Kama hali hii ya ujangili wa tembo itaendelea basi mjue itachukua takriban miaka 5 hadi zaidi kidogo ya miaka 10 kwa tembo wetu kumalizika!
Ingawa ni taarifa ya January 2012 lakini majibu yake yameanza kujitokeza karibuni kwa kukamatwa mfululizo meli mbili (moja baada ya nyingine katika mwezi mmoja) huko Hongkong zilizosheheni nyara za taifa zenye thamani ya mabilioni ya pesa za kitanzania.
Hebu soma mwenyewe kipande cha hii taarifa;
My take
Katika miaka 3 tu tembo wetu 31,348 wameuawa kwa ajili na kuvunwa pembe. Hii ina maana tembo 10,450 kila mwaka.
kwa hesabu ya haraka baada ya miaka 5 hadi 10 au zaidi kidogo watanzania tutakuwa hatuna tembo!
Kama inavyoonyesha hapo juu JK aliahidi kushughulikia hili swala takribani mwaka mmoja uliopita. Ingawa hatukuona kushughulikiwa kwake, ni dhahiri baada ya shehena mbili kubwa kukamatwa huko Hongkong ambapo wamiliki wa meli zilizotumika kufanyia uhalifu huo wanajulikana mmoja wa wamiliki hao akiwa ni Mh Kinana (Kama alivyokiri yeye mwenyewe) basi hata wenye mizigo nao wanajulikana. Pamoja na uchunguzi kuendelea bwana Kinana anapaswa kuwajibika kwa meli yake/zake kuhusishwa na biashara hii haramu.
Hata kama hatapatikana na hatia hii ni kashfa kubwa inayomweka doa kisiasa.
Vinginevyo tutahitimisha kwamba serikali yetu ni dhaifu sana; kama meli zinaweza kuingia Tanzania na kutoka bila kufahamika kilichopo kwenye meli hizo. Kwani hata makundi mengine ya uhalifu yanaweza kusafirisha hata silaha, madini nk kwa kupitia hizi meli za kina Kinana bila kujulikana.
Kwa kawaida chombo kinapokamatwa na nyara za taifa nacho huhusishwa moja kwa moja na pia huwa ni moja ya mashahidi muhimu in the court of law. Mfano mzuri ni 'Samaki wa Magufuli' meli haikuachiwa kwa sababu yenyewe ilitumika tu.
Wanajamvi mnaonaje hili swala limekaaje na nani awajibishwe. Tutafakari kwa manufaa ya nchi yetu sisi na vizazi vijavyo

The latest news is from Tanzania, where reports indicate that elephant numbers have fallen by as much as 42% over the past 3 years. This is a hugely significant number – almost half the Tanzanian elephant population!
The elephant census was carried out at the Selous Game Reserve and Mikumi National Park both important and protected game reserves in Tanzania. The census revealed elephant numbers had plunged from 74,900 in 2006 down to just 43,552 in 2009.
The census was carried out by the east African country's wildlife authority who are deeply concerned about the dwindling population and the escalation of poaching.
...The rapid fall prompted Tanzanian President Jakaya Kikwete to order an investigation, announced his office last Tuesday ( 03.01.2012)
Conservationists estimate Tanzania has a total elephant population of between 110,000 and 140,000