimika kuchangia elimu iliyokuwa inatolewa bure, afya n.k.Wananchi nao hawakuwa wameandalia/wamejiandaa kupokea hali hiyo.Unapopata elimu bure, ni rahisi sana kupeleka watoto shule wakapata anagalau kujua kusoma na kuandika.Inapokuwa kuchangia hadithi inakuwa tofauti na ndiyo maana illiteracy inaongeza kwakiwango cha juu.

Tusisahau pia kuwa Nyerere kwa miaka yote alikua anakataa kukubali dawa hiyo ya IMF/World Bank na hata kuna kipindi wakatofautiana na aliyekuwa Governor wa Benki kuu wa wakati ule - Edwin Mtei.
Wakati wa awamu ya pili ya Ali Hassan Mwinyi- miaka ya katikati ya 80,sera zilibadilika kukawepo na mageuzi makubwa ya kiuchumi ( economic liberalisation) ndipo uchungu wa dawa hiyo ulipoanza kutafuna sekta zote za huduma za jamii.
 
Kumbukumbu:

Sasa sijui hicho nikiite nini. Kimsingi umesema wasilaumiwe waliomfuata bali Nyerere kwa vile "hakuacha kitu kinachojitegemea"!

Hii nadharia wahisani waliicha lini? Ni lini wahisani walibadili mipango ya kusaidia elimu, afya na maji?

Ina maana Nyerere na wahisani waliweza kuleta mafanikio katika afya na elimu lakini AHM, BWM, na JMK na wahisani wao wamefeli katika elimu lakini uchumi umekua!

Hili ni dai ambalo nitafurahi kuona ushahidi wake.

Ina maana hata wakati anaondoka bado literacy ilikuwa juu kuliko miaka ishirini ya kusamehewa madeni, soko huru n.k n.k. Nyerere then was a genius linapokuja suala la literacy!

Mwanakijiji:

Naona katafute dondoo ya jinsi misaada inavyokwamisha maendeleo ya Africa. Na perspectives za wahisani kuhusu matumizi ya misaada.

Bila kufanya hivyo utaendelea na ubishi wako wa kuhesabu mayai ya kuku kama vifaranga.
 
Wakuu,
haya pia ni matokeo ya SAPs za miaka ya 80 ambapo masharti yaliyowekwa na Brettonwood Institutions ( IMF na World Bank)kama njia ya kufufua uchumi yakawa ni kuondoa ruzuku katika huduma za jamii - wananchi wakalazimika kuchangia elimu iliyokuwa inatolewa bure, afya n.k.Wananchi nao hawakuwa wameandalia/wamejiandaa kupokea hali hiyo.Unapopata elimu bure, ni rahisi sana kupeleka watoto shule wakapata anagalau kujua kusoma na kuandika.Inapokuwa kuchangia hadithi inakuwa tofauti na ndiyo maana illiteracy inaongeza kwakiwango cha juu.

Tusisahau pia kuwa Nyerere kwa miaka yote alikua anakataa kukubali dawa hiyo ya IMF/World Bank na hata kuna kipindi wakatofautiana na aliyekuwa Governor wa Benki kuu wa wakati ule - Edwin Mtei.
Wakati wa awamu ya pili ya Ali Hassan Mwinyi- miaka ya katikati ya 80,sera zilibadilika kukawepo na mageuzi makubwa ya kiuchumi ( economic liberalisation) ndipo uchungu wa dawa hiyo ulipoanza kutafuna sekta zote za huduma za jamii.

Wos:

Asante kwa kuleta mtazamo mwingine. Kuanzia 1971-1981, Tanzania misaada yenye thamani ya 3 billioni. Mwaka 1981 wakati Nyerere anakataa masharti, misaada ilifika millioni 600 (50-60% ya bajeti). Hivyo hakuna sekta jamii iliyoweza kujiendesha pekee yake.

Hakuna nchi inayopewa tiba za SAPs, kama nchi hiyo hajavurunda kiuchumi. Na matokeo ya nchi yenye uchumi mzuri ni maendeleo katika huduma za jamii.
 
WomanofSubstance,

..hakuna mtu aliyetushikia kiboko kwenda kuomba msaada wa IMF.

..tulishindwa kujiendesha, tukawafuata IMF na WB, nao waka-prescribe kidonge vya SAP.

NB:

..mpango wa shule za sekondari za kata unarudia makosa yaliyofanyika wakati wa UPE.

..unajua at least Mwalimu tunaweza kumtetea kwamba yeye alikuwa ni mwanzilishi, hakuwa na waliomtangulia ambao angeweza kujifunza toka kwao.

