Tanzania: Maisha ya Tembo wetu hatarini!

Tanzania: Maisha ya Tembo wetu hatarini!

Munyangaa hapa unaonekana una asili ya U-manamba unakusumbua,unatetea hata visivyofaa kutetea?Utawarithisha watoto wako nini?Au na wenyewe waje kuwa manamba?Mimi niliishanga sana hii serikali yetu kwani mwenyewe alishakubali meli iliyoshikwa na nyara ni ya kwake,lakini sikusikia hata akiitwa kuhojiwa wala meli kushikiliwa.Aibu kwa serikili ya ccm,vyobo vya dola na pia ni udhalilishaji kwa mfumo wetu wa sheria na fedheha kwa WATANZANIA.
 
angelikuwa ni mwanachama wa CDM naamini angefikishwa hata the HAGUE
 
Inasikitisha sana namna CCM wanavyokumbatia ujangili huu, wakati mwingine unashindwa kuelewa maadili ya viongozi wa CCM yanamsingi gani
 
TANAPA wanaingiaje hapa? kumbukeni uhalifu mkubwa wa meno ya tembo unafanyika katika mapori ya uhifadhi yasiyo chini ya TANAPA likiwemo pori kubwa linalong'ang'aniwa na idara ya wanyama pori iliyo ndani ya wizara ya maliasili na utalii. huko ndiko wanyama wanakoruhusiwa kuwindwa na nahisi askari wao wanahusika moja kwa moja kwa uwindaji haramu wa tembo. Lawama ziende kwa serikali moja kwa moja kwa kushindwa muwa na mikakati ya usimamizi wa rasilimali zetu za nchi.
 
Kampuni iliyoshughulika kusafirisha mzigo uliokutwa meno ya tembo (Clearing & Forwarding Agent) ni ya Kinana; nae amekiri kuwa ni Kampuni yake ingawa kakanusha kuhusika.

Hapo Kinana kwa njia moja au nyingine ni lazima awajibike as far as "C & F Agent" ni kampuni yake.
 
Chama dhaifu! Serikali dhaifu! Wanachama dhaifu!

Unategemea hatua za dhati kuchukuliwa kweli?!

Umesahau na wananchi Dhaifu, wakipewa khanga na pilau watampigia mwizi wa aina yoyote. usifanye mchezo na khanga, kofia na pilau yenye minofu ya nyama
 
Watanzania wenzangu tuko hapa tulipo kwa sababu ya CCM, LAKINI sio lazima tubaki hapa walipotuhifadhi.

CHADEMA ni muhimu mkaunganisha nguvu ya umma kwenye mambo kama haya na sio lazima tusubiri vikao vya Bunge au Tume.
 
Ndg mnyangaa, lori likikamatwa limekodishwa na pembe za ndovu za magendo mwenyewe akasema sikujua kama ndani ya viroba kilikuwepo pembe za ndovu. Je, lori huwa linaachiliwa upulelezi uliendelea? Au inakuwaje.
 
Ndg mnyangaa, lori likikamatwa limekodishwa na pembe za ndovu za magendo mwenyewe akasema sikujua kama ndani ya viroba kilikuwepo pembe za ndovu. Je, lori huwa linaachiliwa upulelezi uliendelea? Au inakuwaje.

Huu mfano mzuri.

Tena hawa watu wa malori huwa hawana hata vifaa vya kupimia kuangalia ndani ya viroba kuna nini!
 
TANAPA wanaingiaje hapa? kumbukeni uhalifu mkubwa wa meno ya tembo unafanyika katika mapori ya uhifadhi yasiyo chini ya TANAPA likiwemo pori kubwa linalong'ang'aniwa na idara ya wanyama pori iliyo ndani ya wizara ya maliasili na utalii. huko ndiko wanyama wanakoruhusiwa kuwindwa na nahisi askari wao wanahusika moja kwa moja kwa uwindaji haramu wa tembo. Lawama ziende kwa serikali moja kwa moja kwa kushindwa muwa na mikakati ya usimamizi wa rasilimali zetu za nchi.

Kwa hii serikali dhaifu tembo wote wataisha. Wenye pesa watakwenda kuwaangalia uarabuni ambako wengine hupelekwa
 
Tanzania ni nchi ya ajabu sana, ukianza kutafakari namna mambo yanavyoendeshwa utakufa siku si zako. Nimesoma jana hapa hapa jf waraka wa mch. Mtikila juu ya tusi empire na nchi yetu inavyohujumiwa na sasa tena hili la tembo, ooh my Lord wapi tunakwenda.

