Tanzania: Maisha ya watu yanapowekwa rehani dhidi ya maslahi binafsi ya kiuchumi

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
28,106
36,076
Ni kwa masikitiko makubwa ninaandika uzi huu. Ninaandika baada ya kuwa nimechukua muda wa kutosha kufuatilia yanayojiri katika nchi zinazotuzunguka kulingana na hali yetu halisi hapa kama ilivyo sasa.

Hapa kwetu tayari imekuwa ni tanzia baada ya tanzia hata labda, ni muda muafaka sasa kwa mods hapa jf kufikiria kuanzisha jukwaa mahsusi la tanzia peke yake.

Ikumbukwe, tanzia tunazoziona humu, katika muda ambao kabla nasi hatujarejea kwake Maulana bila shaka kwa matatizo yale yale ya kupumua, ni za wale vigogo tu. Vigogo wenye majina yao. Kina kaj**ba nani, nani atawafahamu kiasi cha kuwafanya nao wawe habari inayo merit kuwa reported?

Ikumbukwe pia kama kawaida yao mavuvuzela yaliyoapizwa kuunga mkono kila juhudi (pasipo na kujali) wameongeza juhudi zaidi kufunika mambo kwa mapambio yao ya kusifia na hata kudunisha idadi ya vifo na sababu za vifo, ati kuwa vifo huwa kawaida. Ati kuwa hata kabla ya Corona watu walikuwa wanakufa na ati kuwa kila kifo si Corona.

Wanawafanya watu majuha kwa njaa zao na ati kuwa wengine ni majuha zaidi kuliko wao. Nani asiyejua kifo cha Corona na kisicho cha Corona hata kwa kuona mazishi au handling yake tu? Ila tu mavuvuzela ndiyo yenye kufahamu?

Aibu kwenu (shame on you)!

Mafumbo kawafumbieni wajinga.

Mheshimiwa alitamka mwenyewe kuwa analinda uchumi na kuwa haka ka ugonjwa ni ka upepo tu tena katapita. Anataka tuchape kazi tu, akiitisha kujifukiza kama suluhu ikiwa katatukumba. Watu wanapukutika. Na eti ni dhambi ukweli huo ukitamkwa. Mambo ya ajabu na kweli katika Tanzania ya leo.

Tuko tofauti sana na wenzetu wanaotuzunguka.

Kenya, Kenyatta katamka wazi kuwa katu hata hatarisha maisha ya watu kwa maslahi ya uchumi. Tumerogwa na nani sisi?










Hivi nyie bungeni bajeti ya nini mnayo panga na nani mnaye mpangia, kwa kasi hii ya matanzia tunayo endelea kuyasikia tena kuanzia hapo hapo Dodoma mlipo?

Siyo tamaa kweli ya posho na marupurupu yenu mliyoweka mbele dhidi ya maisha ya watu mkiwamo nyie wenyewe?

Ama kweli tamaa mbele mauti nyuma.

Wenzetu wengine Rwanda na Uganda wenye msimamo kama wa Kenyatta tayari ugonjwa makwao wamesha udhibiti vilivyo. Maambukizi yamepungua mno (hakuna vifo) na taratibu tayari wanaanza kurudi kwenye maisha ya kawaida:

Rwanda 1.jpg
Rwanda 2.jpg


Sisi kwa kuweka maslahi binafsi ya uchumi mbele tuko hapa:

2386468_Corona_State.jpg

Inawezekana namna gani:

Maambukizi mapya 196. Jumla ya maambukizi 480. Lakini wanaofuatiliwa hamna wala wasafiri waliopo quarantine pia hamna? Sisi ndiyo ambao hata mgonjwa wa Corona akionekana sopu sopu anaachiwa kwenda kujifukiza. Kwetu si kuwa, suala la kuambukiza wengine siyo tatizo, ndiyo maana wagonjwa wa Corona wanatoroka mahospitalini kwenda kujifukiza nyungu kama mheshimiwa waziri alivyoweka misisitizo?

Tuna mkakati gani wa kuzuia maambukizi? Tunamkakati gani wa kuutokomeza ugonjwa? Tuna mkakati gani wa kuwahami wananchi na ugonjwa? Tunajifunza nini toka kwa wenzetu hawa ambao wengine ni hohehahe labda hata kuliko sisi?

Maswali ni mengi kuliko majibu, kiasi hata kunapoitishwa kuchangia kupambana na Corona mnatukwaza tu. Kwa hakika si rahisi kuelewa ni kupambana kupi na Corona ambako Tanzania inapanga au imechagua kupambana nako.

Muda unatutupa mkono sana na tusipokuwa makini hata muda wa mawazo mbadala tu, nao utatutupa mkono.

Imekuwa ikiulizwa kwa muda mrefu sasa hadi wafe wangapi au hadi maambukizi yafikie wapi ndipo hatua tofauti na hizi zilizopo, ziweze kuchukuliwa? Au labda hadi nani augue? Au labda hadi nani afe ndiyo hatua tofauti zichukuliwe?

Anasema gwiji Albert Einstein, "Insanity is doing the same thing over and over again and expecting different results." Mwisho wa kumnukuu.

Sote hatuwezi kukubali kuwa sehemu ya 'insanity.'

Waunga juhudi bila kujali ni zipi, hao na mapambio na mavuvuzela yao ya kutetea na hata kutuchanganya (kuleta confusion) kadri walivyotumwa na ma master (mabwana) zao, tunawajua, tunajua watakuwapo na hawatatutisha sote. Hao hatuna haja ya kuwajali wala kuwasikiliza. Ni watu wa kupuuza.

Anasema Messiah Luke 23:34:

"Father, forgive them for they don't know what they are doing." ..... Mwisho wa kunukuu.

Katu, hatuwezi kuwaachia wabinafsi, wasioelewa (yaani wajinga), washamba, washirikina, wafukiza nyungu, nk, kutuamulia na sisi wengine tusiokubaliana nao kuchagua kufa kwa Corona kwa maslahi yao binafsi.

Tumewavumilia vya kutosha, tumewaasa ya kutosha, tumewashauri ya kutosha, uvumilivu wetu sasa unaekekea mwisho. Sasa tunataka kunusuru maisha. Mambo ya uchumi kwa hali ya sasa siyo dili tena.

Mlioko pale Dodoma na Chatto mjue, habari ndiyo hiyo.


 
Yaani mtaani hakuna taharuki kabisa watu wanapambania mkate

Ila ukiingia mtandaoni kwa watu wenye vihela vyao wanadeka kweli
 
Yaani mtaani hakuna taharuki kabisa watu wanapambania mkate

Ila ukiingia mtandaoni kwa watu wenye vihela vyao wanadeka kweli

Vuvuzela #1 tayari bado wengine. Nyote mna chale. Mnajulikana.

Hoja hamna ila kuunga mkono juhudi zozote. I mean it zozote. Heri ya msukule.
 

 
Back
Top Bottom