..mpango wa sekondari za kata ukifeli sijui tutakuwa na maelezo na visingizio gani.
 
Mkuu Jokakuu, Zakumi et al.
Hebu turudi nyuma kidogo katika historia ya kulimbikiza madeni hadi tunafika mahali tunajishindwa.Can anyone refresh my memory kujaribu kuelewa mantiki ya kukopa kipindi kile cha miaka ya late 60s early 70s...hivi did Tz borrow from Arab countries ambazo by then kulikuwa na oil boom na many country were enticed to borrow even though they had no such need?

Mikopo yetu ilikuwa na masharti gani kipindi kile ( most went into social services which were provided free).Unapokopa halafu ukapeleka kwenye sekta zisizozalisha, matarajio ya kurejesha yalikuwa vipi? ( ni kama mtu unaenda kukopa benki na riba halafu unaishia kununua fenicha na chakula ka matumizi ya nyumbani!)
 
mimi ninawasikia vizuri sana mnayosema yaliyotokea wakati wa Mwalimu, swali langu ni how can you explain kinachotokea leo hii? Tunapokea misaada zaidi sasa hivi, tumesamehewa madeni tangu 2000, leo hii bado literacy imeshuka hadi 69%. Nyerere ametoka madarakani 1985. Baada yake wamepita marais wa wawili na sasa yupo watatu.

Kwanini, literacy bado iko chini? Kulaumu misaada sidhani kama inaelezea kwani baada ya Mwalimu kuondoka misaada ndiyo iikatiririka kwa kila aina ni mingi mno. Kwanini haielekezwi kwenye kukuza kujua kusoma na kuandika? Tumejenga shule nyingi wakati huu, tuna vyuo vikuu vingi, tuna magazeti, tv, internet, n.k Kwanini literacy bado iko chini.

Jibu lenu ni misaada na Nyerere! Really?
 
Hoja yangu hapa ni deeper; kama kwenye taifa ambalo ujinga umeongezeka lakini linajiona tajiri ja yawezekana Nyerere hakufanya sahihi kufuta ujinga na watu wakawa maskini? Je watu wenye hela mifukoni, Tv, magari, mitumba, internet n.k lakini hawana elimu ya kujua kusoma na kuandika, wanaona umuhimu gani wa kuwa na elimu?

Kama kujua kusoma na kuandika kulituacha tuwe na umaskini chini ya Nyerere, kutokujua kwetu kusoma chini ya kina Mkapa, Mwinyi na sasa JK kunatuletea "utajiri" kuna umuhimu gani wa kujua kusoma?

Yawezekana ndiyo sababu baadhi ya wizi unatokea wakati huu zaidi kuliko wakati wa Mwalimu?

MMKJJ,

Ukifuta ujinga umefuta umasikini

Watu wenye hayo maluninga , kuvaa mitumba nahayo n.k bado ni wajinga, kwahivyo bado ni masikini!

Umasikini aliotuachia Mwl. Nyerere, nafikiri wengi watakubali ulikuwa hauna ujinga.

Nyerere alitumia bakora yake ipasavyo...aliteketeza adui ujinga!

Atleast hakuna aliyekubali kuwa mjinga.

Tukija kwa hawa wa leo wanaodai kuwa tunahitaji misaada kwa ajili ya kufanya hivyo(elimu, n.k) ni masikini! Wana mtindio fulani wa ujinga kama sio wa ubongo.

Naweza kuagree nawe hapa MMKJJ, in some context- Wajinga waliwao!
 
Womnaofsubstance,

Hapa bibie nashindwa kukubaliana nanyi katika hili..

Mikopo inayopatikana ni lazima tuitumie kwa makini ktk maswala muhimu na sio swala kuweka ktk la uzalishaji tu.. Uzalishaji ni kujumu letu wenyewe wananchi kwa sababu misingi ya uzalishaji ilijengwa pia na itaendelea kujengwa ikiwa tutakuwa makini kupanga priorities zetu..

Ndio tofauti kubwa na Nyerere na viongozi hawa wengine kwani wao wanapangiwa wapi twende wakati sisi hatufahamu tunataka kwenda wapi au huko wanakotupeleka.Tunachoamini ni kwamba lazima huko mbele kuna pepo wakati hatuna mfano hata mmoja wa mtu aliyefanikiwa kwa misaada unayopangiwa masharti..

