Tanzania kushiriki kuishambulia IRAN

king11

JF-Expert Member
Jun 7, 2010
327
79
katika harakati za kuunga mkono uvamizi wa marekani kwa IRAN tanzania imejikuta ikiunga mkono marekani kutokana na mahusiano yake ya karibu na marekani, Tanzania pia imeahidiwa kupata gawio la mafuta kama wakifanikiwa kuiangusha Iran, mikakati hiyo imekamilishwa kwenye ziara ya Bush na jk amekubali kushirikiana na marekani bega kwa bega
 
NtawashangAa sana wakifanya hivyo. We have to learn to mind our own business. Iran inatuhusu nini? Toka lini tuna ujomba na kina Bush tuanze kuwashabikia kama wanatuhusu
 
Huu ni uongo na Bush hayupo kwenye siasa tena!. Iran kuangushwa itakuwa vizuri kwa wa Iran ambao hata kuandamana hawaruhusiwi!!
 
katika harakati za kuunga mkono uvamizi wa marekani kwa IRAN tanzania imejikuta ikiunga mkono marekani kutokana na mahusiano yake ya karibu na marekani, Tanzania pia imeahidiwa kupata gawio la mafuta kama wakifanikiwa kuiangusha Iran, mikakati hiyo imekamilishwa kwenye ziara ya Bush na jk amekubali kushirikiana na marekani bega kwa bega

Haya sasa
 
chanzo cha umbea huwa kina umuhimu wake pia na kuhusu tz kwenda huko ni ujinga usiokuwa na kifani kwa ya kwetu yanatutoa kamasi ya nini ya wengine :):):)
 
Mkuu mbona habari hii ni kubwa lakini haina source? Marekani akugawie mafuta kweli? Jamaa ni mroho kwa mafuta wee acha tu. Ya Iraq amejitwalia mwenyewe hadi washirika wake wakapiga kelele akawaambia kuna mafuta Libya nendeni mkachukue; Ufaransa weamejitwalia visima Libya. Huko Iran huenda anamtafutia visima mshirika wake mwingine ambaye anapiga makelele kwa kunyimwa mafuta ya Iraq na Libya!! Hadi Tanzania ifikiwe kwenye mgawo, mmmmmhhh!
 
Huu ni uongo na Bush hayupo kwenye siasa tena!. Iran kuangushwa itakuwa vizuri kwa wa Iran ambao hata kuandamana hawaruhusiwi!!

mkuu tumia ufikikiri kidogo hujui kuwa us wanataka kuiharibu dunia ili wao wawe juu ambapo hicho kitu watu washaanza kukijua kwa hiyo iran itakapo dondoka ujue china ni next sababu tz tayari walishatupaka hatuongei kila leo njaa tu na kwao ndio furahi ili makampuni yao ya fanyekazi..

mungu ilaana us na isifanikiwe kwenye mipamngo yake isiyo na maana na pia laana iwaendee wote wanaosupport hiyo kitu.

miafrika bwana job true true..A S embarassed:
 
hebu tuanze taratibu.....kwa hiyo sisi tutaenda kuwatwanga waIran tukishirikiana na USA....?
Ndio maana yake inasemekana majeshi ya ardhini ya Tanzania ni hodari kuliko yale ya Uingereza, na Marekani imevutiwa na sisi baada ya Ufanisi wa hali ya juu wa kumuondoa yule Jenerali muasi pale Comoro ambaye alikuwa na majeshi makali sana na ya kisasa yenye dhana nzito nzito.
N:B, Check kama April fool labda imeamishiwa December.
 
si kwamba tuna jeshi au nguvu ya kumsaidia marekani lakini kikubwa ni marekani anataka uungwaji mkono wa nchi nyingi katika UN na tanzania tuna msaidizi wa katibu mkuu (Asha Rose Migiro). ndio sababu kubwa, wengi awajui misaada kama ya MCC na Daraja la maragarasi yalijengwa kwasababu gani
 
katika harakati za kuunga mkono uvamizi wa marekani kwa IRAN tanzania imejikuta ikiunga mkono marekani kutokana na mahusiano yake ya karibu na marekani, Tanzania pia imeahidiwa kupata gawio la mafuta kama wakifanikiwa kuiangusha Iran, mikakati hiyo imekamilishwa kwenye ziara ya Bush na jk amekubali kushirikiana na marekani bega kwa bega
Heshimu jamvi.
 
Hahahhaahahaahaaaa huu upiuuzi umenifanya nicheke sana! Ninyi wa Tanzania mna kipi hasa cha kuwasaidia jesshi la marekani? Upupu tu!
 
hebu tuanze taratibu.....kwa hiyo sisi tutaenda kuwatwanga waIran tukishirikiana na USA....?

Ndo manake! Wewe mwenyewe umejionea wiki hii ile midege yetu mdebwedo ikipasha. Sio sababu ya kusheherekea uhuru tuu! Yapo kikazi zaidi dada. Tukichanganya na elimu yetu ya mambo ya ki -entelijensia, Iran watakoma!
 
hebu tuanze taratibu.....kwa hiyo sisi tutaenda kuwatwanga waIran tukishirikiana na USA....?
Na ungo au hiyo mitumba yenu nayenyewe imeisha kuwa mikukuu!!!kwanza unaanzaje safari kwenda iran ujinga huu hautaiishia tanzania
 
​sio tanzania kushiriki kuishambulia IRAN bali Marekani wameomba Tanzania kuunga mkono Vikwazo dhidi ya IRAN
 
Duh hii habari kali kweli. Amini Usiamini. Mleta hii habari alikuwa keshakunywa supu ya mawe.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom