Tanzania kuna sheria kandamizi sana

Tanzania kuna sheria kandamizi sana

konda msafi

JF-Expert Member
Joined
Sep 5, 2018
Posts
1,752
Reaction score
8,996
Kuna clip moja inasambaa instagram ikimwonyesha kijana mmoja mwanafunzi wa CBE akisindikizwa na askari kanzu kupanda kizimbani Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa kosa la kuwa na blog bila leseni kutoka TCRA.

Hizi sheria za kijinga zinapatikana Tanzania tu. Hivi CCM mbona inatulazimisha tuishi maisha ya kijima kama haya? CCM inadumaza uwezo wetu wa kufikiri, inatufanya tuishi kwa hofu kwenye nchi ya mababu zetu.

Mungu tusaidie kutuondolea huu utawala, Amina.
 
Huu utawala wa ccm umetuharibia sana nchi hii. Sheria za kijinga sana hizi. Halafu sijui nasi watanzania tulipewa uchawi gani wa kuwa mazezeta kama hivi. Tunakandamizwa lakini hata kuonyesha reaction yoyote against hizi sheria kandamizi hakuna. Tunaishi tu kama mazombie, ccm wanatufanya wanavyotaka.
 
Ndio maana nasema kijana yoyote mtanzania msomi anayeshabikia CCM au atakayepigia kura CCM ni punguani na mjinga kabisa.
Badala ya ku support vijana wetu wenye ubunifu na uthubutu wa kujaribu kutoka katika maisha kwa mfano wa kuwa na blog, CCM ndio kwanza inaweka vikwazo na kuminya uhuru wa vijana wetu kujiendeleza.

Kumbuka lengo la sheria hizi za KIPUMBAVU ni kubana na kuzuia sauti za Chadema na wanaharakati. Wanaona ni bora watu wenye mawazo kinzani wabanwe kwa gharama ya kuminya fursa za vijana wetu.

CCM NI NI HOVYO, HOVYO SANA.

Na vijana waliowengi nchi hii wasiposimama wenyewe na kupigania uhuru na haki zao za maendeleo na kuikataa CCM, hakuna atakayewasaidia
 
Back
Top Bottom