Mwalimu aliwekesha katika ELIMU, AFYA, MAJI na UMEME, huwezi kunambia hiyo ni sawa na kununua fanicha na kibaya zaidi wengi mnajaribu kupima mwanzo wa mikakati hii miaka ya 70 na 80 ktk mazingira ya leo..Nilikwisha sema hata gari mathlan Mercedes Benz ya mwaka 70 ya 80 ilikuwa tofauti na leo hii hivyo mapungufu ya gari lile wakati ule huwezi kuyalinganisha na gari la leo ili kujenga hoja..

Mbali na yote hayo ni mashirika mangapi ya Umma yalijengwa wakati wa mwalimu pamoja na kwamba mfumo wa siasa haukuwa bora..Ni mashirika mangapi leo hii tumeuza hadi kupanua mfumo wa serikali na kudai mafanikio makubwa ati wakati wa Mkapa mfuko wa hazina ulikuwa umetuna wakati tumeshindwa kuelewa kuwa mavuno yake hayakuzalishwa isipokuwa tumeuza title ya mirathi..

Matatizo ya mikopo yanajulikana dunia nzima kwamba IMF na WB ni vyombo ambavyo vinachota riba kubwa na masharti yake kwa nchi maskini ni magumu sana kuweza kuleta mabadiliko yoyote yake. Ni vyombo ambavyo vinaendeshwa na mashirika makubwa acha mbali nchi tajiri na mara zote wanahakikisha kuwa uti wa mgongo wa uzalishaji wa nchi husika hukamatwa na nchi hizi ikiwa ni pamoja na Mawasiliano, Umeme, Maji, Banks na mengineyo muhimu..

Nyerere alikuwa akikopa fedha nchi tofauti zenye nia ya kuleta m,aendeleo nchini hata kama nchi yenyewe ina mapungufu yake.. Haijalishi fedha kama zinatoka Arabuni, Israel, Nordic, Iran Marekani, Uholanzi au hata hiyo IMF ili tupate kufikia malengo tuliyoweka, na umuhimu wa mikopo hiyo ni lazima kutazama ni vitu gani tuli invest pamoja na kwamba hali yetu ilikuwa duni zaidi..

Leo hii ndugu zangu ikiwa hata Elimu tunaambiwa kwamba:-

About 40 per cent of children on average don`t continue with education despite doing well in their examinations..

Bado tunatafuta mchawi?..Hivi kweli serikali haiwezi kuweka sheria kwamba hata wale wanaoingia shule za kulipia (Private) shule hizi wanalazimika kuchukua wale wananfunzi ambao wameshinda mtihani isipokuwa wamekosa nafasi za kuendelea mbele ktk shule za serikali..Kwa nini tuna treat ELIMU kama ni biashara badala ya elimisha watu kwa mategemeo ya kupata wataalam walioelimika hivyo kurahisisha maendeleo ya nchi!.

I mean jamani hivi kweli bado mnamhitaji Nyerere kuja kuwaambia kwamba ni Ujinga mkubwa kuona mtu aloshindwa mtihani wa darasa la saba kwa mlolongo wa D na F anaingia sekondary na hata Chuo kikuu kuliko yule aliyeshinda vizuri lakini hana uwezo kifedha..Na kibaya zaidi ktk stage zote za ELIMU nchini mwisho wa yote ni asilimia zaidi ya 70 waliohitimu ni kutokana na uwezo wao kifedha badala ya uwezo wao kieleimu!..

Hivi kweli tuna unda Taifa la aina gani kwa kizazi kijacho?..

Bibie mikopo sio dhambi wala sio kitu kisichokubalika isipokuwa ni mikopo ya aina gani inayozungumziwa.

Mara zote ni mikopo ya IMF ambayo haina tofauti kabisa na Credit card na ndio maana watu wanagomba na hizo stategies zinazoambatana na SAP.. lakini hakuna mtu wala nchi iliyoanza kimaendeleo pasipo mikopo inayolenga uwekezaji ktk kile ulichokusudia kukiendeleza...Hata Malaysia na Vietnam waliokuwa nyuma yetu walikopa kwanza kabla hawajatupa magongo hayo ya mikopo...Leo hii wako mbele yetu na wanatucheka kuona bado tunategemea mikopo..

Hivyo swala sio kukopa isipokuwa utaweza vipi kuondokana na mikopo ikiwa wewe mwenyewe hujandai kuondokana nayo!.. ndivyo mataifa yote hufanya hata sisi watu bianfsi wenye vibiashara vyetu mbuzi tunajipanga kuopndokana na mikopo sio swala la kuwa niliwahi kukopa fedha benk kuwa sababu ya Ku fail kwangu..

