Tanzania, Misri kuanzisha mashamba ya ngano, mpunga

diana chumbikino

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
428
Reaction score
368
SERIKALI ya Tanzania na Misri zinatarajia kusaini mkataba wa makubaliano wa kuanzisha mashamba makubwa ya pamoja kwa lengo la kuinua kilicho cha ngano, mpunga na pamba. Hayo yamebainishwa na Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga baada ya kuzungumza na wataalamu wa kilimo kutoka Misri wakiongozwa na Waziri wa Kilimo na Ardhi wa nchi hiyo, Dk Ezzidine Abu Stiet. Amesema katika mazungumzo hayo wamekubaliana kushirikiana katia sekta ya kilimo husani katika mazao ya mpunga, ngano na pamba ambapo tande zote mbili zitakuwa na mashamba ya pamoja.

“Kama mnavyojua Misri wamepiga hatua katika kilimo hususani kilimo cha umwagiliaji na tekinolojia hivyo tumekubaliana mafaniko hayo yahamie hapa nchini,” amesema Hasunga. “Baada ya mazungumzo ya kina na makubaliano katika maeneo ya ushirikiano, tumepeana miezi mwili ili ikapo mwezi Mei mwaka huu, basi tusaini mkataba wa makubaliano na kuanza utekelezaji"amesema Hasunga.

Amesema eneo lingine ambapo wamekubaliana ni kuimarisha vituo vya utati wa mazao ili kupata mbegu bora na namna bora ya kuzitumia mbegu hizo na pia kuhamisha ujuzi na zana kutoka Misri utakaosaidia kuinua kilimo nchini.
 
Ranchi nyingi za taifa zimekufa ama kutoa maeneo wachungaji wachunge mifugo yao.

Mradi wa Dakawa irrigation scheme nao ndio hivyo tena etc etc etc.

Naamini kwa dhati kabisa, baada ya hii MoU Tanzania ikikabidhiwa hii miradi iisimamie hakuna kitakachoendelea.

Shida ni kuwa na viongozi ambao hawana maono ya kibiashara.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kile chetu cha MPUNGA na WAIRAN pia WAKOREA kiliishia wapi?
Tusipoangalia tulikojikwaa tutaendelea na maumivu yasiyoisha
 
“Kama mnavyojua Misri wamepiga hatua katika kilimo hususani kilimo cha umwagiliaji na tekinolojia hivyo tumekubaliana mafaniko hayo yahamie hapa nchini,”

Uvivu wa kufikiri na kutenda, SUA ipo miaka mingi sana, kwanini isiwezeshwe ikapewa resources ikafanya hayo yote, wanasomesha wataalam maelfu wanakosa ajira, kwanini wasijengewe uwezo wakafanya uzalishaji na hata kwenda kuwekeza Misri

Miaka ya nyuma kulikuwa na uzalishaji mkubwa sana wa ngano na mpunga nyanda za juu kusini tunashindwa nini kutazama wapi tulikosea tukarekebisha
 
Ranchi nyingi za taifa zimekufa ama kutoa maeneo wachungaji wachunge mifugo yao.
Mradi wa Dakawa irrigation scheme nao ndio hivyo tena etc etc etc.

Naamini kwa dhati kabisa, baada ya hii MoU Tanzania ikikabidhiwa hii miradi iisimamie hakuna kitakachoendelea.

Shida ni kuwa na viongozi ambao hawana maono ya kibiashara.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mi nadhani tatizo letu ni kuleta itikadi kwenye kila suala linalohusu maendeleo. Sio ajabu watakaochaguliwa kusimamia huo mradi ni makada wasio na uzoefu wowote na mambo ya biashara

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom