Tanzania na china zakusudia kuandaa tamasha la utamaduni na utalii mwaka 2024

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
738
479
Wizara ya Utamaduni na Utalii kutoka Jamhuri ya Watu wa China imeiomba Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kushirikiana katika kuandaa tamasha kubwa litakalohusisha sekta ya Utamaduni na Utalii mwaka 2024.

Ombi hilo kutoka Serikali ya China limepokelewa Agosti 23, 2023 na Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bi. Neema Msitha kwa niaba ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Aidha, ujumbe huo umesema Serikali ya China kupitia Wizara ya Utamaduni na Utalii inakusudia tamasha hilo litahusisha Tanzania Bara na Visiwani, huku matukio ya ufunguzi na ufungaji kila moja liwe katika nchi mojawapo.

Bi. Msitha ameuambia ujumbe huo kutoka Ubalozi wa China kuwa, Serikali ya Tanzania iko tayari kushirikiana na China katika mambo mengi na watajibiwa kwa maandishi baada ya kuwasilisha barua kwa Waziri mwenye dhamana ili utekelezaji wake uanze.

Kikao hicho kiliongozwa na Katibu Mtendaji wa BMT Bi. Neema Msitha kwa niaba ya Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana na kuhudhuriwa na Bi. Angela Michael kutoka BASATA, Nicholas Mihayo wa BMT, Zhang Weigno kutoka Idara ya Utamaduni na Utalii China, Wang Siping, Che Zhaognang, Chen Lekang, Xn YongLiang kutoka ubalozi wa china nchini Tanzania.View attachment 2727141View attachment 2727142View attachment 2727143View attachment 2727144View attachment 2727145View attachment 2727146View attachment 2727147View attachment 2727148
IMG-20230824-WA0022.jpg
IMG-20230824-WA0020.jpg
IMG-20230824-WA0021.jpg
IMG-20230824-WA0024.jpg
 
Back
Top Bottom