Maendeleo ni pamoja na kuwa na wasomi wengi na kingozi yeyote anayekoip[a ili kuendeleza elimu nchini sii ujinga hata kidogo..sio lazima kutunisha mfuko wa Hazina uwe ndio manufaa ya mikopo..wakati tuna watu kama Rostam.. Huwezi kuiba ELIMU ya wananchi wako, elimu yao ni mhuri kifuani, haitoki na kwa kuelemika huko ndipo unaweza kuendeleza nchi..
 
WomanofSubstance,

..hakuna mtu aliyetushikia kiboko kwenda kuomba msaada wa IMF.

..tulishindwa kujiendesha, tukawafuata IMF na WB, nao waka-prescribe kidonge vya SAP.

NB:

..mpango wa shule za sekondari za kata unarudia makosa yaliyofanyika wakati wa UPE.

..unajua at least Mwalimu tunaweza kumtetea kwamba yeye alikuwa ni mwanzilishi, hakuwa na waliomtangulia ambao angeweza kujifunza toka kwao.

..mpango wa sekondari za kata ukifeli sijui tutakuwa na maelezo na visingizio gani.

J.Kuu Wos,
Naomba kukubali na kukataa;)

Uelevu wangu, hakuna aliyetushikia kiboko, ndio.

Hata hivyo, tuliweza kujiendesha, tulikuwa na maadili na kama sijakosea IMF na WB walijitengeneza ili waweze kuja kututafuta, my belief protectionism iliweza kufanya kazi. Bila kuwalaumu hao IMF na WB; Maadili yetu na Uzalendo umetushuka kwa sasa-tumekubali kuwa wajinga at the pretext ya kuwa 'beggars dont choose'

Visingizio na maelezo kwa kweli havina msingi, wao viongozi haswa wa sasa wanamtindio wa hio prescription, sasa kila mtu na lwake- Huu ni umasikini uliokubuhu na ndio mojayapo ya vyanzo vya ujinga(umasikini wakujitakia) tunashindwa kuweka kipaumbele kwenye kushuhudia ujinga unafutwa na kubaki kulalama IMF, WB, Nyerere na Sasa Kikwete, kama ni kweli tunasema Nyerere alituwekea misingi safi, sasa ni nini kinawafanya viongozi wetu(kwenye nyanja zote na sio Mh. Kikwete tu) kutokuwajibika na kujenga juu ya misingi hiyo?

Wajinga waliwao!

WaTZ Wake up guys!
 
Nadhani hii topic tulishaijadili na ZAKUMI NA WoS somewhere here on JF.

Nadhani swala hapa tujiulize, hiyo 90% ya wasomi aliowaacha Nyerere..ilifanya nini kuendeleza elimu? Kwa lugha nyingine kama mtu alikuwa anajua kusoma na kuandika ingekuwa rahisi kumpeleka mtoto shule. Sasa kama watu hawakupelekwa shule perhaps tatizo siyo ujinga wa kutoelewa maana na umuhimu wa elimu bali ni kukosekana kwa uwezo au ni kwamba hataki kumpeleka mtoto shule. Just thinking.

Zakumi, Mwanakijiji et al..hapa tusiwe apologetic. Ukweli ni kwamba elimu yetu Tanzania imezorota sana. Na wala hapa wa kulaumu siyo Nyerere, WB, IMF wala wahisani. Ni sisi kama taifa. Elimu HATUKUIPA na HATUIPI kipaumbele stahiki yake. Mpaka leo angalia bajeti ya elimu ni kiasi gani (% kubwa inaishia kulipa mishahara ya walimu), tujiulize tunawekeza kiasi gani katika utafiti? Tujiulize..serikali inatoa support kwa raia wa ngapi kila mwaka kwenda kwenye "cutting age institutions" kupata ujuzi? JAMANI hapa ukweli ni kwamba Nyerere alifanikiwa kwa sababu Elimu aliipa kipaumbele. Nukta. Huduma za msingi zilifanikiwa-(mpaka kwetu tukawa na matank ya maji) kwa sababu hizi huduma zilipewa kipaumbele. Simply say..we invested in these critical areas. Na wala siyo swala la wahisani wala nini. KAMA alivyosema Mwanakijiji leo tunapokea misaada mingi sana. Kama tungeamua kuwa na vipaumbele na kuwekeza hizo pesa, hakika..tusingeulizana haya maswali hapa.

