Natanguliza shukrani zangu za dhati kwa kualikwa na serikali ya Uganda kushiriki Kongamano na Maonesho ya Petroli ya Afrika Mashariki

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
6,312
8,213
NAFURAHI NIMEPATA MWALIKO WA KUSHIRIKI KONGAMANO NA MAONYESHO YA 10 YA PETROLI AFRIKA MASHARIKI

Jamhuri ya Uganda inatazamiwa kuwa mwenyeji wa Kongamano na Maonesho ya Petroli ya Afrika Mashariki kuanzia tarehe 9- Tarehe 11 Mei 2023 katika Hoteli ya Serena jijini Kampala.
Lengo kuu la kongamano hilo ni kukuza uwekezaji katika sekta ya mafuta na gesi kwa kuudhihirishia ulimwengu uwezo uliopo ndani ya ukanda wetu wa Afrika Masharaki na kubadilishana taarifa kuhusu hali ya maendeleo ya sekta yetu ya mafuta na gesi katika nchi zetu za Africa Mashariki.

Kongamano hilo litafanyika chini ya kaulimbiu “Afrika Mashariki kama kitovu cha Uwekezaji katika Utafutaji na Utumiaji wa Rasilimali za Petroli kwa Nishati Endelevu na maendeleo ya Kijamii”.

Naongeza tena mwaliko wa kushiriki Kongamano na Maonesho ya Petroli ya Afrika Mashariki ni kwasababu ya serikali hii kutambua mchango wangu katika sekta ya mafuta na gesi.

Hivyo natanguliza tena shukrani zangu za dhati kwa Serikali ya Uganda kwa kuandaa tukio hili muhimu ambalo linakusudia kuongeza uwekezaji katika sekta ya mafuta na gesi.

Nina hakika kwamba tukio hili litakuwa fursa nzuri kwangu kujifunza zaidi na kuchangia katika mjadala wa kukuza uwekezaji katika sekta hii muhimu kwa maendeleo ya Afrika Mashariki.

Tena, natanguliza shukrani zangu za dhati kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwa kunialika na ninatazamia kukutana na washiriki wengine katika mkutano huu wa kihistoria.

Namimi nichukue fursa hii kuwaataarifu watanzania wenzangu juu ya kufanyika kwa kongamano hili katika ukanda wetu wa Afrika Mashariki na kuwaomba tukahudhurie kwa wingi ili sote tukashiriki.

Mwisho kabisa tambua kwamba mimi nawewe ndio tutaweza kuikuza sekta yetu ya mafuta na gesi katika taifa letu. Tufanye makongamano na maenyesho kwa wingi ili tupate kutaarifiana juu ya changamoto na fursa zote zilizopo kwenye sekta yetu ya mafuta na gesi.

Uganda.JPG
 
Karibuni kwenye ujenzi wa mradi wa bomba la mafuta kasi imeanza vizuri tupo kuhakikisha unajengwa na kuleta tija
 
Back
Top Bottom