AMANIPARTY
Member
- Jun 2, 2011
- 15
- 7
WATANZANIA tunao mtaji ambao ni hazina Ndani ya nchi yetu katika mambo makuu matatu:
1. Lugha: Watanzania Tuna Hazina ya Lugha ya Kishwahili ambayo sio chimbuko la kabila mojawapo ndani ya Nchi yetu. Mateso Tuliyoyapata kwenye Biashara kandamivu ya Utumwa, Mchanganyiko wa zaidi ya lugha za makabila 360 ndani ya nchi yetu, pamoja na jitiada binafsi za waasisi wa Taifa Letu akiwemo Marehemu Mwalimu Julias Kambarage Nyerere, zimeleta matunda ya kuwa na Lugha hii. Majirani zetu Kenya na Uganda hawana bahati hii.. Mataifa mfano Japan, China, Korea wote hawana bahati hii, wao wanatumia Lugha ya kabila Moja tu ambalo ndilo lilikuwa asisi la ufalme wa nchi zao na likapewa hadhi ya kuwa Lugha ya mataifa yao na kupoteza kabisa Lugha nyingine na kuziondoa kwenye tasnia ya mawasiliano kiasi kwamba baada ya miongo kadhaa lugha hizo za makabila mengine zikapotea Duniani. Marekani haina bahati hii, wanatumia Lugha ya Kabila la Malkia wa uingereza ambayo wameibadilisha kidogo tu matamshi yake. CHAMA CHA AMANI(CCA) kinamini Kishwahili Chetu kikiheshimiwa na kupewa stahiki yake kama Lugha ya Taifa HURU, kinaweza kutumika kama Lugha si ya mawasiliano tu bali pia Lugha ya biashara, michezo/fani na Elimu.
2. Akili na Uelewa: Watanzania wana Akili na Uelewa wa hali ya juu sana nadhani kuliko Taifa lolote Ulimwenguni. Akili na Upeo wa uelewa huu bado umelazwa. Watanzania bado hawajapata mtu wa kuwaamsha na kuwaambia waanze kutumia akili na uelewa walionao. CHAMA CHA AMANI(CCA)tunamini kwamba akili za watanzania zikiamshwa na kuamrishwa kuanza kufikiri tunaweza kuwa na Taifa lililoendelea kwenye Uvumbuzi na teknolojia ya hali ya Juu sana ulimwenguni na hivyo Watanzania tukawa sio soko la kujaribia teknolojia na bidha za wenzetu. Watanzania wenyewe tutabuni na kutengeneza Viwanda vitavyozalisha bidhaa zinazotufaa kwa matumizi yetu kwanza kabla ya kupeleka mgao kwa majrani zetu. Nchi haiwezi kuwepo ikiwa inatumia bidhaa, technolojia na elimu ya nchi nyingine.
3.Uhuru: Tunaamini kwamba Binadamu wote ni zao la Imani. Mpaka sasa hakuna sayansi wala nchi wala serikali yoyote iliyofanikiwa kufafanua asili ya mwanadamu. Hivyo wote bado tunaamini mwanadamu ni Zao la Imani. kama ni Hivyo basi hakuna mwanadamu mwenye amri kubwa zaidi juu ya mwenzake. Hakuna Taifa lenye mipaka yake na serikali yake linaloweza kuingilia matakwa na kutunisha misuli yake kwenye taifa Jingine. CHAMA CHA AMANI (CCA) Tunamini Hilo, Kwa Hivyo Tuna kila sababu ya kuidai Tanzania HURU. Mataifa yanayojiita yenyewe makubwa.. basi kwa Ukubwa wao uwe pia ukubwa wa uelewa wao, watuelewa Hivyo na kuheshimu Uhuru wa Taifa Hili kama majarida ya Umoja wao yanavyofafanua. Hatutaki Ukloni mamboleo, hatutaki kpangia nini na lini tufanye nini, Tunapohitaji kuchagua viongozi wetu tuacheni tutumie rasilimali na uwezo tulionao sio kupewa msaada na pesa kwenye kila kitu. Tunahitaji kumiliki migodi na rasilimali zote za inchi yetu, ni zetu, tuachieni tufanye kile tunachodhani ni sahihi ndani ya mipaka yetu, hatuhitaji mtufundishie Jeshi letu nani wa kumpiga na wapi pa kumpiga, Tuacheni tujijue wenyewe, kwani Nie nani aliwafundisha? kiasi kwamba mjipe kuwa walimu wa wengine. Hatuhitaji silaha zenu, tunahitaji Kutengeneza na kutumia za kwetu kwa mbinu za kwetu pia. Toka lini mtu akamuuzia adui yake silaha yenye uwezo wa kumpiga yeye mwenyewe? haiwezekani.. Daima mnatuuzia silaha hafifu zinazotugombanisha na kuuana sisi kwa sisi. INATOSHA. Sisi ndio tunapaswa kutoa misaada sio kupewa misaada. Tanzania Mpya Inakuja.. Mimi wewe na sisi Tutaiwezesha. AMANI DAIMA!
Asanteni