Leo serikali iikisema kwamba elimu inapewa priority stahiki. I can assure you..hizi statistics zitabadilika ghafla. Na tunarudi kwa waungwana hapa ambao wamekuwa wakisisitiza kwamba Serikali yetu haina vipaumbele. Huwezi tegemea tuwe na takwimu safi wakati tunawekeza zaidi katika kununua mashangingi, rada, ndege ya raisi, kuiba EPA, mikataba mibovu na kukarabati ikulu kila mwaka. Where are our priorities? Kwa umri wangu na uelewa wangu huu..sijawahi kuona nchi inayoendelea bila kuwa na vipaumbele. We simply lack priorities which reflect our needs. na tunapokuwa na hivyo vipaumbele...ni kama usiku na mchana..maana ha-reflect matatizo yetu.

All in all, sisi kama taifa ndo wa kurudi kwenye drawing board. Tujiulize vipaumbele vyetu ni vipi. Leo tunaongelea MDGs kwamba ndo vipaumbele vyetu. Lakini naomba niwe tofauti na wengi humu na kwingineko. attainment za hizi MDGs si rahisi kutuondolea umasikini. Precisely because, hizi ni priorities zilizo tungwa New York na akina Jeffrey Sachs..akina Kikwete wakaenda kusaini tuu. Sidhani kama tungekaa chini..tusingekuja na vipaumbele vinavyo reflect mazingira yetu. Na asikudanganye mtu..mataifa 190 na ushee..hatuwezi kuwa na goals zinazofanana..wote tuna matatizo..lakini yanatofautiana...Huwezi kuniambia mahitaji ya elimu Burundi ni sawa na New Zealand..ingawa hawa viongozi wote wali-endorse hizo MDGs..ni usanii mtupu. Na kibaya zaidi..wanataka tu-achieve hizi MDGs wakati pesa hakuna..perhaps tungekuwa na za kwetu..ingekuwa rahisi kujiwekea realistic budget...I will be pleasantly surprised kama hizi MDGs zitatuondolea matatizo katika nyanja husika.

Hivyo basi, mchawi siyo Nyerere wala IMF. Ni sisi tunavyopanga mipango yetu. Nadani tufike point tuache kutafuta mchawi kwa makosa yetu wenyewe. Next month ni bajeti..mtaniambia elimu tumeipa kiasi gani na ukarabati wa Ikulu tumetenga ngapi. Thats our state of affairs. Sad but true.

Kusema kwamba Nyerere anahusika na hii current state of our education "we are just losing both of our moral and intellectual bearing.
 
mimi ninawasikia vizuri sana mnayosema yaliyotokea wakati wa Mwalimu, swali langu ni how can you explain kinachotokea leo hii? Tunapokea misaada zaidi sasa hivi, tumesamehewa madeni tangu 2000, leo hii bado literacy imeshuka hadi 69%. Nyerere ametoka madarakani 1985. Baada yake wamepita marais wa wawili na sasa yupo watatu.

Kwanini, literacy bado iko chini? Kulaumu misaada sidhani kama inaelezea kwani baada ya Mwalimu kuondoka misaada ndiyo iikatiririka kwa kila aina ni mingi mno. Kwanini haielekezwi kwenye kukuza kujua kusoma na kuandika? Tumejenga shule nyingi wakati huu, tuna vyuo vikuu vingi, tuna magazeti, tv, internet, n.k Kwanini literacy bado iko chini.

Jibu lenu ni misaada na Nyerere! Really?

Kuhusu suala lako la kuwepo vyuo, TV na bado kuwa na literacy ya 69%. Kuna mambo mengi ya kuangalia. Mojawapo ni kushindwa kwa sera ya vijiji vya ujamaa.

Mara nyingi tuna-overlook muundo wa vijiji vya ujamaa kusaidia kukuza literacy rate.

Sehemu fulani ya kupungua kwa literacy imesababisha na attendance mbovu ya wanafunzi.

Wakati wa vijiji vya Ujamaa, ilikuwa rahisi kufuatilia jinsi watoto wanavyokwenda shuleni. Nakumbuka baadhi ya wazazi walipelekwa jela kwa kushindwa kupeleka watoto shule.

Sasa hivi kuna watu wamerudia maisha kwenye vijiji vyao vya zamani. Ni nani atakayemlazimisha mtoto anayeishi huko kwenda shule?
 
Mbona unajikanganya?

ZK
Unadai kushindwa kwa sera ya vijiji vya ujamaa bado unaendelea kudai muundo wa vijiji vya ujamaa kwa namna moja au nyingine tulipata elimu au ilipunguza literacy rate, vipi hapa?

Attendance?

Kweli katika mda huu na wakati kuna kumlazimisha? Huyo anayelazimishwa naye ni punguani wa aina fulani-Tunashindwa kulazimisha kusitisha ufisadi tutalazimisha mtoto kwenda shule? Haya ndio Maendeleo ya Wajinga

Kwa nini isiwe sera ya elimu?
 