We have nothing to be proud of, we have destroyed our past and now we are busy killing our future.... Pple wake up acheni kulalamika lalamika.
 
Hatua ya kwanza

Watanzania tupige kwa pamoja na hasa wana CCM waungane kumwambia KINANA ajiuzulu kwa kuwa anahusika kwa namna moja ama nyingine na uuwaji, usafirishaji na biashara haramu ya meno ya TEMBO. akikataa tupitishe kura ya maoni kila wilaya walau wanachama 100 na kisha kumpelekea mwenyekiti na CC kwa utekelezaji.

Pili sisi kama watanzania kwa ujumla tupige kelele zetu kwa kutumia silaha kuu mbili vyombo vya habari (Radio, magazeti, TV, social media) mpaka Kinana aachie ngazi na kuwataja walisafirisha meno hayo.

Tatu kupitia vyombo vya kimataifa tutoe rai kwa nchi zote za ULAYA wazuie viongozi wote wakuu wa CCM wasipewe VISA mpaka kinana awajibishwe na kuwataja kwa majina wenye meno.

Nne, Tuiombe jumuiya ya kimataifa kuzuia meli za kampuni ya kina KINANA kujihusisha na usafirishaji wa mizigo mpaka
pale mtandao wa wasafirishaji wa meno ya Tembo watakapotajwa.

Nawakilisha
 
Tukiendelea kulalamika tu, na sisi tutakuwa wananchi dhaifu, hii haihitaji kusubiri 2015, sio suala lachadema, tunaongelea maslahi yetu na ya vizazi vijavyo wawe ccm au cdm.
India mtu kafa kwa kubakwa lakini tumeona wananchi walivyonyesha kwa vitendo jinsi ambavyo hakufurahishwa na hicho kitendo.

Napenda sana amani, lakini hii serikali haihitaji ustaarabu tena, kwa mwendo huu unadhani utawatoa madarakani kidiplomasia au kwa uchaguzi huru ambao haupo? mfumo wote wa serikali umeharibika.

Na hata hiyo katiba mpya ikija, kwangu naona tunapoteza hela bure, watu wanaivunja iliyopo na hakuna kitu kinafanyika.
Matatizo yetu sio ya katiba, ni ya kuwa na viongozi wasio na uzalendo na wapenda rushwa.
 
Uhalifu umeingizwa kwenye utaratibu wa serikali kupitia chama cha mapinduzi. Si siri tena kwamba wahalifu wamekua mhimili wa chama cha mapinduzi kwa namna walivyo "kumbatiana" na viongozi wetu pamoja na mwenyekiti. Swali kunamikakati gani ya kuzuia uchakachuaji na wizi wa kura? Kama sanduku la kura halitazungumza hakuna tunachoweza kukilinda na hakika sio maliasili zetu
 
Hapa niko nchini Hong Kong, taarifa za awali nilizo nazo ni kwamba: Kontena za meno (vipusa) ya ndovu zilizotangazwa kukamatwa huko china siyo mbili kama inavyojulikana. Hali halisi ni kwamba kontena zilizokamatwa ni kumi... lakini mchezo mchafu umechezwa na vigogo serikalini kuzima moto (soo) huo ili ionekane kuwa siyo nyingi kiviiile. Ikumbukwe kuwa Tanzania (serikali) ina-stack kubwa za meno ya tembo katika maghara yake. Ni miongoni mwa-stack hizo wajanja wamekwepua kontena 10. Vigogo wa sirikali wamo... Nafuatilia taarifa za kina zaidi nitaziweka jamvini ASAP... "TUNA MATATIZO MAKUBWA"
 
Mfungwa hachagui gereza mkuu!

Mkuu wangu Buchanan,

Hiyo si ndo inaitwa Provocation? Sasa imagine mtu anaandika vile; mada inahusu nyara za serikali huiko Hong Kong na hujuma anayofanya msomali, halafu anatuuzia chai. Tunauliza, anatu-provoke, ili tutokwe povu, tule ban. Not fair mkuu.

Cc - EMT, Ruta's, AshaDii
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom