Kamanda Asiyechoka
JF-Expert Member
- Sep 13, 2020
- 3,165
- 4,581
Tanzania ni sehemu ya kikosi kilichotumwa chini ya mwamvuli wa SADC kupambana na ugaidi katika mkoa wa kaskazini mwa Msumbiji wa Cabo Delgado.
Awali serikali kupitia waziri wa mambo ya nje Liberata Mulamula alisema kwamba Tanzania haitatuma wanajeshi Msumbiji na badala yake inasisitiza juu ya hitaji la mazungumzo kama njia ya kukuza amani na utulivu nchini Msumbiji.
Msemaji wa Jeshi la Wananchi Tanzania, JWTZ, Brigedia Jenerali Juma Sipe amethibitishia hili BBC akisema kuwa wakuu wa nchi za jumuiya ya maendeleo ya kusini mwa Afrika SADC walikwishaazimia kuwa nchi wanachama wa jumuiya hiyo watasaidia kutatua tatizo linaloendelea nchini Msumbiji.
‘’Makubaliano hayo moja kwa moja yanaihusu pia Tanzania, ikumbukwe Tanzania kwa kihistoria imeisaidia sana Jamhuri ya Msumbiji katika mapambano yake ya kupata uhuru wake na hata baada ya uhuru, pia Tanzania imeshiriki katika harakati nyingi zimesaidia sana kutatua mgogoro uliokuwepo kati ya FRELIMO na RENAMO kwa hivyo tatizo la Msumbiji kwa sasa ni tatizo la kikanda na kimsingi kama Watanzania tuna wajibu wa kushirikiana na wanajumuiya ya SADC katika kutatua tatizo hili.’’ Alisema Brigedia Jenerali Sipe.
Haijabainishwa ni wanajeshi wangapi kutoka Tanzania wanashiriki operesheni hiyo nchini Msumbiji, lakini Brigedia Jenerali Sipe amesema kuwa majeshi yote (nchi zinazoshiriki) yanayokwenda yanayokadiriwa kuwa Brigedi moja yanaratibiwa chini ya SADC kwa ujumla wake.
‘’Kila nchi mwanachama ana kiasi Fulani ambayo itapeleka, wengine watapeleka kwenye hospitali, wengine watakwenda vikundi maalum vya majukumu ya aina mbalimbali, jeshi la wana maji n.k. ‘’ Alifafanua Brigedia Jenerali .
Tanzania inapeleka wataalam gani wa kijeshi?
‘’Operesheni za kijeshi kwa kawaida huchukua vikundi vya aina zote kwa pamoja, vita si kama mechi ya mpira, bali operesheniwakati mnaendelea na mkakati hasa mkakati kama huu wa kupambana na vikundi visivyo rasmi kwa maana ya kwamba si majeshi, bali kikundi ambacho kina asili ya kigaidi kwahiyo wakati huohuo wapo wataalam ambao nao watahitajika ambao pia watasaidia kutathimini aina ya watu tunaokabiliana nao na namna bora ya kushauri ili vikundi vyetu viweze kufanya kazi vizuri zaidi''. Alisema Brigedia Jenerali Sipe.
Hatua hiiimeelezwa kuwa muhimu sana kwa uhusiano wa SADC na ukanda mzima kwa ujumla wake nanchi ya Msumbiji, vile vile usalama wa Msumbiji ni sawa na usalama wa nchi wanachama pia.
Operesheni hiyo ya miezi mitatu inahusisha wataalamu wa kijeshi na vifaa kutoka Afrika Kusini, Botswana, Angola, Tanzania, na Lesotho
Gharama ya awali ya operesheni hiyo ni dola milioni 12M.
Chanzo: BBC