Nadhani hii topic tulishaijadili na ZAKUMI NA WoS somewhere here on JF.

Nadhani swala hapa tujiulize, hiyo 90% ya wasomi aliowaacha Nyerere..ilifanya nini kuendeleza elimu? Kwa lugha nyingine kama mtu alikuwa anajua kusoma na kuandika ingekuwa rahisi kumpeleka mtoto shule. Sasa kama watu hawakupelekwa shule perhaps tatizo siyo ujinga wa kutoelewa maana na umuhimu wa elimu bali ni kukosekana kwa uwezo au ni kwamba hataki kumpeleka mtoto shule. Just thinking.

Zakumi, Mwanakijiji et al..hapa tusiwe apologetic. Ukweli ni kwamba elimu yetu Tanzania imezorota sana. Na wala hapa wa kulaumu siyo Nyerere, WB, IMF wala wahisani. Ni sisi kama taifa. Elimu HATUKUIPA na HATUIPI kipaumbele stahiki yake. Mpaka leo angalia bajeti ya elimu ni kiasi gani (% kubwa inaishia kulipa mishahara ya walimu), tujiulize tunawekeza kiasi gani katika utafiti? Tujiulize..serikali inatoa support kwa raia wa ngapi kila mwaka kwenda kwenye "cutting age institutions" kupata ujuzi? JAMANI hapa ukweli ni kwamba Nyerere alifanikiwa kwa sababu Elimu aliipa kipaumbele. Nukta. Huduma za msingi zilifanikiwa-(mpaka kwetu tukawa na matank ya maji) kwa sababu hizi huduma zilipewa kipaumbele. Simply say..we invested in these critical areas. Na wala siyo swala la wahisani wala nini. KAMA alivyosema Mwanakijiji leo tunapokea misaada mingi sana. Kama tungeamua kuwa na vipaumbele na kuwekeza hizo pesa, hakika..tusingeulizana haya maswali hapa.

Leo serikali iikisema kwamba elimu inapewa priority stahiki. I can assure you..hizi statistics zitabadilika ghafla. Na tunarudi kwa waungwana hapa ambao wamekuwa wakisisitiza kwamba Serikali yetu haina vipaumbele. Huwezi tegemea tuwe na takwimu safi wakati tunawekeza zaidi katika kununua mashangingi, rada, ndege ya raisi, kuiba EPA, mikataba mibovu na kukarabati ikulu kila mwaka. Where are our priorities? Kwa umri wangu na uelewa wangu huu..sijawahi kuona nchi inayoendelea bila kuwa na vipaumbele. We simply lack priorities which reflect our needs. na tunapokuwa na hivyo vipaumbele...ni kama usiku na mchana..maana ha-reflect matatizo yetu.

All in all, sisi kama taifa ndo wa kurudi kwenye drawing board. Tujiulize vipaumbele vyetu ni vipi. Leo tunaongelea MDGs kwamba ndo vipaumbele vyetu. Lakini naomba niwe tofauti na wengi humu na kwingineko. attainment za hizi MDGs si rahisi kutuondolea umasikini. Precisely because, hizi ni priorities zilizo tungwa New York na akina Jeffrey Sachs..akina Kikwete wakaenda kusaini tuu. Sidhani kama tungekaa chini..tusingekuja na vipaumbele vinavyo reflect mazingira yetu. Na asikudanganye mtu..mataifa 190 na ushee..hatuwezi kuwa na goals zinazofanana..wote tuna matatizo..lakini yanatofautiana...Huwezi kuniambia mahitaji ya elimu Burundi ni sawa na New Zealand..ingawa hawa viongozi wote wali-endorse hizo MDGs..ni usanii mtupu. Na kibaya zaidi..wanataka tu-achieve hizi MDGs wakati pesa hakuna..perhaps tungekuwa na za kwetu..ingekuwa rahisi kujiwekea realistic budget...I will be pleasantly surprised kama hizi MDGs zitatuondolea matatizo katika nyanja husika.

Hivyo basi, mchawi siyo Nyerere wala IMF. Ni sisi tunavyopanga mipango yetu. Nadani tufike point tuache kutafuta mchawi kwa makosa yetu wenyewe. Next month ni bajeti..mtaniambia elimu tumeipa kiasi gani na ukarabati wa Ikulu tumetenga ngapi. Thats our state of affairs. Sad but true.

Kusema kwamba Nyerere anahusika na hii current state of our education "we are just losing both of our moral and intellectual bearing.

Masanja:

If you don't learn from your past mistakes, you are likely to repeat them. Ndugu yangu Jokakuu na mimi tunamwita Nyerere pioneer au Mwanzilishi. Likehood ya pioneer ku-introduce failure ni kubwa sana kuliko wanaomfuatia.

Hivyo mtu akileta mada kuhusu mafanikio yaliopatikana wakati wa Nyerere ni lazima tueleze makosa. Kwa sababu kama mafanikio hayo hayakuwa ya nguvu za gas basi yangeendelea kuwepo.

Kwa mfano JK na Lowasa wali-model mfumo wa elimu wa sekondari za kata kwa kutumia mfumo wa elimu ya UPE. Lakini inaeleweka wazi kuwa UPE ilikuwa na nguvu za gas.

Vilevile huwezi kuhesabu mayai ya kuku kama vifaranga. Elimu hili iweze kutoa matunda ni lazima iwe ya muda mrefu.

Tulikuwa na programs za elimu lakini hazikukaa kwa muda mrefu. Hivyo baadhi ya jamii au familia mipango hii ya elimu haikuingia damuni. Hivyo wao kutompleka shule mtoto ni kitu cha kawaida. Hivyo unaweza kuwa na literacy kubwa pale unapowalazimisha watu kwenda shule, lakini ukiacha kila mtu anarudi kwenye maisha yake ya kawaida.
 
................Hivyo mtu akileta mada kuhusu mafanikio yaliopatikana wakati wa Nyerere ni lazima tueleze makosa. Kwa sababu kama mafanikio hayo hayakuwa ya nguvu za gas basi yangeendelea kuwepo........

vipi kama mengine aliyoanzisha Mwl JKN yalihujumiwa kwa makusudi ili kunufaisha UFISADI wa wakati huo na unaoendelea hivi sasa?
 
Zakumi,
If you don't learn from your past mistakes, you are likely to repeat them. Ndugu yangu Jokakuu na mimi tunamwita Nyerere pioneer au Mwanzilishi. Likehood ya pioneer ku-introduce failure ni kubwa sana kuliko wanaomfuatia.
..
Mkuu labda unashindwa kuelewa kwamba mambo yote yanayofanywa sasa toka kuanzishwa kwa mikakati ya SAP ni kuondokana na makosa ya Nyerere na matokeo yake ndio mafanikio ya ELIMU imefikia hapa tulipo..Hakuna hata moja ambalo tunalifanya leo limetokana na mfomu wa Ujamaa.. hakuna.

Kitu kimoja tu unachoshindwa kuelewa (kutoka report ile) ni kwamba kati ya wanafunzi 100 leo hii 50 hushinda mtihani wa kwenda mbele (hii tunafahamu toka report ya waziri wa Elimu) lakini kati ya hao asilimia 50 walioshinda (convert to 100%), asilimia 40 kati yao hukosa nafasi za kuendelea na masomo yaani
Haya madudu haya hayatokani na Ujamaa wala rekord ya kuhudhuria shule tena basi tukiweka na asilimia ya watoto wanaoshindwa kuhudhuria sijui tutakuwa tunazungumzia asilimia ngapi!..

Hii yote ina maana ni karibu asilimia 30 ya watoto wote ndio wanaopata nafasi za kuendelea na masomo..Na tukitazama hadi hatua ya chuo kikuu sijui huko huwa tunabaki na asilimia ngapi..
Kuondokana na vijiji vya Ujamaa haikuwa failure ya mwalimu bali sisi wenyewe tumeachana na mfumo na leo hii miji yetu mikubwa ndio kila mtu anahamia kiasi kwamba kiwanja tu kimefikia mshahara wa mtu wa mwaka mzima..Nina hakika kabisa kwamba leo hii tukifanya sensa nadhani itakuja gundulika kwamba wananchi wengi wanaishi mijini kuliko vijijini..Bado tunatumia takwimu za wakati wa Mwalimu kuijenga Tanzania mpya ambayo ni tofauti kabisa na ile ya Kijamaa.

Mkuu wangu nchi kama China walikuwa ranked chini ya 50 after the collapse of Cold war, Russia ilikuwa nchi ya 40 kiuchumi baada ya kuvunjika kwa USSR na kuundwa kwa Russia federation, leo hii Russia ni nchi ya 7 na China inakimbilia kuwa Super power, tena basi wote hawa bado kabisa wanatukuza mazuri yote yaliyotokana na Uongozi uliotangulia badala ya mabaya ya viongozi kwa sababu wamepata jawabu na mbinu za kujiendeleza sio kutokana na kuchunguza mabaya.

Mkuu wangu tunapojifunza kutokana na makosa yaliyopita ni muhimu sana kufahamu jawabu la makosa yale na sio kuyasoma makosa yenyewe ili upate jawabu kutokana na makosa yenyewe..Mfano 2+2=5, ni makosa na huwezi kujifunza lolote kutokana na maandishi haya zaidi ya kutafuta mbinu zinazotakiwa upate jawabu lililokuwa sawa na utarudi tu kutazama makosa uiloyafanya baada ya kufahamu kwa nini 2+2=4..
 
The 69% is simple logic! There is no connection between academic achievement and anything! Being a bright child in school does not provide you a scholarship! Finishing on top of your class does not provide you a job! Doing research does not give you a voice! There are no awards for outstanding students! No celebration for intellegence!

In short the system of reward and punishment in education is not working. Going to school is a procedure which finds no significancy attachment between academic and chances of success! You could get a job even if you flank your exams. You became a ministry of natural resources even if you have studied art! Specialization is not full respected. Where there is a country crisis, political commitee hold more power more than field experties! what do we expect!

Nchi inaenda kimishemishe tu! So, why should one toil while there are other avenues for success! Until we find that link between education and people well being, until we make education as a main avenue for success, center for development plan and the only route for addressing inequalities the literacy rate will keep falling down.
 
Last edited:

Bob, hili ndo somo ambalo watanganyika hatujawahi kubahatika kulielewa.

Tuzidi kupambana iko siku kitaeleweka.

Its completely unfair kulaumu ujamaa kwa failure katika sector ya elimu tuliyonayo leo. Kwa hiyo sasa tuseme hata huduma za hospitali na maji...mbona wakati huo wa ujamaa maji yalikuwa yanafika vijijini? kipi kimefanya maji yakakauka kwenye mabomba? After all mabomba yalikuwepo tayari...sasa sjui tutalaumu Nyerere..wakati alishafanya kazi kubwa ya kuunganisha mabomba..kitu ambacho sisi tunatakiwa kufanya ni kuhakikisha maji yanazidi ku-flow. Hilo tuu. Hapana, kama anavyosema Bob Tatizo tunalo sisi wenyewe. Hainingii akilini leo Kikwete anashindwa kushughulikia tatizo la umeme..anabaki analaumu mikataba ya IPTL na mengineyo..wakati angeangalia ni wapi kosa lilipofanyika..na kurekebisha hiyo mikataba.
 
Masanja na Mkandara:

Mnaanza kuleta side shows sasa. Hili suala la kukua kwa elimu katika miaka ya 70 na kuboronga baadaye alikutokea Tanzania peke yake. Limetokea katika nchi nyingi ukiondoa za South East Asia ambazo zimejitahidi kuvuka threshold ya umasikini. Hivyo sio suala la Ujamaa.

Bila haya mna-compare China na Urusi. China ina continuous civilization kwa zaidi ya miaka 3000. Waligundua baruti, karatasi, matumizi ya noti, alphabet na mambo mengi. Mambo mengi waliyofanya miaka 1000 iliyopita bado hayajafikiwa katika jamii yetu leo hii.

Mnazungumzia Urusi nchi inayotoa Brilliant Mathematicians kwa zaidi ya miaka mia moja tena kwenye taasisi zilizojengwa na wafalme na sio comrades.
 
The 69% is simple logic! There is no connection between academic achievement and anything! Being a bright child in school does not provide you a scholarship! Finishing on top of your class does not provide you a job! Doing research does not give you a voice! There are no awards for outstanding students! No celebration for intellegence!

In short the system of reward and punishment in education is not working. Going to school is a procedure which finds no significancy attachment between academic and chances of success! You could get a job even if you flank your exams. You became a ministry of natural resources even if you have studied art! Specialization is not full respected. Where there is a country crisis, political commitee hold more power more than field experties! what do we expect!

Nchi inaenda kimishemishe tu! So, why should one toil while there are other avenues for success! Until we find that link between education and people well being, until we make education as a main avenue for success, center for development plan and the only route for addressing inequalities the literacy rate will keep falling down.

PH:

Kuna ukweli kwenye posti yako. Hii percent ya 69% ina-reflect Tanzania nzima. Hivyo kama Mtwara wana 40% na Kilimanjaro wana 95%, jibu tutakalopata ni kuwa Tanzania nzima bado ni 69% kwa sababu hii ni stats ya kitaifa.

Tukiwa na data za mikoa, huu mjadala mzima utakwisha kwa sababu education is incentive driven.
 
Back
Top Bottom